Mheshimiwa Zitto, kwa hili umekosea

Hajamsoma vizuri wakati amemnukuu,halafu mheshimiwa akayeyusha?
Wakuu nakubaliana na hoja ya zitto na cdm kwa ujumla juu ya sera yao ya uchumi na hata mm ningependa sana mjadala uwe na mtizamo huo.lakini napenda kumuunga mkono Mwanakijiji hasa nini cdm kama chama cha siasa na hasa mantiki nzima ya siasa kutokuwa ma consultant wa ccm.wanapaswa kunadi sera zao mbadala ambazo watuhakikishie ccm hawawezi kuzitekeleza.kazi yao ni kufanya ccm ikataliwe na wananchi ili lengo la kwanza la chama cha siasa kutawala litimie.siasa ina definition yake na itabaki hivyo na faida yake ni kila chama kuwa makini kibaki madarakani kwa kufanya yale wanayotaka wananchi.otherwise juhudi binafsi za kufanya DSE kuwa more liquid ni nzuri kiuchumi hasa tukiwahamasisha hata watu wa kawaida kuwekeza kwani naamini ordinary citizen wengi wakiwa na share pale maana rahisi ni kurudisha uchumi kwa public.
 
Tatizo ni kwamba kwa vyovyote vile na hali halisi, huwezi ku-reform uchumi ukiwa ma reformist ni wanasiasa na uongozi uliopo. Wafanyakazi kutokwenda kazini yani kugoma ni ili kufanikisha kung'oa uongozi uliopo.

Sitaki kuomba, lakini ninavyoona wafanyakazi watagoma kwenda kazini siku za usoni wakiwa tayari wapo ktk frustration kali.

I tend to agree with you MkamaP. Inawezekana umefika mahali ukaona ugumu kama ninaouona mimi, kuwa unajiuliza hivi hata mtu akikupa nchi ikiwa katika hali hii utaanzia wapi? Uishie wapi? Nani atakuwa wapi kufanya nini? Kusema kweli tumefika mahali pagumu sana.
Wakati mwingine nahisi kuwa labda tulizowea mno kujaziliziwa bajeti na wahisani, sasa wamegoma kujazia kwa sababu ya uchaguzi mbaya uliopita. CCM walionywa na jamii ya kimataifa hawakuelewa sasa ndiyo inawaingia akilini. Yeyote anayelipenda Taifa letu kwa dhati atafurahia jambo hili la wahisani kupunguza misaada maana imetulemaza sana. Na imefanya chama tawala kuwa na kiburi na ubabe usiojenga taifa bali kulibomoa kwa kasi sana.
Mtoa hoja amegusia nchi zilizopata kuwa katika hali sawa na nchi yetu miaka ya sitini, yaani Korea Kusini, Singapore, Thailand nk. Hapa ndipo penye siri kubwa ya maendeleo ya nchi. "These countries invested in their people" Sisi wakati wao wanafanya hivyo "we were investing in Politics" Na hilo ndilo linaloendelea mpaka leo. Ndiyo maana Utaalam haudhaminiwi kabisa, hata kwenye mashule vijana hawataki kabisa kuteseka na masomo ya sayansi. Tuliofuzu masomo ya sayansi nchini mwetu wengi ni wanyonge sana kimapato. Tatizo hili limeendelea kukua mpaka hata kuzalisha umeme imekuwa siasa tupu. Wataalam weka pembeni piga siasa, na mwenye kuliongoza shirika muhimu kama la kuzalisha umeme anatakiwa awe anatoa mchango wake kwa chama tawala kilichomuweka madarakani. Asipotoa mchango anaondolewa anapewa dawati wizarani anawekewa faili mbili pale juu.
Watanzania tumekaa kimya tukiangalia Mashirika Muhimu kabisa yakihujumiwa yakafa na kuuzwa kijinga jinga tuu, General Tyre, Viwanda vya Nguo, Mang'ula, NECO, MWANANCHI ENGINEERING CO. MECCOnk nk. hata nyumba za serikali zikauzwa halafu tunaangalia maofisa wa serikali wakipangishwa kwenye Hoteli na nyumba za watu binafsi kwa gharama za juu sana. Sasa huo uchumi utakua je??? Foundation ya uchumi tunaozungumzia itakuwa ni nini kama hakuna tunachozalisha kwa ufanisi hata kimoja?? Not even Power itself! We have become total consumers! we don't produce anymore! Imefika mahali ambapo ni pagumu sana maana hata vile viwanda ambavyo mali ghafi zote hupatikana humu humu nchini bila hata haja ya kuzi-process bado tumeshindwa kuzalisha ya kutosha na kufanya packaging yenye ubora na uzito unaokubalika, leo eti tunaagiza Cement toka Pakistan. Watumiaji wanakiri wazi wazi kua hiyo ya nje ni bora zaidi na kilo ni sahihi.
Bila kupata kiongozi mkali na dikteta aliye makini kama wa Rwanda nchi yetu hatutoki tulipofikishwa na CCM, imeimaliza nchi, imeuza nchi kwa mafisadi. Tulipofika siyo mahali pa rahisi, kunahitajika mambo mazito kufanyika. Mambo makubwa na ya kijasiri kweli kweli, siyo haya ya NBC, Airtel hata kidogo! Huko ni kuwapa watoto pipi saa tisa mchana wapunguze njaa!
Nilikuwepo!
 
