Mhe. Freeman Mbowe, Salva Rweyemamu, Waunguruma BBC Kuhusu Mkutano wa JK na CHADEMA!

Salva is a piece of shit. Huyu ndiye aliwachafua wagombea bora wa CCM akimpigia debe bwanaake Njaa Kaya. Na alaaniwe milele kwa kusaliti taaluma ya habari kwa njaa za kitambo.
 
Kuna mambo tunayafumbia macho pengine kwa kuelekeza macho yetu tunapotaka. CUF ambao wamelalamikia katiba hata kufikisha rasimu ya kwao wameungana na CCM katika mchakato usio na uhalali. Hauna uhalali kwasababu wananachi hawakupata nafasi ya kuujadili na sasa wanasukumiwa kitu wasichokiandaa.

Kwa miaka 50 tumekuwa na katiba ambayo sote bila kujali itikadi zetu tunakubaliana kuwa imepitwa na wakati.
Kundi la vijana ambalo ni tegemeo na watumizi wakubwa wa katiba mpya limekaa kimya bungeni kulinda mlo wao na si masilahi yetu.

Na sasa sisi tumeanza kugawanyika kati ya 'sisi na wao'. Sisi na wao kwasababu kauli ya 'Hope for the best and prepare for the worst' inaashiria hivyo. Hii ni katiba yetu na si ya CUF,CCM au Chadema.

Kuna kanuni, sheria na kitu kingine kinaitwa busara. Busara si usahihi ni upeo wa kuliangalia jambo kwa umuhimu wake, faida na athari zake. Hakuna anayejadili kipengele chochote isipokuwa watu wana wasi wasi na mchakato kwasababu uundwaji wake hauna tofauti na tume ya Nyalali, Kisanga, Bomani n.k. Zote ziliundwa kwa 'utekaji nyara' wa hoja za wananchi na tunajua matokeo yake sote.

Spika Makinda ameshindwa kutumia busara na kudhani kanuni na sheria ni muhimu zaidi hata pale aliposhindwa kuzitumia.
Kutoka nje kwa Chadema si jambo la kuupuzwa ni ishara ya wananchi kutoridhika bila kujali ni kiasi gani. Hata hivyo kwa chama cha upinzani idadi yake haipaswi kupuuzwa hata kidogo.
Ni hatua ya kiungwana ya kuonyesha kutoridhishwa na jambo.

Bado busara zinatumika kujaribu kutafuta mahali kati (middle point) na ni wakati muhimu sana kwa Kikwete kuonyeshabusara.
Kama atausaini mkataba kabla ya majadiliano alau kuwasikiliza wawakilishi wa upinzani atakuwa ameungana na Makinda katika kukosa busara. Hadi hapo Chadema watakuwa na busara na kitakachofuata ni busara zao kutamkwa na kila mmoja.

Pasco, kama ulivyopigia mstari neno 'UTASAINIWA' napenda nikuhakikishie kuwa hilo linawezekana hata dakika hii.
Kwamba vifaru na FFU watatumika hilo linawezekana hata dakika hii. Ni uwezekano huo huo uliomlazimisha Moi wa Kenya kupoteza madaraka, Kibaki wa Kenya kuliingiza taifa katika machafuko, Mubarak kufungwa pingu akiwa katika machela, Abde Ali kuugulia Saudia, na Baab AL Azizia kule Libya kuwa maegesho ya magari. Orodha ni ndefu.

Busara zinatuma watu wajiulize ni bora kusaini ili kuonyesha ubabe uliowashinda wababe au kutumia busara kupata muafaka wa kitaifa kwa jambo zito na muhimu kama hili.
Ni wapi duniani nguvu ya dola iliwahi kushinda nguvu ya umma?
 
Salva kasema Ikulu na Kamati ya CHADEMA itabidi wapange tarehe ambayo wajumbe wa pande zote mbili watakuwepo.

Jibu la Mbowe ni kuwa wao walipendekeza katika barua yao iwe kabla ya tar 01.12.2011 kwa kuwa mswada unataja kuwa sheria hiyo itaanza kutumika 01.12.11. Lengo la CHADEMA wakutane na Rais kabla hajasaini muswada huo kuwa sheria.

My take: Ikulu wanaanza sarakasi.

