Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

Thi walikuwa wamekaribia kufanya mitihani thatha itakuwaje?makubwa haya
 
hivi ni kweli serikali inashindwa kuwalipia mkopo 100% au ndo hivyo wanazungushia kwenye mabussiness yao?
Fikiria kuna watu pale wamesoma secondary za kata kwa ada za kuunga unga sasa iweje umwambie alipie 40% atatoa wapi kama kwenye shule za YEBO YEBO alisoma kwa kubangaiza hiyo 40% atapata wapi???Nyie viongozi mlio soma kwa mkopo enzi hizo mpaka leo hamjalipa deni hilo mtuambie atapata wapi?
Au ,mnajua wote wanatoka famiria bora zinazo soma st.marys?
 
ANAYESEMA kwamba haiwezekani wanafunzi kupewa mkopo asilimia 100 kawauliza Barricks, DeBeers, Anglo-American na wenye migodi wengine. Mimi nadhani huo mrabaha au mrahaba ukiongezwa hadi asilimia 10 tu basi shida zote za wanafunzi zitakwisha.

Pili taasisi inayotoa mikopo ifutwe. Mikopo itolewe na TIGGO kupitia kwenye simu zao za mkononi kwa fedha za matumizi na zile za kulipa Chuo zipewe Benki yangu nitakayoianzisha kwa mtaji wa fedha toka BOT kama haki yangu baada ya wenzangu wa EPa kunitosa mapema mwaka juzi!

Halafu tuache hii tabia ya kuona kwamba matatizo yako upande wa WANAFUNZI DAIMA DAWAMU?

Mnataka kunamambia Wakuu wa vyuo hawachemshi tena kwa saaana! Mnataka kunambia idara ya fedha na administrators wengine hawana vijambo na vijambazi vyao?

Tuwe watu wa haki. Na hivi huko kwa kina OBama mbona sijasikia migomo ya wanafunzi. Siri ya mafanikio yao nini. Balozi wa Marekani wape vijana tripu wakajifunze kwanini Marekani wanafunzi hawagomi labda iwe bahati mbaya mmoja wao avute bangi au unga kisha apige wenzie na walimu risasi tu....
 
hivi ni kweli serikali inashindwa kuwalipia mkopo 100% au ndo hivyo wanazungushia kwenye mabussiness yao?
Fikiria kuna watu pale wamesoma secondary za kata kwa ada za kuunga unga sasa iweje umwambie alipie 40% atatoa wapi kama kwenye shule za YEBO YEBO alisoma kwa kubangaiza hiyo 40% atapata wapi???Nyie viongozi mlio soma kwa mkopo enzi hizo mpaka leo hamjalipa deni hilo mtuambie atapata wapi?
Au ,mnajua wote wanatoka famiria bora zinazo soma st.marys?

exactly...na ukiwambiwa fedha zinazotakiwa kutosheleza huo wanaoita mkopo kwa asilimia 100 utashangaa...ukilinganisha na hela zinazotengwa kwa 'matumizi mengine'
 
Nyerere alisema usipothamini elimu una uhakika wa kuwa na taifa lenye wajinga...Nadhani JK na serikali yake wanataka kuturudisha kwenye ujima. Haingii akilini taasisi kama Chuo kikuu wanafunzi wanaweka madai ya msingi then serikali inaona kama mchezo.Sijui na huyo Maghembe asingesoma kwa huruma na sera za Nyerere huenda angebaki kuwa Mganga wa Tiba za Jadi Mwanga huko...Ananiudhi sana huyo bwana!!!
 
