Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

Mkuu Ibrah,

Washiri ni viongozi wa kimila wa kabila la waMeru ni kama Olaigwanani wa kabila la waMaasai.Washiri wa kabila la waMeru wakitoa maagizo chini mti wa Mringaringa hata kama ni maagizo yanayovunja sheria yatatekelezwa sasa CCM wamebaini maji yapo shingoni wamekuja na mbinu ya kuwatumia washiri mnaweza kuona ni jambo la kijinga lakini nawahakikishia njia ya Moshi Arusha itakuwa haipitiki wengi hapa ni wakizazi cha dot com wengine tunakilometa za kutosha tuna uzoefu kama Tembo jike tuna kumbu kumbu nzuri ya mgogoro wa Meru dayosisi.

Kwa hapa mkuu nimekuelewa,i got u wrong before!nafikiri ni taadhari nzuri umeitoa,sorry kwa kutokukuelewa awali
 
Hao ni wazee wa ccm...washili wana taratibu zao ..taarifa zote zinazohusu jamii zao hutoka baada ya kufanya vikao tena chini ya mti(mkuyu)..sasa hao wazee walikaa lin chini ya mti wakatoa hilo tamko?.......
 
KUTOKANA NA KAULI ALIYOTOA MSAJILI WA VYAMA SIASA NCHINI,HII NI DHAHIRI HATUA MADHUBUTI ZINAPASWA KUCHUKULIWA

‘Tendwa alisema hayo jana kwa waandishi wa habari wakati akizungumzia mambo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Alisema utovu wa nidhamu alioonesha Lema siku ya maziko ya aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo, Jeremiah Sumari, kiliwakera Washiri na kumtaka asikanyage jimbo hilo wakati wa kampeni.

Alisema yeye alikwenda katika jimbo hilo kuonanana wakuu wa Serikali na taasisi zake kupanga mkakati wa uchaguzi, lakini ghafla alikutana na wazee hao waliosema mbele yake, kuwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini, hawataki kumwona katika kampeni, vingivevyo damu inaweza kumwagika juu yake.

’Washiri wamesema hawataki kumwona Lema katika kipindi cha kampeni kwani alileta dharau kubwa na utovu wa nidhamu siku ya maziko ya Sumari, hatua ambayo iliwakera wazee hao … ni busara tu, Lema kwenda kuwaomba radhi wazee hao kama anataka kufanya kampeni ya mgombea wa chama chake- Chadema,” alisema Tendwa. Pia Tendwa amesema Lema asipowaomba radhi huenda damu ikamwagika.

Msajili alivitaka vyama vya siasa kuheshimu mila na desturi za makabila, ili kuepuka umwagaji damu na kushauri kuwa ni vema vyama vya siasa katika kampeni kuzingatia hilo.

Mkuu Ibrah,

Washiri ni viongozi wa kimila wa kabila la waMeru ni kama Olaigwanani wa kabila la waMaasai.Washiri wa kabila la waMeru wakitoa maagizo chini mti wa Mringaringa hata kama ni maagizo yanayovunja sheria yatatekelezwa sasa CCM wamebaini maji yapo shingoni wamekuja na mbinu ya kuwatumia washiri mnaweza kuona ni jambo la kijinga lakini nawahakikishia njia ya Moshi Arusha itakuwa haipitiki wengi hapa ni wakizazi cha dot com wengine tunakilometa za kutosha tuna uzoefu kama Tembo jike tuna kumbu kumbu nzuri ya mgogoro wa Meru dayosisi.
Kwahiyo, Washiri hao ni wanaCCM?

Turudi kwenye Hoja, usipindishe,
Tendwa anaona ni sahihi kwa mtu/kundi la watu kumtishia mtu mwingine tena kwa kusema damu itamwagika kwa sababu ya hisia ya kufikiri wametukanwa?

Kwa mujibu wa post nilizozisoma humu, ni kwamba, Lema alionyesha alama ya Vidole viwili (alama inayotumika na CHADEMA, na vyama vingine vya upinzani duniani) wakatuwa mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Meru mashariki. Sijui mazingira yaliyopelekea kufanya hivyo. Lakini naamini kwamba hilo sio tusi kwa yeyote, labda ni tusi kwa wanaCCM.

Anyways. issue ni kwanini kiongozi wa calibre ya juu kabisa kama Tendwa, badala ya kuwaambia vyombo vya usalama walinde na kutoa ulinzi, yeye anasema Lema awaombe Washiri radhi au asiend Meru?

Mkuu kwa badinko lako, unataka kutuaminisha kwamba, Meru hakuna wafuasi wa vyama vingine ikiwamo CHADEMA?
 
Wachaga na wameru ni tom & jery . Kwahiyo chadema ijue jinsi ya kurusha karata yake .
 
Who are those Washiris, do they have power to prohibit a prrson to get in Meru?
Tendwa ni mtu wa ajabu sana, yaani yeye anaishi Dar, Washiri Arusha, Lema Arusha. Hao Washiri wameshindwa kufikisha ujumbe Arusha hadi wamtume Tendwa !
Wameru ni nuksi ! Hao jamaa wakitumika na magamba hapatatosha ! Watu ambao walikuwa na ujasiri wa kuwafukuza settlers enzi hizo !
 
