Miaka 27 huna mtoto? Jichunguze

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,449
Kama wewe ni mwanaume au mwanamke na umetimiza miaka 27 lakini huna hata mtoto wa kusingiziwa na hata kutoa mimba hujawahi basi unapaswa kujichunguza huenda una matatizo ya kizazi.

Haiwezekani mtu anaefanya ngono hadi kufikisha umri huo hana mtoto, hilo ni tatizo maana maisha ya sasa ni mafupi sana! Sasa kama hutaacha legacy basi ni hatari sana kwako au subiri tu kuitwa babu au bibi na watoto wako.

Wenzako wanaacha kuzaa wewe ndio unaanza

1625724699316.png

 
Nilipata mtoto wa kwanza nikiwa na 24yrs old. Thank you God, now this year anamaliza std 7 then nampeleka kwa kipingu akapige soka maana ni mwanasoka na tangu last year alikua timu ya Shule na mwaka huu pia yupo timu ya Shule.
 
Mkuu lazima ufahamu kwamba kila mtu has gotten his own perspective juu ya maisha, na through hiyo perspective ndipo anapoendesha maisha yake.

Hiyo moja, lakini pili unachoamini wewe kuwa ndio purpose of human life na source of happiness to human life sio lazima na wengine waamini hivyo.

Tatu, kuna issue ya being endowed naturally, kwa maana ya kwamba kuna baadhi ya watu hukosa vizazi, je nao wayachukie maisha kwa sababu wanashindwa kuzaa kipindi watakacho wao?

KUNA WATU WANGAPI WAMEZAA MAPEMA, LAKINI BADO WAKO NA MISERABLE LIFE, LAKINI HAPO HAPO WAPO WATU NI AGED NA HAWANA HAO WATOTO/WANAO KATIKA UMRI MKUBWA STILL WAKO HAPPY WITH THEIR LIFE?

Maisha ni jinsi unavyoyataza tu, has gotten nothing with its events.
 
Kama wewe ni mwanaume au mwanamke na umetimiza miaka 27 lakini huna hata mtoto wa kusingiziwa,na hata kutoa mimba hujawahi basi unapaswa kujichunguza huenda una matatizo ya kizazi.haiwezekani mtu anaefanya ngono hadi kufikisha umri huo hana mtoto.hilo ni tatizo maana maisha ya sasa ni mafupi sana.sasa kama hutaacha legacy basi ni hatari sana kwako.au subiri tu kuitwa babu au bibi na watoto zako..wenzako wanaacha kuzaa wewe ndio unaanza

Kama unachosema ni sahihi basi wengi tupo pabaya kwa kweli.

Nchi za wenzetu walioendelea hua wanasema "Bila tafiti hakuna ruhusa ya kuzungumza"

Sina shaka kama hujafanya tafiti ya ulichozungumza. Shaka yangu ni moja tuu, Je, umefanya tafiti ya hicho ulichosema ????
Na je wale waliopata watoto wao wakiwa na zaidi ya miaka 27 inakuaje ??
Mh.Reginald Mengi amepata watoto mapacha akiwa na 50 yrs plus,
Ndugu zetu wa mitaani waliochelewa kupata watoto baada ya ndoa nao vipi ??
Waliooana mapema ktk ujana wao angali na miaka 24-25 tu lakini hawakupata watoto ndani ya ndoa kwa zaidi ya miaka mitatu mpaka mitano Je ??
Wasomi wengi huchelewa kuoa, wengi wao huoa na umri wa miaka 30, lakini hakuna tafiti inayooanisha mojakwamoja kati ya wasomi na ukosefu wa watoto. Je ??

Tunahitaji tafiti madhubuti kabla ya kuamini falsafa yako hii, vinginevyo tunaomba mtizamo wa kitaalamu wa wataalam wa Afya ktk hili.
 
Ndio maana mnazaa watoto wanaishia kuzagaa mitaani na mkiwapeleka shule basi zile za kidumu mkononi,1st born wangu nilikua na 30 years nilikua na uhakika wa kumlea katika njia sahihi ingawa wadogo zangu walinitangulia ila niliweka malengo mtoto aje anikute nimefanya ABC's sio nisake mtoto kisa umri.

Pata mtoto ukiwa na miaka 18 na mimi 30 ila muhimu wapate malezi bora sioni sababu ya kukimbizana kama wataishia mtaani tu,kwa wale ambao wanahisi wamechelewa fanyeni vitu kwa mipango siku hizi hakuna zile za mtoto kulelewa na babu na bibi au ba'mdogo lazima tujipange hakuna haja ya kuwasikiliza haw wanaowaaminisha eti lazima mtoto aje ukiwa umri fulani.
 
We nawe una watoto ambao huduma zitakuwa za kimagumashi, bora uvae condom
Mana ulikuwa na 3 kila mmoja na mamake ambapo sina uhakika km unawahudumia ipasavyo Kisha ukasisitiza huvai Tena condom....... maana unazidi kuongeza idadi tu wewe!!!!!
 
Kama wewe ni mwanaume au mwanamke na umetimiza miaka 27 lakini huna hata mtoto wa kusingiziwa na hata kutoa mimba hujawahi basi unapaswa kujichunguza huenda una matatizo ya kizazi.

Haiwezekani mtu anaefanya ngono hadi kufikisha umri huo hana mtoto, hilo ni tatizo maana maisha ya sasa ni mafupi sana! Sasa kama hutaacha legacy basi ni hatari sana kwako au subiri tu kuitwa babu au bibi na watoto wako..

Wenzako wanaacha kuzaa wewe ndio unaanza
Tatizo la watu wa uswahilini na mawazo yao.
 
Back
Top Bottom