KUNA TAARIFA KUWA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KIMEFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA KUTOKANA NA WANAFUNZI KUENDELEA NA MGOMO LICHA YA WAZIRI WA ELIMU PROF MAGHEMBE KUWASISITIZIA WAINGIA MADARASANI IFIKAPO LEO SAA MOJA ASUBUHI, PIA KUNA HABARI KUWA MGOMO HUU UNAMASLAHI YA KIITIKATI ZA KIVYAMA NA INASEMEKENA KUNA NGUVU KUBWA YA CHAMA KIMOJA KIKUBWA CHA SIASA( hayo ni maneno ya wanafunzi wenyewe)

'Fisadi siku zake nyingi Idi, lakini kuna siku ya siku hatokaa afaidi!
Japo anakunywa maji kwenye debe,
atakunyima wewe ya mkebe,
Kama baba mlevi awapo kwenye pombe,
Huwanywesha na kuwalisha wengi,
Lakini akirudi nyumbani kiama,
watoto wako macho sio kwa kupenda ili kutokana na njaa inavyouma!
Mwana huacha kitanda
akalala chini mgongo kapinda,
Ili aidanganye njaa kashiba!'
 
Nyerere alisema usipothamini elimu una uhakika wa kuwa na taifa lenye wajinga...Nadhani JK na serikali yake wanataka kuturudisha kwenye ujima. Haingii akilini taasisi kama Chuo kikuu wanafunzi wanaweka madai ya msingi then serikali inaona kama mchezo.Sijui na huyo Maghembe asingesoma kwa huruma na sera za Nyerere huenda angebaki kuwa Mganga wa Tiba za Jadi Mwanga huko...Ananiudhi sana huyo bwana!!!

Lakini tunapaswa kukumbuka kuwa serikali ya wakati huo haikuwa na watu wengi kama waliopo serikali ya sasa, mimi nakumbuka kabisa chuo hiki kilikuwa kimya all the time, huwezi kusikia makelele ya kijinga jinga na mamiziki huko kwenye mabweni kama ilivyo sasa, na serikali ya wakati wa nyerere wanafunzi hawakuwa wengi kama walivyo sasa, vyuo havikuwa vingi kama vilivyopo sasa maisha hayakuwa juu kama yaliyopo sasa so sometime inabidi tukubaliane na hali na kutii yale tunayoambiwa, tukisema tushindane na serikali kwa kweli matokeo yake ndo haya, walisema utakuwa mgomo usio na kikomo na hata wakiondolewa chuo hawataondoka lakini cha kushangaza wote wapo busy kutafuta usafiri ili waondoke, sidhani kama suluhisho lilikuwa kugoma kuingia darasani.
 
Kwakweli inasikitisha sana,ivi kweli katika viongozi wote hakuna mwenye mtoto pale au? hii ishu ilikua iwe muhimu sana pale bungeni kutatua ili tatizo mana wasomi hawa ndio viongozi wa badae mambo ya comes around goes around yatakuja kutumaliza huko mbeleni.

Anyway nawahurumia ndugu zangu tu wenye kupata elimu kwa mbinde. sidhani hata wakimaliza watakua na hamu ya kurudisha mikopo yenyewe kwanza!!!!
 
Waga,
Nchi yoyote ile idadi ya raia wake huongezeka na si kupungua. Suala kuwa kwa sasa watu wamekuwa wengi hivyo rasilimali hazitoshi si kweli. Kwa mtazamo wangu tatizo si wingi wa wanafunzi bali mipango mibovu ya serikali yetu. Utashi wa viongozi wachache wenye uchu wa kifisadi ndio hupelekea matatizo yanayotokea sasa. Ukirudi katika masuala machache yanayopigiwa kelele kila wakati kama mikataba ya kifisadi katika madini, Ubadhirifu wa pesa za umma katika maeneo mbali mbali ndio yametuweka katika kona ngumu hii.

Kwa kweli kama sekta ya madini, maeneo mengine ya uchumi yangeendeshwa kwa uwazi na umakini Tanzania ina uwezo wa kuwalipia ada wafunzi wote waliopo vyuo vikuu ada. Tatizo tumefika mahali walioko madarakani wanaona sasa elimu sio priority tha's why wanavuruga mambo.

