Gagurito
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 5,600
- 803
Huyu bwana BOGUS sijawahi ona duh! Hovyo sana!
Maji Marefu:
Chama Cha Mapinduzi, CCM Regional Economic Secretary 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Economic Secretary, Korogwe rural 2007
Lusinde:
Chama Cha Mapinduzi, CCM Secretary, Tarime 2007 na kuna wakati alikuwa eti ACCOUNTANT
Sidhani kama Lusinde ndiye yuko under microscope. Otherwise, utakuwa una-narrow tatizo na kufanya solution isipatikane. Tatizo hapa ni Watanzania wenyewe. Kama walikuwa tayari kuwa pale kusikiliza na kushangilia kwa yale waliokuwa wanayasikia, basi wao ndio wanatakiwa kuwa under microscope. Labda na wale waliomchagua pia. Kumbuka Lusinde ni mwakilishi wa watu na possibly ata-reflect waliomchagua.
Kama hao Watanzania wangekataa kusikiliza matusi, angeyasemea wapi? Ndio maana hata chama chake kinaweza kisimchukulie hatua zozote kwa sababu kinajua wazi walio na tatizo ni akina nani.
Kwa hiyo, badala yake, hotuba yake ya matusi ingekufanya binafsi upende kujua kwa undani baadhi ya mambo ya msingi kuhusu Watanzania waliokuwa wanamsikiliza na kumshangilia kama:
1. Wanazo akili timamu kweli?
2. Kama hawana akili sheria inasemaje kwa mtu asiye na akili?
3. Kama wanazo kwa nini walishangilia matusi yale?
4. Je historia yao ikoje?
5. Malezi yao yalikuwaje?
6. Na mengine ambayo wadau mtapenda kuongezea.
Hakika mzee. Wanaopaswa kuwa under scrutiny ni hao watu waliokua wakishangilia matusi na maneno ya kiuwendawizimu yaliyokuwa yakitoka mdomoni mwa Livingstone Lusinde!!
Lakika licha ya hivyo, bado kuna haja ya kumtathmini huyu mtu; kwani hayuko kawaida. Tathmini hii pia inapaswa kufika hadi kwenye chama alichopo huyu mtu; nacho hakipo kawaida. Haiwezekani, mtu kama huyo aendelee kuwepo kwenye kikundi cha watu wenye kuwa na mtazamo na itikadi zinazoshabihiana!!
Inasikitisha kwa kweli kuwa na hayo makundi matatu ambayo yanapaswa kuwa under microscope.
Mkuu, ukipewa Leseni ya Piki Piki au ya gari dogo huwezi ukaendesha Semi Trella unless uwe una kipaji cha ajabu sana na umakini wa hali ya juu.
Lusinde Elimu yake ni darasa la saba, hicho ndicho tunachojua mpaka sasa unless kama kuna mtu ana data zaidi.
Sasa kama kweli elimu yake ni darasa la saba, piga picha uwezo wa walio wengi walioishia darasa hilo katika kuchanganua mambo. Kisha piga picha sasa kapewa Semi Trella ya kuingia bungeni na kupiga Kampeni na kutunga sheria na kutumikia kamati za Bunge. Ni nini unachotegemea?
WYSIWYG . . .
Sawa. Lakini kama alivyosema mzee EMT, hili suala lazima tuliangalie kwa mapana zaidi.
Ni kweli Lusinde ana matatizo ya akili (kwa kutumia reference ya hiyo hotuba); lakini mimi bado naendelea kuamini wenye matatizo zaidi ni hao watu waliokuwa wakimshangilia na kumtaka aendelee kuporomosha matusi!! Kwa maana kwa watu wenye utashi na uelewa, wasingeweza kuvumilia kusikiliza maneno machafu kama yale!!
Yaani ni sawa na mtu anayeoga mtoni, kisha "chizi" akaja kukwapua nguo zake, kisha mtu huyo akaanza kumkimbiza "chizi" yule, akiwa "mtupu". Sasa hapa tutamlaumu "chizi" tu bila ya kumshangaa na huyo mtu anayemkimbiza "chizi" akiwa mtupu?! Namaanisha kwamba, pamoja na kumsema Lusinde, lakini "audience" yake kwa siku hiyo haiwezi kuachwa kusemwa pia. Kwani walikua na haki na uwezo wa ku-walk out na kumwacha huyo "chizi" akimbie na nguo!!
Mkuu, ukipewa Leseni ya Piki Piki au ya gari dogo huwezi ukaendesha Semi Trella unless uwe una kipaji cha ajabu sana na umakini wa hali ya juu.
Lusinde Elimu yake ni darasa la saba, hicho ndicho tunachojua mpaka sasa unless kama kuna mtu ana data zaidi.
