Mimi huwa nafanya kinyume na mke wangu…………!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Napenda kukiri wazi kwamba nina tabia ya ajabu sana katika mahusiano yangu na mama Ngina. Sijui niite ni ila mbaya au ni udhaifu au ujinga.

Katika maisha yangu na mke wangu tangu tuoane, nimekuwa nikifanya mambo kinyume na matarajio yake, pale anapotarajia jibu la hapana huwa ninasema ndiyo, na pale anapotarajia jibu la ndiyo mimi nasema hapana.

Kwa mfano, mke wangu anaweza kuniomba tufuatane kwenye mwaliko wa sherehe fulani ambayo amealikwa, mimi naweza kukataa kuandamana naye nikidai nina kazi nyingi za kufanya hapo nyumbani, anaweza kunibembeleza, na mimi nikakataa katakata, lakini akishajiandaa na kutaka kutoka namuomba anisubiri tuandamane. Wakati akiwa ameshikwa na butwaa, mimi nabadilisha nguo haraka haraka na kuongozana naye.

Mfano mwingine, inatokea tunataka kufanya jambo fulani, yeye anaweza kuja na maoni yake mazuri tu, na akayajengea hoja mpaka nikaelewa, lakini kutokana na kupenda kwangu kutofautiana naye, naweza kupinga wazo lake na kujenga nadharia yangu ya kufikirika na kwa sababu hapendi kubishana na mimi anakubali wazo langu. Lakini wakati wa utekelezaji, nafuata ushauri wake kama alivyotaka, basi huwa anabaki ananishangaa.

Amekuwa hanielewi na anawaeleza hata rafiki zake kuwa mimi ni mtu nisiyeeleweka kabisa, lakini ndio keshanizoea mumewe kimeo..................!
 
U sound like my boss!
Ni bora anakuelewa maana ningekuwa mimi napunguza creativity na ninakuachia ucome up with ideas as u r mr noeverything!

Honestly speacking boss wetu anaboa kishenzi na akitumia idea yako anajimilikisha na kujisifia kuwa yeye ndiye super brain!
 
Kwa hiyo unanishauri niache hii tabia?
Nimejaribu kuiacha lakini nimeshindwa kabisa, sijui nitumie mbinu gani?
 
Wewe ni gwanda orijino, wamekataa mjadala wa katiba bungeni, wakasusa, dakika ya mwisho wakaomba kuonana na Rais na kukubali. Una tofauti ipi na viongozi wako wa chadema?
 
ni katabia ka wivu na ubinafsi endelea kujichunguza hata nje ya ndoa yako...
 
Mzee mwenzangu,

Mbona sasa ushamrahisishia mambo? Hivi sasa anajua ukikataa ndo umekubali!!

Mzee mwenzio mimi, siku nyingine nikimpinga nampinga kweli lakini sikunyingine nampinga kimagumashi. Mwisho wa siku huwa hajui kabisa msimamo wangu.
 
Hii tabia ina-apply nyumbani tu mkuu, huko kibaruani mimi sio decision maker kabisaa, na hata mtaani kwenye social activities ni msikilizaji tu katika vikao, ila nyumbani ndio sehemu yangu ya kujidai na kujikweza.............LOL
 
Wewe ni gwanda orijino, wamekataa mjadala wa katiba bungeni, wakasusa, dakika ya mwisho wakaomba kuonana na Rais na kukubali. Una tofauti ipi na viongozi wako wa chadema?
Duh! Mkuu ushahamia kwenye SIHASA!
 
Wewe Mtambuzi huna adabu, ebo!

Mimi nilishachuma fimbo baada ya kusoma heading nikidhani wewe na mama Ngina mna kale kamchezo, kumbe unazungumzia kufanya mambo kidumedume, lah!

Anyway, bahati yako

Mwenyewe heading ilinishtusha nikajiuliza ni nani anaguts za kusema ana-do kinyume na mkewe,kumbe wanatofautianaga mawazo
 
Mzee mwenzangu,

Mbona sasa ushamrahisishia mambo? Hivi sasa anajua ukikataa ndo umekubali!!

