Godbless Lema: Kishindo cha wakoma wanne kihusike kuikomboa nchi

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,110
22,563
Salaam, Shalom!!!

Jana, CHADEMA ilikuwa na mkutano wa hadhara na Maneno hayo ameyasema Nabii Lema akiwa Tunduma.

Niliwahi kuandika thread iliyosema,

WAKOMA wageuka mashujaa na kuikomboa nchi- Rabbon.

Kwa ufupi kisa cha wakoma 4 kulikuwa hivi.

Israeli ilipata habari juu ya maadui kuizingira Israel,

Israeli iliamuru Malango ya mji yafungwe Ili kujilinda.

Palikuwa na wakoma 4 ambao walikuwa wametengwa sababu ya ugonjwa wao,

Kwa kuwa njaa ilikuwa Kali sana mjini sababu Malango yalikuwa yamefungwa hakuna chakula kuingia Wala Kutoka. Njaa ilizidi sana, ikafikia time watu walianza kununua mavi ya njiwa na kuyala.

wakoma wakasemezana kwamba, ndugu zetu waisraeli wamejifungia hawatusaidii nasi tunakaribia kufa Kwa njaa.

Kuliko kufa Kwa njaa, ni kheri twende kuomba chakula katika kambi ya Washami.

Wakituua sawa maana tukikaa hapa tutakufa vile vile Kwa njaa. Wakituacha hai yote kheri.

Mungu alionao ujasiri wa wakoma 4, na walipoanza kutembea kuelekea kambi ya Washami maadui wa Israeli, Mungu aliwasikilizisha Washami sauti ya hatua zao na zilisikika kama kishindo kikubwa cha majeshi mengi.

Washami walikimbia wakiamini Israeli imekodi majeshi kuja kuwashambulia, walitimua mbio na kuacha Kila kitu.

wakoma 4 walipofika kambi ya Washami, walishangaa kuona hakuna mtu ila vyakula ,silaha nk nk vipo, na walishangaa zaidi kukuta mavazi ya wanajeshi Washami waliotimua mbio wa mnyama!!

Walipokula na kuteka Mali, pesa na Dhahabu, walirudi kuwaarifu wanajeshi wa Israel waliojifungia Kwa woga Ili watoke kuteka nyara.

Tangu siku Ile, wakoma 4 waliandikwa ktk historia ya mashujaa hadi leo.

Nabii Lema asema, wananchi tuige mfano wa wakoma 4, Mungu atatusaidia.

Kuelekea November, tuungane na Manabii wetu Slaa, Mwabukusi, Madeleka, Mdude, Lissu katika kudai TUME HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Na maandamano hayo ni ya Amani bila kubeba silaha yoyote, maandamano yanayoruhusiwa kikatiba.

Aluta continua.
 
Lema asema, wananchi tukiweka WOGA na HOFU pembeni, halipo litakalotuzuia kuikomboa nchi yetu.
Watanganyika siyo waoga wala hawana hofu bali wanamatarajio hewa ya kupata manufaa binafsi kupitia mfumo uliopo.

Mfano, mtu anayo nafasi ya kuhamasisha wananchi wadai katiba mpya lakini ananyamaza kwa vile anataka kugombea kupitia ccm. Jambo ambalo hawajiulizi ni kuwa hivi akiongoza kura za maoni mbele ya mtoto wa kigogo say Abdul Hafidh ni nani kati yake na Abdul atateuliwa kuwa mgombea wa ccm?
Maana ya huu mfano ni hii:-
Katiba mbovu ya nchi na kukosekana kwa tume huru ya uchaguzi inasababisha wana ccm wanaopendwa na wananchi kuenguliwa kuwapisha maswahiba wa viongozi.
Zamani ilikuwa watu wakienguliwa wanaenda upinzani lakini sasa hivi ccm wana kasumba ya kutoa jina kwa siri tena siku ya mwisho ili kuziba mwanya wa mgombea aliyeongoza kutimkia upinzani.

Hivyo basi kama wewe siyo mtoto wa kigogo, uana ccm wako hauna thamani ikiwa katiba hii inavyoitwa kijitabu tu itaendelea. Watanzania tuungane kudai katiba mpya tuache kuishi kwa matumaini hewa ya uccm.
 