Haaa ha hhaaa CCM nacho bana; chama kinazeeka vibaya kila uchao ni mawazo ya mwaka wa 47, mwe mpaka huruma vile!!!!!!!

Bahati nzuri zaidi ya 80 % ya wapiga kura Arumeru ni vijana wenye umri kati ya 18 ha 47. Kwa propaganda hizi ubwete CCM wakula ya chuya nakuambieni. Machalii wote wa Arumeru kazi ni
KULA KWA CCM LAKINI KURA KWA CHADEMA.

Mabadiliko ya kweli mbeeele kama tai mpaka kwa Washiri wa mwisho hapo kijijini.
 
Hatuna Waandishi habari makini wa kuwabana muflisi wa kisiasa kama hawa akina Tendwa. Wangembana maswali mazuri Msajili huyu:
-Lema ni nani AruMeru?
-Lema anahusikaje na uchaguzi mdogo wa AruMeru Mashariki?
-Kauli hizi za Washiri Tendwa kazisikia wapi?
-CHADEMA ni Lema tu?
-Mgombea wa CHADEMA atateuliwa na Lema?
Mzee Tendwa aiombe radhi CHADEMA kwa kauli zake za jana.
 
Mkuu WildCard,

WaMeru walikuwa na mgogoro wa makabila mawili waChagga na waArusha migogoro yote ni kwaajili ya maslahi.

WaChagga walikuwa wamewameza waMeru katika dayosisi ya kaskazini KKKT,miradi yote ya kanisa ilijengwa Kilimanjaro eg KCMC,Machame Hospital,Marangu Hospital na nk.WaMeru wakalilia dayosisi yao wakapewa baada ya vurugu kubwa na umwagaji wa damu ni A L Mrema aliyeweza kusuluhisha mgogo huo Mzee A H Mwinyi akamzawadi cheo cha naibu waziri mkuu.

WaArusha walikuwa wamewameza waMeru kisiasa zaidi kabla Arumeru haijagawanywa mara mbili Mashariki na magharibi waMeru hawakuwahi kutoa mbunge kila uchaguzi ukifanyika mbunge mwarusha lazima ashinde nadhani eneo lote la Meru kabla halijagawanywa idadi ya waArusha ni kubwa kuliko waMeru.

WaMeru sasa wana halmashauri yao,mbunge wao na Askofu wao,vyote hivi walivipata kwa kutumia nguvu kubwa kupita kiasi ni watu waliozoea harakati wakitaka jambo lao lazima litimie.Hili CCM wanalijua hili,Madereva wa daladala wanalijua hili ni shida sana kupata usafiri wa daladala kwenda eneo la USA na Tengeru kuanzia saa mbili usiku na kuendelea,ni hatari sana kuharibikiwa na gari muda wa usiku maeneo ya Tengeru,USA hadi kwa Mrefu.

Yaani CHADEMA nao wafanye kama CCM ilivyofanya kwa Nape kule Igunga? Sidhani kama hatua hii inahitajika ingawa nafahamu pia ipo chuki nyingine ya miaka mingi kati ya Wameru na Wachagga ambao wana-share hadi majina. Kuna watu walitaka Dr Slaa aende huko nadhani kwa kutowafahamu Wameru.
Tendwa anafanya kazi isiyo yake. Anajiandaa kwa 2015 akagombee kwao kwa tiketi ya CCM.
 
huwa napata shida sana kumuelewa tendwa...nakumbuka aliwahi kusema kwa kuwa jua linachelewa kuzama kigoma na saa moja na nusu usiku inakuwa bado kuna mwanga basi JK aendelee kupiga kampeni...huyu mzee apimwe akili
 
Mkuu Memo,

Mkuu wangu Arumeru wapo wafuasi wa vyama vya upinzani CDM kikiwemo ukitaka kujua upinzani Arumeru Mashariki ni mkubwa angalia matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2010 Bwana mdogo Nassari alipata kura 29,0000 dhi ya kura 32,0000.

Washiri ni viongozi wa kimila si viongozi wa vyama lakini wanaweza kutumiwa vibaya kama dalili zinavyoonekana.Unajua CCM wakitaka ushindi watatatumia kila zana au umesahau sakata la Hijjab.

Kwahiyo, Washiri hao ni wanaCCM?

Turudi kwenye Hoja, usipindishe,
Tendwa anaona ni sahihi kwa mtu/kundi la watu kumtishia mtu mwingine tena kwa kusema damu itamwagika kwa sababu ya hisia ya kufikiri wametukanwa?

Kwa mujibu wa post nilizozisoma humu, ni kwamba, Lema alionyesha alama ya Vidole viwili (alama inayotumika na CHADEMA, na vyama vingine vya upinzani duniani) wakatuwa mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Meru mashariki. Sijui mazingira yaliyopelekea kufanya hivyo. Lakini naamini kwamba hilo sio tusi kwa yeyote, labda ni tusi kwa wanaCCM.