Tanzania ilipopata uhuru ilikuwa masikini wa kutupwa na ndio maana nyererea alikuwa anahangaika kutafuta mifumo itakayoweza kuwafanya raia wake waelimike na kujiweka mahali ambapo wanaweza kujijengea uchumi wao. Nadhani JK angechukua nchi hii baada ya uhuru tu nina uhakika tungeshuhudia mambo ya ajabu sana. Kama leo hii amekuta nchi iko imesimama waliomtangulia wameng'oa visiki na kutoa vichaka uwanja mweupe anachemka ingekuwaje wakati huo?

Kuna tatizo na serikali yetu mi ndio msimamo wangu. Suala kuwa chuo kikuu kumekuwa na kelele za muziki siku hizi si hoja. Mlipie mwanafunzi stahili zake then muache yeye mwenyewe aamue kama kusikiliza muziki au kusoma, mitihani itatoa majibu. So kuwavuruga watu hapa.
 
Tetesi ambazo zimezagaa ni kuwa chuo kitafungwa mpaka january na kila mwanafunzi atatakiwa kuandika barua ya kujifunga kuwa hatagoma tena na atalipa ada yote ya shule inayostahili
 
Hiki chuo vipi? kuna watu wanajilipia ada wenyewe na wengine wanalipiwa na waajiri au wafadhili wao! sasa wanafukuzwa kwa issue zisizo wahusu, niwakati sasa kukishitaki chuo mahakamani kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kwani wanafunzi hawa walishalipa ada zao kamili.

kama mwanafunzi hana ada wamzuie kuingia chuoni hadi alipe hiyo fedha kama anaikopa saccos au helsb!
 
Waga,
Nchi yoyote ile idadi ya raia wake huongezeka na si kupungua. Suala kuwa kwa sasa watu wamekuwa wengi hivyo rasilimali hazitoshi si kweli. Kwa mtazamo wangu tatizo si wingi wa wanafunzi bali mipango mibovu ya serikali yetu. Utashi wa viongozi wachache wenye uchu wa kifisadi ndio hupelekea matatizo yanayotokea sasa. Ukirudi katika masuala machache yanayopigiwa kelele kila wakati kama mikataba ya kifisadi katika madini, Ubadhirifu wa pesa za umma katika maeneo mbali mbali ndio yametuweka katika kona ngumu hii.

Kwa kweli kama sekta ya madini, maeneo mengine ya uchumi yangeendeshwa kwa uwazi na umakini Tanzania ina uwezo wa kuwalipia ada wafunzi wote waliopo vyuo vikuu ada. Tatizo tumefika mahali walioko madarakani wanaona sasa elimu sio priority tha's why wanavuruga mambo.

Tanzania ilipopata uhuru ilikuwa masikini wa kutupwa na ndio maana nyererea alikuwa anahangaika kutafuta mifumo itakayoweza kuwafanya raia wake waelimike na kujiweka mahali ambapo wanaweza kujijengea uchumi wao. Nadhani JK angechukua nchi hii baada ya uhuru tu nina uhakika tungeshuhudia mambo ya ajabu sana. Kama leo hii amekuta nchi iko imesimama waliomtangulia wameng'oa visiki na kutoa vichaka uwanja mweupe anachemka ingekuwaje wakati huo?

Kuna tatizo na serikali yetu mi ndio msimamo wangu. Suala kuwa chuo kikuu kumekuwa na kelele za muziki siku hizi si hoja. Mlipie mwanafunzi stahili zake then muache yeye mwenyewe aamue kama kusikiliza muziki au kusoma, mitihani itatoa majibu. So kuwavuruga watu hapa.

Nimekuelewa mkuu
 
Thanks Waga kwa kuelewa and I like your signature hao wanaotembelea mashangingi na Ma-Lexus yenye viyoyozi ndio wanaotuvurugia mambo nchi inaonekana kama haina mwenyewe bora Somalia kusikokuwa na serikali mtu unaweza kuelewa hakuna wa kummuliza mwenzie..
 
I really feel these students. Maisha ya mlimani ni magumu, bila bumu hali ni ngumu.