Well said🙏
 
Salaam, Shalom!!!

Jana, CDM ilikuwa na mkutano wa hadhara na Maneno hayo Ameyasema Leo Nabii Lema akiwa Tunduma.

Niliwahi kuandika thread iliyosema,

WAKOMA wageuka MASHUJAA na kuikomboa nchi- Rabbon.

Kwa ufupi kisa Cha WAKOMA 4 kulikuwa hivi.

Israeli ilipata habari juu ya maadui kuizingira Israel,

Israeli iliamuru Malango ya mji yafungwe Ili kujilinda.

Palikuwa na WAKOMA 4 ambao walikuwa wametengwa sababu ya ugonjwa wao,

Kwa kuwa njaa ilikuwa Kali sana mjini sababu Malango yalikuwa yamefungwa hakuna chakula kuingia Wala Kutoka,

Njaa ilizidi sana, ikafikia time watu walianza kununua MAVI ya njiwa na kuyala.

WAKOMA wakasemezana kwamba, ndugu zetu waisraeli wamejifungia ,hawatusaidii nasi tunakaribia kufa Kwa njaa,

Kuliko kufa Kwa njaa, ni kheri twende kuomba chakula katika kambi ya Washami,

Wakituua sawa maana tukikaa hapa tutakufa vile vile Kwa njaa. Wakituacha hai yote kheri.

Mungu alionao ujasiri wa WAKOMA 4, na walipoanza kutembea kuelekea kambi ya Washami maadui wa Israeli, Mungu aliwasikilizisha Washami sauti ya hatua zao na zilisikika kama kishindo kikubwa Cha majeshi mengi.

Washami walikimbia wakiamini Israeli imekodi majeshi kuja kuwashambulia, walitimua mbio na kuacha Kila kitu.

WAKOMA 4 walipofika kambi ya Washami, walishangaa kuona hakuna mtu ila vyakula ,silaha nk nk vipo, na walishangaa zaidi kukuta mavazi ya wanajeshi Washami waliotimua mbio wa mnyama!!

Walipokula na kuteka Mali, pesa na Dhahabu, walirudi kuwaarifu wanajeshi wa Israel waliojifungia Kwa woga Ili watoke kuteka nyara.

Tangu siku Ile, WAKOMA 4 waliandikwa ktk historia ya MASHUJAA Hadi Leo.

Nabii Lema asema, wananchi tuige mfano wa WAKOMA 4, Mungu atatusaidia.

Kuelekea November, tuungane na Manabii wetu Slaa,Mwabukusi Madeleka Mdude, Lisu , katika kudai TUME HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Na maandamano hayo ni ya Amani bila kubeba silaha yoyote, maandamano yanayoruhusiwa kikatiba.

Aluta continua.
LEMA KTK PAGE ZAKE ZA TWITTER NYINGI ANA REPOST ISREAL KUONESHA ANAFURAHIA YANAYOFANYIKA KUULIWA WAISLAM GAZA.
Anaiharibia chadema mwambieni
 
KATIBA ILIYOPO WATANZANIA WANAIFAHAMU KWA KINA KIPENGELE HADI KIPENGELE?, KWA UJUMLA WAKE?, TUISOME KWANZA TUIELEWE VIZURI ILI TUTAKAPOANZA KUITOLEA MAONI TUFAHAMU TUNATAKA WAPI NA WAPI PAREKEBISHWE.
::ALUTA CONTINUA!
 
Lema asema, wananchi tukiweka WOGA na HOFU pembeni, halipo litakalotuzuia kuikomboa nchi yetu.
Ni lini mwananchi amekuwa muoga ?

Mwananchi ndio atajikomboa mwisho wa siku na sio mtu wala mwanasiasa yoyote; tunakoelekea matabaka yanazidi na watu kuzidi kuchakaa na itakapofika watu have nothing to loose ndio hapo patachimbika (ila itakuwa too late na kurudi kwenye reli itachukua karne)

Hayo ya wanasiasa kuwaambia kwamba wananchi ni waoga wakati wao on their part (wanalima, wanachakaa kila siku kutafuta mkate wao wa kila siku na kulipa matozo) hence they are the ones who are making this country move ni matusi ya rejareja.....
 