Suala la liquidity ya DSE nadhani Zitto umeshalizungumza saana hasa kwenye mifuko ya pensheni. Lakini, ili market iwe sustainable formation yake inatakiwa iwe natural. Yaani nchi kazi yake isiwe kuuza hisa zake bali kujenga mazingira ya wananchi kutumia soko lile lakini pia kuwajengea uwezo wananchi wa kuwa na disposable income ili wainvest. Hivi ukiuza shares leo hii hao wakulima wa Sumbawanga watanunua? Au watanunua kina nani? Kwahiyo kama ilivyo ambavyo ukipitia literature za originality ya stock market, tuliache soko lile liwe formed automatically kwa kulegeza masharti na kuandaa miundombinu badala ya kugeuka wauzaji wakuu.
Lakini pia tunapaswa tukumbuke, kizazi hiki kilikuta rasilimali zilizoandaliwa na wengine, kama si tutauza kila kilichopo mikononi mwetu basi huenda wenzetu wasikute kitu na sina hakika kama tusingekuta vya kuuza leo hii tungeuza nini.
Hoja ya inflation haitibiwi kwa kuuza share. Serikali inamechanisms nyingi za kuzuia inflation hata kuadjust interest rates, kutengeneza miundo mbinu imara, kutoa elimu vijijini, kusimamia mapato na matumizi nk.
Mwisho niseme kwamba; sisi hatuna utaalam wa kuuza maana toka tumeanza kuuza hatuoni hayo mapato yakitunufaisha kwahiyo ni vyema tuache uuzaji.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Kabwe Zitto, aliwaambia wananchi katika mikutano yake kuwa chama hicho kimepanda chati kwa asilimia 400, kati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na 2010, kwani kabla ya uchaguzi wa mwaka jana kilikuwa na madiwani 101 sasa wameongezeka kufikia 466, huku wabunge wakiongezeka kutoka 11 mpaka 48.

Huku akiwataka wananchi kuendelea kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, kuhakikisha chama hicho kinashinda na kuchukua dola, Bw. Zitto alisema kuwa mgombea urais wa CHADEMA uchaguzi mkuu mwaka jana, Dkt. Willibrod Slaa alishinda lakini matokeo yake 'yakachakachuliwa'.
Huyu simbishii yeye si rafiki na JK na Jack Zoka ukiona kasema hivyo jua anajua jinsi rafiki zake walivyochakachua.
 
Nashukuru sana. Nipo Sumbawanga. Hujanielewa. Ninashauri kufanya IPO ya Airtel na NBC ili kwanza kupata mapato kwa serikali lakini pili kwa kumilikisha uchumi kwa umma. IPO ni kwa wananchi kupitia soko la hisa.

Hukunielewa vema na ninaomba unielewe. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha DSE inakuwa more liquid. Nataka tuwe na kampuni nyingi sana DSE. Hii itawezesha uwazi.

Aise hta me cjakuelewa pia unaposema hisa ziuzwe kwenye ipo na bidae dse,izo hisa ni zinazomilikiwa na nani?gvt au hao airtel na nbc?mana tucfanye ujinga kma wa nmb selikali kuuza hiza dse kwa wananchi,me naona haya makampuni ikiwezekan gvt iwe ni hisa 50% ili we kwenye decision making bodies
 
Tax cuts for the rich ni republican philosophy/idea/policy/sera....and he is following it!..privatisation is CDMs sera/philosophy/idea....na tunaifuata sasa hivi ingawa mnajitahidi kuyeyusha.Azimio la Zanzibar halikuleta wawekezaji,ni Mtei/IMF Deal ndiyo inatunyonga sasa hivi.And I will never stop saying this.....it's just a FACT
Hizo ni sera za republicans na walimwambia azifuate
Mkuu wangu nikusahiuhishe kidogo.. Privatization sio sera ya Chadema wala CCM, ila ni mfumo wa kiuchumi unaoendana na wakati huu..Sio sera ya Kulia wala kushoto na unapotosha zaidi unaposema Ujamaa haukuleta wawekezaji kwa sababu hakuna kitu Ujamaa kwa mtazamo wa kizamani ule wa vita baridi. Mbona ktk kuyanurusu mabenki na bail, Obama alikataa kwamba serikali yake haitaifishi Mabenki hayo ila ni njia ya kuyanusuru kama yeye ni Mjamaa si angekubali tu. Ujamaa ni kutaifisha na Ubepari ni Kubinafsisha..


