CAMARADERIE
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,419
- 1,920
Kama serikali inamiliki Tanesco kwa asilimia 100 na kuisajili kama kampuni binafsi tunaweza kweli kusema ni kampuni binafsi au ya umma? I'll argue kwamba Tanesco ni shirika la umma kwani linamilikiwa kwa asilimia 100 na wananchi wa Tanzania lakini siwezi kusema ni kampuni binafsi. Lakini pia kwa vile haina hisa ambazo zinaweza kununuliwa na "watu" binafsi zinaweza kufanya Tanesco iwe binafsi kwani maamuzi yote yanayuusiana na uendeshaji wake yanafanywa na serikali na uongozi wake huingizwa na serikali. Nadhani tuna uwezo wa kutosha tu wa kufikiria ni jinsi gani tuibadili Tanesco ili iwe tunavyoitaka na mimi naamini njia mojawapo ni kuwaweka wanasiasa pembeni na shirika liwe la kibiashara zaidi.
Mzee Wetu,
Kwanza Nonda hajambo?
Nadhani Mh.Zitto alikuwa anamaanisha kuwa kuna mashirika na taasisi za umma amabazo zimeanzishwa kwa sheria zao maalumu na kuna yale yaliyoanzishwa chini ya Cap.212 (Companies Act 2004). Ni haya ya mwisho (TANESCO) ambayo ni rahisi kuya float kuliko yale ya sheria maalum (TPA) ambayo inabidi Bunge litengue sheria zilizoyaanzisha na kuyarudisha katika Comanies Act. PSRC ilikiuka sana hili na mashirika mengi yaliuzwa kwa kuvunja sheria na iko siku itabidi lianzishwe hili jambo.