Elections 2010 Mh Slaa amkoromea Kikwete: Disco au Sera?

kikwete.JPG


Hapa anatoka kwa mganga wa kienyeji Kikwete
 
Uchaguzi ni wiki mbili zijazo, watanzania kweli tutaondokana na UFISADI? Tutakuwa Salama UdINI?
 
Sipati picha huyo Vicky anavyomtazama mama Salma usoni.....
Kweli ukiyaona ya MAHIMBO utastaajabu ya...............................

CCM mmeishiwa sasa mnalazimisha saikolojia ya kuiba kura ili ionekane kwamba Slaa ni kama kilaza mrema.

Siwapi kura yangu kwa hiari wala kununulia bora muiibe
 
kama kweli hapa ni nyumbani kwa Great thinkers hoja kama hizi si za kujadili
 
Dr. Slaa 45%; JK (Doctor wa mezani) 40%....Wera wera wera.....CCM pressure inapanda pressure inashuka
 
Hii ni alama ya kuwa mambo kwa Mh Slaa hayaendi vizuri, na ameshaona kuwa hata lile lengo lake la 25% huenda asilifikie. Na ukizingatia kuwa siku zilizobaki ni chache ndio kiwewe kimempanda.
Uko wapi mwenzetu?
 
Sasa mambo yameiva, asiye na mwana aeleke jiwe!

Mwaka 2005 katika kampeni za uchaguzi CCM walishangazwa na CHADEMA kutumia Helkopta kufanya kampeni katika nchi masikini kama Tanzania. Katika uchaguzi mdogo wa Mara CCM wakaiga matumizi ya Helkopta, lakini baada ya uchaguzi Makamba akapiga marufuku kwa CCM kutumia Helkopta. Kwani mfuko ulitoboka sana bila mafanikio.

Mwaka huu CCM wamekuja na mpya 'Bongo flavor' mpaka asubuhi. Usisahau usafiri wa malori. Baada ya kuona mtindo huo umefanikiwa sana katika kuwakusanya vijana, ukimya wa Mh Slaa umemuishia na sasa ameshaanza kunena. Lakini jibu la KIKWETE NI RAHISI, KAZI NA BURUDANI. Kusanya watu kwanza ndio wape SERA.

Hii ni alama ya kuwa mambo kwa Mh Slaa hayaendi vizuri, na ameshaona kuwa hata lile lengo lake la 25% huenda asilifikie. Na ukizingatia kuwa siku zilizobaki ni chache ndio kiwewe kimempanda.

Hali sio hiyo tu bali mbaya zaidi ni kwamba mfuko wa CHADEMA umeshatoboka wakati ule wa CCM ndio kwanza unajaa.

Sasa Mh Slaa amechanganyikiwa na hajui afanye nini. Pengine kama hapa JF mtapitisha mchango kwani ni Rahisi mkiweka A/C namba.

Mpaka jibu halijapatikana, dawa iliyobaki ni kumkoromea Kikwete ili aachane wa wasanii bora, kitu ambacho ni vigumu kuwezekana.
waulize TCIB watakwambia nani anakubalika zaidi sasa, hapo kwenye red kuna EPA nyingine
 
waulize TCIB watakwambia nani anakubalika zaidi sasa, hapo kwenye red kuna EPA nyingine
Inanichekesha kwakweli!
1. Redet
2. Synovate
3. TCIB
yaani jamaa inashuka tuu niliwaambia ifikapo tarehe 31 jk itakuwa negative!
Yaani sijataja ya
1. radio free africa
2. mwananchi Gazeti
3. Jamiiforum
4. Uhuru (ilifutwa ila takwimu tunazo)
CCM bado mnajipa moyo tuuuu hali mbaya tujipange kuiba tuuuu!
 
Ukikubali kujiunga na JF lazima uwe dynamic na current situation, watu tunatafiti mambo tunakuja na data hapa. We are Great Thinkers forever.
 
Kura mpya ya maoni: Dk. Slaa ampiku JK

• WAZEE WENGI NI WA KIKWETE, VIJANA WA DK. SLAA

na Bakari Kimwanga




KURA nyingine ya maoni iliyoendeshwa na taasisi ya Tanzania Citizens Information Bureau (TCIB) inaonyesha kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ndiye mgombea anayekubalika zaidi katika uchaguzi wa mwaka huu kuliko mwingine yeyote.
Matokeo ya kura hiyo ya maoni yaliyotangazwa jana jijini Dar es Salaam yanaonyesha kuwa Dk. Slaa alikuwa ndiye mgombea aliyekuwa akipewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda urais mwaka huu na ambaye pia angepigiwa kura na watu wengi zaidi waliohojiwa katika utafiti huo.

