Mh. Samweli Sitta: Waziri wa Afrika Mashariki Ameiasi Serikali ya CCM?

Hosida

Member
Oct 21, 2008
71
12
Habari wana JF,

Nimekuwa na maswali mengi sana kuhusu utawala wa serikali ya kimabavu ya JK na bado sijajiridhisha na baadhi ya majibu niliyopata. Hivyo naomba wana JF mnisaidie kutafakari pamoja juu ya suala hili.

Suala lenyewe ni kuhusu kauli mbili za aliyekuwa spika wa Bunge lililopita na waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa sasa Mh. Samweli Sitta.

Kauli ya kwanza ni ile ya kupinga tamko la waziri mwenzake Mganga Ngeleja hadharani kwa kusema kuwa Dowans ni wizi wa kwenye makaratasi. Je, kauli ya Ngeleja haikuwa msimamo wa baraza la mawaziri?

Kauli ya pili ile ya kumpinga waziwazi waziri mwenzake wa katiba na Sheria juu ya kuandikwa kwa katiba mpya. Je, kauli ya Waziri wa katiba hakuwashirikisha mawaziri wenzake? Kama aliwashirikisha iweje Sitta atofautiane na mtazamo wao kama serikali?

Suala la kutafakari: Je, Rais mbabe JK anafahamu kuwa Sitta ameshamwasi yeye na Baraza lake la mawaziri? Na kama anafahamu mbona asitumie ubabe wake kumwajibisha? Au anaogopa nguvu aliyonayo huyu mwanaharakati?

Kufikiri ni jadi ya kila binadamu lakini uwezo wa kufikiri hutofautiana!!!!!
 
amguse hajipendi yatamkuta makubwa saana! thus why anaogopa.
 
Nadhani hukumsikiliza Mh. Samuel Sitta vizuri, he said " Ngeleja faced the public without having an authorization from the ministers' cabinet" Hivyo ngeleja anajua anachokifanya. On the other hand, we say CHUKUA CHAKO MAPEMA though, at the end of the day, you will end up in badly
Habari wana JF,

Nimekuwa na maswali mengi sana kuhusu utawala wa serikali ya kimabavu ya JK na bado sijajiridhisha na baadhi ya majibu niliyopata. Hivyo naomba wana JF mnisaidie kutafakari pamoja juu ya suala hili.

Suala lenyewe ni kuhusu kauli mbili za aliyekuwa spika wa Bunge lililopita na waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa sasa Mh. Samweli Sitta.

Kauli ya kwanza ni ile ya kupinga tamko la waziri mwenzake Mganga Ngeleja hadharani kwa kusema kuwa Dowans ni wizi wa kwenye makaratasi. Je, kauli ya Ngeleja haikuwa msimamo wa baraza la mawaziri?

Kauli ya pili ile ya kumpinga waziwazi waziri mwenzake wa katiba na Sheria juu ya kuandikwa kwa katiba mpya. Je, kauli ya Waziri wa katiba hakuwashirikisha mawaziri wenzake? Kama aliwashirikisha iweje Sitta atofautiane na mtazamo wao kama serikali?

Suala la kutafakari: Je, Rais mbabe JK anafahamu kuwa Sitta ameshamwasi yeye na Baraza lake la mawaziri? Na kama anafahamu mbona asitumie ubabe wake kumwajibisha? Au anaogopa nguvu aliyonayo huyu mwanaharakati?

Kufikiri ni jadi ya kila binadamu lakini uwezo wa kufikiri hutofautiana!!!!!
 
Lakini tamwogopa mpaka lini? Cause Bunge likianza sijui litakuaje kwa kweli.
 
Serikali imepoteza mwelekeo, sasa hivi everybody ni msemaji, kwani hujasikia ya yule kitanda wa Arusha?

Sisi kazi yetu ni kuwasikiliza wanavyotoa siri zao. tumekaa mkao wa kula, leo sijui nani atakuja kivingine.
 
Ukiangalia sana siasa anazofanya Samwel Ssita ni kama Siasa za kama majirani zetu wakenya haogopi wala hamumunyi mumunyi maneno anasema kile anachoamini hata kama anajua kabisa kitamgharimu yeye bunafsi au serikali. Kama Mkwere ana busara aachane naye ampotezee ila akijaribu kumfuta kazi kwa kumfukuza au kutoa kwenye cabinet atampa umaarufu kama anavyowapa chadema kupitia jeshi la polise.
 
Si wote wanapenda madudu ya CCM! Ndani yao pia kuna wapinzani na sita ni mmoja wao.
 
Sitta aachie ngazi ya uwaziri ili awachome vzr hawa wezi... hivi serikali haina mawakili??? au na wenyewe ni wezi tu kuchelewesha kasi ili waiibie serikali??? Mungu wangu hii Tz inapelekwa wapi na hawa wababaishaji???.

Ipo siku mambo haya yataifika kikomo wataiba sana lakini watarudisha mali zetu siku moja.
 
Nadhani ni vyema ukatafakari kabla ya kuandika kinachotoka kinywani. Ishu ikipita kwenye Baraza la Maawaziri hua Halitoki nje.....kwa mmoja mmmoja..bali linakua msimamo wa serikali. Hivyo basi, Mh. Sitta , ngeleja na Celina Kombani wanatudhihirishia kua Sirikali yetu ni mbovu na ya kibanafsi. Swala la kwenye Baraza linasemwa na kila mtu...Jamani hii sio serikali....kina jey kei ni wababaishaji!!
 