Lema asema, wananchi tukiweka WOGA na HOFU pembeni, halipo litakalotuzuia kuikomboa nchi yetu.
Huyo mpumbavu asiwadanganye. Yeye ana passport na tiketi ni dakika moja kuwafuata mkewe na wanaye walioko Canada.

Anakuja anawadamganya huku kwa kutumia story za Biblia. Mimi nawashauri ifuatavyo; Kama uko jobless na desperate ingia maandamano hayo ambayo yameandaliwa na watu waliokata tamaa. Mdude, Slaa na Mwabukusi hawana wanachotamani kwenye maisha. Wameshapoteza ladha ya kuishi, kwa hiyo wako tayari lolote litokee kwao.

TAFUTENI HELA VIJANA, acheni UJINGA. Hao WANASIASA WANAWATUMIA KIZEMBE
 
Salaam, Shalom!!!

Jana, CHADEMA ilikuwa na mkutano wa hadhara na Maneno hayo ameyasema Nabii Lema akiwa Tunduma.

Niliwahi kuandika thread iliyosema,

WAKOMA wageuka mashujaa na kuikomboa nchi- Rabbon.

Kwa ufupi kisa cha wakoma 4 kulikuwa hivi.

Israeli ilipata habari juu ya maadui kuizingira Israel,

Israeli iliamuru Malango ya mji yafungwe Ili kujilinda.

Palikuwa na wakoma 4 ambao walikuwa wametengwa sababu ya ugonjwa wao,

Kwa kuwa njaa ilikuwa Kali sana mjini sababu Malango yalikuwa yamefungwa hakuna chakula kuingia Wala Kutoka. Njaa ilizidi sana, ikafikia time watu walianza kununua mavi ya njiwa na kuyala.

wakoma wakasemezana kwamba, ndugu zetu waisraeli wamejifungia hawatusaidii nasi tunakaribia kufa Kwa njaa.

Kuliko kufa Kwa njaa, ni kheri twende kuomba chakula katika kambi ya Washami.

Wakituua sawa maana tukikaa hapa tutakufa vile vile Kwa njaa. Wakituacha hai yote kheri.

Mungu alionao ujasiri wa wakoma 4, na walipoanza kutembea kuelekea kambi ya Washami maadui wa Israeli, Mungu aliwasikilizisha Washami sauti ya hatua zao na zilisikika kama kishindo kikubwa cha majeshi mengi.

Washami walikimbia wakiamini Israeli imekodi majeshi kuja kuwashambulia, walitimua mbio na kuacha Kila kitu.

wakoma 4 walipofika kambi ya Washami, walishangaa kuona hakuna mtu ila vyakula ,silaha nk nk vipo, na walishangaa zaidi kukuta mavazi ya wanajeshi Washami waliotimua mbio wa mnyama!!

Walipokula na kuteka Mali, pesa na Dhahabu, walirudi kuwaarifu wanajeshi wa Israel waliojifungia Kwa woga Ili watoke kuteka nyara.

Tangu siku Ile, wakoma 4 waliandikwa ktk historia ya mashujaa hadi leo.

Nabii Lema asema, wananchi tuige mfano wa wakoma 4, Mungu atatusaidia.

Kuelekea November, tuungane na Manabii wetu Slaa, Mwabukusi Madeleka Mdude, Lissu katika kudai TUME HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Na maandamano hayo ni ya Amani bila kubeba silaha yoyote, maandamano yanayoruhusiwa kikatiba.

Aluta continua.
Upuuzi
 
LEMA KTK PAGE ZAKE ZA TWITTER NYINGI ANA REPOST ISREAL KUONESHA ANAFURAHIA YANAYOFANYIKA KUULIWA WAISLAM GAZA.
Anaiharibia chadema mwambieni
Acha Udini,,, Mbona ninyi mnafurahia waisraeli wanapokufa???Hamna Hata Haya,,kipindi marekani imelipuliwa Hao Watu wako Wengi walifurahi Sana,, Kichwani mmejaa Udini tuuu,,Waombeeni alubadiri waisraeli... Hapo Ndio Akili kuntu Ujue Mungu yupi Ana Nguvu..
 
