Mgomo Umemalizika Rasmi!. Jee Bado Kuna Umuhimu Rais Kukutana na Wazee wa Darisalama?!.

Haya tumekusikia nenda kachape kazi jenga taifa..
Acha kulaumu JK kila siku, do your part...
Mdrs wameshaelewa walikuwa wamelewa wameelewesha wameelewa..
Nchi hii ina watu mil.40, matatizo lukuku toka enzi ya st. nyerere..
chapeni kazi no easy ride...mshahara na maslahi ni mchakato..go and tell them
Hakuna lawama ni ukweli usiohitaji fikra kuwa Rais Kikwete ameshindwa uongozi hadi kufikia watu kupoteza maisha. Ni facts!

Huwezi kujenga taifa ukiwa umelala au ndugu amelala kitandani kwa maradhi.
Matatizo yapo na haionekani kama tunajifunza. Kikwete hajajifunza. Mgomo wa kwanza alikuwa waziri katika serikali ya Mkapa. Hakujifunza lolote, wananchi wanakufa anapaa kwenda Dovos.

Kama niliyoyaandika ni lawama, onyesha wapi namlaumu na si kumwambia ukweli.
Damu ya wananchi itabaki mikononi mwake na legacy yake ni kushindwa kuliongoz taifa! period
 
Ni washauri ndo wanafanya kazi sa hivi maana so siri hali ni mbaya kiutawala ndo mana amekuwa anachelea kusema anahisi kila jambo anakosea
 
Hakuna lawama ni ukweli usiohitaji fikra kuwa Rais Kikwete ameshindwa uongozi hadi kufikia watu kupoteza maisha. Ni facts!

Huwezi kujenga taifa ukiwa umelala au ndugu amelala kitandani kwa maadhi.
Matatizo yapo na haionekani kama tunajifunza. Kikwete hajajifunza. Mgomo wa kwanza alikuwa waziri katika serikali ya Mkapa. Hakujifunza lolote, wananchi wanakufa anapaa kwenda Dovos.

Kama niliyoyaandika ni lawama, onyesha wapi namlaumu na si kumwambia ukweli.
Damu ya wananchi itabaki mikononi mwake na legacy yake ni kushindwa kuliongoz taifa! period

Haya tumeshakusikia wewe pekee ndio huwa unasema ukweli a.k.a facts

Hivi wewe na mwenzako mwanakijiji tutegeme mseme JK ameweza maweeeeeeeeeee (sawa ameshindwa)

Haya nendeni mkachape kazi, mshahara na maslahi ni mchakato nchi ni ina majalala ya matatizo tangu enzi ya st. nyerere...

Tumewasikia tutaendelea kuyafanyia kazi kadri uwezo wa serikali utakavyo ruhusu...
 
Of course ameweza hili halina shaka. Ameweza kuwalazimisha madaktari warudi kazini swali ni kwanini hakuweza siku ya kwanza ya mgomo mwezi Januari au wiki mbili baadaye; kwanini amekuja "kuweza" siku ya tatu ya mgomo wa pili? Of course, majibu ya haya kwako ni irrelevant kwa sababu yatakulazimisha kusema usichotaka kusema.
 
HIli itabidi tuzidi kulionesha kwa sababu kama aliweza kukaa nao kwa masaa machachef na wakasitisha mgomo kilichomfanya ashindwe kufanya hivyo kwa wiki mbili za mwanzo za mgomo ni nini? Kama mgomo umeweza kumalizwa na Rais kwanini haukuweza kuzuiliwa toka mwanzo na Rais? tena hadi mgomo wa pili unaanza kwa siku tatu halafu wapo wanataka tuimbe "hongera Kikwete, hongera Kikwete"?
Pengine kwa kuona ukweli ndiyo maana wenzetu wanataka tuanze na nderemo na vifijo ili kuziba mwanya wa kuonyesha ni jinsi gani tatizo limeathiri jamii, na je kulikuwa na ulazima wa haya yote kutokea!

Watu hawataki kuonyesha udhaifu wa kiongozi wetu kwani utazidi kushadidia udhaifu alio nao.
Tutaendelea na kujitathmini bila kumuonea au kumhurumia mtu.

Tutapigaje vigelele, nderemo na vifijo wakati tumepoteza ndugu zetu kwa jambo la kizembe kama hili.
Tupige makofi na hoi hoi kwa masaa 3 aliyokaa na Madktari ili tusahau mwezi mzima wa hofu, majonzi na simanzi vilivyotusibu!

Tutandelee kutathmini yaliyojiri na kauli mbiu yetu ' Tumkumbushe Kikwete mikono yake ina damu za Wananchi'.
 
Kwa mfano kipi nisichotaka kusema?
 
Mimi naona spinning zenu hazikufanikiwa kwani mdrs wanaendelea kufanya kazi na kuokoa maisha ya wananchi..kwani mlipenda wananchi wafe eti na support mgomoooo..

Yaani nyie ni wale watu ambao kama mtu unatofautiana naye kiitikadi basi "unaomba aharibikiwe hata kama gharama zake ni kufa watu"..

