eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 15,660
- 13,801
Nakubaliana na jamaa aliye zungumzia kuhusu Wachina kutaka kujua Kingereza kwa hudi na uvumba - Wachina sio wajinga wanajua fika umuhimu wa kujua kuzungumza Kingereza. Tukubaliane kwamba Kingereza kinaongoza kwenye nyanja za kisayansi, kibiashara nk nenda nchi yoyote Duniani kama umekwama uwezi kukosa raia ambaye hajui kuzungumza kingereza hata kama ni cha kuhunga hunga. Ntakupa mfano: Tafuta website yoyote ya mataifa yanayo tumia character kwenye maandishi yao - nchi kama Uchina, Japan, Korea hata kiaarabu, sasa vuta mouse pointer kwenye dilogue box chagua character yoyote, alafu angalia chini kwenye task bar utaona imeandikwa kingereza! Kwa nini? Hii ina maana hata kama hujui kuzungumza lugha za mashiriki ya mbali hata nyingine za Ulaya unaweza kujaza form kwenye mtandao wao kwa kutumia mouse na kuangalia kingereza kina sema nini kuhusu kuhusu character uliyochagua.
mimi ninachopinga ni kwamba most (if not all) of the knowledge is stored in English...... si kweli..... maana ukiwa francophone watu wa nchi hizo huamini kwamba most if not all of the knowledge is stored in French.... watu wa luthophone wanaamini kuwa ujuzi uko katika Kireno, spanscaphone huamini kuwa ujuzi au elimu iko kwenye Kihispania....
Hivyo elimu/ujuzi hutegemea lugha ambayo kwa mara ya kwanza ilibeba ujuzi..... kwetu sisi kiingereza ndiyo lugha ya kwanza...... na ndiyo tunakiona ni lugha ya kitaalam...... na ndiyo maana hata mtu anapoelezea jambo fulani utakuta anasema kwa lugha ya kitaalam anataja jina la kiingereza (eti kwa kitaalam)......