Sarakasi is part of JK tactics
 
Pasco, it sounds like you have a prophecy and you really want it fulfilled in your way. Kwa nini tusisubiri na kuona nini kitatokea?. Kama JK hakuwahi kuongea na NEC wala CC kuhusu kukubali mchakato wa katiba mpya jambo ambalo liliwashtua hata makada wa CCM. Ni kwa nini tujihangaishe na kufikiri nini atafanya JK from now? Kwa nini akubali kuonana na CHADEMA halafu ghafla iwe vyama vyote vya upinzani? Kwa nini unafikiri ni lazima asaini huo muswada kabla ya kukutana na CHADEMA? Aywayz uzuri wa hii ishu ni kwamba kwa sasa mpira uko on JK's court ni uamuzi wake kuutuliza na kupanga mashambulizi ya ushindi au kuondoka nao kama zile enzi zetu mwenye mpira akitaka utoke ukagoma anaondoka na mpira wake.

Kukutana na vyama vyote??? - Ili CCM na CUF wakapigilie msumari kuwa mchakato ni sahihi kama na vyama vingine kama TLP vikapokee posho na kuunga mkono hoja ya CCM na CUF. Hivyo wakija kuhesabu kura (si hoja) itaonekana ni CHADEMA tu ndiyo inayopinga huo mchakato. Magamba kwa faulo hawajambo!!!
 
Kukutana na vyama vyote??? - Ili CCM na CUF wakapigilie msumari kuwa mchakato ni sahihi kama na vyama vingine kama TLP vikapokee posho na kuunga mkono hoja ya CCM na CUF. Hivyo wakija kuhesabu kura (si hoja) itaonekana ni CHADEMA tu ndiyo inayopinga huo mchakato. Magamba kwa faulo hawajambo!!!

Yaani mambo ya bongo huwa yanachekesha sana mkuu, and guess nani anawasemea hao wapinzani wengine, CCM...... walewale waliokuwa wanawazomea CHADEMA na kuwapiga vijembe eti leo wanawaombea wapinzani wengine wawe pamoja na CHADEMA kwenda kuonana na JK. Hivi ina maana akina Lipumba, Cheyo, Mrema mpaka wawasilishwe na CCM? Haiwezekani wao kujiwakilisha na kutuma maombi ya kuonana na mkulu kama walivyofanya CDM mpaka CCM iwaombee?
 
JK kuwa makini na hawa chadema ukiongea nao peke yao pale Ikulu bila wenzao wa upande wa upinzani watatoka na maneno mengi ya uongo Ikulu bora kupata mashahidi kutoka upinzani. maneno yamekuwa mengi hata kabla hujawafungulia mlango wa IKulu watakugeuka hawa na kusema ambayo hukusema

We mpumbavu nini, nikisema ni mjinga ntakuwa nimekupendelea. hivi waandishi wa habari wakiwepo si mashahidi tosha, mpaka hao CUF, wenu wawepo ndo utaona kuna ushahidi? hebu tumia kichwa kufikiri
 
Mkuu yawezekana kweli atausaini lakini sidhani kama JK ni mjinga kiasi hicho.. Kwanza kukubali tu kukutana na Chadema ni jambo ambalo hakuna mtu alikusudia. Katika moja ya Tweet zake nilizowahi kuzisoma JK anasema:-
"Best and wise decisions are to be made in major turning points; otherwise you might create a future crisis..."

This is heavy statement!...Na maneno haya nimewaweka ktk nukuu ya favorites zangu...Na hakuna mahala pazuri ambapo JK anaweza jizolea sifa ni hapa. Hii ndio legacy yake, misifa wonna make history! na sidhani kama atakuja ipoteza nafasi kama hii kuandika Katiba ambayo within next 5 yrs itakufa...
Hivyo naweka tumaini siwezi kulipoteza hadi dakika ya mwisho japokuwa simwamini JK... well, simuamini mwanasiasa yeyote!

Je umesikia kuwa Kamati Kuu ya CCM imeamua JK akutane na vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni, hapo kma sio malumbano nin nini? Kwa maoni yangu CDM tunaoteza muda kuomba kukutana na JK, tunavuna tulichopanda lkuwekeza nguvu zetu kwenye suala moja tu ka umeya wa Arusha na kutelekeza mabo mengne yote. Ni vyema tukakubali hili limekwisha a tuanze upya tujifunze kutokana na makosa.
 
Hiyo condition ya !st December imekaaje; ni kwamba lazima sheria ianze kufanya kazi tarehe 1 December hata kama haijasainiwa na rais?
 
