Mh. Livingstone Lusinde Under Microscope?

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
WanaJF

Nadhani wengi tumepata bahati ya kusikia Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM kule Arumeru Mashariki katika moja ya mikutano ya Kampeni ya CCM. Ni wazi kuwa katika kampeni vijembe vya hapa na pale kwa vyama pinzani haviwezi kukosekana. Hata hivyo vijembe vinapogeuka consinstently kuwa matusi tena mbele ya kadamnasi ya watu wakiwepo watoto wadogo wa shule, ni wazi kuwa mhusika anakuwa amevuka na kuvunja maadili ya ustaarabu wa kawaida wa Watanzania.

Hotuba yake ya matusi imenifanya binafsi nipende kujua kwa undani baadhi ya mambo ya msingi kuhusu Mh. Lusinde kama:


  1. Mh. Livingstone Lusinde anazo akili timamu kweli?
  2. Kama hana akili Katiba inasemaje kwa mtu asiye na akili kuwa kiongozi?
  3. Kama anazo kwa nini aliporomosha matusi yale?
  4. Je historia yake ikoje?
  5. Malezi yake yalikuwaje?
  6. Na mengine ambayo wadau mtapenda kuongezea.

Wakati tukiendelea kumweka mh. Lusinde katika Microscope, naomba pia tuendelee kukusanya kumbukumbu zake za kila namna kuridhisha hasa ni mtu wa namna gani.
 
Sidhani kama Lusinde ndiye yuko under microscope. Otherwise, utakuwa una-narrow tatizo na kufanya solution isipatikane. Tatizo hapa ni Watanzania wenyewe. Kama walikuwa tayari kuwa pale kusikiliza na kushangilia kwa yale waliokuwa wanayasikia, basi wao ndio wanatakiwa kuwa under microscope. Labda na wale waliomchagua pia. Kumbuka Lusinde ni mwakilishi wa watu na possibly ata-reflect waliomchagua.

Kama hao Watanzania wangekataa kusikiliza matusi, angeyasemea wapi? Ndio maana hata chama chake kinaweza kisimchukulie hatua zozote kwa sababu kinajua wazi walio na tatizo ni akina nani.

Kwa hiyo, badala yake, hotuba yake ya matusi ingekufanya binafsi upende kujua kwa undani baadhi ya mambo ya msingi kuhusu Watanzania waliokuwa wanamsikiliza na kumshangilia kama:

1. Wanazo akili timamu kweli?
2. Kama hawana akili sheria inasemaje kwa mtu asiye na akili?
3. Kama wanazo kwa nini walishangilia matusi yale?
4. Je historia yao ikoje?
5. Malezi yao yalikuwaje?
6. Na mengine ambayo wadau mtapenda kuongezea.
 
Maana inabidi ujiulize na hao waliomchagua kuwa mmbunge wao kama wana akili timamu vilevile.

My take nikwamba kuna watu sehemu zingine za Tanzania wamechoka tena kusikia majina yale-yale kwenye chaguzi zao ilimradi yeyote mwenye kipaza sauti lakini si fualni.

Lakini kweli ameweza pita vipi kwenye kura za maoni huko chamani na hata kuja kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu, kwakweli ignorance bado ni tatizo kubwa kwenye jamii yetu.
 
natabiri motto mkali kumuwakia lusinde hapo CCM itakapopoteza jimbo jumapili hii . lawama nyingi zitamwendea yeye na wengine wengi akiwemo wasira kwa kuongea uongo wa dhahiri kwani hizo zitakuwa ni kati ya factors zitakazowafanya CCM kushindwa pamoja na udhaifu wa mgombea
 
Hizi ni baadhi ya Kumbukumbu zake kutoka katika tovuti ya Bunge:

General:

Salutation: Honourable
First Name: Livingstone
Middle Name: Joseph
Last Name: Lusinde
Member Type: Constituency Member
Constituent: Mtera
Political Party: CCM
Office Location: Box 50, Dodoma
Office Phone: +255 755 453327/+255 785 679927

EDUCATIONS

Mbigili Primary School: 1980 – 1987 - PRIMARY CERTIFICATE
CCM College Ihemi: 2007 -2008 - CERTIFICATE


EMPLOYMENT HISTORY


Member of Parliament - Mtera Constituency - 2010 -2015



Ministry/Political Party/LocationPositionFrom To
Chama Cha Mapinduzi, CCMSecretary - Tarime District20062010
Chama Cha Mapinduzi, CCMAssistant Secretary/Accountant20062007
CHADEMAMember - National Executive Board1995
Civic United Front, CUFSecretary - Kawe Constituency19921995
Chama Cha Mapinduzi, CCM
Secretary


