Mheshimiwa Zitto, kwa hili umekosea

Nashukuru sana. Nipo Sumbawanga. Hujanielewa. Ninashauri kufanya IPO ya Airtel na NBC ili kwanza kupata mapato kwa serikali lakini pili kwa kumilikisha uchumi kwa umma. IPO ni kwa wananchi kupitia soko la hisa.

Hukunielewa vema na ninaomba unielewe. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha DSE inakuwa more liquid. Nataka tuwe na kampuni nyingi sana DSE. Hii itawezesha uwazi.

Kama mwana uchumi huyo hajakuelewa vipi wananchi unaowahubiria watakuelewa? tunakusubiri utoke huko subawanga
 
Mchambuzi, kweli uchambuzi umetulia.

Kama nimepata lilo moyoni ni kumpinga Mh. Zitto asishauri serikali kuuza share zake za Aiertel na NBC ili kuweka ruzuku kwenye petrol na bidhaa zake.

Nimesoma mara mbili analysis yako, zaidi ya ushauri wako wa kukaza mkanda katika ukusanyaji wa kodi kwenye vyanzo vilivyopo (juhudi zilizofeli) sijaona wapi umetoa wazo mbadala la kunusuru hali hii ya bei ya petrol kupanda!

I'm apprehensive to your comments; binafsi naona anachoshauri Mh. Zitto ni kwa manufaa ya taifa na si chama. Kama yangekuwa yamependekezwa na upande wako ungetoa full support.

Na utakuwa unawafanyia heri wana Kinondoni kama utamfuata mwakilishi wenu bungeni ukampe ushauri huu auwakilishe.
 
umejitahidi sana kutoa hoja na uchambuzi mzuri-nimeipenda!! Mkuu karibu CDM.
 
Kwa jinsi nilivyomuelewa Zitto hapo juu, anataka Wananchi wanunue hisa katika mashirika hayo kama njia ya ya umiliki wa moja kwa moja kwa wananchi katika mashirika hayo, lakini wasiwasi wangu ni kwamba utaratibu huu si mzuri, kwa sababu Wananchi wachache wenye hisa ndo watakuwa wamiliki wa mali hizo, na si watanzania wote.

Maana yake ni nini, maana yake ni kwamba wananchi wakulima hohehahe wa kule kamachumu, au bumbuli hawatapata fuko la pesa za zahanati, ambazo zingetokana na pesa za NBC au Airtel!, wakati wananchi wachache wangenufaika sana kwa infrastructures zilizojengwa kwa miaka mingi na Watanzania wengi, waliowengi wangewekwa kando.

So far, badala ya kuishauri serikali iuze hisa zake kwa wananchi wachache, ni bora ikatafuta namna ya kuongeza hisa zake kwa manufaa ya Watanzania wengi!.

Chadema msitake kubinafsisha miundo mbinu ya msingi na kuiacha nchi yote ikawa tegemezi kwa sekta binafsi, lazima ifikie mahali serikali ichore msitari mwekundu kwamba Mali hizi na zile, ni za Umma na si za watu binafsi, vitu kama benki za serikali, Maji, reli, posta, bandari, umeme si vya kuachia sekta binafsi ivimiliki.
 
Hii sasa ndo Jamii Forums kwenye great thinkers. Ahsante sana kwa uchambuzi. Ahsante sana Zitto nawe kwa majibu yako.
Hakika mchambuzi wangu CCM wanakufunika tu ndo maana walikuchakachua kwenye kura za maoni. Yaani wewe kiukweli kabisa bila fitina, nyumbani pako ni CDM. Zitto tafadhali apewe kadi yake.
 
Zitto, kusema ukweli zile tuhuma kuwa umechakachuliwa na jembe na nyundo zilikuwa zikinisononesha sana. Hata pale ambapo hukuonekana katika shughuli za kichama niliumia zaidi maana wewe ni mmoja wa viongozi ninaovutiwa nao sana.

Lakini hivi karibuni, nimefurahi kukuona washiriki vema kundini. Tuijenge nchi yetu, tuipiganie hadi kieleweke.

Hongera na ahsante sana kwa speech zako zenye mashiko.

Kila la kheri.
 
