Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

MSAJILI wa Vyama vya Siasa, John Tendwa amemshauri Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuwaomba radhi wazee wa kimila wa kabila la Wameru ‘Washiri’ vinginevyo hali ni mbaya kwake na kundi lake.

Tendwa alisema hayo jana kwa waandishi wa habari wakati akizungumzia mambo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Alisema utovu wa nidhamu alioonesha Lema siku ya maziko ya aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo, Jeremiah Sumari, kiliwakera Washiri na kumtaka asikanyage jimbo hilo wakati wa kampeni.

Alisema yeye alikwenda katika jimbo hilo kuonanana wakuu wa Serikali na taasisi zake kupanga mkakati wa uchaguzi, lakini ghafla alikutana na wazee hao waliosema mbele yake, kuwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini, hawataki kumwona katika kampeni, vingivevyo damu inaweza kumwagika juu yake.

‘’Washiri wamesema hawataki kumwona Lema katika kipindi cha kampeni kwani alileta dharau kubwa na utovu wa nidhamu siku ya maziko ya Sumari, hatua ambayo iliwakera wazee hao … ni busara tu, Lema kwenda kuwaomba radhi wazee hao kama anataka kufanya kampeni ya mgombea wa chama chake- Chadema,” alisema Tendwa. Pia Tendwa amesema Lema asipowaomba radhi huenda damu ikamwagika.

Msajili alivitaka vyama vya siasa kuheshimu mila na desturi za makabila, ili kuepuka umwagaji damu na kushauri kuwa ni vema vyama vya siasa katika kampeni kuzingatia hilo.

Alisema eneo la Arumeru Mashariki ni tete na lenye ushindani mkubwa wa kisiasa na kutokana na hilo, aliwataka wagombea wa vyama vyote na viongozi katika kipindi cha kampeni, kufuata kanuni na sheria za maadili ya uchaguzi tofauti na hapo hali inaweza kuwa mbaya.

‘’Hatutaki uvunjifu wa amani uwepo kwa kupindisha demokrasia na maadili ya uchaguzi,
hivyo kila mgombea anapaswa kuzingatia hilo mara moja na vyama vinapaswa kukubali matokeo na si kuchukua sheria mkononi,” alisema.

Msajili alisema; ‘’ujambazi wa siasa’’ hautaruhusiwa katika kampeni za jimbo hilo kama vile
kupigana risasi na kumwagiana tindikali, kwani ofisi yake kwa kushirikiana na Polisi watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa asilimia 100.

Tendwa alisema matusi, udini, jinsia na kashfa, ni kauli zinazopaswa kuepukwa katika kampeni hizo, kwani zinaweza kuleta madhara makubwa ya umwagaji damu na ni kinyume na maadili ya uchaguzi, lakini viongozi
nao wanapaswa kuziepuka.

Source:Habari Leo

Mazee mengine bwana,yanaacha kushughulika na shughulika wanazostahili kufanya na yamekua majitu ya propaganda ya chama fulani,watu wazima wasio na busara kama hawa hawakuwepo kipindi ch Mwalimu
 
Kuna element za kosa la jinai hapa,Lema fungua kesi ya kutishia kuua kwa maneno ,Tendwa atakuwa shahidi wako mzuri aeleze exactly nani ametoa hivyo vitisho ili sheri ichukue mkondo wake,huu sio wakati wa kitchen or bathroom politics,purely political masturbation by a high profile leader
 
Source: Habari leo.Ingawa chanzo cha habari ni tata lakini ninavyowajuwa Wameru ni watu wa vurugu mtindo mmoja CCM wanaweza kutumia nafasi hiyo kupenyeza sumu ya uasi mara wakigundua maji yako shingoni.Ni vyema CDM wakamwondoa G Lema katika kampeni za Meru vinginevyo watajuta na uenda ukawa mwanzo mbaya wa CDM katika siasa za kanda ya kaskazini.

Ikumbukwe Laigwanani Elowassa atapenda kuonyesha bado ni mwanasiasa muhimu katika eneo la Arusha na Manyara ili ndoto zake za urais mwaka 2015 zizidi kung'aa.Sijui Lema alitamka maneno gani ila ninachojua ni mmoja wa wanasiasa wachovu kupindukia wasiojua ABC ya siasa ni bahati mbaya sana nilitoa taadhari mapema lakini hakuna aliyetaka kusikia au kuamini nilichosema.

G Lema asiende Arumeru kama hawajui wameru angewauliza Rais wa awamu ya pili A H Mwinyi,A L Mrema na Askofu Dr Thomas Laiser na Askofu Dr Erasto Kweka katika mgogoro wa KKKT kanda ya kaskazini.Wameru ni rahisi sana kutumika hasa katika zama hizi ambazo vijana hawana ajira.

Ukishaona mtu anaweka mbona,ingekua,kama hajui awaulize kina fulani,jua huyo mtu ni hasiye na hoja makini na aliyekata tamaha kifikra
 
Kwani uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru ni wakimila ? Tendwa uwe na ufahamu wa kutofautisha,
Serikali na mila za Washiri, ni vitu viwili haviingiliani katika uchaguzi. CDM majukumu yenu katika huo
uchaguzi yawe kama ilivyopangiliwa, Mh. Lema na wahusika wote wa kampeni muwepo jimboni,
msiogope hayo mazingira ya vitisho. Kwani Ccm, hofu imewajaa na ndio maana wanatayarisha njia
ya kuvuruga uchaguzi.
 