Na ni katika kutoelewa huku kuna watu wanaamini Nyerere alikuwa Mjamaa toka alipokuwa Uingereza kwa sababu tu alikuwa akihudhuria semina za Liberal bila kuelewa kwamba Ujamaa huu ni mrengo ndani ya Ubepari wakishinikiza siasa za kihuduma na sio mfumo wa kiuchumi ktk kuzindua Azimio la Arusha na ubinafsishaji. To be a Liberal haina maana wewe ni mkomunist ingawa Republican wanataka tuamini hivyo.

Labda nirudi ktk mifano yangu ya dini. Mara nyingi husema kwamba siasa ni sawa na dini zetu, na kutokuwa mkatoliki ukawa Lutheri haina maana umebadilisha dini na kuwa Muislaam.

Yapo maswala mengi ya Kijamaa yanayokubaliwa na Liberal lakini haina maana wanapinga Ubepari au privatization, na nachozungumza mimi hapa kiimani ni kwamba ipo tofauti kubwa sana ya mtu kusisitiza sala au niseme ibada fulani kwa wananchi wote lakini sii rahisi kwa Muislaam kumwambia Padre asalishei kiislaam ili waumini wake wapate kuongoka kutokana na imani yako za kiroho..Kumbuka tu kwamba hizi imani ndizo zilizomfanya Mkristu asiwe Muislaam kwanza na kama unataka kuitangaza dini yako humwambii Padre ila unawauzia wananchi..

Sasa tunapokuja kwa maswala ya Pilato, huku tunatawaliwa na imani za kimwili na tofauti zake tunazipata ktk siasa na itikadi..Sii kazi ya Zitto kuwaelekeza CCM jinsi ya kutawala, hawa wana ibada zao kazi kubwa ya Upinzani ni kupingana na UTEKELEZAJI wa sera hizo kwa imani kwamba haziwezi kufanya kazi..Ila sera zinazoweza kufanya kazi ni hizi za chama changu hivyo unaomba ridhaa ya wananchi na sii kuwakabidhi CCM sera ambazo zitawajenga na kuendelea kuongoza.

Na labda nikukumbushe tu kwamba kukata tax ya matajiri ni ILANI ya Bush ambayo huwezi kuiweka kama ndio Urepublican, Republican wanaamini lower taxes and fewer regulations zinawawezesha waajiri kukuza biashara zao hivyo kuongeza hesabu ya ajira na moja kwa moja ongezeko ktk pato la serikali..Kwa hiyo, hii ni kama sala ambayo Bush kachagua kwenda na matajiri tu kitu ambacho wapo Republican wanaopinga. Na hata hivyo, it's not a magical elixir kwani uchumi wa Marekani haujabadilika zaidi ya kuharibika zaidi.

Alichofanya Obama ni sawa na baadhi ya Republican kukubali bail out ya mashirika ingawa sii sera yao, hivyo kuna tofauti kubwa baina ya kuiga au kukubali utekelezaji wa sera fulani na kuwauzia wapinzani sera zako.. Hii ndio silaha yako na CDM wataitumia tu pale wanapopata mwanya.. Waache wenyewe CCM waige, waibe au wakubaliane na CDM ktk sera zake..
 
