Jaluo_Nyeupe
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 2,697
- 1,962
kugwangalua = kuchakachua jina la mtu aliyefaulu.
yaani maneno pekee ya Kiswahili sanifu kwenye sentensi yako ni "jina la mtu aliye faulu"asante kwa kuwaona wana jamvi ni mapunguani.kugwangalua = kuchakachua jina la mtu aliyefaulu.
huenda ila je laptop inaitwaje kwa kiswahili?
watch-mosquito watch -sambusaWatch-mak,samak
uja-mass,ujauzito
kiyestaday,kijana
Kuperemba-kusimamia, fuatilia hotuba ya bajeti mkulo:serikali itaperemba mashirika yote yaliyobinafsishwa kujua ubora wake. Sasa kama ni kutongoza haitaleta maana..
watch-mosquito watch -sambusa
katelephone- kasimu
six six chicken love u- sita sita kukupenda wewe
Kuna haja ya kujulkishana misamiati mipya ya lugha yetu adhimu. Kila siku lugja yetu inakua na misamiati inaongezeka kila siku.
Hapa kuna baadhi ya misamiati, pia naomba ndugu zangu muongezee baadhi ya maneno ya Kiswahili sanifu.
Tafrija mchapalo ni cocktail party.
Kanguvuke ni jenereta
Rununu ni simu ya mkononi
Weledi ni profesionalism
baobonya ni keyboard
Puku ni mouse.
Ngamizi ni kompyuta
.wavuti ni internet
tovuti ni website
Kichakata matini ni word processor
Runinga ni television.
Naomba tuongezee misamiati mingine
kweli Kiswahili kigumuJamani Bujibuji hatusemi misamiati, neno sahihi na sanifu ni msamiati iwe katika wingi ama umoja.
Ndugu Katavi,
Salaam. Nimekupigia rununu yako bila majibu. Nilitaka nikufahamishe hitimisho la sakata ya kanguvuke ya Dowans kama ilivyojadiliwa bungeni.
Suala limejadili bila weledi na hii inanipa kihoro kuhusu hatima ya mgao wa umeme. Kwa mintaarafu ya yaliyojiri imebidi iundwe kamati ndogo ya kamati ya madini ili kuanzisha taftishi, na haiyumkiniki kuwa muktadha wa jambo hili utakuwa katika siku za usoni.
Nimeona katika runinga aina mpya ya ngamizi zenye baobonye ambazo puku zake hazitumii waya. Nimepewa dokezo kuwa kinakishi na nukushi vinapatikana kisutu madukani mkabala na jengo la mfuko wa jamii. Jaribu kutembelea wavuti ya JF ili kubaini uwezo wa kichaka matini yake kabla hujaagiza.
Usisahau kumwambia bujibuji ujumbe wake murua nimeupata. Ukiweza kumtia machoni Dena Amsi muulize kulikoni? ni muda sijasikia kutoka kwake. Vipi unategmea kuhudhuri kongamano aliloaanda Lizzy, mimi nitakuwa na warsha na nadhani AD, Hapanuchi nao watajumuika nami.
Tadhali usomapo ujumbe huu naomba usuli. Wajulie hali akina invisible, malaria sugu na Masanilo. Nasikia hamkani si shwari kwao walipata ban je ni kweli. Nasikia pia MMU wanaomba uanisho mtu anapofungiwa, je mchakato wa suala hilo umeshamfikia Melo.
Maslaam
Kaka Nguruvi.
Duh.......... Hii mpyapataninga - video