Nashukuru sana. Nipo Sumbawanga. Hujanielewa. Ninashauri kufanya IPO ya Airtel na NBC ili kwanza kupata mapato kwa serikali lakini pili kwa kumilikisha uchumi kwa umma. IPO ni kwa wananchi kupitia soko la hisa.

Hukunielewa vema na ninaomba unielewe. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha DSE inakuwa more liquid. Nataka tuwe na kampuni nyingi sana DSE. Hii itawezesha uwazi.
Mkuu wangu shukran sana kwa uchambuzi wako maana hata mimi nilishangaa kusoma yaliyotangulia, lakini maadam umeliweka wazi nadhani that is the way to go..

Isipokuwa tu hii ni itikadi inasukuma sera za CDM kuonekana zenye mtazamo tofauti na ule wa chama tawala kwa hiyo kuishinikiza serikali iuze hisa zake za NBC na Airtel (go public) kunaweza kuleta hatari kubwa zaidi nikizingatia kwamba CCM imeshikwa na Mafisadi na yawezekana kabisa kufanya tusiyotegemea..Nia njema lakini utekelezaji wake unaweza kuwa tofauti kabisa na hesabu zenu kiuchumi..

Maadam nchi yetu leo hii hatufuati sheria wala hatuna mwongozo, nadhani ni busara sana tujaribu kutazama tahadhari za uwezekazaji kabla ya maamuzi kwani tunapoteza zaidi kila tunapofanya maamuzi ya kiuchumi pasipo kuzingatia Watu na Mazingira tuliyopo..Kwa hali tulokuwa nayo leo hii mimi nadhani swala kubwa liwe CDM kuingia madarakani, kukomesha Ufisadi kisha vitu kama hivi vifuate kwa sababu mtakuwa responsible na accountable zaidi ya kujaribu kuwabatiza mafisadi huku mkiwaonyesha matamanio yao.
 
Mchambuzi umejieleza vizuri sana ila naomba nikubainishie nilivyomuelewa mie Zitto,

Kuhusu suala la mafuta umezungumzia kuwa ni tatizo na kikwazo kikubwa. Nakunukuu hapa umesema hivi:-
Kwa mtazamo wangu, ni sahihi kabisa kulipeleka suala hili bungeni mwezi ujao kama ulivyoelezea kwa kirefu kwani kama serikali yetu haina ubunifu juu ya kutafuta au kuimarisha vyanzo vya mapato, ni kosa kubwa kukimbilia kiholela kwenda toza kodi za ajabu kwenye sekta ambazo ni life blood ya maisha ya mtanzania kiuchumi. Bei ya mafuta na petrol isipodhibitiwa, hali itakuwa mbaya sana ndani ya miezi tisa ijayo. Mafuta na petroli ni injini ya uzalishaji viwandani, usafirishaji wa bidhaa toka mashambani n.k. Kama ulivyoainisha, maeneo haya ya uzalishaji kama yatakuwa yanalemewa kutokana na gharama za mafuta na petroli kuwa juu, itaendelea leta matatizo makubwa ya kiuchumi nchini. Waziri mkullo katika taarifa yake ya hali ya uchumi na mikakati kwa mwaka 2008-2012 aliainisha kwamba mkakati ni kuwa na mfumuko wa bei in single digits yani usiofikia asilimia kumi. Kuna taarifa kwamba atatolea maelezo hoja zenu za Mbeya, lakini natumai atajibu pia in the context of alichotueleza katika taarifa yake ya hali ya uchumi (see above), wewe ukiwa ndani ya bunge lile.