Mkandara,
Nadhani hii si mara ya kwanza tuna bump heads on philosophical point of view.Jammi/umma ni maneno ya kiarabu,ujamaa umetokana na maneno hayo na maana yake ni taifa kuhodhi mali as a big ass family.Nyerere kwenye kitabu cha "The crusade for the liberation" ametafsiri ujamaa kama "Familyhood".
Kwenye interview na Gazeti la "The Courier" Edwin Mtei alisema ujamaa hata siku moja hautaijenga nchi hii,akasema private sector ndio itaijenga nchi hii.
Hivi sasa,GoT inacontrol 12% ya GDP yetu,na USA wana control 34% ya uchumi wao kama ni public sector.Sasa hebu niambie ni nchi gani ya kijamaa zaidi?
With the private sector controlling 88% ya total GDP,watanzania wameona maisha yao yakienda na maji huku uzalishaji wa madini kama ya dhahabu ukiongezeka kwa kasi na kilimo kikipungua kama ndio base ya uchumi wetu na kuwaacha wakulima hoi.
Tukisema sera za IMF zimetusaidia,hapo tutakosea,we have to suffer a lot kama tutataka watoto wetu wanufaike na maliasili yetu.....tusiwachekee wabinafsi hata kidogo!!
CHADEMA'S INPUT:
Kumkemea rais au serikali ipunguze bei ya sukari na vyakula...hii imesababisha serikali kuondoa import tarriffs na kuwanufaisha wafanyabiashara na kuwapunguzia mapato walalahoi.
Kusimamisha uzalishaji wa umeme kwa kampuni ya DOWANS.....hii ilileta upungufu mkubwa wa umeme ambao ulikuwa cheaper than IPTL na ulikuwa more consistent compared to others...matokeo ni faini ya bilioni 94!
Sasa hivi tena,wanataka kuuza shares za parastatals kuziba pengo la mapato,....huu ni uhuni uliokithiri kwani hii itanufaisha wafanyabiashara na si wakulima.
MY POINT?
Mlengo wa kati ambao CDM sasa wanasema ndio falsafa yao,hautuelezi kinagaubaga serikali itapataje fedha za kugharamia elimu,afya na ulinzi.Serikali imetumia kiasi gani?....na je,tukiondoa haya matumizi,tutaimarisha elimu na afya kwa kiasi gani?.....Hivi haya mafuta yanamnufaisha mkulima wa matombo? As compared to Bakhresa?
THATS THE ISSUE AND NOT WHO CAME UP WITH WHAT.
 
Mkandara,
Nadhani hii si mara ya kwanza tuna bump heads on philosophical point of view.Jammi/umma ni maneno ya kiarabu,ujamaa umetokana na maneno hayo na maana yake ni taifa kuhodhi mali as a big ass family.Nyerere kwenye kitabu cha "The crusade for the liberation" ametafsiri ujamaa kama "Familyhood".
Kwenye interview na Gazeti la "The Courier" Edwin Mtei alisema ujamaa hata siku moja hautaijenga nchi hii,akasema private sector ndio itaijenga nchi hii.
Hivi sasa,GoT inacontrol 12% ya GDP yetu,na USA wana control 34% ya uchumi wao kama ni public sector.Sasa hebu niambie ni nchi gani ya kijamaa zaidi?
With the private sector controlling 88% ya total GDP,watanzania wameona maisha yao yakienda na maji huku uzalishaji wa madini kama ya dhahabu ukiongezeka kwa kasi na kilimo kikipungua kama ndio base ya uchumi wetu na kuwaacha wakulima hoi.
Tukisema sera za IMF zimetusaidia,hapo tutakosea,we have to suffer a lot kama tutataka watoto wetu wanufaike na maliasili yetu.....tusiwachekee wabinafsi hata kidogo!!
CHADEMA'S INPUT:
Kumkemea rais au serikali ipunguze bei ya sukari na vyakula...hii imesababisha serikali kuondoa import tarriffs na kuwanufaisha wafanyabiashara na kuwapunguzia mapato walalahoi.
Kusimamisha uzalishaji wa umeme kwa kampuni ya DOWANS.....hii ilileta upungufu mkubwa wa umeme ambao ulikuwa cheaper than IPTL na ulikuwa more consistent compared to others...matokeo ni faini ya bilioni 94!
Sasa hivi tena,wanataka kuuza shares za parastatals kuziba pengo la mapato,....huu ni uhuni uliokithiri kwani hii itanufaisha wafanyabiashara na si wakulima.
MY POINT?
Mlengo wa kati ambao CDM sasa wanasema ndio falsafa yao,hautuelezi kinagaubaga serikali itapataje fedha za kugharamia elimu,afya na ulinzi.Serikali imetumia kiasi gani?....na je,tukiondoa haya matumizi,tutaimarisha elimu na afya kwa kiasi gani?.....Hivi haya mafuta yanamnufaisha mkulima wa matombo? As compared to Bakhresa?
THATS THE ISSUE AND NOT WHO CAME UP WITH WHAT.


Thats it! brother. Nakuunga mkono kwa hoja yako hii. Unajua sisi Watanzania tunashindwa kuona kwamba hii System ya uchumi tuliyokuwa nayo hatupaswi kuifuata Kibubusa tu, bali tunatakiwa tufanye vitu kwa kuzingatia Mazingira yetu.

