MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Huyu ni mke wa Rais Mstaafu Barrack Obama!
Huyu ni mwanamke mweusi aliyewahi kushika nafasi kubwa zaidi kisiasa hapa duniani, THE FIRST LADY OF USA. Lakini, pia ni msomi ambaye alibahatika kusoma vyuo vikubwa duniani kama Harvard University na Princeton.
Ukimsikiliza kwenye mahojiano yake haya kuhusu maisha yake ya familia hasa ndoa na malezi, utafahamu fika kwamba huyu mama ana kitu cha ziada ambacho kizazi cha leo hatuna. Kwenye ndoa kasema kuna wakati utakuwa unafanya zaidi kuliko mwenzako, na kama hutakuwa makini unaweza kukata tamaa na kuacha ndoa. Lile la 50/50 huwa haliji ghafla tu kama ambavyo wengi tunajarajia.
Amesema kazi kwa mwanamke ni muhimu sana, lakini pia ni lazima mtu ajifunze kuweka uwiano baina ya maisha na kazi yake binafsi. Haya utayapata vizuri kuanzia dakika ya tano (5) uzuri ni kwamba, mahojiano hayo yamewekea vipande hivyo unaweza kuangalia ambacho amekisema.
Baada ya kumsikiliza, nisema tu kwamba mimi siyo shabiki wa Michelle lakini, ukweli ni kwamba Raisi Obama alihitaji mwanamke mwenye hulka na akili kama Michelle ili aweze kufika pale alipofika. Huyu mama ana kitu cha ziada, ndiyo maana hata MUNGU akamfanya kuwa FLOTUS.
She's ethical, humble, emotional stable and matured: Simply Phenomenal.....