Michezo utotoni

kula mbakishie baba, kabla haujaingia kwenye game, unaulizwa mapema, "utaweza?"

halafu mnakumbuka mchezo wa bong'oa? ukiinama tu, umepigwa bonge la teke.
ha ha ha ha unanikumbusha mbali mkuu,kuna cku nilikutana na jamaa m1 anajifanya yy ni MTZ,Lkn nilimtilia mashaka kutokana uongeaji wake,bac nikamuambia amalizie nyimbo ifuatayo: KULA MBAKISHIE BABA KULA..........Roho iliniuma sana ndugu zangu maana alishindwa kumalizia
 
Kuna mchezo mmoja tulikuwa tunakaa ktk duara alafu anasimama mmoja akiwa na mpira kisha anaaza kuzunguka duara kwa nyuma akichagua ni nani wa kumwekea mpira kwa siri nyuma yake. Kisha anaendelea kuimba " Nampenda nampenda......tunauliza nani.... Ni mweupe kidogo...nani?....Amevaa gauni...nani..." basi ataja sifa za huyo mtu alomwekea mpira bila kutaja jina lake mpaka atakapojijua na kusima kuchukua huo mpira na kuendeleza zoezi.
Asipojitambua mpaka yule aloweka anafika kwa maranyingine eneo alokaa basi atapigwa ngumi ya mgongoni.

Basi ulikuwa unatufanya tuwe makini sana na rangi za nguo tulovaa, umbile, rangi ya ngozi zetu
 
kuna mchezo mmoja mnacheza kwa kusimama mkitengeneza duara, huku mnaimba ulingoo bayoyo then kuna maneno yakisemwa mnaanza kukata kiuno mpaka chini. Mwingine mkisema neno linalofanana na mwenzako kwa wakati mmoja atayewahi anamfinya mwenzake huku akisema neno pinchi. Michezo ilikuwa mizuri sana kwani mara nyingi ukiwa mzembe au umezubaa zubaa utajikuta unaumia au kupata adhabu mara mara na hivyo kukufanya uwe makini muda wote.
 
Nakumbuka nilipenda mno kuwa baba wakati huo namchagua nani awe mama. Acha tu.. Utoto mtamu jamani, ndo maana ambao hawakupitia michezo ya utoto wanarudia ukubwani ili watimize steji za ukuaji
Mkuu vuta pcha jitu kubwa zima halikucheza kombolela/kidali poo/kula mbakishie baba,lataka cheza sasa hv itakuwaje?mchezo rahisi kwao kuucheza ni kibaba
 
watoto wa siku hizi wanacheza game za computer,virtual image etc teknolojia noma!
 
Kuna mchezo ulikua unaitwa 'Stop' ule ni kiboko. Waweza pigwa stop wakati unapeleka kijiko mdomoni ukakaa na njaa saa nzima! Wapi 'naam kijogoo', 'eleza'? Halafu kulikua na msimu wa magari ya makopo. Mafuta ya kula 'korie' mtu unaombea yaishe upate kopo. Uibe kandambili za kuchongea matairi.. Ah, utoto..
 
yai bovu x2 linanuka x2 linanukaje x2.bwi bwi kabwela.nina ndoo yangu(itikia hivi:Eh)ya kuchota maji ...malizia.utoto raha
 
Iikuwa babu kubwa mmetaja games kibao na kunikumbusha vitu na watu wengi tuliokua nao kipindi hicho cha 80s
Watoto wa sasa si mambo ya digital PS 2, Video games and so on hawawezi kuwa kama sie
 
Kwa boy kuna gololi, kuzungurusha visoda, one touch, tobo bao, tobo busu,kuwinda ndege na kupiganisha mbwa....
 
kujipikilisha tu ndo ilikua fani yangu.
tunachukua chenga za mchele nyumbani na nyanya mbovu na vimkaa,tunazunguka nyuma ya nyumba kujipikilisha.lol
 
yote tisa kumi, ule mchezo unaitwa "cha mkononi" i mean ukiwa unakitu mkononi kitu cha kula kama ice cream au biskuti, kitumbua, andazi, mwenzako akikwambia tu cha mkononi lazima utoe, sio chako tena.
so fun, now im glad nilikulia uswahilini.

Hahaha....dawa ya chamkononi ilikuwa ni Hakiombeki.....ukimuona rafiki yako unawahi hakiombekiiiiii
 
Back
Top Bottom