Ukweli ni kwamba zaidi ya asilimia 50 ya watu wetu ni masikini wa kutupwa, asilimia chache sana ya Watanzania ni middle class, na wachache kupindukia ndo wakwasi, leo unapotaka Serikali iuze share zake ambazo imezishikilia kwa niaba ya Watanzania wote kwa Watanzania "Wajanja wachache", maana yake unaondoa umiliki wa hizo mali kwa Watanzania wengi, na bila shaka hii ni dhulma!.

Ni vyema serikali ikatafuta namna ya kuongeza Umiliki wake, maana kwa kufanya hivyo inaongeza umiliki wa wananchi indirectly kwa niaba yake.

Siyo kila kitu kitakachofanikiwa katika system ya uchumi wa Marekani, kitafanikiwa katika system ya uchumi wa Tanzania, Serikali ya China ina Umiliki wa Benki ya China, Ina Umiliki wa Benki ya viwanda na Biashara ya China, sasa hivi hii benki inajitanua duniani kwa mafanikio.

Mistake ya Kuiuza NBC si vyema ikarudiwa kwa kuuza hata kale kadogo kaliko baki, Serikali itafute vyanzo vingine vya kupata mapato, ili iweze kulipa mishahara na huduma nyingine, maana ukiuza leo, kesho ukakosa pesa za kulipa tena mishahara utauza nini?.

Watanzania inabidi tuachane na uchumi wa Vitabuni, lazima tufuate mbinu zitakzofanya kazi katika mazingira yetu, kama ni mbinu za kibepari mahali fulani, kama ni mbinu za kijamaa katika sehemu fulani, ilimradi ziwanufaishe wananchi wengi!.

Kiufupi mfumo bora kwa Tanzania ni ule utakaowainua Watanzania waliowengi kutoka katika lindi la Umasikini, na si kuwaongezea Wachache Ukwasi at the expense of the poor majority.
 
Nyerere alihoji kwanini NBC tuliivunja wakati haikuwa na hasara? Ni kana kwamba tuliambiwa ni "mwiko" kwa Watanzania kupitia serikali yao kumiliki njia za uchumi hivyo kama watu tuliopagawa tukaanza kuachilia kila kilicho chetu ili tuchukue chao!
 
Nyerere alihoji kwanini NBC tuliivunja wakati haikuwa na hasara? Ni kana kwamba tuliambiwa ni "mwiko" kwa Watanzania kupitia serikali yao kumiliki njia za uchumi hivyo kama watu tuliopagawa tukaanza kuachilia kila kilicho chetu ili tuchukue chao!


Absolutely!. JKN alikuwa sahihi katika hilo, NBC ilijengwa na Watanzania kwa muda wa miaka zaidi ya 30, Watanzania katika muda huo waliinvest pesa nyingi kuliko bei ambayo serikali iliiuza.

besides Benki hiyo ilikuwa inajiendesha kwa faida. sasa unajiuliza, je baada ya hiyo benki kuuzwa kwa bei ya kutupa, Watanzania wamenufaika na nini!.

Binafsi ninadhani katika hili suala la kuuza hisa za serikali za NBC, Chadema wako wrong!. Jiulize hata wakiuza hizo hisa, ni watanzania wangapi watakuwa na share za kutosha za kuwa na sauti katika hiyo benki. tusiangalie pesa ambazo serikali itapata kwa kuuza share hizo bali tuangalie hata nguvu ya maamuzi ambayo itapotea kwa kuuza share hizo kwa "vijitajiri" vidogovidogo.
 
WanaJF kwanza nimpongeze Mchambuzi kwa kurudi tena dimbani na kuleta mada nzito, pili nimpongeze Mh. Zitto kwa kukubali kuja jamvini na kujibu hoja kwa hoja na tatu niwapongeze wote waliochangia mada kwani hili linaonyesha ni jinsi gani tunaweka utaifa mbele mambo mengine nyuma.

Nianze kwa kuangalia madhara (implication) ya ongezeko la bei ya mafuta nchini Tanznaia. Ukweli ni kwamba ongezeko la bei ya mafuta ni chocheo kubwa sana la mlipuko wa bei ya kila kitu sio Tanzania tuu bali dunia nzima. Tatizo la mlipuko wa bei ya mafuta nchini Tanzania ni combinations of more than one things. Hivyo sidhani kama tutakuwa sawa kama tukisema kodi ndio chanzo kikuu cha mlipuko wa bei. Biashara ya uagizaji (import) wa mafuta is not regulated by anybody, madhara yake ni kwamba Oil supplier wanapanga bei ambazo wao wanaona ni profitable enough. Hivyo nadhani ni muhimu kwa viongozi wetu wa bunge mkatafuta njia mbadala ya kucontrol hii sector, am strong advocate of capitalism, however if you don't have the know-how then capitalism can be chaos.