Lakini napenda kuangalia upande wa pili wa shilling. Leo hii 80% ya watanzania wanaishi vijijini wakitegemea jembe la mkono. zaidi ya raia million kumi na tano wako kwenye UMASIKINI WAKUTUPWA. Walio na nafuu wengi wao wanabangaiza mno. Kwa hiyo swala kwamba watoto wengi wanaosoma mlimani ni watoto wa wakulima ni kweli lakini hilo inabidi tufike point tulitafutie muafaka. Nchi yetu ina matatizo mengi mno. Wewe atleast unalalamika lakini kuna millions ambao hata hiyo chuo kikuu ni ndoto ya mchana. wanataka tuu wapate ugali wa mchana. Kuna akina mama wanakufa kwa sababu hawana aspirini, kuna sehemu umeme ni anasa, maji ya bomba ni ndoto..and on and on...Sasa jamani haya ni matatizo ambayo yanaiangalia hiyo hiyo bajeti na kodi zetu.....Think about it..matatizo ni mengi mno....Ingawa watu ni mafisadi wanaiba..lakini hatuwezi kuendelea kutumia kigezo cha umasikini forever...

Tanzania haiwezi KUWAKOPESHA wanafunzi WOTE wa elimu ya juu. Huo uwezo hata kama upo....itatuchukua miaka mingi kuwa na vigezo halali vya kujua nani anastahili...especially kipindi hiki ambacho kila mtu ni fisadi anadanganya... Mimi naamini ile ya kukopesha (60% not sure) was the best way kuwasaidia watoto wa wakulima.... Wazee elimu ya siku hizi ni aghali mno......

Swala kwamba tuna raslimali ambazo zinaweza kuwakopesha wanafunzi kama zingetumika vyema..ni kweli I agree..lakini wote tunajua kabisa..nchi haiendeshwi hivyo...Hata mimi ningesema..yale mabillion ya EPA yangerudishwa..hali za watanzania zingekuwa bora zaidi..lakini we all know what is happening.

Ushauri wangu kwa wanafunzi wa mlimani na kwingineko..inabidi wajue kwamba maisha na zama zimebadilika. huwezi kuishi kwa zile slogans zetu eti..mbona "serikali zamani ilikuwa ikiwasomesha watu wake bure". Hizo slogans hazisaidii tena. Lazima wanafunzi wakae chini waangalie hiyo 40% inapatikana vipi. Mgomo siyo suluhisho....Serikali haina wajibu wa kukusomesha! na wala haina wajibu wa kuwapa mikopo! ni swala la sera tuu.

Kifupi wanafunzi wa elimu ya juu...inabidi waanze kusolve matatizo yao kiutu uzima..sana sana leo wamegoma...watoto wa wenye uwezo..wataenda zao nje..mtoto wa mkulima utarudi Kigoma (kama bado una nauli)..after two moths utaambiwa uandike barua uitume kwa registered mail ya kuomba kurudishwa chuo na masharti yale yale au zaidi! upo hapo?

hivi kweli na hizi shule za Yebo yebo za Lowassa...in ten years kutakuwa na thousands wanaingia chuo kikuu..do you expect serikali iwakopeshe wote? you are kidding! Tujiulize tunaoandika hapa kwenye forum..ni wangapi tumeshalipa mikopo yetu kuwasaidia wenzetu wa nyuma?

Hili swala ni gumu halihitaji mgomo wala papara...
 
Mkuu Masanje,,

kama utakuwa umefatilia, pia hao wanafunzi wanaigomea hiyo 'sera' ya kukopeshwa 60%

hawajasema kuwa wapewe hela kama grants, ila wanataka wakopeshwe kwa 100% na uwezo huo serikali inao kabisa wala usiitetee

Migomo sio suluhisho, ni kweli lakini ni njia ya kufikia suluhisho, na historia inaonyesha kuwa mambo mengi ya maslahi kwa wanafuzni wa elimu ya juu yamekuwa yakienda kwa migomo migomo tu!
 
Back
Top Bottom