Mfumuko wa bei utaendelea kuwa tatizo kwani mchango mkubwa wa bei kufumuka unatokana na bei ya vyakula kuwa juu sana kutokana na tatizo la bei kali za mafuta na petroli ambazo ni key input kufanikisha chakula kifike sokoni. Na hapa hatujafikia mwezi wa ramadhani, tunaweza jikuta katika hali mbaya sana kwani kwa mazoea, ni kawaida kwa bei ya vyakula kuwa juu sana wakati wa mfungo. Sasa ramadhan ikichanganyikana bei kali za mafuta na petrol na vile vile speculation za wazalishaji utaopelekea creation of shortage, hapatakalika"

Hili suala ni gumu sana kulitatua kwa vile mafuta sisi hatuchimbi tunanunua katika masoko ya kimataifa hivyo oil price inakuwa determine na market forces (demand and supply). Nchi zilizoendelea zimekuwa zikitoa subsidies katika njia fuel duty kupunguza gharama ya mafuta isiwe kubwa au kupunguza tax katika bei ya mafuta. Tanzania tunaweza kupunguza kodi ya mafuta ili bei ipungue ila ni vema kabla hatujaamua kuanzisha hivyo tufikirie kodi inayokosekana katika mafuta inapatikana wapi na vyanzo vyenyewe vya kodi ni haba? Pia tunaweza kupunguza mfumuko unaotokana na mafuta kwa kuhamasisha utumuaji wa nishati nyengine kama gesi. Tanzania ina utajiri wa gesi ila hadi leo faida yake ni ndogo sana. Matumizi ya mafuta yanaweza kupunguzwa kwa utumiaji wa nishati nyengine kama gesi ila hilo linategemea na kiwango cha explorations kilichofanyika kuwezesha kufikia kiwango cha kuruhusu utumiaji wa gesi (natural gas).

Njia nyengine ni kutatua suala la umeme. Hili tatizo ni msiba kwa Tanzania kimaendeleo kwani bila ya umeme uzalishaji utashuka, shughuli za utendaji zitasimama na mwisho wa siku gharama za maisha zinapanda. Ni vema serikali ya CCM ikajitahidi kulitatua tatizo hili haraka iwezekanavyo kuweza kusaidia demand ya mafuta kama ni nishati za uzalishaji kufidiwa na umeme. Mifano hai ni majenerata ambayo wanachama wenzako akina Rostam na wenzie ndio wanafaidika na uagizaji wa mafuta ya bei mbaya kwa kigezo cha uhaba wa umeme. Serikali ya Tanzania inatumia mabilioni kwa siku kuzalisha umeme. Tungelikuwa na upatikanaji wa umeme wa uhakika mahitaji ya mafuta yangelipungua na kusaidia Serikali ya Tanzania kupunguza mzigo wa kugharamia mafuta ya uendeshaji wa magenerator. Hivyo hivyo ingelipunguza gharama za uzalishaji kwa watu binafsi kwani sasa hivi wanatumia magenerator yao binafsi na kusababisha gharama za uzalishaji kukua kwa kiwango kikubwa.

Je Tanzania ina hela za kusubsidies gharama ya mafuta unakuta jibu ni kuwa hapana. Serikali inakusanya kodi kwa kiwango kidogo kuliko matumizi yake. Serikali je itoe wapi pesa kuinject katika mzunguko jibu ni kuuza assets zake kama NBC, Airtell, etc. Hii ni kwasababu pesa itakayopatikana katika mauzaji haya itumike kupunguza gharama za maisha. Hili kiuchumi lina manufaa zaidi kuliko hasara kwasababu zifuatazo:-

a. Wakiuza assets watakuwa na excess liquidity (pesa ya ziada kufanyia shughuli za maendeleo). Hili litawasaidia kuweza kupunguza gharama za mtanzania. Venginevyo wakakope benki mzigo utakaokuwa mkubwa kwani itabidi walipe deni na interest juu kitu kitakachowafanya walipe mara nne ya amount ya mwanzo.

b. Wakiuza asset katika DSE watasaidia kukuza soko la hisa kuongeza vile uwajibikaji na ufanisi. Hii ni kwasababu mashirika yakiwa public inabidi kila mwaka wawe wanatoa ripoti kwa jamii hvyo wale akina Caspian (RA), EL watakuwa hawawezi tena kuendelea kufaidi keki. Kwani kila kitu kitakuwa katika public arena (Hili ndio kosa alilolifanya Mkapa kwani aliyauza mashirika pasina kuangalia ufuatiliaji utakuwaje na ndio mifano ya NBC inarudi kutuumiza). Wakiyaruhusu mashirika haya kuuzwa katika DSE yatakuwa Public na hivyo jamii itajua nani anamiliki na utendaji wao ukoje na hivyo kusaidia kuwekea uwazi zaidi.