Namshangaa Jk kwa nini kawakubalia kwenda huko Ikulu nyinyi watata sana alitakiwa tu kusonga mbele. kawakubalia sasa mna maneno mengi hata kabla hamjaonana naye
Kipepeo acha ujinga na ushabiki, unafikiri mazungumzo ya CDM na JK ni kwa manufaa ya nani kama si ya watanzania wote including you wanaopenda kuliona taifa lao likiendelea mbele kwa ustawi wa watu wake?. Vinginevyo kama kuna kamisheni unapata kutoka kwa wanaokutuma kuandika ujinga endelea, lakini pia ujinga huo usio na tija haukubariki hapa jf.:hatari:
 
Namshangaa Jk kwa nini kawakubalia kwenda huko Ikulu nyinyi watata sana alitakiwa tu kusonga mbele. kawakubalia sasa mna maneno mengi hata kabla hamjaonana naye
Kipepeo acha ujinga na ushabiki, unafikiri mazungumzo ya CDM na JK ni kwa manufaa ya nani kama si ya watanzania wote including you wanaopenda kuliona taifa lao likiendelea mbele kwa ustawi wa watu wake?. Vinginevyo kama kuna kamisheni unapata kutoka kwa wanaokutuma kuandika ujinga endelea, lakini pia ujinga huo usio na tija haukubariki hapa jf.:hatari:
 
Mzee Zomba kanitonya kuwa Pasco ni System na Rweyemamu ni System na Mohamed Rweyemamu ni system na Salva anamlinda Fatma (shemejie) madudu aliyofanya, nasikia anapewa tenda zote za kuchimba visima wakati ana mashine moja tu ya kuchimbia visima. Tena hamalizi kazi. Jee kuna ukweli?
Dada Faiza Fox, hapo ni kweli kabisa, uko very right . Kwa kawaida kazi zetu huwa ni siri, maadam Faiza Fox, umefichua siri hii, basi sasa sio siri tena!

Naomba nichukue fursa hii, kuwakaribisha wana jf wenzangu kazini kwangu, karibuni tuu mnitembelee, ofisi zetu zipo lile jengo kubwa jipya jirani na St. Peters pale kwenye miti miti. Mkija nitawatembeza idara mbalimbali na kuwaelekeza jinsi sis TISS tunavyofanya kazi zetu. Njooni tuu getini uniulizie, mkifika pale, niulizieni kwa jina la kiofisi, mule ndani hatuitani majina haya, kila mtu ana jina lake, mimi jina langu la kazini naitwa "CHIFU', hivyo ukifika tuu getini sema nakwenda kwa 'Chifu' hivyo utaletetwa kwangu!.

You are most welcome!.
 
"Kama CUF ni CCM B nyinyi mnaenda Ikulu kwa CCM A" - Julius Mtatiro naibu katibu mkuu CUF Bara
 
Namshangaa Jk kwa nini kawakubalia kwenda huko Ikulu nyinyi watata sana alitakiwa tu kusonga mbele. kawakubalia sasa mna maneno mengi hata kabla hamjaonana naye

You go and get a life....!! Naona bado unaishi kwenye zama za kale za mawe!
 
Hiyo condition ya !st December imekaaje; ni kwamba lazima sheria ianze kufanya kazi tarehe 1 December hata kama haijasainiwa na rais?
Jabulani,
Kila Dola ina mihimili mikuu mitatu, Serikali, Bunge na Mahakama, vyombo hivi vitatu vinatakiwa vile huru huku kila kimoja kikichunga kingine ili kisitumie madara vibaya (the doctrine of separations of powers).

Rais ndiye mkuu wa serikali, jaji mkuu ndio mkuu wa mahakama na spika ndiye mkuu wa bunge.
Ili kanuni ya separation of powers ifanya kazi vizuri, ilitakiwa rais asiwe sehemu ya bunge, wala mahakama. Kwa mujibu wa katiba yetu, rais ndiye mkuu wa serikali, rais ni sehemu ya mahakama kwa kuteua jaji mkuu na majaji wote, ndiye husaini capital punishment na kutoa misamaha kwa wafungwa. Rais pia ni sehemu ya bunge, yeye ndio huliunda bunge na ndie hulivunja. Bunge likishatunga sheria, sheria hiyo si lolote si chochote mpaka rais atakapoweka saini yake ndipo huanza kutumika. Rais akiamua, anaweza kulivunjilia mbali bunge wakati wowote akiona inafaa. Kwa hiyo kwa mujibu wa katiba hii, rais ndiye kila kitu!, ndiye alfa na omega wetu.