 
Mkuu ingawa yale maneno yalikuwa makali kiaina fulani lakini ilionekana kama anajibu mapigo ya upande fulani, sasa kwanza kabla ya kumjadili Lusinde tujiulize kama ni kweli yale aliyoyaita majibu kuwajibu baadhi ya viongozi wa CDM yalitamkwa na hao viongozi?
Kimsingi kama ni kweli yupo mweshimiwa wa CDM aliyesema SIOI ni shoga ilikuwa haijatulia, wakati tunajadili haya lazima tukiri kuwa wapo baadhi ya viongozi katika vyama vya siasa wasiotofautisha kati ya mitaani/vijiweni na kwenye kampeni.
 
Mimi ombi langu moja tu kuhusu hii heading. Nafikiri 'Mh.' au Mheshimiwa haifai tena kutumika kwa Lusinde, Iweje mtu asiyejiheshimu aitwe mheshimiwa?. It is a disgrace to all MPs!, ningekuwa mbunge ningepeleka hoja binafsi bungeni kuhusu jinsi wabunge wanavyotakiwa ku-behave kwenye public. Kuna vijembe na misimu na misemo katika changuzi ila MATUSI sidhani kama yanajenga precendence nzuri katika siasa za Tanzania.

CCM kama kweli ni viongozi wanatakiwa kutoa mfano kwa kumwadhibu huyu mbunge wao, otherwise watakuwa wamebariki matusi na 2015 itakuwa worse na tutashindwa ku-control.
 
Hizi ni baadhi ya Kumbukumbu zake kutoka katika tovuti ya Bunge:

General:

Salutation: Honourable
First Name: Livingstone
Middle Name: Joseph
Last Name: Lusinde
Member Type: Constituency Member
Constituent: Mtera
Political Party: CCM
Office Location: Box 50, Dodoma
Office Phone: +255 755 453327/+255 785 679927

EDUCATIONS

Mbigili Primary School: 1980 – 1987 - PRIMARY CERTIFICATE
CCM College Ihemi: 2007 -2008 - CERTIFICATE



Hicho chuo in red wanafundisha nini?
 
Jambo "zuri" naloliona kutokana na huo upuuzi wake ni gharama ya mwelekeo wa siasa za Chama Cha Mapinduzi kutumia ""ujinga" wa baadhi ya wananchi kama mtaji wa kisiasa. Kwa kweli ni aibu sana!
 
Nimejitahidi kutafuta elimu yake katika tovuti ya Bunge, hakuna details nyingi. Angalia post number 7. Bila ya shaka alisoma sekondari na labda chuo. Walio na details tunaomba mtupatie.
 
Mkutano wa Kampeni za CCM kata ya Makiba

4.%2BLivingstone%2BLusinde%2Baka%2BKibajaji%2Bakihutubia%2BMakiba.jpg



Mbunge wa Mtera, Mjumbea wa NEC ya CCM, Livingstone Lusinde aka Kibajaji akihutubia Makiba. Angali watoto wadogo mbele yake. Picha kwa hisani ya: FULL SHANGWE: MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM KATA YA MAKIBA WATIA FORA
 
Mkuu ingawa yale maneno yalikuwa makali kiaina fulani lakini ilionekana kama anajibu mapigo ya upande fulani, sasa kwanza kabla ya kumjadili Lusinde tujiulize kama ni kweli yale aliyoyaita majibu kuwajibu baadhi ya viongozi wa CDM yalitamkwa na hao viongozi?
Kimsingi kama ni kweli yupo mweshimiwa wa CDM aliyesema SIOI ni shoga ilikuwa haijatulia, wakati tunajadili haya lazima tukiri kuwa wapo baadhi ya viongozi katika vyama vya siasa wasiotofautisha kati ya mitaani/vijiweni na kwenye kampeni.
Hapana aliyesema sioi ni shoga. Hii movie ilikuwepo hapa JF tangu mwanzo, nadhani yeye lusinde ni member humu na ndiko alikoitoa. Mtizamo wangu tu.
 
04_11_4s6769.jpg




Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozana na watoto Levina Lusinde (kushoto) na Isaya Lusinde kutoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma juzi. Hawa ni watoto wa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Je hawa watoto wanajua lolote kuhusu baba yao? Na malezi yao yakoje?
 
Back
Top Bottom