c. Kuepuka mzunguko mkubwa wa pesa. Kama unavyojua thamani ya shillingi imeshuka sana sasa hivi. Kuna theory moja katika uchumi inasema hivi ukiongeza mzunguko wa pesa katika uchumi unachangia ziadi kushuka kwa thamani ya shillingi na kuongeza inflation (Fisher Quantity Theory of Money). yaani MV=PT. Hivyo basi kama serikali inaongeza mzunguko wa pesa jua kwamba shillingi ya Tanzania itazidi kuporomoka na inflation itaskyrocketing na ndio mwanzo kuelekea kuwa kama Zimbabwe. This is not a wise option kwa nchi kama ya Tanzania.

d. Kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali kuanzia bungeni mpaka serikalini. Wafute ubunge wa viti maalumu, safari kwa wingi na kupunguza matumizi mengine ya serikali kutasaidia kuongeza liquidity serikalini. Swali je wanaweza (Kimtazamo wangu hili ndio bora zaidi kuliko kuuza mashirika ya umma ila sijui kama linaweza kutekeleza nchini kwetu).

Mheshimiwa Zitto kwa hilo la kuuza mashirika ya umma nakuunga mkono ila yauzwe DSE kama ulivyosema. Na sababu zangu ni hizo hapo juu.

Nilikuwapo!!!
 
Maadam nchi yetu leo hii hatufuati sheria wala hatuna mwongozo, nadhani ni busara sana tujaribu kutazama tahadhari za uwezekazaji kabla ya maamuzi kwani tunapoteza zaidi kila tunapofanya maamuzi ya kiuchumi pasipo kuzingatia Watu na Mazingira tuliyopo..Kwa hali tulokuwa nayo leo hii mimi nadhani swala kubwa liwe CDM kuingia madarakani, kukomesha Ufisadi kisha vitu kama hivi vifuate kwa sababu mtakuwa responsible na accountable zaidi ya kujaribu kuwabatiza mafisadi huku mkiwaonyesha matamanio yao.

Bado hujamuelewa Zitto... nadhani hisa zinazouzwa DSE ni kwa agili ya public... yaani wewe na mimi tununue hisa... sasa hapo kuna tatizo gani? Zitto hasemi Kampuni ziuze hisa nje ya DSE... nje ya DSE ndio unamilikisha kwa mtu mmoja au kampuni moja na viwango vya hisa vinakuwa vikubwa... mfano 20%, 49%, 51%... Amka mzee wangu... enzi za ujamaa zimeshaondoka.
 
Nashukuru sana. Nipo Sumbawanga. Hujanielewa. Ninashauri kufanya IPO ya Airtel na NBC ili kwanza kupata mapato kwa serikali lakini pili kwa kumilikisha uchumi kwa umma. IPO ni kwa wananchi kupitia soko la hisa.

Hukunielewa vema na ninaomba unielewe. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha DSE inakuwa more liquid. Nataka tuwe na kampuni nyingi sana DSE. Hii itawezesha uwazi.
Kama hakukueewa, nashauri chukuna muda jibu kwa urefu kidiogo ili ulete uelewa si kwa huyu tu, bali na kwa sisi wengine ambao nao hatukukuelewa.

Kwangu mimi, kulazimisha serikali iuze hisa zake inaweza kuwa njia nzuri ya kuifamarisha liquidity ya stock markeyy lakini inaweza isiwe muafaka kwa kushughuklikia tatizo la kiuchumi loinalotukabili.

Nadhani unaelewa Zitto kwua tatizo lililopo ni zaidi ya kuifanya DSE iwe active sana. hata serikali ikiuza hisa zake hizo, bado hatuna uhakika na iwapo fedha hizo zitatumika ipasavyp. Tunaweza kukosa mwana na maji ya moto-hisa zikauzwa na fedha zikaliwa vilevile.