Kwa hivyo unafurahia Lema kufanya hivyo
 
Huyo mpumbavu asiwadanganye. Yeye ana passport na tiketi ni dakika moja kuwafuata mkewe na wanaye walioko Canada.

Anakuja anawadamganya huku kwa kutumia story za Biblia. Mimi nawashauri ifuatavyo; Kama uko jobless na desperate ingia maandamano hayo ambayo yameandaliwa na watu waliokata tamaa. Mdude, Slaa na Mwabukusi hawana wanachotamani kwenye maisha. Wameshapoteza ladha ya kuishi, kwa hiyo wako tayari lolote litokee kwao.

TAFUTENI HELA VIJANA, acheni UJINGA. Hao WANASIASA WANAWATUMIA KIZEMBE
Ni Kweli kabisa,

Wananchi tupo desperate, hatuna Imani na mfumo uliopo ndo maana tutaungana na manabii wetu Mwabukusi, Madeleka, Lissu, Mdude,Lema na CDM .

Sisi ni sawa tu na WAKOMA, hatuna Cha kupoteza zaidi ya minyororo tuliyofungwa na CCCm!!!
 
Yale maandamano yao ya UKUTA lema aliandamana,? Waanze kwanza kuandamana wao viongozi wa CHADEMA tuwaone
 
Salaam, Shalom!!!

Jana, CHADEMA ilikuwa na mkutano wa hadhara na Maneno hayo ameyasema Nabii Lema akiwa Tunduma.

Niliwahi kuandika thread iliyosema,

WAKOMA wageuka mashujaa na kuikomboa nchi- Rabbon.

Kwa ufupi kisa cha wakoma 4 kulikuwa hivi.

Israeli ilipata habari juu ya maadui kuizingira Israel,

Israeli iliamuru Malango ya mji yafungwe Ili kujilinda.

Palikuwa na wakoma 4 ambao walikuwa wametengwa sababu ya ugonjwa wao,

Kwa kuwa njaa ilikuwa Kali sana mjini sababu Malango yalikuwa yamefungwa hakuna chakula kuingia Wala Kutoka. Njaa ilizidi sana, ikafikia time watu walianza kununua mavi ya njiwa na kuyala.

wakoma wakasemezana kwamba, ndugu zetu waisraeli wamejifungia hawatusaidii nasi tunakaribia kufa Kwa njaa.

Kuliko kufa Kwa njaa, ni kheri twende kuomba chakula katika kambi ya Washami.

Wakituua sawa maana tukikaa hapa tutakufa vile vile Kwa njaa. Wakituacha hai yote kheri.

Mungu alionao ujasiri wa wakoma 4, na walipoanza kutembea kuelekea kambi ya Washami maadui wa Israeli, Mungu aliwasikilizisha Washami sauti ya hatua zao na zilisikika kama kishindo kikubwa cha majeshi mengi.

Washami walikimbia wakiamini Israeli imekodi majeshi kuja kuwashambulia, walitimua mbio na kuacha Kila kitu.

wakoma 4 walipofika kambi ya Washami, walishangaa kuona hakuna mtu ila vyakula ,silaha nk nk vipo, na walishangaa zaidi kukuta mavazi ya wanajeshi Washami waliotimua mbio wa mnyama!!

Walipokula na kuteka Mali, pesa na Dhahabu, walirudi kuwaarifu wanajeshi wa Israel waliojifungia Kwa woga Ili watoke kuteka nyara.

Tangu siku Ile, wakoma 4 waliandikwa ktk historia ya mashujaa hadi leo.

Nabii Lema asema, wananchi tuige mfano wa wakoma 4, Mungu atatusaidia.

Kuelekea November, tuungane na Manabii wetu Slaa, Mwabukusi, Madeleka, Mdude, Lissu katika kudai TUME HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Na maandamano hayo ni ya Amani bila kubeba silaha yoyote, maandamano yanayoruhusiwa kikatiba.

Aluta continua.
Sioni mbowe kwenye hili listi nini maoni yake!
 
Mkoma mwenzetu yakizidi anatimkia Canada na akirudi anasema kazi za vijana ambao wameamua kujitafutia kwa kuendesha bodaboda wanafanya kazi ya laana.
 
Back
Top Bottom