Sasa spinning zimefika mwisho nendeni kachapeni kazi .."narudia mshahara na maslahi ni mchakato" nchi hii ina watu mili.40 ina matatizo mengi tangu enzi za st. nyerere..

tutafanya kile tu kilichopo ndani ya uwezo wa serikali..no easy ride...maweeee.
 
Mkuu Pasco,nianze na hii kauli yako baada ya kufuatilia majadiliano. Kwa hili, Rais Kikwete hastahili pongezi au huruma kabisa. Nitafafanua kwanini hastahili pongezi lakini kwanza nashindwa kuelewa kwa hakika unasimamia wapi.

Umeandika mgomo umekwisha na watu wawe kitu kimoja hakuna mshindi au aliyeshindwa. Naendelea kukusoma ukisema mgomo umekwisha 'unconditional' na umerudia mara nyingi sana. Ukifuatilia thread zako za nyuma na hasa zile zilizosema' watakiona cha mtema kuni' n.k. napata taabu kukubali kuwa hakuna ushabiki na je tumebaki watu wamoja bila kuwa na loser or winner na kama unasimamia ulichoandika au una chagiza ushabiki!

Kuhusu Kikwete, unafahamu kuwa Rais ana mamlaka makubwa sana juu ya usalama wa raia. Ni yeye peke yake anayeweza kutengua au kuidhinisha adhabu kama ya kifo. Ni rais ambaye ni mtumishi namba 1, mwajiri wa watumishi wa umma na mwajiriwa wa wananchi. Hakuna nafasi ya Rais kufanya uzembe au kosa linalogharimu maisha ya watu halafu tukampongeza. Kuna msemo unasema 'The buck stops with him'

Nikupe mfano, Marekani kulikuwa na mgonjwa katika mashine'life support' ambaye madaktari walisema hawezi kuishi bila mashine na hawana la kufanya. Mgogoro kati ya mumewe na wanafamilia wa mgonjwa ulikuwa ni je mashine itolewe au isitolewe? Kesi ilienda mahakama kuu ya Marekani hadi senate na hata Rais (Bush) kwani maamuzi ya senate alipaswa ayatie saini ili yawe sheria. Wakati senate ikiwa na kikao cha dharura Rais Bush alikatiza mapunziko yake kutoka Ranchi yake Mexico na kurudi Ikulu akisubiri kutia saini ya mgogoro wa mgonjwa mmoja ambao haukuwa wa dharura.

Kwa mfano huo tu wa uwajibikaji wa marais wa wenzetu, na nguvu kubwa aliyonayo Rais wetu hata ya kuamua hatima ya maisha ya mtu, inasikitisha sana kuona hakuweza kushughulikia tatizo hilo kwa kiwango cha Urais, mwajiri na mwajiriwa wa wananchi. Mgogoro unaohusisha hospitali kubwa za rufaa ulitosha kumrudisha nyumbani hata kama alikuwa katika hotuba UN. Kwa bahati mbaya maumivu ya mgomo yatabaki kwa waathirika na nchi isiyo na takwimu kama yetu tutabaki kuamini hakuna madhara, ukweli ni kuwa mamia na maelfu ya watu wamedhurika sana.

Kuna mwenzetu hapa JF kama walivyowengine alipoteza mtoto mikononi na hadi kumlazimu kuzunguka na mtoto wake aliyepoteza maisha mikononi.

Kuna wagonjwa wameletwa kwa rufaa na nduguz zao hawapo Dar ambao wamekutwa na mauti bila 'dignity'.
Kuna watu wapo katika madeni makubwa ya hospitali za binafsi kutokana na mgomo.
Watu wote hao wanaposikia kuna wenzetu wanampongeza Rais na si kumutuhumu ni kuwaongezea machungu yasiyo ya lazima.

Tatizo hili lilipaswa liingiliwe kati na Rais kwa maamuzi yoyote yaleharaka sana, hakufanya hivyo na kuacha akina Pinda wakiwa hawana la kufanya au kutojua wafanye nini.

Hapa kuna mapungufu makubwa ya uongozi (lack of leadership) na kumpongeza ni kuimarisha na kutukuza uzembe kwa gharama za Watanzani. Jambo hili halihitaji political score point hata kidogo.

Mkuu Pasco, Rais JM Kikwete, hakushauri kwa ufasaha, hakutumia weledi kama mzazi na kiongozi, hakutumia uzoefu kama kiongozi alioupata mgomo wa mwanzo na hakuwajibika katika kushughulikia mgogoro huu kama kiongozi wa taifa.

Ni wazi amekosa sifa za uongozi hata kama angefanya kikao na malaika.
Hakumaliza mgogoro kwa kufuata kanuni na misingi ya uongozi. Hakulinda mali na maisha ya Watanzaniakama katiba inavyomtaka.

