Mimi huwa nafanya kinyume na mke wangu…………!

Kaka mkubwa kwa heshima yote inayokustahili naomba uende usome stori iitwayo 'A boy who cried wolf' utaona maudhui yake. Kwa sababu unachofanya hapo ni kumfanya aelewe your positive 2b negative and your negative to be positive. Sasa tatizo litakuja utakapomkataza kitu na yeye akafanya coz anajua umemaanisha kinyume chake. Don't be sitaki nataka, let positive be positive and negative be negative (That is true leadership). Halafu mpe credit kwa mchango wake wa mawazo katika kusukuma gurudumu ya maendeleo ya familia she deserves it!
 
naelekea hupendi kushindwa ikiwa hujui lolote

Si ndio maana nikasema nina udhaifu au sijui niseme nina ujinga..............Uzuri ni kwmaba mtu akijua tabia yake, hasa kama ni mbaya, ujue anayo nia madhubuti ya kutaka kuiacha, hapa natafuta msaada wa Kisaikolojia mwenzenu..............
 
we mtambuzi!hebu tambua unaelekea kubaya!tabia yako ya kupenda kufanya kinyume siku moja utapotea njia!ipo siku mkeo atakuita akupe tendo la ndoa akalala chali we kwa kupenda kinyume utamlaza kifudifudi!angalia sana mzee wangu utaharibu mambo uzeeni acha kabisa kupenda kufanya kinyume na kawaida!
 
Haya, sasa umeelewa, hebu nipe maoni yako...........Je niache hii tabia au?

Nimekuelewa mkuu na ninaona ujitahidi uachane na hako katabia na kama anatoa mawazo mazuri mpe support atajisikia naye ana mchango katika familia,pia atakuwa huru kutoa mawazo yake siku nyingine
 
Mtambuzi huko nyuma ulipata kusema kwamba wewe una wivu kwa sababu hata Mungu mwenyewe ana wivu.

Kwa vile shemeji keshazoea hii hali basi huna cha kubadilisha kwani mwisho wa siku huwa unatenda kama alivyoshauri!
 
Mkuu heshima yako....!?
Nadhani unavyokuwa unapinga ni kwa faida..! si kwa hasara...!
Kwa kuwa mama ngina ni Brave woman anakupa maushauri ya manufaa..!
Na wewe kwa kuwa ni Clever man unapinga kwa udadisi zaidi ili mama ngina autolee ufafanuzi mzuri na wa kueleweka ushauri wake aliokupa.
Mwisho wa siku kwa kuwa mama ngina ashakunyambulishia kwa ufasaha, na wewe katika mtima wako umeridhika kwa dhati kabisa, unaamua kuufuata ushauri wake.
Hivi ndio kupinga/kubisha kwa faida, kubisha/kupinga ili ujue.
 
Wewe Mtambuzi huna adabu, ebo!

Mimi nilishachuma fimbo baada ya kusoma heading nikidhani wewe na mama Ngina mna kale kamchezo, kumbe unazungumzia kufanya mambo kidumedume, lah!

Anyway, bahati yako

Siyo wewe hata mimi nilidhani jamaa kapinda kumbe longolongo lakini inabidi kumjuq Mtambuzi kama ID yake ilivyo.
 
Mtambuzi, ndugu yangu una mambo mengi, ila kwa kifupi mkeo, ambaye ni shemeji yangu yaani mama Ngina nampongeza maana anafahamu kwa undani nini maana ya ndoa na amejitahidi kuelewa tabia zako, na kuzikubali na hivyo hizo changamoto na tabia unazomuonyesha ambazo kwa kiasi hata wewe mwenyewe unazishtukia, yeye anazichukulia poa.

Cha msingi na wewe jitahidi kumuelewa mama Ngina na kuvumilia kwa udhaifu wa kawaida wa kibinadamu unaojitokeza ili kuwa na miaka mingi ya ndoa ya amani na furaha. Usizibadili hizo tabia kama yeye amezizoea na kuonyesha kuzipenda maana unaweza kushtua na kukuona huna msimamo. Nashawishika kwa sehemu ndogo kuamini vituko vyako na majanga yaliyokukuta kwenye maisha ndiyo yaliyomvutia akupende.
 
Mheshimiwa mbona unavujisha siri zetu za ufanyaji wa maamuzi ya kifamilia? Ila hicho kichwa cha habari sikukielewa mwanzo mpaka niliposoma ujumbe wenyewe.
 
Wewe ni gwanda orijino, wamekataa mjadala wa katiba bungeni, wakasusa, dakika ya mwisho wakaomba kuonana na Rais na kukubali. Una tofauti ipi na viongozi wako wa chadema?

No politics please,utabadilisha hii thread iwe ya kisiasa.Wana-MMU ni wanasiasa pia lakini wapo hapa kwa kupeana uzoefu mwingine wa maisha kwani nchi yenyewe hii "IMESHAUZWA"
 
Napenda kukiri wazi kwamba nina tabia ya ajabu sana katika mahusiano yangu na mama Ngina. Sijui niite ni ila mbaya au ni udhaifu au ujinga.

Katika maisha yangu na mke wangu tangu tuoane, nimekuwa nikifanya mambo kinyume na matarajio yake, pale anapotarajia jibu la hapana huwa ninasema ndiyo, na pale anapotarajia jibu la ndiyo mimi nasema hapana.

Kwa mfano, mke wangu anaweza kuniomba tufuatane kwenye mwaliko wa sherehe fulani ambayo amealikwa, mimi naweza kukataa kuandamana naye nikidai nina kazi nyingi za kufanya hapo nyumbani, anaweza kunibembeleza, na mimi nikakataa katakata, lakini akishajiandaa na kutaka kutoka namuomba anisubiri tuandamane. Wakati akiwa ameshikwa na butwaa, mimi nabadilisha nguo haraka haraka na kuongozana naye.

Mfano mwingine, inatokea tunataka kufanya jambo fulani, yeye anaweza kuja na maoni yake mazuri tu, na akayajengea hoja mpaka nikaelewa, lakini kutokana na kupenda kwangu kutofautiana naye, naweza kupinga wazo lake na kujenga nadharia yangu ya kufikirika na kwa sababu hapendi kubishana na mimi anakubali wazo langu. Lakini wakati wa utekelezaji, nafuata ushauri wake kama alivyotaka, basi huwa anabaki ananishangaa.

Amekuwa hanielewi na anawaeleza hata rafiki zake kuwa mimi ni mtu nisiyeeleweka kabisa, lakini ndio keshanizoea mumewe kimeo..................!

lol.......Babu yangu mtata kweli weye mi nlivyoona heading ilivyo nkachanganyikiwa babu tena nini hii ya chumbani hapa barazani! kumbe unamanisha mfumo dume? badili katabia hako si kazuri katakuharibia siku isiyo na jina.
 
mfumo dume bado unakutawala kichwani, na unaona kama vile ukimkubalia wazo zuri moja kwa moja ataonekana anajua sana kuliko wewe
 
Back
Top Bottom