Mzee mwenzio mimi, siku nyingine nikimpinga nampinga kweli lakini sikunyingine nampinga kimagumashi. Mwisho wa siku huwa hajui kabisa msimamo wangu.
Mkuu huwa napima upepo kabla ya kufanya uamuzi ili kujua anatarajia nini.................Huwa nakuja na majibu asiyoyatarajia mara zote....................suprise eh!
 
Wewe Mtambuzi huna adabu, ebo!

Mimi nilishachuma fimbo baada ya kusoma heading nikidhani wewe na mama Ngina mna kale kamchezo, kumbe unazungumzia kufanya mambo kidumedume, lah!

Anyway, bahati yako
Mkuu umeenda mbali bana..................!
 
Wewe ni gwanda orijino, wamekataa mjadala wa katiba bungeni, wakasusa, dakika ya mwisho wakaomba kuonana na Rais na kukubali. Una tofauti ipi na viongozi wako wa chadema?

Hii ndio shida ya kuongozwa na jazba. Sasa kwa akili yako unadhani CHADEMA walishindwa au? Ngoja nikufafanulie kabwanamdogo:
Baada ya CHADEMA kumwaga data magogoni, somo lilieleweka lkn Baba Mwanaasha akawa anawahofia wanamagamba wenzake kama watamuelewa. Hata hivyo akakaza moyo na kuurudisha muswada mjengoni (ina maana hata hii hukusikia, unaishi wapi wewe). Baada ya migomo ya hapa na pale hatimaye wanamagamba wa mjengoni waliamua kukubali kwa shingo upande huku wengine wao kwa unafiki wakisema kuwa ni hoja nzuri (waliogopa baba mwanaasha angelazimika kuvunja bunge).

Hayo ndio yaliyojiri ndugu, kigeugeu ni wabunge wa magamba waliogomea kikao na bosi wao na baadaye wakakubali na wakaonesha jinsi walivyo shallow kwa kusaini marekebisho bila hata kuyajadili. Poor you and your magamba compatriots.
 
Mwenyewe heading ilinishtusha nikajiuliza ni nani anaguts za kusema ana-do kinyume na mkewe,kumbe wanatofautianaga mawazo
Haya, sasa umeelewa, hebu nipe maoni yako...........Je niache hii tabia au?
 
Hii ndio shida ya kuongozwa na jazba. Sasa kwa akili yako unadhani CHADEMA walishindwa au? Ngoja nikufafanulie kabwanamdogo:
Baada ya CHADEMA kumwaga data magogoni, somo lilieleweka lkn Baba Mwanaasha akawa anawahofia wanamagamba wenzake kama watamuelewa. Hata hivyo akakaza moyo na kuurudisha muswada mjengoni (ina maana hata hii hukusikia, unaishi wapi wewe). Baada ya migomo ya hapa na pale hatimaye wanamagamba wa mjengoni waliamua kukubali kwa shingo upande huku wengine wao kwa unafiki wakisema kuwa ni hoja nzuri (waliogopa baba mwanaasha angelazimika kuvunja bunge).

Hayo ndio yaliyojiri ndugu, kigeugeu ni wabunge wa magamba waliogomea kikao na bosi wao na baadaye wakakubali na wakaonesha jinsi walivyo shallow kwa kusaini marekebisho bila hata kuyajadili. Poor you and your magamba compatriots.
Haya amekuelewa.............Sasa turudi kwenye topic..................:focus:
 
Wewe ni gwanda orijino, wamekataa mjadala wa katiba bungeni, wakasusa, dakika ya mwisho wakaomba kuonana na Rais na kukubali. Una tofauti ipi na viongozi wako wa chadema?

Magamba bana... siasa hata pasipo siasa....nadhani gamba ulovua limeanza kuota jingine.... ndo shida ya magamba huwa hayakawii kuota...
 
Sasa hizo alizoelezea kama si siasa ni nini? kwi kwi kwi teh teh teh.

Wewe unafikiri siasa ziko nje ya majumba yetu tu? kuna u ccm, u cuf, u nccr na u cdm mpaka kwenye 6x6. Kalagabaho!
 
labda unataka kumuonyesha nani mwenye 'mamlaka?'
'nani mwenye maamuzi?"
naona kama mnagombea "power"(sijui umenielewa?)
:wink2:
 
Back
Top Bottom