Haihitaji kupongezwa bali kukumbushwa kuwa mikono yake imjeaa damu ya Raia wasio na hatia.
Mkuu Nguruvi3, mimi ni father of 6!. Watoto wakiwa wengi hugombana mara kwa mara, kuna wakubwa 3 na wadogo watatu, sasa hawa wadogo kila wakileta fujo, mama yao anawatetea na kuwazua wale wakubwa wasiwaadhibu as a result hawa wadogo wanakuwa viburi. Dawa ya kuondoa viburi vyao ni kuwaacha wapigane huku baba na mama mnaangalia, yule kiburi mdogo ataendelea kuleta kiburi kwa sababu anajua mama yuko upande wake, anapozidi kupokea mkong'oto huku mama anashudia ndipo sasa atajenga heshima kwa wakubwa zake maana sasa kajua atashikishwa adabu mama awepo au asiwepo inakuwa sasa ni heshima na adabu!.

Sometimes hata ukiwaona watoto wanagombana, sometimes ni vizuri kuwaacha bila kuwaingilia waumizane kidogo wataacha wenyewe na wataheshiniana!. JK kama baba mwenye busara, aliacha na ulipofika wakati muafaka ndipo ameingilia kati na kumaliza mambo!.

JK ni baba, Pinda na Mponda ni mama katika familia moja na wale madaktari ni watoto wa familia hiyo!.

Baba unasafari ya kikazi (Davos) wakati unajiandaa kutoka unawaona watoto waleta fujo (mgomo wa mwanzo), utaahirisha safari wakati mama yupo tena na Anti wao?. Wewe utaendelea na safari, mama (P) kwanza anamtuma anti wao (Dr. Mp) aliposhindwa akawaita wakagoma, akatishia kuwaadhibu wasipokuja na mwisho akaamua kuwafuata huko huko chumbani na kuwambeleza kuacha fujo, wakaacha!. Baba ukapokea taarifa watoto wametulia!. Kosa la baba liko wapi?. Si alimwachia mama nyumba na karudi kakuta salama?.

Baada ya muda watoto wale wale wakaanzisha tena fujo, safari hii wakitaka anti wao afukuzwe pale nyumbani, mama akawatuliza wakagoma ndipo baba ukawaita na kuwakanya kuwa waache fujo, na wewe ndio utaamua hatma ya anti wao kwa wakati wako, hapo wewe kama baba, si utakuwa umetimiza wajibu wako?.

Kwenye huu mgogoro wa madaktari ulipoibuka JK alimwachia Pinda akamaliza!, ulipoibuka tena Pinda hakusikikuzwa ndipo JK akaingilia mwenyewe, kosa lake liko wapi?.

Hawa madaktari wanaotumia human shield kwa kuzitumia roho na damu ya poor innocent Tanzanians kama bakora ya kuichapia serikali kushinikiza madai yao
pale mwanzo serikali ikawapigia magoti ndipo sasa wakaota pembe na kutoa amri kwa mkuu wa nchi!. Walichokipata ni kipi?.

Anyway kwa vile mgomo umekwisha, tusitafute mchawi, winner wala looser wasije tuchoma sindano za sumu!. Kesho tumsikilize mkuu wetu wa nchi atupe mwekekeo tusonge mbele!.
 
Mimi naona spinning zenu hazikufanikiwa kwani mdrs wanaendelea kufanya kazi na kuokoa maisha ya wananchi..kwani mlipenda wananchi wafe eti na support mgomoooo..

Yaani nyie ni wale watu ambao kama mtu unatofautiana naye kiitikadi basi "unaomba aharibikiwe hata kama gharama zake ni kufa watu"...
Je wale waliofariki nani abebe lawama za kushindwa kuokoa maisha yao.
Hakuna anayeomba Kikwete aharibikiwe, yeye mwenyewe na udhaifu uliokithiri wa uongozi ndio unamharibia.

Hatuna jema la kusema kwani hakufanya lolote jema kuokoa maisha ya watu.
Kikwete ameshindwa kama kiongozi mwenye washauri na vyombo vyote vya umma.
Ameshindwa kujifunza kama waziri wakati tatizo lilipojitokeza enzi za Mkapa
Ameshindwa kufikiria machungu ya maradhi kama mzazi, baba na Babu
Ameshindwa kusoma machungu ya anaowaongoza wakati wa shida na dharura

Kwenye tatizo kubwa kama hili hakupaswa kupanda ndege na kuzunguka zunguka damu za wananchi zikimwagika

Hana jinsi bali kuiangalia mikono yake iliyotapakaa damu za wananchi wasio na hatia.
 
..Huwa najiuliza hivi pale Ikulu kuna nini, "nna mashaka pale Getini kuna kitu kimewekwa ukiingia tu kutaka kuonana na Baba Riz unalainika". Walianza Chadema na issue ya Katiba wakalainika, leo hii na Madaktari wamelainika.
Kuna nini Ikulu.

...Juice
 
Je wale waliofariki nani abebe lawama za kushindwa kuokoa maisha yao.
Hakuna anayeomba Kikwete aharibikiwe, yeye mwenyewe na udhaifu uliokithiri wa uongozi ndio unamharibia.

