Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,821
- 59,427
Leo asubuhi nilikua nafikiria kitu nikajikuta naangalia mahusiano na ndoa kwa namna ambayo sikuwahi kabla. Mimi na wewe ni kama vipande vya puzzle ....you've got your share and I have got mine.Ukiviweka pamoja either unapata picha/umbo kamili ama hupati.
kila mmoja ana shape na size tofauti.Inapotokea wewe kama puzzle umemchagua mtu ambae yeye kama puzzle hana shape zinazoendana na vipande ulivyonavyo ndipo matatizo na migongano inapoanza.Utajitahidi kunoa na kuongeza zile sehemu zisizofit vizuri kwako au kwake ila mwishoni unashangaa pamoja na jitihada zako zile sehemu zinapwaya na ukiendelea kulazimisha zinavunjika na kuvunjika.
So jambo la muhimu hapa ni kutafuta vile vipande ambavyo vinaendana na vyakne that is complementary to yours....one that accomodates your needs.
Linapokuja swala la ndoa ndo kabisa umakini wa hali ya juu unahitajika.Hapa kinachofanyika ni kuvishikanisha vipande vyako na vya mwenzako kwa glue.Hata kama haviendani at first havitakua na jeuri juu ya glue....ila baada ya muda utashangaa huku kunameguka...na vikianguka tu vinavunjika vunjika.Ila kama vitakua vinaendana ni rahisi kustahimili mitikisiko na mianguko.Hata sehemu ikimeguka ni rahisi kuirudishia.Kwahiyo kuweni waangalifu....usichukue tu vipande ni vipande...
....bali tafuta vile vinavyokufaa!!
Mchana mwema!!
So jambo la muhimu hapa ni kutafuta vile vipande ambavyo vinaendana na vyakne that is complementary to yours....one that accomodates your needs.
Mchana mwema!!