Ndio maana sheria hiyo mpya inampa rais mamlaka zote kubwa kwa mujibu wa katiba hii. WAanaopiga kelele rais apunguziwe madaraka, wanafukuzana na upepo, au kutaka kupigana na ukuta kwa sababu madarake yale ndiyo yaliyoko kwenye katiba hii mbovu iliyopo.

Namna pekee ya kuyapunguza madaraka ya rais, ni kwenye katiba mpya, ndio maana nawashauri wanaupinga muswada huo ukishasainiwa, wavunje hizo kambi zao na kuipa tume ushirikiano yakiwemo hayo mapendekezo ya kupunguza madaraka ya rais.

Hata Chadema, watakapokutana na JK, ushauri wa kumtaka ajipunguzie madaraka katika mchakato huu, ni sawa na kumshauri, alikate tawi alilokalia!.

Count down ya kutumika kwa sheria hiyo mpya ni zimebaki siku 7!, Alhamisi ijayo sheria mpya inaanza kazi!.
 
Mhe. Freeman Mbowe, Salva Rweyemamu, Waunguruma BBC Kuhusu Mkutanoo wa JK na Chadema!

Wameunguruma katika kipindi cha Dira ya Dunia, kinachoendela sasa!

Walikuwa wakihojiwa na Mtangazaji Aboubakar Mfamao.

Mhe. Mbowe alieleza lengo lao la kuzungumza na JK. Salva alieleza walivyokubaliwa.

BBC ikauliza Kikao ni lini?. Salva akajibu watafanya mawasiliano ya kiofisi kupanga lini wote watakuwa na nafasi.

Mhe. Mbowe amesema Chadema wako tayari wakati wowote, hivyo determinant ni JK tuu.

Angalizo!. JK yuko kwenye kikao cha NEC Dodoma kwa siku mbili, hivyo huo mkutano lazima uwe Jumatatu au Jumanne kwa sababu JK atausani ule muswada siku ya Jumatano ili Alhamisi tarehe 1 Desemba, sheria hiyo ndio inaanza kutumika!.
Kitendo cha JK kukubali kukutana na Chadema, ni dalili njema, ila kwa kumbukumbu yangu, JK ni very strict na (arrogant) kwenye issue za kuhatarisha usalama wa taifa letu, kama nilivyo shuhudia wakati wa ile hotuba yake ya 'Mbayuwayu' naombeni niwape maandalizi ya kisaokolojia ya wale wote wenye Great Expectetions na JK kuwa hatausaini, plese just "Hope for the best, but prepare for the worst!" kwa sababu, ATAUSAINI!

Muswada kusainiwa ni lazima,kinyume chake bunge itabidi livunjwe.Kinachotakiwa ni sheria kupelekwa tena haraka bungeni kufanyiwa marekebisho kulingana na mapendekezo ya CDM kama yatakubaliwa.
 
Dada Faiza Fox, hapo ni kweli kabisa, uko very right . Kwa kawaida kazi zetu huwa ni siri, maadam Faiza Fox, umefichua siri hii, basi sasa sio siri tena!

Naomba nichukue fursa hii, kuwakaribisha wana jf wenzangu kazini kwangu, karibuni tuu mnitembelee, ofisi zetu zipo lile jengo kubwa jipya jirani na St. Peters pale kwenye miti miti. Mkija nitawatembeza idara mbalimbali na kuwaelekeza jinsi sis TISS tunavyofanya kazi zetu. Njooni tuu getini uniulizie, mkifika pale, niulizieni kwa jina la kiofisi, mule ndani hatuitani majina haya, kila mtu ana jina lake, mimi jina langu la kazini naitwa "CHIFU', hivyo ukifika tuu getini sema nakwenda kwa 'Chifu' hivyo utaletetwa kwangu!.

You are most welcome!.

Una "confuse" Pasco, kuwa system si lazima uwe UWT, unaweza ukawa UWT na usiwe system na unaweza ukawa system na usiwe UWT.

Kuwa "system ni kuwa kwenye circle ya elite ruling class" ambapo humo ni nani anamjuwa nani na nini kinakukwaza umuone nani. Hayo ni kwa uchache sana na nnadhani mpaka sasa itakuwa umenielewa.
 
Back
Top Bottom