Mheshimiwa sana, mfikirie Ndugu Mtatiro ukuu wa Wilaya Tunduru ikikupendeza!

Hakuna jambo zuri kama kuandika humu JF halafu jambo hilo likatokea kama ulivyo andika. Inakuwa ni ushindi na rejea nzuri.
Hongera sana mleta uzi kwa andiko lako. Sasa endelea muandika wengine nikiwemo mimi maana rais anakuamini sana
 
Kwanza napenda kukupa hongera kwa utendaji mzuri na uliotukuka wa majukumu yako kama kiongozi mkuu wa nchi hii. Najua changamoto ni nyingi lakini tuna imani na wewe kwa jinsi unavyoendelea kuzipunguza na kuzitatua. Kazi unayofanya ni kazi ngumu sana Duniani na ni kazi ya lawama, hasa unapoendesha nchi masikini.

Huwa nawaambia watu, kuongoza nchi tajiri kama Marekani au Ujerumani ni kazi rahisi sana kwa sababu mambo huwa yanajiendea yenyewe. Ila kuongoza nchi masikini ni mzigo mzito sana kwa kuwa mambo usipoyasukuma hayaendi.

Kutokana na weledi wako uliotukuka wa kuona mbali hivyo kuanza kuwapika vijana na kuwaandaa kushika nafasi mbali mbali za uongozi (succession program) ningependa kukuletea ombi, iwapo itakupendeza umfikirie ndugu Julius Mtatiro kwa nafasi iliyo wazi ya ukuu wa wilaya ya Tunduru au nafasi nyingine inayofanana na hiyo.

Nimesukumwa kumpendekeza kwa kuwa kwa sehemu, namfahamu ndugu Mtatiro kama kijana mwenye uwajibikaji wa hali ya juu, na mwenye nia ya dhati ya kutumikia wananchi. Nimemfahamu kijana huyu kwa miaka mingi tangu tuko chuo na ninaona kwa kiasi kikubwa atasaidia kusukuma gurudumu la maendeleo iwapo atapewa nafasi.

Si kijana mwenye tamaa ya mali kama walivyo baadhi, sio mpenda sifa na pia ni mtu mstaaraabu mwenye uwezo wa kusaidia kujenga heshima ya serikali kwa kusaidia kutatua changamoto za sehemu husika...

Nakuomba ukiangalie kipaji hiki kisipotee kwani kina umuhimu na mchango mkubwa kwa Tanzania yetu yenye neema.
Mwisho nakutakia kazi njema ya kuihudumia na kuiongoza nchi yetu... Najua majukumu ni mengi sana na yamekubana kweli kweli... Ila yatakapo pungua, usijisahau kwa kujipa mapumziko maana ni siku nyingi sijakuona ukienda likizo huenda kutokana na kutingwa na majukumu mengi.

Wasalaam...
Naona Mtatiro anakutafuta akupatie shukrani maana ndoto zako zimetimia
 
Hongera sana mkuu
 
Dah aisee watu walichungulia mbali.
Ila Kuna kitu kidogo sijaelewa kwa huyu mtoa mada,ni kwa nini aliwaza mtatiro apewe uongozi kwenye wilaya ya Tunduru na si wilaya zingine na mikoa mingine?
Kuna uhusiano gani Kati ya Mtatiro na Tunduru?
Nafasi ilishakua wazi tangu may dc wa tunduru alipelekwa katavi.
 
Sasa nimeamini Rais wetu mpendwa Mh. JPM huwa anapita kusoma soma huku JF. Napendekeza ianzishwe thread moja iwekwe sticky ya sisi vijana kumshauri masuala na mipango mbali mbali ya namna ya kuijenga hii nchi yetu ili isonge mbele kimaendeleo kwa kasi zaidi. Katika huo uzi kusiwe na matusi wala lawama.

Huo uzi ambao utakuwa hauna lawama watakuwa wanachangia malaika, matusi inawezekana yasiwepo lakini sio lawama. Ni vyema uzi wa hivyo upelekwe kwenye blog ya ccm na login password iwe namba ya kadi ya ccm kwani yuko kwa ajili ya wanaccm.
 
Back
Top Bottom