Mgomo wa Madaktari leo

Mbeya Referal, KCMC, bugando, Ifakara, Dodoma, kote watu wameweka tools down.
Ni balaa.
 
Kama mahakama inajukumu la kuweka usawa baina ya pande zinazo pingana mbona kwa hili ni kinyume?. Mahakama inatoa amri ya kuwa hakuna kugoma na mazungumzo hakuna yalikwishavunjika. So hawa wakimbilie wapi na kesi huwa zinachukua hata miaka 7 bila kutolewa hukumu. Huu ni Ubabe ambao ni dhahiri hauhitaji hadubini kuweza kuubaini! Mzee usiyekuwa na aibu unayepelekwa kama kondoo asiyejua anakwenda wapi haya unayajua ndo maana unawaambia waende mahakamani coz unajua by the time kesi inakwisha utakuwa tayari umeshaaga kwenye siasa{siyo kwa mapenzi yako}.Lakini hakika jamaa watakutafuta. Hili mmelikanyaga litamtafuna mmoja baada ya mwingine!!!!!!
 
Watz tutaendelea kuumia na kupoteza ndugu zetu mpaka lini? Ni wakati wetu sasa kuwa kitu kimoja na kuingia barabarani kudai haki yetu kwanini serikali inashindwa kututimizia angali kodi tunalipa, tukiendelea kuumia sisi wakati wao wakienda kutibiwa india? Tujue tu sisi wananchi ndio tuna kauli ya mwisho sasa kama mahakama ndiyo ilikuwa tegemeo letu ila kwasasa nayo imetawaliwa na siasa na usawa umekuwa haupatikani tena pale badala yake imekuwa na chombo cha kumkandamiza mnyonge kwa manufaa ya wachache wanaotunyonya kwa garama yoyote
 
I can't believe this. Even experimental animals can't be treated like this. It is shocking,,where is our country headings!
 
Hivi hawaoni aibu jamani sekta nyeti mara ya 3 wanagoma serikali haijali kwa nini hawamalizani nao?walikimbilia ikulu kufanya nini??au kusafiri?
 
Back
Top Bottom