Kama hoja ni kuifanya DSE iwe active, tunaweza kuyahimiza na kuyawezesha makampuni katika sekta binafsi kuingia huko DSE na kuuza hisa zao. Hivi mpango wa barrick kuuza hisa umeishia wapi? Hao Zain nao si wana hisa zao ukiondoa zile za serikali, kwa nini nao wasiende, Vodacom na vipi? IPP, Mwananchi, bakhresa, METL na mengine kama hayo? nadhani hawa wakiingia huko DSE itachangamko kuliko kwa serikali peke yake kuuza hisa sake.

Najiuliza iwapo serikali ikimaliza kuusa hisa zake kwenye IPO, nini kitatokea (maana uzoefu unaonyesha kwua wanaonunua hisa wengi wanazinunua kwa lengo la kuzishikilia). Soko bado litaendelea kudumaa hata kama serikali itafanya IPO ya hisa zake.

La kufanya hapa, pamoja na kuyahimiza makamapuni kuuza, watanzania nao wachangamkie bishara hiyo. Uchangamfu wao unaonekana kwenye IPO tu kiasi kwamba nyingi zinakuwa oversubscribed, baada ya hapo, kila mtu anabaki na hisa zake kusubiri dividends.

Tafadhali rudi tena Zitto utupe ufafanuzi
 
Ni kweli, Zitto Una mvuto wa kipekee katika siasa. Tulia kwa kuwa una nafasi kubwa ya kufanikiwa. Na usidanganyike, nje ya CHADEMA hakuna pengine pa kung'arisha nyota yako. Kwa sasa jenga chama kwa ushirikiano na wenzako.
 
Nashukuru sana. Nipo Sumbawanga. Hujanielewa. Ninashauri kufanya IPO ya Airtel na NBC ili kwanza kupata mapato kwa serikali lakini pili kwa kumilikisha uchumi kwa umma. IPO ni kwa wananchi kupitia soko la hisa.

Hukunielewa vema na ninaomba unielewe. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha DSE inakuwa more liquid. Nataka tuwe na kampuni nyingi sana DSE. Hii itawezesha uwazi.

Many more thanks for this......
 
...Napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kurejea bungeni kwa kishindo lakini pia kwa kupata vijana wenzako wengine wapiganaji kama kaka yangu Tundu Lissu, na wadogo zangu Mnyika, Mdee, Shilinde na wengineo. Tunawategemea sana kama vijana, napenda kusititiza tena - Tanzania Kwanza, Siasa Baadae - na tunaomba msituangushe na Mungu awaongoze katika hilo.

... Katibu Mkuu wako Dr. Wilbrod Slaa aliulizwa swali na Makwaia Kuhenga katika kipindi cha Je Tutafika kwamba kwenye luninga Channel Ten– Je, Chadema ina sera gani mbadala za uchumi, mbona hazipo wazi sana? Dr. Slaa akajibu kwa ufasaha swali hilo kwa kuziweka bayana...

Nilivutiwa sana na sera za Chadema alizozitoa Dr. Slaa, nikabaki kuduwaa ...


Tanzania Kwanza, Siasa Baadae.

Sina hakika kama unacho sisitiza "Tanzania Kwanza, Siasa Baadaye" ndicho unachokiamini! Inakuwaje vijana wenzako uliowataja wanapigania Tanzania wewe ukajiweka kando na kusema "..unawategemea..." badala ya kuungana nao kwenye Chama Chao kuunganisha nguvu!

Kwenye vyama tunafuata "sera", kama ulivutiwa sana na sera za CHADEMA, bado unampango gani na kuachana na sera za magamba?

Wewe hauko serious na Tanzania Kwanza unapiga siasa za kukumbatia ufisadi kwa sababu uko pamoja nao. Waache wanao maanisha waendeleze mapambano yao mpaka kieleweke!
 
Zitto,

Ukigombea urais na ukikuta umepata kura moja basi ujue hiyo kura ni yangu mimi! You are today the only leader among the leaders in CDM i can listen and think about what you have spoken... don't forget Kitila MKUMBO is my PM!

Mara nyingi watu wengi hawakuelewi lakini I know why!!! you can PM me and will tell you why?

Average people want you to speak their language achana nao... hivyo ni vitu vya muda mfupi... angalia mbali kama unavyofanya... fanya misimamo ambayo even 10years to come unaweza kuitetea... achana na politics za siku mbili za washikaji kama wale wa A-town... wewe sio mmoja wao ndugu yangu.