Akitangaza matokeo ya kura hiyo ya maoni katika Hoteli ya Courtyard, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Vincent Leyaro, alisema utafiti huo ulikusanya maoni ya wananchi katika mikoa 15 ya Tanzania Bara kwa kuchagua jimbo moja kila mkoa, kata mbili mbali na vijiji na mitaa miwili katika majimbo husika.

Dk. Leyaro alisema miongoni mwa watu 3,047 waliohojiwa katika utafiti huo ulioendeshwa katika kipindi cha kati ya Septemba 27 na Oktoba 10, asilimia 48 walimpa Dk. Slaa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu, huku mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete akipata asilimia 38 na nafasi ya tatu ikishikwa na Profesa Ibrahimu Lipumba anayegombea kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) ambaye alitajwa na asilimia 9 ya waliopiga kura hiyo ya maoni.

Mbali ya hilo, utafiti huo uliwauliza waliohojiwa iwapo uchaguzi ungefanyika siku walipohojiwa wangemchagua mgombea gani kuwa rais, asilimia 45 walimtaja Dk. Slaa, asilimia 41 wakisena watampigia kura Kikwete na asilimia 10 wakimtaja Profesa Lipumba.

Matokeo hayo ya TCIB, taasisi inayojumuisha wanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanamfanya Rais Kikwete kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano kuporomoka kutoka katika kuongoza kura za maoni hadi kushika nafasi ya pili nyuma ya mgombea kutoka kambi ya upinzani.

Akiendelea kueleza namna walivyofanya utafiti wao, Dk. Leyaro alisema katika washiriki wote 3047 waliohojiwa, asilimia 18.3 walisema wao ni wanachama au mashabiki wa CCM, wakati asilimia 15.6 walijitanabahisha na CHADEMA na asilimia 12 wakijifungamanisha na CUF.

Mbali ya hao watafiti hao walisema asilimia 31. 6 ya watu wote waliohojiwa walijitaja kuwa watu ambao hawakuwa wanachama au mashabiki wa chama chochote cha siasa miongoni mwa vyama 18 vilivyo katika daftari la msajili wa vyama.

Katika uchambuzi wa upigaji kura kwa mtazamo wa vyama, matokeo ya kura hizo za maoni yalionyesha kuwa asilimia 72 ya watu waliohojiwa ambao walisema walikuwa hawafungamani na chama chochote cha siasa walimtaja Dk. Slaa kuwa ndiye chaguo lao, akafuatiwa kwa mbali na Kikwete aliyepata asilimia 11 na Lipumba akapata asilimia 10.

Katika eneo jingine kura hiyo ya maoni inaonyesha kuwa wakati Kikwete anaungwa mkono na asilimia 80 ya wapiga kura wa ndani ya CCM, Dk. Slaa alikuwa akiungwa mkono na asilimia 90 ya wana CHADEMA huku Lipumba akiungwa mkono na asilimia 38 ya mashabiki na wanachama wa CUF.

Utafiti huo ulitoa matokeo mengine ya kushangaza baada ya kuonyesha kwamba asilimia 15 ya wanachama na wapenzi wa CCM walikuwa wakimuunga mkono Dk. Slaa wa CHADEMA huku wana CUF wafikao asilimia 48 wakimuunga mkono Kikwete badala ya mgombea wao wa urais, Profesa Lipumba.

Dk. Leyaro alisema utafiti huo pia ulifanya uchambuzi wa wahojiwa kirika na kubaini kuwa vijana wengi zaidi miongoni mwa waliohojiwa walisema watamchagua Dk. Slaa, huku sehemu ya kundi la watu wa umri wa zaidi ya miaka 50 likisema kuwa litamchagua Kikwete.

“Tulipofanya uchambuzi kwa makundi ya umri wa wahojiwa, ilijitokeza kuwa vijana wengi walimchagua mgombea wa CHADEMA (Slaa) wakati wahojiwa wa umri wa zaidi ya miaka 50 walimchagua mgombea wa CCM,” alisema Dk. Leyaro.