Hatuna jema la kusema kwani hakufanya lolote jema kuokoa maisha ya watu.
Kikwete ameshindwa kama kiongozi mwenye washauri na vyombo vyote vya umma.
Ameshindwa kujifunza kama waziri wakati tatizo lilipojitokeza enzi za Mkapa
Ameshindwa kufikiria machungu ya maradhi kama mzazi, baba na Babu
Ameshindwa kusoma machungu ya anaowaongoza wakati wa shida na dharura

Kwenye tatizo kubwa kama hili hakupaswa kupanda ndege na kuzunguka zunguka damu za wananchi zikimwagika

Hana jinsi bali kuiangalia mikono yake iliyotapakaa damu za wananchi wasio na hatia.

Naona unajifurahisha nilishasema JK hategemei wala haitatokea wewe na wenye akili kama zako (in fact tunajua mnawakilisha kina nani, siyo siri tena) aweze..hata kama kama akifanikiwa mtafanya spinning..

Ameweza st. nyerere pekee au siyo?
 
HIli itabidi tuzidi kulionesha kwa sababu kama aliweza kukaa nao kwa masaa machachef na wakasitisha mgomo kilichomfanya ashindwe kufanya hivyo kwa wiki mbili za mwanzo za mgomo ni nini? Kama mgomo umeweza kumalizwa na Rais kwanini haukuweza kuzuiliwa toka mwanzo na Rais? tena hadi mgomo wa pili unaanza kwa siku tatu halafu wapo wanataka tuimbe "hongera Kikwete, hongera Kikwete"?
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Mkuu Nguruvi3, and the like, with due respect, ombi langu kwenu, kwenye hii issue ya mgomo wa madaktari, tuachane na "dhana" twende kwenye "reality", ya ukweli halisi!.

Mimi nimekuwa biker, miaka yangu yote wakati wife na kids wana drive magari!. Na kwa vile nilikuwa na driver big bike, sipakizi mtu kwa sababu ni hatari, na pia sipakizwi na mtu kwa sababu nahisi anayenipakiza is not a 'perfect driver", dereva makini ni mimi tuu!. Hata sasa naendeshwa na wife kwenye gari yake, mimi niliyekaa siti ya abiria ndio kila mara nakanyaga breki (empty) kuzuia ajali, kwa vile namuona wife kama sio dereva makini!.

Vivyo hivyo kwa wapenzi wa mpira, japo wao ni watazamaji tuu, hujidhania ndio wachezaji bora, hivyo hupiga wao mipira kufunga mabao kimoyomoyo kila kunapotokea chance golini na goli lisipoingia, husikitika na kuwish, ningekuwa mimi, ningepiga shuti kali na kuingiza goli!.

Katika mgomo huu wa madaktari, nyinyi ndio wale madereva makini, ambao ukiendeshwa na mwingine, unakosa amani, na katika ile mechi, nyinyi ndio hao watazamaji wanaofunga magoli kwa macho, hiyo ndiyo "dhana" ninayoisemea mimi, ni tofauti na game halisi yenyewe, sasa wachezaji ndio wanaojua reality ya hiyo game, sasa nawaombeni tusiliendeleze hili suala kwa "dhana", twendeni kwenye reality, mgomo umekwisha, tusonge mbele!.

Hizo lawama kwa JK kuwa alipaswa kufanya hiki na kile kabla, yeye afanye mangapi?, hao wasaidizi wake kina Mponda, kina Pinda, kazi yao ni nini?. Si amewaachia kazi, wamefanya walichoweza, walipofika mwisho wao si ndio yeye ameingilia kati na kumaliza kila kitu!. Mlitaka anaanze yeye, hao wengine wangefanya nini?!.

Nyinyi wote si mna nyumba zenu?, hivi kila kesi ingeletwa kwa baba, mngeamua mangapi?!. Nyumbani si kuna baba na mama, na dada na watoto?. Hivi ni baba huamua kila kitu, au yale makubwa kabisa ndio huletwa kwa Baba?!.

Tangu ule mgomo wa mwanzo, nilisuggest wangefukuziwa mbali na kuwashikisha adabu!. Ingekuwa enzi za Nyerere, hata viboko wangelambwa!. Pinda akatishia nyau na baadae kwenda kuwalamba miguu ndio akawapa bichwa!. Walipogoma mara ya pili kwa conditions, nilitamani sio tuu wafutwe kazi, bali wapelekwe keko waka ... debe, na baadae kupandishwa kizimbani kwa murder case kuwa liable kwa kila kifo kilichotokana na mgomo batili ambao sio halali!.

Bahati nzuri JK akaingiahuruma, utu na busara zikatawala, akawaita pale Ikulu na kuwabembeleza!, hili nalo jamani tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, hili sio jema?!. Aliyeumaliza huu mgomo ni nani haswa?, ni madaktari kwa ridhaa yao, au baada ya kuitwa ikulu?. Si wameumaliza mgomo wao kwa heshima ya Mkuu wa nchi?, hili nalo jamani ni baya?!. Mliunga mkono madaktari wagome, watakaokufa na wafe!, leo madaktari wamemaliza mgomo, wale wakufa hawafi, jamani hili sii jambo jema la kupongezwa kwa kumaliza mgomo?.

