Milioni 50 zatumika kumpeleka Arusha Freeman mbowe

Nd. Mnyanza, nakujulisha kwamba pombe haipunguzi mawazo ILA mawazo hupunguza pombe. Afrika kote,wameanza waarabu, marais au vyama vilivyokaa madarakani kwa muda mrefu wananchi wamevichoka. CCM 'wana-magamba' nao wamechokwa. Wenyewe wamejigundua wamekaa muda mrefu wanastahili kujivua magamba sio ya rushwa tu, ila mauaji ya kimbali kupitia polisi wao; mauaji ya albino kama walivyoagizwa na waganga wao, vifoo vya mamia hospitalini kwa huduma duni zinazotolewa na serikali ya CCM. CCM hawana tofauti na wauaji wa kimbali huko Rwanda. Tena Rwanda waliwauwa kwa muda mfupi, CCM imeanza kuuwa toka JK Nyerere atoke uongozini, tukianzia Loliondo wakati wa Mwinyi na ruksa zake za kuuwa uwa, hadi mwembechai.
 
sio kazi rahisi sana kwa polisi waliomsafirisha Mbowe kujua gharama halisi na kwa kuwa mbowe alisafirishwa kwa ndege si kweli kwamba kila wilaya walipangwa polisi ilihali ndege inapita angani. Si vema kukuza jambo ingawa gharama kwa ndege haziepukiki ikilinganishwa na usafiri wa barabara.

Jf
polisi waliohusika na shughuri ya kumsafirisha Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe kutoka Dsm kwenda Arusha wanasema ni zaidi ya milioni 50 zilitumika kwa safari hiyo

lakini pia kila wilaya kulikuwa na polisi waliowekwa tayari kupambana na wanachama wa chadema ambao wangeonekana kuleta fujo na polisi wote hao wamelipwa posho zao

Pia yaliandaliwa magari yenye maji ya kuwasha na yote hayo yalijazwa mafutwa kwa pesa ya serikali

hivyo basii polisi hao wanalalmika kwa nini pesa zote hizo zitumike kwa kumkamata mtu mmoja tu ilihali mpaka leo wao kama polisi wanadai malimbikizo ya mishahala yao na hawajalipwa mpaka leo

kazi ipo jamani,tutafika kweli?
 
Mbowe ni mwanasiasa maarufu hapa nchini na mwenye wafuasi wengi isingekuwa busara kumpeleka kwa barabara ambapo ingetokea ajali ya kumdhuru au kufa hakuna kati yetu ambaye angajitoa kulaumu kuwa ni ajali ya kupangwa. Kimsingi, ajali ya gari inaweza kupangwa lakini sio ajali ya ndege.
 
Ili kuwahi muda wa kesi mahakamani Arusha kulikuwa hakuna jinsi ya kukwepa usafari wa anga ambao ungemfikisha mbowe mahakamani kwa muda uliopangwa lakini pia kukwepa wafuasi wake ambao wangejua aina ya usafiri ambao mbowe angetumia wangeweza kujipanga barabarani kwa nia ya kutoa shinikizo lolote lile dhidi ya polisi. hatuwezi kupuuza kwamba pengine hakukuwa na ndege ingine ya abiria ambayo ingemfikisha Mbowe kwa muda muafaka mahakamani. inaelezwa kwamba ndege hiyo iliondoka usiku wa manane na kutua alfajiri Arusha ili kuepusha ghasia na vurugu kutoka kwa wafuasi wa mbowe au chadema jambo ambalo mimi naona ni jema.
 
Back
Top Bottom