Katika eneo hili, utafiti huo ulibainisha kwamba asilimia 25 ya wahojiwa wenye umri wa chini ya miaka 25 walisema watamchagua Kikwete wakati asilimia 55 ya waliohojiwa wenye umri wa miaka chini ya miaka 50 walisema watamchagua Dk. Slaa.

Utafiti huo ulionyesha pia kwamba kwa wahojiwa wenye umri wa kati ya miaka 46 na 55 asilimia 50 walisema watamchagua Kikwete huku watu wa kundi hilo wapatao asilimia 35 wakimtaja Dk. Slaa, hali inayoonyesha kwamba mgombea wa CCM alikuwa akiungwa mkono zaidi na wagombea wenye umri mkubwa na wazee wakati Dk. Slaa akiungwa mkono zaidi na vijana na watu wenye umri wa kati.

Kwa upande wa mikoa na namna wagombea hao walivyoonekana kuungwa mkono, Kikwete aliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko wengine katika mikoa ya Dodoma (59.3%), Lindi (43.4%) Mbeya (50%), Rukwa (54.3%), Ruvuma (55%) na Tabora (42%).

Wakati Kikwete akiongoza katika mikoa hiyo sita, Dk. Slaa yeye aliongoza katika mikoa minane ya Arusha (60%), Dar es Salaam (42%), Iringa (58.2), Kagera (49%), Kilimanjaro (71%), Mara (54%), Manyara (79.8%) na Mwanza (42.1%) huku Profesa Lipumba akiwa haongozi katika mkoa wowote na akafanikiwa kushika nafasi ya pili katika mkoa mmoja tu wa Lindi (38.1%).

Hata hivyo Dk. Leyaro, alisema kuwa matokeo hayo ni kura ya maoni sio lazima yawe taswira halisi ya siku ya kupiga kura na kusisitiza kuwa hali halisi ya matokeo itajulikana baada ya wananchi kupiga kura katika uchaguzi ulio huru na haki.

Alisema taasisi hiyo haitarajii wagombea na wapiga kura wao kubweteka au kukata tamaa kwa sababu ya matokeo ya kura za maoni na kutoa changamoto kwa kufanywa mara nyingi kwa kura hizo za maoni na mashirika mengi ambayo ni huru yasiyoegemea upande wowote.

Hata hivyo alisema matokeo hayo yanaweza kusaidia wagombea kujikita vizuri katika muda wa kampeni uliobaki kwa kuzingatia wapi wanakubalika zaidi na makundi gani ili waweze kuelekeza nguvu zao ipasavyo katika muda wa kampeni.

Wiki chache zilizopita taasisi ya Synovate ikionyesha mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Slaa, kupanda kwa alama nne, huku mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, akishuka kwa alama 10.

Matokeo hayo yalipishana na yale yaliyotolewa na taasisi ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) ambayo ilimpa Kikwete asilimia 71.2, Dk. Slaa (12.3) na mgombea wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (10.3).


I think Dr Slaa is doing very well.sijui mtoa mada anatoa wapi issue zake?
 
Duhh! Kichuguu sasa tuanze kuandika Kichina humu kwenye jamvi!!!!
坦桑尼亚有大概四千万多人口。只有一万会说汉语。 我觉得我们应该用swahili语。我爱你查的吗(chadema)
 
sera ya ccm ni kuhonga wapinzani, na wapinzani mamluki hununulika, ila wale wakakamavu hakika wanaunguruma kupigania Taifa hili. wameishiwa sera, mikutanom yao ni kusanyiko la wanataarabu na bongoflavor, mipasho tupi.
 
Dr. Slaa 45%; JK (Doctor wa mezani) 40%....Wera wera wera.....CCM pressure inapanda pressure inashuka

Kwa hiyo Data za TICB nio za uongo.

Na kama hivyo ndivyo una maanisha kuwa wale wenye ndoto kuwa baada ya tar 31.10 Mh Slaa atatinga ikulu hayawezekani. Maana ili kuingia Ikulu nuatakiwa kupata 50+.

Kwa maana hiyo unakuja na hoja mpya kuwa hakuna mgombea atayepata 50+, hivyo tungojee round ya pili kama ilivyokuwa kwa Mugabe na Tshangirai.
 
Back
Top Bottom