Swala la pili ni kuuza sera za Aitel and NBC, hapa kuna mambo mawili ambayo lazima tuangalia kwenza ni cost-benefit ratio. Jee serikali yetu inapokea kiasi gani kama gawiwo (dividend) kutoka kwnye hizi kampuni, jee kama tuta float hizo share kwenye market how much will Tanzania government raise during IPO? sababu after IPO hakuna cash flow tena from this two particular companies. Compare to Cash Flow from dividend will that benefit of IPO outnumber the PV of the cash flow? If yes then by how much? Nadhani kabla hatujasema nini kifanyike lazima haya mambo tuyatizame kwa undani sana. Jee kupunguza tax kwa 50% kutashusha bei mafuta kwa asilimia ngapi? and how long will it last? Is it a permanent solution or political gotcha?

Kuna mambo mengi ambayo inabidi tuanze kuyaweka into place kama tunataka kushinda bei ya mafuta moja wapo kutengeneza government reserve ambayo itakuwa ina float during time kama hizi ili kupunguza makali ya unregulated market, long term solution ni kurudisha mashirika kama Tanzanian and Italian Petroleum Refining Company Limited (TIPER). Tukiweza kurefine oil nchini hili litaweza kwa asilimia kubwa sana kupunguza makali ya bei ya mafuta kwani refine companies nyingi zina nunua oil under future contract hivyo wana power ya kuhedge price.

Kuhusu swala DSE nadhani tunaitaji topic ya peke yake, ukweli ni kwamba liquidity into that market haitasababishwa na number of companies listed into that market. Bali different financial vehicles, more education kwa watanzania kuhusu stock market and smart regulations.

Most of government own enterprises have poor management structure na ndio maana zinakufa, problem is not capital bali ni management structure.
 
Kwanini Tanesco isiuzwe kwa wananchi na wao wakapewa hisa na hiyo ikasaidia kuipatia equity zaidi? Ukifikiria sana unaweza kuona kuwa Tanesco ndiyo inapotential kubwa ya kurudisha return nzuri kama itawekwa mikononi mwa wannachi kwa njia ya hisa huku serikali ikibakia na strategic shares (say 1 share). Tena tunaweza kufanya share za aina tatu za mtu mmoja mmoja, za taasisi na makampuni mengine na hiyo ya serikali. sema makampuni na taasisi nyingine zinapewa share asilimia 49 na Kampuni moja ikikatazwa kuwa na shares zaidi ya asilimia fulani ili kuondoa monopoly na wananchi wapewe nafasi ya kununua asilimia 50 na kuwa ni majority owners wa Tanesco huku vile vile mwananchi mmoja au familia moja ikizuiwa kiutaratibu kuwa na hisa kiasi fulani.

Tuiache NBC ilivyo au tuiboreshe lakini tubinafsishe Tanesco kimkakati bila kuhatarisha usalama na uhuru wetu wanishati.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
cooperatization ilikuwa ni solution nzuri kwa nchi yetu ya Tanzania. Lakini hat hivyo ni bora kwa watu(Wachumi) kama nyinyi kutathmini hali hii ya kufanya cooperatization na vilevile kuangalia uwezekano wa kutengeneza Village Economy planning ( demonstrated example) ambayo itakuwa ni mfano kwa serikali. Naunga mkono ushauri wako kwa Zito na usiwe kwa Zito tu na iwe kwa Vijana, Wazee na Chipukizi wanaojitokeza katika siasa za Tanzania. Kwa wewe mwana CCM, nimefurahia sana ulichokiandika hapa, maana hata mimi ni CCM. Kwa kweli ukisoma Katiba ya CCM, haina mikakati ya kiuchumi kuwaondoa watu wake kwenye umaskini, kutokea Shina , Tawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa vilivyoandikwa humo ni kuhakikisha ushindi wa kishindo kwenye chaguzi za serikali ya mitaa na uchaguzi mkuu. Sijaona mahali panapo hamasisha elimu endelevu ya kuinua pato la mtu hasa huko vijijini, miji midogo na hata miji na jiji. In short people are not educated katika uzalishaji wa mali mbalimbali, nilikuja na mfano mmoja wa kufundisha wanakijiji kimoja jinsi ya kutumia HANDLOOMS katika utengenezaji wa sweater na socks au vitop vya kinamama, kitu hii haihitaji umeme ni mikono tu, na unaweza tengeneza sweater nyingi ukauza nchi za baridi kama Marekani kwa mpango wa AGOA au hata China kwa mpango wa Africa goods into China zero Tarriff. Lakini wakulima wengi huko kijijini wanategemea kilimo cha mvua , mvua ikigoma basi wanashika tama, na serikali inangoja msaada wa wahisani, wahisani wasipotoa msaada basi nayo inashika tama inaangalia watu wakilia..... Shukrani Mchumi uliyeleta mada hii Ya Taifa mbele, siasa baadae napenda kukupongeza sana na mimi nitakjuja Kinondoni next election nikupe kura yangu. We need change in the Katiba for sure. Nidhamu kazini ni muhimu sana na wafanyakazi serikalini wafanyekazi kwa moyo safi. Mwisho TECHNICAL KNOW WHO imetawala sana Tanzania, matokeo yako kuna watendaji wabovu wengi serikalini kwa sababu ya kitu hiki.
 