Kwenye ile mada yangu ya kuandaa vipindi vya TV nilishauri, wana JF wenzangu, tumezidi mno kulalamika!. Kila kukicha sisi ni kubeza tuu hili na lile, hivi kweli hakuna jema lolote la kusifiwa?!. Nawaombeni sasa tutoke kwenye stage ya kulalamika tuu, twende hatua moja mbele ya kutenda!. Kwenye mada yangu ya mazuri ya Kikwete, nilishauri, tuwe na appreciation ya zuri lolote no matter ni dogo kiasi gani!, kwenye mazuri tusifu, na mabayo tubonde!. Kwa jinsi JK alivyoumaliza huu mgomo, ni jambo la kustahili pongezi!. Kwenye mada yangu ya mabaya ya JK, nilishauri tukosoe kwa nia ya kujenga, kuonyesha kama hili ni baya, jee tufanye nini kupata zuri?.

Siku zote tunasisitiza, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, tukifanyiwa mabaya, tunalalamika, hata tukifanyiwa mema pia bado tunalalamika?!. Hivi tunataka tufanyiwe nini?. Nilisema humu JF tuna mabingwa wa ukosoaji, njooni basi nyumbani, tuingie kwenye game, tuonyeshe kwa vitendo kuwa tunaweza, tusikalie maneno maneno na kulalamika tuu!. Mwenzetu mmoja, Mkuu William ameonyesha njia, baada ya kupiga sana kelele humu,ameona kelele pekee hazitoshi, amepiga hatua moja mbele kwa kuamua kuja kuona hali halisi na labda kujitathmini kama atumbukize mguu au laa, hii ni action! Tufuate nyayo zake tuingie ground zero tufanye mambo!. Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3 na wakosoaji wengine humu, sasa tuache kuicheza hii ngoma kwa kusikilizia kwa mbali, sasa njooni nyumbani, tuingie uwanjani tuicheze hii ngoma kiukweli na sio kuendeleza hadithi za jinsi sisi tunavyojua kucheza ngoma huku tukiwalaumu walio ngomani kuwa hawajui!. Ukitaka kuujua utamu wa ngoma, uingie ucheze!.
 
Mkuu Nguruvi3, mimi ni father of 6!. Watoto wakiwa wengi hugombana mara kwa mara, kuna wakubwa 3 na wadogo watatu, sasa hawa wadogo kila wakileta fujo, mama yao anawatetea na kuwazua wale wakubwa wasiwaadhibu as a result hawa wadogo wanakuwa viburi. Dawa ya kuondoa viburi vyao ni kuwaacha wapigane huku baba na mama mnaangalia, yule kiburi mdogo ataendelea kuleta kiburi kwa sababu anajua mama yuko upande wake, anapozidi kupokea mkong'oto huku mama anashudia ndipo sasa atajenga heshima kwa wakubwa zake maana sasa kajua atashikishwa adabu mama awepo au asiwepo inakuwa sasa ni heshima na adabu!.

Sometimes hata ukiwaona watoto wanagombana, sometimes ni vizuri kuwaacha bila kuwaingilia waumizane kidogo wataacha wenyewe na wataheshiniana!. JK kama baba mwenye busara, aliacha na ulipofika wakati muafaka ndipo ameingilia kati na kumaliza mambo!.

JK ni baba, Pinda na Mponda ni mama katika familia moja na wale madaktari ni watoto wa familia hiyo!.

Baba unasafari ya kikazi (Davos) wakati unajiandaa kutoka unawaona watoto waleta fujo (mgomo wa mwanzo), utaahirisha safari wakati mama yupo tena na Anti wao?. Wewe utaendelea na safari, mama (P) kwanza anamtuma anti wao (Dr. Mp) aliposhindwa akawaita wakagoma, akatishia kuwaadhibu wasipokuja na mwisho akaamua kuwafuata huko huko chumbani na kuwambeleza kuacha fujo, wakaacha!. Baba ukapokea taarifa watoto wametulia!. Kosa la baba liko wapi?. Si alimwachia mama nyumba na karudi kakuta salama?.

Baada ya muda watoto wale wale wakaanzisha tena fujo, safari hii wakitaka anti wao afukuzwe pale nyumbani, mama akawatuliza wakagoma ndipo baba ukawaita na kuwakanya kuwa waache fujo, na wewe ndio utaamua hatma ya anti wao kwa wakati wako, hapo wewe kama baba, si utakuwa umetimiza wajibu wako?.

Kwenye huu mgogoro wa madaktari ulipoibuka JK alimwachia Pinda akamaliza!, ulipoibuka tena Pinda hakusikikuzwa ndipo JK akaingilia mwenyewe, kosa lake liko wapi?.

Hawa madaktari wanaotumia human shield kwa kuzitumia roho na damu ya poor innocent Tanzanians kama bakora ya kuichapia serikali kushinikiza madai yao
pale mwanzo serikali ikawapigia magoti ndipo sasa wakaota pembe na kutoa amri kwa mkuu wa nchi!. Walichokipata ni kipi?.

