Mh.Freeman Mbowe wa CDM ndiye huyu ?

Mbowe kajipanga anataka kugombea urais mwaka 2015 alimuachia Dr Slaa, mwaka 2010 akashindwa anataka naye ajaribu tena.
 
Kwa kweli juhudi za kamanda MBOWE zinaonekana wazi huyu ni kiongozi SHUPAVU na si mchumia tumbo kikubwa zaidi hapendi umaarufu wa wazi wazi kama wanavyofanya wengine.
Give me a break!!!!alipouzia chama magari mabovu anaprove ni kiongozi shupavu na si mchumia tumbo??acheni kumwagia sifa wakti anamapungufu kibao nyuma ya pazia!!!
 
unataka kumsahau mwalimu kwasababu ya mbowe. unadhani mbowe akitawala hii nchi miaka 23 ataondoka maskini kama nyerere.

mmmmmmm kiongozi...kiukweli kumfikia yule mzee kwa kizazi hiki itachukua karne nyingi sana au haiuwezekani kabisa
 
Ubunifu wake umewafanya waTZ wengi kutambua haki na wajibu wao ktk taifa lao
 
Ni kitambo toka afahamike kama mtu machachari na anayejiamini na msimamo endelevu kwa manufaa ya wengi


Hakika ni wachache wenye ujasiri huu, au kuishi ndani ya siasa bila kuchuja kwa muda mrefu kama alivyo kamanda huyu.


Mh. huyu kwa sasa ameanza kugusa wengi hususani wazee na vikongwe ambo awali walikua waogopa upinzani hususani baada ya kujiimarisha katika kutoa hoja na kuzitetea kwa kujieleza kwa umahiri mkuu.


Kaka Mbowe kwa sasa anaonekana kuwa ameiva katika kufikisha ujumbe kwa makundi mbalimbali...hu ndio uongozi kaka yangu.


Nimekufuatilia toka january mwaka huu hadi sasa...kwa kweli umenikosha kwa staili yako nzuri ya siasa na uwezo wakuteka mass... heko kwa hili


Lamsingi hapa tunamwomba Mh. awaelekeze baadhi ya makamanda wa juu yuu ya umuhimu wa siasa zipendwazo ambazo kwa kweli hapa CHADEMA wanasimama kama wanaharakati wa Taifa hili changa ila lililozeeka kwa ukosefu wa ubunifu wa maendeleo ya kweli.

Kuna aliyevuliwa ubunge kule kaskazini, anaonekana kuwa bado na siasa zenye madoa kidogo lamsingi hapa awateke vijana au sijui ni kwamba ni nia ya Chama kujaribu kuteka watu wa kada mbalimbali kwa wasifu mbalimbali.


Je hapo alipo pametosha au tusubiri mengi mazuri toka kwake ktk elimu ya M4C?



Bravo HQ Leaders.......peoplesssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssss''''sssssssssssssssssssss'

....acha kumsifia DJ wewe anachumia tumbo lake, kauzia chama magari mabovu tena kwa bei kubwa,tz sio madagascar
 
Mnamshabikia mpiga Disco kweli nyinyi ni wachovu khaa

pole rafiki, mcheza disco anafahamika hata kwa mtoto mdogo wa kijijini kwani kazi zake za msingi zimemshinda totally, amebaki kuwa wa matamasha, safari za nje na ku-assasinate watu (good eg. Dr Uli)
 
Laiti ingelikuwa amri yangu ningependekeza Mbowe awe Mkiti wa kudumu huku Dr Slaa awe Katibu mkuu wa kudumu...........

Kwahiyo unataka turudi kwenye zidumu fikira sahihi za Mwenyekiti? Wapo wanamageuzi wengi tu ambao wanaweza kufanya kama Dr. Slaa na Mbowe au hata zaidi yao.


Inatosha tu kuwapongeza na kuwatakia kila la heri kwa mapambano ya mageuzi wanayoendeleza sasa lakini kamwe siyo kuwa na fikira finyu kama hizi za kufikiria mwenyekiti au katibu wa kudumu.

Tena mimi nawashauri wanatakiwa waandae successor wazuri watakaoendeleza mapambano haya hata pindi wao watakapoondoka madarakani. Chama ni cha wanachama na siyo cha watu wawili.
 
Laiti ingelikuwa amri yangu ningependekeza Mbowe awe Mkiti wa kudumu huku Dr Slaa awe Katibu mkuu wa kudumu........

Umechemka wewe! Hao ni binadamu, utafika muda watazeeka na watakufa tu, uongozi wao wa kudumu itakuwaje? Wacha ushabiki dogo.

Ukweli ni kwamba viongozi hawa wako makini sana katika shughuli za CDM.
 
Give me a break!!!!alipouzia chama magari mabovu anaprove ni kiongozi shupavu na si mchumia tumbo??acheni kumwagia sifa wakti anamapungufu kibao nyuma ya pazia!!!......

Hii ya kuuzia chama magari mabovu ni upotoshaji wa makusudi uliofanywa na akina Zitto. Hayo magari Freeman aliyanunua kwa hela yake mwenyewe wakati chama kilikuwa hakina uwezo kifedha.

Yametumika na chama wakati wote na yanaendelea kutumiwa na chama. Hayakumwingizia fedha zozote kibiashara na chama kilipokuwa na uwezo wa kuyalipia akashauri kiyanunue.

What is wrong with that? Freeman na mzee Ndesamburo wametumia fedha zao binafsi kukisaidia na kukinyanyua chama. Hata pick up aliyotumia Zitto kwenye kampeni yake ya kwanza alipewa na Freeman. Sasa hii dhana ya magari mabovu mmeitoa wapi?
 
Mbowe kupitia chama chake anatambua matatizo mengi ya watanzania. Amefanikiwa kuwaunganisha viongozi mbali mbali wenye dhamira kama yake chini ya mwavuli wa CDM. Mafanikio ya vuguvugu la mabadiliko Tanzania limetokana na kujitolea kwake. CDM inafanikiwa kwa sababu ya uongozi wake makini,
 
Kiukweli tukiacha ushabiki Mbowe ni kiongozi hasa, nakumbuka ile juzi wakiwa pale Serena kuchangisha hela za M4C, aliporekebisha kauli ya Kamanda Lema alivyosema lines zote za mitandao watazitupa chooni kama wakihujumiwa, Mbowe akaja baadae akasema wanaamini kuwa ni matatizo tu ya mitandao hivyo wananchi waendelee kujaribu. Ukweli jamaa namkubali hasa, namna tu anavyojinyenyekeza huwezi amini kama ni mtu aliyekulia kwenye utajiri toka utotoni, tumwombee afya njema na asije akakutana na peop mbaya, kwani wakati mwingine wanansiasas huwa hawatabiriki
 
nilimsifia sana siku ile ya M4C dsm, wakati Lema akiongea kama mtoto mdogo kwa kutoa vitisho na maneno machafu, yeye alikuja kutuliza na kuongea kama mtu mzima...safi sana.
 
Mnamshabikia mpiga Disco kweli nyinyi ni wachovu khaa
Heri ya mpiga Disco aliyeliinua disco lako from the root level mpaka katika international level kuliko mchumi ambaye tangu amalize kuusoma hakuwahi kuufanyia kazi na hata sasa baada ya kupwa kiongozi mkubwa kabisa hata hajui namna ya ku apply taaluma yake ili kuijenge nchi.
 
Back
Top Bottom