Kama mwana uchumi huyo hajakuelewa vipi wananchi unaowahubiria watakuelewa? tunakusubiri utoke huko subawanga

Kuwa mwanauchumi siyo issue... jk mwenyewe mchumi lakini kichwa maji... zipo kafafanua its al abt ipo... uchumi urudi kwa raia usicho elewa ni nini?
 
Kwanini Tanesco isiuzwe kwa wananchi na wao wakapewa hisa na hiyo ikasaidia kuipatia equity zaidi? Ukifikiria sana unaweza kuona kuwa Tanesco ndiyo inapotential kubwa ya kurudisha return nzuri kama itawekwa mikononi mwa wannachi kwa njia ya hisa huku serikali ikibakia na strategic shares (say 1 share). Tena tunaweza kufanya share za aina tatu za mtu mmoja mmoja, za taasisi na makampuni mengine na hiyo ya serikali. sema makampuni na taasisi nyingine zinapewa share asilimia 49 na Kampuni moja ikikatazwa kuwa na shares zaidi ya asilimia fulani ili kuondoa monopoly na wananchi wapewe nafasi ya kununua asilimia 50 na kuwa ni majority owners wa Tanesco huku vile vile mwananchi mmoja au familia moja ikizuiwa kiutaratibu kuwa na hisa kiasi fulani.

Tuiache NBC ilivyo au tuiboreshe lakini tubinafsishe Tanesco kimkakati bila kuhatarisha usalama na uhuru wetu wanishati.
Kama tunataka kusambaza umeme vijijini,itabidi TANESCO iwe overhauled na ioperate at a break even point to minimize costs kwa wanavijiji,sidhani kama hii ni recipe nzuri kwa private investors,otherwise tanesco ingeshakuwa na private captal kubwa tu!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kwanini Tanesco isiuzwe kwa wananchi na wao wakapewa hisa na hiyo ikasaidia kuipatia equity zaidi? Ukifikiria sana unaweza kuona kuwa Tanesco ndiyo inapotential kubwa ya kurudisha return nzuri kama itawekwa mikononi mwa wannachi kwa njia ya hisa huku serikali ikibakia na strategic shares (say 1 share). Tena tunaweza kufanya share za aina tatu za mtu mmoja mmoja, za taasisi na makampuni mengine na hiyo ya serikali. sema makampuni na taasisi nyingine zinapewa share asilimia 49 na Kampuni moja ikikatazwa kuwa na shares zaidi ya asilimia fulani ili kuondoa monopoly na wananchi wapewe nafasi ya kununua asilimia 50 na kuwa ni majority owners wa Tanesco huku vile vile mwananchi mmoja au familia moja ikizuiwa kiutaratibu kuwa na hisa kiasi fulani.

Tuiache NBC ilivyo au tuiboreshe lakini tubinafsishe Tanesco kimkakati bila kuhatarisha usalama na uhuru wetu wanishati.

Lengo ni kufloat tanesco in the near future. Tanesco ni kampuni binafsi inayomilikiwa na serikali kwa asilimia 100. Maana yake ni kwamba tanesco imesajiliwa kupitia cap 212 kama kampuni nyingine yeyote, hivyo kuiorodhosha hisa zake katika soko la hisa ni rahisi zaidi.