Anyway kwa vile mgomo umekwisha, tusitafute mchawi, winner wala looser wasije tuchoma sindano za sumu!. Kesho tumsikilize mkuu wetu wa nchi atupe mwekekeo tusonge mbele!.
Pasco naona umezidi ushabiki,jk ndio kawaita ikulu mwenyewe wala hatujui waliongea nini,wewe nakufananisha na wale watu walioshangilia jk kusaini mswada wa mabadiliko ya katiba wakifikiri chadema wamekomoleka ila baadae unajua nini kilichofuata
 
Naona unajifurahisha nilishasema JK hategemei wala haitatokea wewe na wenye akili kama zako (in fact tunajua mnawakilisha kina nani, siyo siri tena) aweze..hata kama kama akifanikiwa mtafanya spinning..
Ameweza st. nyerere pekee au siyo?
Ni miaka 13 tangu Nyerere afariki, miaka 26 tangu aache madaraka, hakuna lolote linalomhusu kwa hili. Unachotaka ni kutumbukiza mada za Mwl ili kuvuruga hii mada.
Unadhani ya kuwa masuala muhimu kama haya utaweza kutumbukiza chembe za imani ili kuvuruga ukweli.
Hutatuondoa katika ukweli na mada iliyopo mbele yetu ni Kikwete, mdahifu na sasa amejaa damu viganjani

Mtanzania wa kawaida kabisa aliguswa toka siku ya mwanzo ya mgomo.
Mazungumzo vijiweni na kwenye majumba ni hatima ya maisha yao.
Hofu ikiwatanda na kila kukicha heri ya jana. Licha ya kupigika kutokana na inflation iliyofikia 20%.watu wakajikuta wana mzigo mwingine wa kukimbia huko na huko kuokoa maisha ya wapendwa wao.

Wengine bahati mbaya wakajikuta katika misiba, hata kama ni kazi ya mwenyezi mungu lakini kumuona nduguyo anakata roho bila msaada inasikitisha na kuhuzunisha.

Rais Mrisho Jakaya Kikwete akiwa na vyombo vya dola vinavyompa taarifa juu ya hali ya nchi hakuweza kufanya lolote. Akaawachi akina Blandina Nyoni washughulikie yeye akiwa katika mikutano huku na huko. Muda huo watu wanafariki

Hata aliporejea hakutoa kauli au kuwasiliana na umma uliokuwa umejaa hofu juu ya hatima yao na familia zao.
Tukamsikia akiwa Arusha ili hali akijua kuwa Waziri mkuu Pinda ameshindwa kutafuta suluhu.

Ni Kikwete ambaye kwa fikra za kawaida tu ilibidi awaambie mawaziri wake waliohusika wajiuzulu kwani hakukuwa na kuaminiana kati yao na Madaktari. Kunapotekea vifo visivyokusudiwa ilikuwa ni wajibu wa waziri husika kujiuzulu au kuwajibishwa. Rais akaamini kuwa wale walioshindwa kufikia maafikiano wangeweza kuleta mabadiliko mengine.
Mgogoro ukaibuka mara ya pili.

Baada ya maafa na madhara makubwa ndipo akaamua kutafuta huruma za wazee wa jiji. Kabla hajafanya hivyo akawaita madaktari na kukaa nao kwa masaa 4 na kuwa na muafaka.

Kikwete angeweza kukaa nao kabla hajaenda Dovos, au aliporudi kama si kwenda Arusha. Hakufanya hivyo.
Yeye kama waziri wa siku nyingi alipaswa kuona ukubwa wa tatizo kuliko kiongozi mwingine.
Hakuliona hilo alichokiona ni safari. Yeye kama Baba, Babu na mzazi hakutakiwa kufundishwa nini maana ya ulezi na familia. Halioni hilo.

Utaratibu huu ndiyo legacy yake. Rais Kikwete hapendi kumuudhi mtu iliaonekana mzuri hata kama ni kwa gharama ya maisha ya watu. Sioni kwanini Haji Mponda aendelee kuwa waziri na naibu wake huku wakiwa wametapakaa damu zilizomchafua rais. Hii inaongeza ukubwa wa damu alizobeba na hakika yeye kama Mwanadamu, Rais, Baba, Babu, Mume ni lazima akae chini na kuiangalia mikono yake kwasababu sisi wananchi tunaiona imejaa damu.

Tusione aibu kumkumbusha Mheshimiwa rais, mikono yake imejaaa damu. Na ni makosa tukimsifia kwa uzembe uliogharimu maisha ya watu. Rais ni lazima asome hali ya jamii yake. Hakupaswa kusubiri Pinda na Blandina wanaleta hadithi gani.

Ninasema kwa uchungu sana, hili Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameshindwa kulihudumia taifa kama alivyoshindwa mambo lukuki.
Alipowasamehe wahalifu na kuwazawadia ustaafu tumevumilia tukijua miaka 4 itakwaisha.

Hili la maisha yetu na watu wasio na hatia, hivi kweli si tutakuwa wendawazimu tukimpigia makofi, nderemo, vifijo ! Kwa kitu gani chema alichofanya zaidi ya damu viganjani mwake. Ataishi nalo na kila tukimuona tunaona suti halafu viganja vina rangi nyekundu.
 
Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3 na wakosoaji wengine humu, sasa tuache kuicheza hii ngoma kwa kusikilizia kwa mbali, sasa njooni nyumbani, tuingie uwanjani tuicheze hii ngoma kiukweli na sio kuendeleza hadithi za jinsi sisi tunavyojua kucheza ngoma huku tukiwalaumu walio ngomani kuwa hawajui!. Ukitaka kuujua utamu wa ngoma, uingie ucheze!.

Hili ndio kosa kubwa unalolifanya; kuwepo nyumbani siyo sababu ya kukufanya ufikirie ni bora zaidi na hivyo una haki zaidi ya kusema masuala ya nyumbani. Mtanzania yeyote, popote anayo haki sawa ya kuzungumzia nchi yake bila kuomba kibali kwa yeyote. Aneyetaka kurudi nyumbani anafanya haki kwani ni nyumbani, anayeamua kwenda nje ya nchi hanyang'anywi haki ya kutolea maoni mambo ya Tanzania!

Kuna mambo mengi makubwa na mazito tumeyafanya sisi tulio nje yanchi na wakati mwingine mwingi kwa kushirikiana na wale walioko nyumbani lakini hatujidai hata kidogo kuwa kwa mchango wetu basi kumetupa "utanzania" bora zaidi. Wewe kama unataka kufanya makubwa yafanye tu mahali popote ulipo wala usijione duni wala kuwaona wengine duni.
 
mbona hawaeleweki. tumemaliza mgomo unconditional. hapo hapo wanasema hawana imani na waziri na naibu wake na wala hawatawapa ushirikiano. maana yake ni nini?
 
JK ni baba, Pinda na Mponda ni mama katika familia moja na wale madaktari ni watoto wa familia hiyo!.

Baba unasafari ya kikazi (Davos) wakati unajiandaa kutoka unawaona watoto waleta fujo (mgomo wa mwanzo), utaahirisha safari wakati mama yupo tena na Anti wao?. Wewe utaendelea na safari, mama (P) kwanza anamtuma anti wao (Dr. Mp) aliposhindwa akawaita wakagoma, akatishia kuwaadhibu wasipokuja na mwisho akaamua kuwafuata huko huko chumbani na kuwambeleza kuacha fujo, wakaacha!. Baba ukapokea taarifa watoto wametulia!. Kosa la baba liko wapi?. Si alimwachia mama nyumba na karudi kakuta salama?.

Baada ya muda watoto wale wale wakaanzisha tena fujo, safari hii wakitaka anti wao afukuzwe pale nyumbani, mama akawatuliza wakagoma ndipo baba ukawaita na kuwakanya kuwa waache fujo, na wewe ndio utaamua hatma ya anti wao kwa wakati wako, hapo wewe kama baba, si utakuwa umetimiza wajibu wako?.

Kwenye huu mgogoro wa madaktari ulipoibuka JK alimwachia Pinda akamaliza!, ulipoibuka tena Pinda hakusikikuzwa ndipo JK akaingilia mwenyewe, kosa lake liko wapi?.

Hawa madaktari wanaotumia human shield kwa kuzitumia roho na damu ya poor innocent Tanzanians kama bakora ya kuichapia serikali kushinikiza madai yao
pale mwanzo serikali ikawapigia magoti ndipo sasa wakaota pembe na kutoa amri kwa mkuu wa nchi!. Walichokipata ni kipi?.

Anyway kwa vile mgomo umekwisha, tusitafute mchawi, winner wala looser wasije tuchoma sindano za sumu!. Kesho tumsikilize mkuu wetu wa nchi atupe mwekekeo tusonge mbele!.

Mfano (analogy) yako ya Rais kama baba na raia kama watoto ni miongoni mwa mifano mibaya kabisa kutumiwa kuonesha uhusiano kati ya rais na raia wake katika nchi iya kidemokrasia ambapo rais hupita na kuomba kura za raia. Mawazo haya ni ya hatari kwa sababu yanamfanya raia awe na hisia (affinity) ya ukaribu wa kumuona rais kama baba yake na hivyo hata kujisikia vibaya kumkosoa au kuonesha mapungufu yake. Matokeo yake ni kuwa vyombo vya habari - ambavyo ni jicho la raia kwa watawala - inabidi viwe vinafumba fumba macho kumhusu "baba" yao kwa sababu wanajisikia vibaya kumkosoa au kuonesha mapungufu yake.

Rais wa nchi kama ya kwetu siyo kama baba na hapaswi kutazamwa kama baba; rais ni mtumishi na mwajiriwa wa wananchi. Wakati anapita kuomba kura mara mbili RAis Kikwete hakuwa anaombwa kuwa "mzazi" wa Watanzania au kuwa kama baba kwao; alikuwa anaomba ajira ambayo sisi wananchi tulikuwa na hiari ya kumkubalia au kumkatalia. Hakuna mtu ambaye amewahi kuombwa kibali cha kuwa mtoto mbele ya baba yake mzazi! Mzazi na mtoto hakuna demokrasia! Rais basi anatakiwa kuangaliwa kama mtumishi wa kwanza kabisa wa juu nchini na ambaye anapaswa kusimamiwa na wananchi wake.

