Michezo utotoni

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,652
13,077
Habari zenu wana JF,

Katika pitapita zangu nikaliona gari limeandikwa Utoto mtamu, basi nikakumbuka tulivyokua tunacheza kombolela. Je, mwenzangu ni michezo gani uliicheza utotoni?
 
Ha ha ha KOMBOLELA, kuna Signature ya mdau mmoja inasema "Butua uwakomboe wenzio" so funny. ila sasahivi sidhani kama hii michezo bado ipo.
kuna mchezo ulikuwa unaitwa malede(kwa wanawake) na nilikuwa napenda sana ule mchezo wa baba na mama au mnachanga hela ikifika ijumaa mnafanya harusi,mnamchagua mmoja wa kike kama bi harusi na wakiume bwana harusi,mnapika pilau mnaimba. hadi raha.
 
makida makida, au kujipikilisha, kuruka kamba,manakumbuka ule mchezo wa kuzungusha tairi la gari, ukifika msimu wa matairi utakuta kila mtoto anatairi la gari,ukitoka shule huyo unatairi lako,mnafanya mashindano ya kukimbia huku mnazungusha tairi mpaka apatikane mshindi.
au mchezo mwengine wa ringi, unakuwa na ringi la baiskeli,unalifunga kamba, halafu kila unapokwenda unaringi lako,hata ukitumwa dukani.

na unakumbuka ikifika jioni kila mtu kwenda kwao kuna kuwa na kidalo poo, ukalale nacho.
watoto wa uswahilini tulifaidi sana.
asante kwa hii thread, umenikumbusha mbali sana, sana kuna mtu alikuwa anaishi mitaa ya Uwanja wa Taifa humu ndani miaka ya 88-1996 nipe shout.
 
mchezo wa dimba, unakimbia kutoka dimba moja mpaka lengine, huku ukiukwepa mpira, au kuna mchezo ulikuwa unaitwa mateka(ni aina pia ya malede,including dimba).
au kuna ule mchezo wa kutaja nchi(sikumbuki vizuri)ila ukishindwa kutaja nchi kuna aina ya adhabu unapata(nakumbuka kila ikifika zamu yangu basi nataka unguja LOL) hiyo unguja ikiwahiwa basi nimeisha.
 
Ha ha ha KOMBOLELA, kuna Signature ya mdau mmoja inasema "Butua uwakomboe wenzio" so funny. ila sasahivi sidhani kama hii michezo bado ipo.
kuna mchezo ulikuwa unaitwa malede(kwa wanawake) na nilikuwa napenda sana ule mchezo wa baba na mama au mnachanga hela ikifika ijumaa mnafanya harusi,mnamchagua mmoja wa kike kama bi harusi na wakiume bwana harusi,mnapika pilau mnaimba. hadi raha.
Mitoto ya siku hizi hata haijui hii michezo!
 
makida makida, au kujipikilisha, kuruka kamba,manakumbuka ule mchezo wa kuzungusha tairi la gari, ukifika msimu wa matairi utakuta kila mtoto anatairi la gari,ukitoka shule huyo unatairi lako,mnafanya mashindano ya kukimbia huku mnazungusha tairi mpaka apatikane mshindi.
au mchezo mwengine wa ringi, unakuwa na ringi la baiskeli,unalifunga kamba, halafu kila unapokwenda unaringi lako,hata ukitumwa dukani.

na unakumbuka ikifika jioni kila mtu kwenda kwao kuna kuwa na kidalo poo, ukalale nacho.
watoto wa uswahilini tulifaidi sana.
asante kwa hii thread, umenikumbusha mbali sana, sana kuna mtu alikuwa anaishi mitaa ya Uwanja wa Taifa humu ndani miaka ya 88-1996 nipe shout.

Mdau hapa ulivyotamka uwanja wa taifa nakumbuka mwaka 1992,Nilitoka Ubungo msewe na mdundiko mpaka uwanja wa taifa ilikuwa balaa hiyo cku sintoisahau kamwe
 
umenikumbusha mbali na mdundiko." nimeina nimeinuka nimeokota kidudee.. noli noli kidudeee"
 
KULA M'BAKISHIE BABA.........ole wako kijiti kiangukie upande wako hayo magumi utakayopata.
na KIDALI CHA KWENYE MITI;;;;;;;;;watu mnaruka km nyani sasa kimbembe ni pale unaporukia tawi lililokauka:clap2::clap2::clap2:
 
du nimecheza michezo mingi mpaka imenitoka,mandei,mdundiko,kibaba na mama,kombolela hahahaha watoto wa kota poleni sana:coffee:
 
harusi,ole wako upigwe doba. Usipowahi kugusa mti au ukuta kuzimia ndio kunakuokoa toka kipigoni.
 
KULA M'BAKISHIE BABA.........ole wako kijiti kiangukie upande wako hayo magumi utakayopata.
na KIDALI CHA KWENYE MITI;;;;;;;;;watu mnaruka km nyani sasa kimbembe ni pale unaporukia tawi lililokauka:clap2::clap2::clap2:

kula mbakishie baba, kabla haujaingia kwenye game, unaulizwa mapema, "utaweza?"

halafu mnakumbuka mchezo wa bong'oa? ukiinama tu, umepigwa bonge la teke.
 
yote tisa kumi, ule mchezo unaitwa "cha mkononi" i mean ukiwa unakitu mkononi kitu cha kula kama ice cream au biskuti, kitumbua, andazi, mwenzako akikwambia tu cha mkononi lazima utoe, sio chako tena.
so fun, now im glad nilikulia uswahilini.
 
Back
Top Bottom