Sitta tatizo huko uliko ndiyo tatizo, achana na Si Si Em.

Uko katika Kichaka cha majizi
 
Kuwa mkweli; kwani mkanganyiko kwenye serikali ya JK kumeanzia na Sitta? Chukua ili suala la katiba mpya; waziri wa sheria na katiba alilipiga teke, waziri mkuu akaliunga mkono, pamoja na hayo Mwanasheria Mkuu akalipiga tena teke, hatimaye rais mwenyewe akaliunga mkono. Hii inatoa picha gani? Kwangu mimi, inaonekana hivi sasa huko serikalini hakuna uamuzi wa pamoja, kila waziri anatoa mawazo yake binafsi na anachukulia hayo kuwa ndio msimamo wa serikali. Umemusikia Ngereja akisema ya kuwa serikali imeamua kuilipa Dowans, lakini Mkullo amenukuliwa akisema kuwa serikali haina hela hizo labda wizara ya nishati na madini ilipe yenyewe! Kauli kama hiyo inaonyesha dhahili ni kwa kiwango gani mawaziri wenzake wamechoka na usanii wa Ngereja.
 
Ukiangalia sana siasa anazofanya Samwel Ssita ni kama Siasa za kama majirani zetu wakenya haogopi wala hamumunyi mumunyi maneno anasema kile anachoamini hata kama anajua kabisa kitamgharimu yeye bunafsi au serikali. Kama Mkwere ana busara aachane naye ampotezee ila akijaribu kumfuta kazi kwa kumfukuza au kutoa kwenye cabinet atampa umaarufu kama anavyowapa chadema kupitia jeshi la polise.

Naomba wajuzi wa masuala ya sheria na utawala wa Dola wanijuze kama nimepotoka:

Nijuavyo, malipo ya suala kama hili kiongozi yeyote hawezi kulitolea uamuzi wa kulipa au la hadi yafuatayo yote yafanyike:
1. AG apitie hukumu na kutoa maoni yake kwa serikali
2. Serikali inategemewa kuzingatia maoni ya AG lakini hailazimiki kufuata ushauri wake kama itajiridhisha kuwa AG alipotoka.
3. Lazima serikali ifikie uamuzi wa pamoja kwa njia ya mjadala na kura katika Baraza la Mawaziri.
4. Lazima hukumu isajiliwe Mahakama Kuu na hapo Mahakama ina uwezo wa kukosoa iwapo sheria za nchi zilikiukwa na hivyo inaweza kusema malipo hayo hayastahili kulipwa.

Hivyo kitendo cha waziri Ngeleja kuharakisha uamuzi wa kulipa wakati Baraza la Mawaziri halijajadili na wala Mahakama Kuu haijajadili ni mapungufu makubwa.
 
Huu ni ushahidi kura za wananchi zilichakachuliwa na nec. Watanznia sio mabwege kuchagua viongozi wa namna hii. Ila nimefurahi sana wanavyolipuana -hakuna chenye mwanzo kisichokuwa na mwisho. Mzimu wa nyerere unawasumbua vibaya mno. Ndani ya serikali hii kila mmoja kuna kundi analitumikia watanzania wamesahaulika angalau sitta anatetea mapesa yanayoporwa mchana kweupeeeeeeeeeeee, pale mdaiwa anaposisitiza malipo mdaiwa hajakamilisha anachotakiwa kufanya. Mzee kisumo nilimpenda alilia na katiba mpya, sasa amelia na zengwe la arusha-bora akimbie chama cha chukua chako mapema
 
Tatizo kubwa lililopo Serikalini na CCM ni kuwa kuna ombwe (Vacuum) kubwa katika uongozi wa juu. Hivyo wanachama ama mawaziri wameliona hilo, kwa hivyo kila mmoja wao yuko huru kufanya kivyakevyake akijua hakuna litakalomtokea. Wengine wanatafuta umaarufu wa papo kwa papo. Cheap politics!
 
kuna kauli nyingine aliitoa kuhususiana kuondolewa kwenye mchakoto wa u-spika na ya Dowans amefikisha mara mbili kuzungumzia hili waziwazi, anachokifanya Sitta ni kupiga yowe ili mimi na wewe tuamke na kuchukua hatua....
 
Mzee Sita endelea kutuletea vijimambo vya kiintelijensia toka upande huo, wakikutimua hamia tu cdm kuendeleza mapambano!
 
Sitta; ok na sawa kwa unayoongea lakini tunakulaumu sana wewe. Tukikumbuka sakata la Richmond na hatimae Dowans kule bungeni wakati ukiwa spika, naweza tu kusema yafuatayo:
Tulimkaba nyoka shingoni tukakuambia "Sitta umeshika fimbo piga kichwa" ukapiga mkia, tukasema umekosea - "piga kichwa kiko huku", ukatujibu kuwa huyo si nyoka - akaachiwa!!. Sasa hivi huyo nyoka ameshafura amenyanyuka kwa hasira za kuumizwa mkia, kichwa kiko juu; Unatuambia sasa "jamani ni nyoka" nani atamshika?.
Kwa vyovyote kabla nyoka huyu hajashikwa tena na kuuawa lazima naye ataumiza (kuua) wengi. Ilianza Buguruni, sasa Arusha.
Sitta, malalamiko yako sawa lakini unapaswa kukiri hadharani kuwa ulikosea sana huko nyuma!!
 
Back
Top Bottom