Anyways. issue ni kwanini kiongozi wa calibre ya juu kabisa kama Tendwa, badala ya kuwaambia vyombo vya usalama walinde na kutoa ulinzi, yeye anasema Lema awaombe Washiri radhi au asiend Meru?

Mkuu kwa badinko lako, unataka kutuaminisha kwamba, Meru hakuna wafuasi wa vyama vingine ikiwamo CHADEMA?
 
Mkuu WildCard,

WaMeru walikuwa na mgogoro wa makabila mawili waChagga na waArusha migogoro yote ni kwaajili ya maslahi.

WaChagga walikuwa wamewameza waMeru katika dayosisi ya kaskazini KKKT,miradi yote ya kanisa ilijengwa Kilimanjaro eg KCMC,Machame Hospital,Marangu Hospital na nk.WaMeru wakalilia dayosisi yao wakapewa baada ya vurugu kubwa na umwagaji wa damu ni A L Mrema aliyeweza kusuluhisha mgogo huo Mzee A H Mwinyi akamzawadi cheo cha naibu waziri mkuu.

WaArusha walikuwa wamewameza waMeru kisiasa zaidi kabla Arumeru haijagawanywa mara mbili Mashariki na magharibi waMeru hawakuwahi kutoa mbunge kila uchaguzi ukifanyika mbunge mwarusha lazima ashinde nadhani eneo lote la Meru kabla halijagawanywa idadi ya waArusha ni kubwa kuliko waMeru.

WaMeru sasa wana halmashauri yao,mbunge wao na Askofu wao,vyote hivi walivipata kwa kutumia nguvu kubwa kupita kiasi ni watu waliozoea harakati wakitaka jambo lao lazima litimie.Hili CCM wanalijua hili,Madereva wa daladala wanalijua hili ni shida sana kupata usafiri wa daladala kwenda eneo la USA na Tengeru kuanzia saa mbili usiku na kuendelea,ni hatari sana kuharibikiwa na gari muda wa usiku maeneo ya Tengeru,USA hadi kwa Mrefu.
Mbowe atakwenda kwenye kampeni hizi? Dr Slaa na Ukatoliki wake je? Siasa za AruMeru ni hasa. Tendwa naye anazidi kuwachafua CHADEMA.
 
Kwa hiyo tendwa badala ya kuwaambia jeshi la polisi kuzidisha ulinzi anashadadia mbunge kutishiwa kuuwawa kwani amefanya kosa gani kubwa kiasi cha kufanya wasiiri hao wasionane na Lema yaishe. Tendwa ni mzushi kwani kushabikia mbunge kuuawa ni sawa na kuchochea mauaji hayo. Kama alivyosema mchangiaji mmoja inatakiwa basi kama kuna watu wametishia kuua kwa vyoyote sheria za nchi haziruhusu na hivyo lazima watuhumiwa wakamatwe na Tendwa akaisadie polisi ili kuepusha vurumai.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wana JF kitendo cha Msajili wa vyama vya siasa Jonn Tendwa kazungumza na Waandishi wa habari na kusema kuwa katika tathimini yake katika uchaguzi wa Arumeru Wazee wa kimila wamemwambia kuwa wanamwonya Lema asiende kwenye kampeni eti watamuuwa kauli hii imenisikitisha kama si kunishangaza kuwa Tanzania kuna tatizo gani?.

Hii bila kumumunya maneneo ni makakati wa ndani wa CCM wa kuandaa mazingira ya vurugu ili ikionekena CCM inashindwa waanzishe vurugu katika kampeni ili watu waumizwe waogope kwenda kupiga kura.

Hili naomba CHADEMA wajiandae mapema . Haingii akilini mtu wa heshima kama msajili wa vyama kuongelea vitu vya vurugu kutoka kwa watu wa kimila waabudu mizimu na wasiomjua Mungu. Nasema hakika haya mnayofanya laana ya Mungu na damu zitakazo mwagika bila hatia itakuwa juu yako na familia yako na vizazi vyako.

Mimi nadhani wazee hawa ilikuwa ni wakati wa kujenga Tanzania yenye amani zaidi kwa kuweka mazingiza ya watu kushindana kwa hoja na kwa amani ili ichi yetu ambayo imepata heshima kubwa iendelee kuwa nchi ya amani.

Tuachane na mawazo mgando kuwa ni lazima nyie muendelee kutawala na kutumia mbinu hata zisizofaa jamani tuamke watu wa aina ya Tendwa ni ukoma kwa Taifa.

Sasa tunapicha inavyokwenda katika ofisi ya Tendwa, Mh Lema ashikwe na mafua sasa hivi Tendwa analo la kuwajibu vijana. Atambue vijana hatuogopi ofisi yake ila tunaiheshimu na yeye anatakiwa kuheshimu. Huu uongozi wa kupeana na kulipana fadhila unamatatizo kweli. Tendwa atajiharibia na uzee wake, Gadaffi angekuwa na sikio la kusikia umauti na kujificha kwenye mtaro ya maji machafu yasingemfika.
 
Back
Top Bottom