Mheshimiwa sana, mfikirie Ndugu Mtatiro ukuu wa Wilaya Tunduru ikikupendeza!

Binafsi nawapongeza wale wote waliokuwa upinzani na kuteuliwa baada ya kujiunga CCM, na Sisi wafuasi wao ni Bora tufurahi Kwa wenzetu kupewa nafasi za kutumikia wananchi.
Hii ni nafasi ya wao kuonyesha kile walichokuwa wanapigania wakiwa nje kama wapinzani Kwa kuonyesha Kwa vitendo, kuna wengine wamepewa nafasi nzuri ambazo wanaweza kuleta tofauti kutokana na misimamo yao, mtu kama Prof. Mkumbo alikuwa muongeaji mzuri alipokuwa chadema na ATC wazalendo na sasa amepewa wizara ya maji kama katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa wizara ni nafasi ya kuonyesha umahili wake wa kuwaletea maendeleo wananchi Kwa kuja na solutions za matatizo ya maji Kwa wananchi ili sasa tuamini Kwa kile wanachokisema na misimamo yao upinzani wakija kuongoza wanaweza kuja na solutions za matatizo ya wananchi ambazo CCM wameshindwa, naamini wengi mtasema hawawezi kufanya chochote Bali ni utekelezaji wa ilani ya CCM, lakini naamini ilani ya CCM na chadema zote ni nzuri na kama kiongozi ni mzuri anaweza kutekeleza regardless chama gani kinatawala.
Lakini pia hii kuteuliwa kutaonyesha umahili wa utendaji kazi wa hawa waliokuwa wanapiga kelele wakisema CCM inakosea kwenye utendaji kazi wake, maana kuongea ni kitu kingine lakini pia utendaji ni Jambo lingine.
Duniani hapa wapo watu wengi Sana walionyesha ni wazuri kwenye kuongea kama akina Zitto, Lissu lakini walipopewa madaraka walifeli Kwa sababu walifikilia kinadharia zaidi kuliko vitendo.
Mtatiro ukuu wa wilaya au mkoa ni madaraka ambayo unaweza kuonyesha umahiri katika utendaji wa kazi tunaomba utuonyeshe umahiri wako angalau Kwa sehemu ndogo uliyopewa kuongoza, kuna wakuu wa mikoa na wilaya ambao wameonyesha tofauti na jamii imewakubali kama Yule wa Simiyu na Arusha, ni vijana walioonyesha wanaweza kuleta mawazo tofauti kwenye serikali ya CCM.
Mtatiro karibu utuonyeshe uwezo wako wa kutumikia wananchi
Na nyie ongezeni juhudi ya kupiga makofi na vigeregere huku wenzenu wakila teuzi kutoka mnapoita unyumbuni.
 
Duuu!!!! Yaani Magufuli katekeleza yote mawili aliyoombwa, kwenda likizo na kumteua Mtatiro kule kule Tunduru. Taarifa ya Msigwa inatoka CHATO!!! kwa kweli kama ni kulenga jamaa alilenga
 
Sasa hivi ni zamu ya BAK then atakuja Pascal... Kabla ya mwaka huu haujaisha, BAK atakuwa amelamba teuzi :D:p
Aisee uko vizuri. Yaani umeshauri Magu aende Likizo, kweli kaenda. Umeshauri amteue Mtatiro Tunduru, kafanya hivyo hivyo. Mimi naomba umshauri apandishe mishahara ya wafanyakazi
 
Hahahahaha hapana Mkuu mie na teuzi za kinafiki hatuwivi kwenye chungu kimoja. Kumsifia huyo nduli na dikteta siwezi hata kwa sekunde moja na huo uteuzi nitaupiga chini. Nadhani nitakuwa wa kwanza kupiga chini uteuzi wa chatu wa chato 😜😜😜

Sasa hivi ni zamu ya BAK then atakuja Pascal... Kabla ya mwaka huu haujaisha, BAK atakuwa amelamba teuzi :D:p
 
Hahahahaha hapana Mkuu mie na teuzi za kinafiki hatuwivi kwenye chungu kimoja. Kumsifia huyo nduli na dikteta siwezi hata kwa sekunde moja na huo uteuzi nitaupiga chini. Nadhani nitakuwa wa kwanza kupiga chini uteuzi wa chatu wa chato 😜😜😜
hautakuwa wa kwanza! kuna yule wa Vodacom !!!!
 
Back
Top Bottom