Ukishaondoa mtazamo huu wa kumuona Kikwete kama baba yako na kumuona kama mtumishi wako hautapata shida hata kidogo kumuona kuwa amefeli katika kushughulikia mgomo wa madaktari. Angeweza kabisa kuzuia lakini hakufanya hivyo. Hili ni doa kubwa kabisa na linafanana na lile la Geoge Bush na Hurricane Katrina au Barak Obama na Big Spill.
 
Hili ndio kosa kubwa unalolifanya; kuwepo nyumbani siyo sababu ya kukufanya ufikirie ni bora zaidi na hivyo una haki zaidi ya kusema masuala ya nyumbani. Mtanzania yeyote, popote anayo haki sawa ya kuzungumzia nchi yake bila kuomba kibali kwa yeyote. Aneyetaka kurudi nyumbani anafanya haki kwani ni nyumbani, anayeamua kwenda nje ya nchi hanyang'anywi haki ya kutolea maoni mambo ya Tanzania!

Kuna mambo mengi makubwa na mazito tumeyafanya sisi tulio nje yanchi na wakati mwingine mwingi kwa kushirikiana na wale walioko nyumbani lakini hatujidai hata kidogo kuwa kwa mchango wetu basi kumetupa "utanzania" bora zaidi. Wewe kama unataka kufanya makubwa yafanye tu mahali popote ulipo wala usijione duni wala kuwaona wengine duni.
Sorry!
 
Mfano (analogy) yako ya Rais kama baba na raia kama watoto ni miongoni mwa mifano mibaya kabisa kutumiwa kuonesha uhusiano kati ya rais na raia wake katika nchi iya kidemokrasia ambapo rais hupita na kuomba kura za raia. Mawazo haya ni ya hatari kwa sababu yanamfanya raia awe na hisia (affinity) ya ukaribu wa kumuona rais kama baba yake na hivyo hata kujisikia vibaya kumkosoa au kuonesha mapungufu yake. Matokeo yake ni kuwa vyombo vya habari - ambavyo ni jicho la raia kwa watawala - inabidi viwe vinafumba fumba macho kumhusu "baba" yao kwa sababu wanajisikia vibaya kumkosoa au kuonesha mapungufu yake.

Rais wa nchi kama ya kwetu siyo kama baba na hapaswi kutazamwa kama baba; rais ni mtumishi na mwajiriwa wa wananchi. Wakati anapita kuomba kura mara mbili RAis Kikwete hakuwa anaombwa kuwa "mzazi" wa Watanzania au kuwa kama baba kwao; alikuwa anaomba ajira ambayo sisi wananchi tulikuwa na hiari ya kumkubalia au kumkatalia. Hakuna mtu ambaye amewahi kuombwa kibali cha kuwa mtoto mbele ya baba yake mzazi! Mzazi na mtoto hakuna demokrasia! Rais basi anatakiwa kuangaliwa kama mtumishi wa kwanza kabisa wa juu nchini na ambaye anapaswa kusimamiwa na wananchi wake.

Ukishaondoa mtazamo huu wa kumuona Kikwete kama baba yako na kumuona kama mtumishi wako hautapata shida hata kidogo kumuona kuwa amefeli katika kushughulikia mgomo wa madaktari. Angeweza kabisa kuzuia lakini hakufanya hivyo. Hili ni doa kubwa kabisa na linafanana na lile la Geoge Bush na Hurricane Katrina au Barak Obama na Big Spill.
Mzee Mwanakijiji, kwenye hili, nakiri udhaifu, ila bado nasimama kwenye hoja yangu ya tupuguze "dhana", twende kwenye "reality", rais ndio kila kitu!. Rais ni mwenzetu pale tuu anapoomba kura, ndio maana tumemuona mpaka anapiga magoti, anakaa chini kwenye nyasi, vumbi, only when begging for votes!. Baada ya kuchaguliwa, yeye sio mwenzetu tena!.

Siku Chadema wanamgomea pale bungeni Dodoma, nilikuwepo, na sitaki kurudia alichowaambia, ila ukimuondoa Mungu Baba, na wazazi wetu, yaani Baba na Mama zetu, rais ndio kila kitu kinachofuata, huu ndio ukweli halisi in plain reality, hiyo ya rais kuwa ni mtumishi wetu, sisi ndio tumemuajiri, anapaswa kututumikia tunavyotaka sisi, vinginevyo tunaweza kumfuta kibarua, ni "dhana" tuu!.

Naomba tusirudi kwenye mjadala kati ya "what is" vs "ought to be", mimi nasimama kwenye "is" ambao ndio ukweli halisi, wakati "ought to be", ni ukweli ulivyokuwa supposed to be!.
 
Afadhali madokta wamemaliza huo mgomo wao. Nilijua tu yaani JK ashiriki kumaliza migogoro ya Kenya na Zanzibar pamoja na ule ww Mauritania wakati akiwa Mwenyekiti wa AU halafu leo ashindwe kumaliza mgogoro wa madaktari. Ilikuwa haiingii akilini.

Mgomo umeisha, madokta fanyeni kazi kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya.

Ni muhimu Rais akutane na wazee aongelee sakata zima la mgomo hadi alipoingilia jana na kuumaliza kidiplomasia.
Siamini kabisa kama hilo linawezekana!
 
Back
Top Bottom