Mguu kutetemeka unapopunguza speed

mwambyetete

Senior Member
May 17, 2018
126
196
Hello ndugunina tatizo nahitaji mnisaidie,

Nna Gari yangu Toyota premio ambapo imekuwa ikitetemesha mguu unapopunguza mwendo hasa ukiwa kuanzia speed 60
Tatizo hili limedumu kwa miez miwili sasa. Awali fund aliikagua ambapo alinishaur kubadili habu zote za mbele na kuzichonga upya router disk na kubadili break pads za mbele zote!


Tatizo liliisha but baada ya siku kama tano nilihisi tatizo kuwepo bado! Hivyo niliiamua kununua route disk zingine ambazo n used Japan! Jana nikitokea ubungo kwenye mteremko Wa kujia Jangwan nilikimbia speed 80 nilipojaribu kupunguza mwendo huo mtetemo huo ulinitikisa had usukan ulitikisika kama awali!

Hivyo bas naomba mnisaidie nin cha kufanya au ni wap naweza pata fund mwaminifu ambae atanisaidia hili tatizo maana linanyima raha na kuniingiza gharama kila siku Mara kununua pads mpya Mara kuuziwa pads mbovu!! Kila MTU na ushaur wake!
Naamin ntapata msaada juu ya hili.

Niko Dar es Salaam kigamboni!

Nawashukuru saaana kwa mtakaonishaur!! Mtakao nitania sawa tu kikubwa nipate msaada!
 
Inawezekana ni roto au vinginevyo humu tutapiga tu story majibu kila mtu na yake njoo PM nikuelekeze tuicheki hiyo mashine kama upo dar
 
Inawezekana ni roto au vinginevyo humu tutapiga tu story majibu kila mtu na yake njoo PM nikuelekeze tuicheki hiyo mashine kama upo dar
Najaribu kukutext pm inagoma!! Nashukuru kwa msaada!! Kama unaweza nitext contact zako pm ili nikutafute
 
Ulivyonunua route disk ulibadilisha na pads? Kama ulitumia pads zile zile za zamani inawezekana zimetengeneza matuta ambayo hayaonekani kwa macho kutoka kwenye zile route mbovu, na kama haukuweka pads mpya na hzo route hata kama mpya zitaambukizwa ugonjwa kutoka kwenye hizo pads za zamani, jaribu kufungu kila kitu kipya kwa siku moja kwa ushauri wangu..
 
Sijajua huo mtetemo ni mkubwa kiasi gani ila ninachojua kwa gari zenye mfumo wa ABS huwa huo mtetemo ni wa kawaida hasa pale unapotaka kusimama ghafla kama ulikuwa kwenye speidi kubwa au kama unashuka kwenye mteremko mkali unaweza kuhisi mtetemo kwenye pedal ya break...hapo inamaana mfumo wa ABS una...unlock breaking system za break zisijilock na kupelekea matairi kuburuzika..
Ila kama mtetemo ni mkali zaidi waone wataalamu.

Ila hapo ni mfumo wa ABS unapambana na mfumo wa break ili matairi yasijilock.

Mafundi wasioelewa gari za kisasa watakushauri wadisconnect mfumo wa ABS na tatizo litakwisha ila tegemea gari kutokusimama kwa umbali uliokadiria kwa sababu matairi yataburuzika hasa kama lami imelowa
 
kwa uzoefu wangu drum limetanuka ndani yani kama mawimbi so brake ikikamata sehem inakaza sehemu inalegeza kwasabu ina rotating ndo maana una feel vibration
 
Hata mm yangu ilikuwa inazngua hvyhvyo..nilichofanya nilibadili kila kitu ikiwemo shock absorver..sasa hv nateleza kama kawa
 
Sijajua huo mtetemo ni mkubwa kiasi gani ila ninachojua kwa gari zenye mfumo wa ABS huwa huo mtetemo ni wa kawaida hasa pale unapotaka kusimama ghafla kama ulikuwa kwenye speidi kubwa au kama unashuka kwenye mteremko mkali unaweza kuhisi mtetemo kwenye pedal ya break...
Tatizo hilo lilinikuta nikiwa na IST kumbe Fundi wakati anabadili bearing aliiumiza shanga ya ABS, (ABS ROTOR) hebu kagua zots kama ziko sawa, kama zina madhara badili, moja ya dalili ya hii ni kwamba break fruid hujaa ghafla tofaut na level yake ya awali.
 
Hata mm yangu ilikuwa inazngua hvyhvyo..nilichofanya nilibadili kila kitu ikiwemo shock absorver..sasa hv nateleza kama kawa
kama kiasi gani cha pesa iliku-cost bro.
Sasa hivi najitahidi kupitia nyuzi za magari nijifunze vitu. Niache kupigwa na mafundi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom