Napenda nifafanue zaidi. Kwanza napenda mjadala huu. JF inapaswa kuwa hivi. Kujadiliana masuala ya kisera. Pili, kwanza sote tunakubaliana kwamba gharama za maisha zimepanda sana. Mwananchi wa kawaida ndiye anayeathirika zaidi na kupanda huku kwa gharama za maisha kuliko mwananchi mwenye kipato kikubwa. Hii inatokana na sababu kwamba bei zinapanda haraka zaidi kuliko kipato cha mwananchi wa kijijini ambacho ni cha msimu.
Kumekuwa na pengo kubwa sana kati ya matajiri na masikini. Sababu kubwa ni kwamba sekta za uchumi zinazokua zinafanya matajiri wawe matajiri zaidi. Sekta ya Kilimo inayoajiri watanzania takribani asilimia 65 haikui inavyotakiwa na hivyo masikini wanakua masikini zaidi.
Kwa kuwa watu masikini wanauza bidhaa zao kwa bei za vijijini, lakini wananua mahitaji yao kama sukari, mafuta nk kwa bei za mijini, basi mfumuko wa bei husukuma watu masikini kwenye lindi la umasikini. Policy intervention inapaswa kuokoa hawa masikini wasiwe masikini zaidi. Tunafanyaje -
Mosi, katika 'basket of goods and services' ambayo mtanzania hutumia kwa siku, chakula ni asilimia 47, umeme na mafuta 11 na usafiri 3. Kwa hiyo NBS wanapokokotoa inflation, asilimia 61 ni masuala hayo. Food inflation inapaswa, narudia, inapaswa kudhibitiwa kwa kuongeza uzalishaji wa chakula na kuhakikisha kinaingia sokoni. Hili ni suala la msimu maana kilimo chetu ni cha mvua. Hivyo inabidi kudhibiti bei ya mafuta.
Sisi hatuna visima vya mafuta ( kuna 1bn barrels of oil in mtwara yet to be officially declared). Bei ya mafuta hatuna mamlaka nayo. Sisi tuna mamlaka na kodi tunazotoza kwenye mafuta. CHADEMA inapendekeza tupunguze kodi hizi kwa asilimia 50.
Sasa tunazibaje pengo hilo la kodi? Ndio tunapendekeza mambo 3- kupunguza misamaha ya kodi kutoka 2.5% ya GDP sawa na 630bn tshs kwa mwaka mpaka 1% ya GDP sawa na kuokoa takribani 400bn tshs. Pili, tunataka kumilikisha umma uchumi. Tunauza hisa za serikali katika Airtel kwa njia ya IPO. Serikali ina hisa 40%, tutauza 25% na kupata takribani 324bn ths. Tutauzakwa IPO hisa za NBC 15% na kupata takribani 200bn.
Hizi ni njia za muda mfupi. Njia za muda mrefu ni kuongeza uzalishaji wa chakula na kuboresha miundombinu chakula kifike sokoni.
Tunapaswa kukuza uchumi na kuweka usawa ie growth with equity.
Ngoja niwahi kikao cha tathmini
Bei ya mafuta hatuwezi kuincontrol mpaka tuchimbe mafuta wenyewe na tuwe na uwezo wa kuyatumia wenyewe. Njia peke tunaweza kupunguza gharama za mafuta ni kupunguza kodi, kuweka subsidies katika wauzaji wa mafuta.
Venginevyo tuzalishe mafuta wenyewe (Mtwara au Makunduchi Zanzibar).
Mkuu Zitto unasomeka vizuri sana wasiokuelewa basi ila watanzania sasa hivi ni waelewa vizuri