Sasa kama kweli elimu yake ni darasa la saba, piga picha uwezo wa walio wengi walioishia darasa hilo katika kuchanganua mambo. Kisha piga picha sasa kapewa Semi Trella ya kuingia bungeni na kupiga Kampeni na kutunga sheria na kutumikia kamati za Bunge. Ni nini unachotegemea?
WYSIWYG . . .
Kamanda Nzi, mimi sina tatizo la arguments zako au EMT, hili jambo lina wigo mpana zaidi kama tutalifanyia upembuzi. Kama tukiamua kuwa focused zaidi tatizo hili si la wanaomsikiliza tu, bali ni mfumo mzima wa kuchagua viongozi. Kama Lusinde hii ndo tabia yake halisi na style yake ya leadership basi hakupaswa afike hapa alipom ukienda mbele zaidi utagundua pamoja na mfumo mbaya wa uchaguzi, kuna suala zima la kihistoria, elimu nk.
Na ukienda kwa mapana zaidi ukaangalia mfumo wote wa kiutendaji serikalini na siasa za maji taka ndani ya vyama, utagundua hata mimi na wewe tuna matatizo, ni mangapi tumetukanwa na viongozi direct au indirect lakini tumekaa kimya kama kondoo na kuona sawa tu? vingapi tumenyanyaswa? Tumepuuzwa? Tumeonewa, Tumedharauliwa? nk?
Hata kama suluhu ni katiba mpya kwa namna moja au nyingine, lakini bado suala zima la uongozi bora bado liko palelepale. Hilo nalo linaendana sambamba na attitude za watu na Elimu kwa ujumla. It is a Viscous Cycle hata sijui tutaanzia wapi . . . . The reason why I hate to be a Politician . . . may be I can, but only If I can be a President ili nisiwekewe kiwingu na yetote, then I know only what guts I have and the love for my country.
If you cant be a better and a Patriotic Politician, better not be one! Nawapongeza Wanasiasa wote ambao katika mfumo mbovu wa siasa tulionao sasa hivi wanasimama kidete kutetea maslahi ya nchi na umma kwa uzalendo wa hali ya juu. Though, I am not sure how many we have maana pia kuwa Opportunist si kuwa Mzalendo!
WanaJF
Nadhani wengi tumepata bahati ya kusikia Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM kule Arumeru Mashariki katika moja ya mikutano ya Kampeni ya CCM. Ni wazi kuwa katika kampeni vijembe vya hapa na pale kwa vyama pinzani haviwezi kukosekana. Hata hivyo vijembe vinapogeuka consinstently kuwa matusi tena mbele ya kadamnasi ya watu wakiwepo watoto wadogo wa shule, ni wazi kuwa mhusika anakuwa amevuka na kuvunja maadili ya ustaarabu wa kawaida wa Watanzania.
Hotuba yake ya matusi imenifanya binafsi nipende kujua kwa undani baadhi ya mambo ya msingi kuhusu Mh. Lusinde kama:
- Mh. Livingstone Lusinde anazo akili timamu kweli?
- Kama hana akili Katiba inasemaje kwa mtu asiye na akili kuwa kiongozi?
- Kama anazo kwa nini aliporomosha matusi yale?
- Je historia yake ikoje?
- Malezi yake yalikuwaje?
- Na mengine ambayo wadau mtapenda kuongezea.
Wakati tukiendelea kumweka mh. Lusinde katika Microscope, naomba pia tuendelee kukusanya kumbukumbu zake za kila namna kuridhisha hasa ni mtu wa namna gani.
Mkuu,
ukipewa Leseni ya Piki Piki au ya gari dogo huwezi ukaendesha Semi
Trella unless uwe una kipaji cha ajabu sana na umakini wa hali ya juu.
Lusinde Elimu yake ni darasa la saba, hicho ndicho tunachojua mpaka
sasa unless kama kuna mtu ana data zaidi.
Sasa kama kweli elimu yake ni darasa la saba, piga picha uwezo wa walio
wengi walioishia darasa hilo katika kuchanganua mambo. Kisha piga picha
sasa kapewa Semi Trella ya kuingia bungeni na kupiga Kampeni na kutunga
sheria na kutumikia kamati za Bunge. Ni nini unachotegemea?
WYSIWYG . . .
Wewe nawe ukilaza kweli,unataka kusema wewe unamjua sana Lusinde? haya ngoja akubajaji mwenzio
Haaaa haaa Mzee wa Sikonge leo umenifurahisha sana. Isije ikawa umetekwa na Malaria Sugu . . .
Livingstone Joseph Lusinge inawezekana akawa ni Mwislamu maana jina si lazima liwe ni hatimiliki au liashirie dini fulani.
Lakini kwa matusi haya yenye harufu mbaya ya kama CHOO CHA CITY najua hata Waislamu tutamkana.
baada ya miaka ishirini ndo effects zake zitadhihirika kwa wengi.