You are a natural leader... and we thank God for that!!!

God bless you
 
Nashukuru sana. Nipo Sumbawanga. Hujanielewa. Ninashauri kufanya IPO ya Airtel na NBC ili kwanza kupata mapato kwa serikali lakini pili kwa kumilikisha uchumi kwa umma. IPO ni kwa wananchi kupitia soko la hisa.

Hukunielewa vema na ninaomba unielewe. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha DSE inakuwa more liquid. Nataka tuwe na kampuni nyingi sana DSE. Hii itawezesha uwazi.
UMMA?Brother hapa ni lazima uende deep,IPOs za mashirika haya,hazitambenefit mtanzania wa kawaida bali ma*********.....but explain how you gonna go about it?......uh,emperically!
 
Naomba nichangie kuhusu hii IPO kwa msaada wa internet ili sote tunufaike:

An initial public offering (IPO), referred to simply as an "offering" or "flotation", is when a company (called the issuer) issues common stock or shares to the public for the first time. They are often issued by smaller, younger companies seeking capital to expand, but can also be done by large privately owned companies looking to become publicly traded.In an IPO the issuer obtains the assistance of an underwriting firm, which helps determine what type of security to issue (common or preferred), best offering price and time to bring it to market.

When a company lists its securities on a public exchange, the money paid by investors for the newly-issued shares goes directly to the company (in contrast to a later trade of shares on the exchange, where the money passes between investors). An IPO, therefore, allows a company to tap a wide pool of investors to provide it with capital for future growth, repayment of debt or working capital. A company selling common shares is never required to repay the capital to investors.Once a company is listed, it is able to issue additional common shares via a secondary offering, thereby again providing itself with capital for expansion without incurring any debt. This ability to quickly raise large amounts of capital from the market is a key reason many companies seek to go public.There are several benefits to being a public company, namely:
  • Bolstering and diversifying equity base
  • Enabling cheaper access to capital
  • Exposure, prestige and public image
  • Attracting and retaining better management and employees through liquid equity participation
  • Facilitating acquisitions
  • Creating multiple financing opportunities: equity, convertible debt, cheaper bank loans, etc.
  • Increased liquidity for equity holder
 
Uchumi umedoda na ndo kiama kwa Taifa, ninavyofahamu mie jinsi tulivyo naomba Mungu tu mvua zinyeshe wakulima mama/bibi zetu wajipatie mazao ya kutosha njaa isiwamalize.

Na bahati mbaya balaa hili linaukumba Tanzania wakati nchi nyingi wanaotupa msaada nao wapo ktk hali ngumu. Soln, ni kuipindua utawala, tupilia mbali uongozi wote na wabunge waliopo. Ije serikali mpya kabisa na wala sio kutoka vyama vilivyopo. 2015 mbali sana.

Wafanyakazi wagome kwenda makazini, wasiandamane bali wagome tu kwenda makazini. Hii ndo soln ya kureform uchumi.
 
UMMA?Brother hapa ni lazima uende deep,IPOs za mashirika haya,hazitambenefit mtanzania wa kawaida bali ma*********.....but explain how you gonna go about it?......uh,emperically!


Pole b'se you do not know that public listed companies are the one which are most regulated, thus they are the most secure to invest waiting for airtel to go public as i must be among the investor...!!!
 
Somtime mnakosea kuleta mada nzuri mnaziweka kisiasa mwisho wa siku watu watajadili kisiasa na siasa za vyama badala ya kujadili mada na hoja kuu ambayo kwa uzi huu ni ya UCHUMI na HISA

Because watanzania wengi tunapenda siasa hii thread ingekuwa kwenye uchumi wala isingepata response hii. So tusiojua mambo ya uchumi tunategema tutaona wachumi na wenye knowlwdge wakishuka mambo hapa . So na sisi watanzania tubadilike
 
Hadithi ndeeefu ina mantiki nimeipenda. Naunga mkono hoja hivyo ilivyo ikiwa siyo umeileta hapa kutetea maslahi yako iwapo hoja ya Zitto itapitishwa na bunge.
 
Back
Top Bottom