Hapa ndipo haja ya katiba mpya inaongezeka. Ona makada wa CCM walivyo katika vyombo vilivyotakiwa kuwa na watu huru.
:canada:
 
Mazee mengine bwana,yanaacha kushughulika na shughulika wanazostahili kufanya na yamekua majitu ya propaganda ya chama fulani,watu wazima wasio na busara kama hawa hawakuwepo kipindi ch Mwalimu

Hivi huyu bwana atastaafu lini?? Au kazi yake ni ya wastaafu kama ya NEC??
 
Source: Habari leo.Ingawa chanzo cha habari ni tata lakini ninavyowajuwa Wameru ni watu wa vurugu mtindo mmoja CCM wanaweza kutumia nafasi hiyo kupenyeza sumu ya uasi mara wakigundua maji yako shingoni.Ni vyema CDM wakamwondoa G Lema katika kampeni za Meru vinginevyo watajuta na uenda ukawa mwanzo mbaya wa CDM katika siasa za kanda ya kaskazini.

Ikumbukwe Laigwanani Elowassa atapenda kuonyesha bado ni mwanasiasa muhimu katika eneo la Arusha na Manyara ili ndoto zake za urais mwaka 2015 zizidi kung'aa.Sijui Lema alitamka maneno gani ila ninachojua ni mmoja wa wanasiasa wachovu kupindukia wasiojua ABC ya siasa ni bahati mbaya sana nilitoa taadhari mapema lakini hakuna aliyetaka kusikia au kuamini nilichosema.

G Lema asiende Arumeru kama hawajui wameru angewauliza Rais wa awamu ya pili A H Mwinyi,A L Mrema na Askofu Dr Thomas Laiser na Askofu Dr Erasto Kweka katika mgogoro wa KKKT kanda ya kaskazini.Wameru ni rahisi sana kutumika hasa katika zama hizi ambazo vijana hawana ajira.
Yaani CHADEMA nao wafanye kama CCM ilivyofanya kwa Nape kule Igunga? Sidhani kama hatua hii inahitajika ingawa nafahamu pia ipo chuki nyingine ya miaka mingi kati ya Wameru na Wachagga ambao wana-share hadi majina. Kuna watu walitaka Dr Slaa aende huko nadhani kwa kutowafahamu Wameru.
Tendwa anafanya kazi isiyo yake. Anajiandaa kwa 2015 akagombee kwao kwa tiketi ya CCM.
 
Mkuu Ibrah,

Washiri ni viongozi wa kimila wa kabila la waMeru ni kama Olaigwanani wa kabila la waMaasai.Washiri wa kabila la waMeru wakitoa maagizo chini mti wa Mringaringa hata kama ni maagizo yanayovunja sheria yatatekelezwa sasa CCM wamebaini maji yapo shingoni wamekuja na mbinu ya kuwatumia washiri mnaweza kuona ni jambo la kijinga lakini nawahakikishia njia ya Moshi Arusha itakuwa haipitiki wengi hapa ni wakizazi cha dot com wengine tunakilometa za kutosha tuna uzoefu kama Tembo jike tuna kumbu kumbu nzuri ya mgogoro wa Meru dayosisi.

Who are those Washiris, do they have power to prohibit a prrson to get in Meru?
Tendwa ni mtu wa ajabu sana, yaani yeye anaishi Dar, Washiri Arusha, Lema Arusha. Hao Washiri wameshindwa kufikisha ujumbe Arusha hadi wamtume Tendwa !
 
Msaada tunaouhitaji Tanzania ni zaidi ya ule unaoweza kupatikana hapa duniani. Kufunga na maombi ni mhimu sana.
 
Tendwa anatakiwa aisaidie polisi kuwataja wazee wa kimila wanaotishia kumuua Lema ili wadhibitiwe mapema!
 
Ni vyema ukisoma kabla ya kuchangia hoja.

Ukishaona mtu anaweka mbona,ingekua,kama hajui awaulize kina fulani,jua huyo mtu ni hasiye na hoja makini na aliyekata tamaha kifikra
 
nashindwa kushangaa, huyu tendwa ni mwandishi wa habari au ni mtu maalum aliyeteuliwa na tume maalum kukusanya maoni na kero za wapigakura?
 
Mkuu Ibrah,

Washiri ni viongozi wa kimila wa kabila la waMeru ni kama Olaigwanani wa kabila la waMaasai.Washiri wa kabila la waMeru wakitoa maagizo chini mti wa Mringaringa hata kama ni maagizo yanayovunja sheria yatatekelezwa sasa CCM wamebaini maji yapo shingoni wamekuja na mbinu ya kuwatumia washiri mnaweza kuona ni jambo la kijinga lakini nawahakikishia njia ya Moshi Arusha itakuwa haipitiki wengi hapa ni wakizazi cha dot com wengine tunakilometa za kutosha tuna uzoefu kama Tembo jike tuna kumbu kumbu nzuri ya mgogoro wa Meru dayosisi.
Na hasa kama Mzee wa siasa katili, Lowasa, atakuwa nyuma ya hawa WASHIRI kwa ajili ya mkwewe.
 
Back
Top Bottom