Tatizo tanesco bado haijaanza kufanya faida. Sheria ya capital markets inataka kampuni iwe inafanya faida kwa angalau miaka mitatu mfululizo kabla ya kulist DSE.
Tumewapa lengo hilo tanesco, hasara imekuwa ikishuka sana lakini bado hawajaweza kupata faida.
Ni kweli kwamba wingi wa makampuni peke yake hauleti liquidity. Lakini ni hatua mojawapo muhimu kwa kila soko la hisa ie market capitalisation. Wingi wa hisa unasaidia kupata products mbalimbali katika soko na financial engineers wanasaidia kupanua soko. Hivyo ni muhimu sana kuongeza kampuni katika soko.
Kuhusiana na cost-benefit, mtanganyika atakuwa anafahamu kuwa ile dividend badala ya kwenda serikalini sasa itakwenda kwa wananchi moja kwa moja. Pia serikali itaendelea kupata kodi ie corporation tax na witholding tax on dividend. Hivyo ni suala la kuangalia na kusema glasi ipo half full au half empty!
Tukumbuke, listed companies zinakuwa na uwazi zaidi kwa mujibu wa sheria. Sababu kubwa ambayo imesababisha serikali ishindwe kukusanya kodi katika mauzo ya zain to airtel (tshs 470) ni kampuni hiyo kutokuwa listed pamoja na udhaifu wa sheria yetu ya kodi. Pamoja na kwamba kila mteja alinunuliwa kwa takribani dola 227 wakiwemo watanzania, TRA collected zero.
ABSA pia wameuzwa kwa Barclays ikiwemo NBC yetu (mtakumbuka nyerere alitaifisha barclays na kuiita NBC in 1967). Mauzo hayo pia hakuna kodi tuliyokusanya. Listing itaweka mambo mengi wazi, market ita react na itasaidia sana nchi.
Tupeleke umiliki wa uchumi kwa umma kwa kuwawezesha kumiliki baadhi ya makampuni. Tuanze na yale ambayo serikali ina hisa
 
Kama serikali inamiliki Tanesco kwa asilimia 100 na kuisajili kama kampuni binafsi tunaweza kweli kusema ni kampuni binafsi au ya umma? I'll argue kwamba Tanesco ni shirika la umma kwani linamilikiwa kwa asilimia 100 na wananchi wa Tanzania lakini siwezi kusema ni kampuni binafsi. Lakini pia kwa vile haina hisa ambazo zinaweza kununuliwa na "watu" binafsi zinaweza kufanya Tanesco iwe binafsi kwani maamuzi yote yanayuusiana na uendeshaji wake yanafanywa na serikali na uongozi wake huingizwa na serikali. Nadhani tuna uwezo wa kutosha tu wa kufikiria ni jinsi gani tuibadili Tanesco ili iwe tunavyoitaka na mimi naamini njia mojawapo ni kuwaweka wanasiasa pembeni na shirika liwe la kibiashara zaidi.
 
Nijirudie:

Siyo Jukumu la Chadema kuikosoa CCM ili ijisahihisha na kutawala vizuri; ni jukumu la Chadema kuidhoofisha CCM ili isitawale vizuri na hatimaye ikataliwe na wananchi na kuondolewa madarakani. Jukumu la Chadema ni kuifanya CCM isikubalike na wao wakubalike zaidi ili hatimaye wapewe nafasi ya kuunda serikali na kutekeleza sera na itikadi yao. Sielewi hawa wanaojifikiria kama "mbwa wa tajiri" wanajiona hivyo kwa msingi gani? Nilikuwepo.

...Una maana, ukiwa mbwa wa tajiri hautakuwa tajiri, kamwe.

...Mkjj, niliisoma hiyo article yako, kwa mtu wa kawaida inamchanganya, haiko straight, ingawa mwisho wa siku aliyeelewa anatambua unataka cdm waachane na mambo ya kubweka, wajiandae kumiliki mbwa.

...Kama msomaji wa article zako nina ushauri mdogo. Itakuwa vyema na nafuu kwa wasomaji wa kawaida kama utapangilia vizuri zaidi mtiririko wa hoja zako, kwa kuanza na vipengele muhimu na kuvijengea hoja na ikiwezekana kuvitolea mifano. Au, staili nyingine yeyote ili mradi msomaji aelewe kiurahisi mtiririko na apate ujumbe kwa wepesi. Nadhani unajua watanzania wengi tu wavivu wa kusomasoma.
 
Sitaki kuomba, lakini ninavyoona wafanyakazi watagoma kwenda kazini siku za usoni wakiwa tayari wapo ktk frustration kali.

...Watagoma wengi si wafanyakazi pekee. Umesikia huko Uganda sasa kina mama nao wameingia na masufuria matupu barabarani?

...Tatizo watu wana downplay magnitude ya hii hali ya uchumi na siasa. Its getting worse, not better.
 
Back
Top Bottom