Mgomo Umemalizika Rasmi!. Jee Bado Kuna Umuhimu Rais Kukutana na Wazee wa Darisalama?!.

..Huwa najiuliza hivi pale Ikulu kuna nini, "nna mashaka pale Getini kuna kitu kimewekwa ukiingia tu kutaka kuonana na Baba Riz unalainika". Walianza Chadema na issue ya Katiba wakalainika, leo hii na Madaktari wamelainika.
Kuna nini Ikulu.
Weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!! tena acha kabisa, CHDM noma waliruka hiyo mizizi hapo getini wewe hukuona JK anafanya kitu ambacho sidhani kama kuna rais yeyote aliwahi kufanya, kusaini muswada kuwa sheria tena kwa mbwembwe kisha kuurudisha bungeni kwa marekebisha hata kabla haijatumika na kisha kusema aliogopa shinikizo la wabunge wa CCM ( alisaini kuwafurahisha wana CCM)
 
Madaktari rudini kazini na msubiri JK atekeleze yale aliyoahidi,lakini lawama zote anazibeba yeye kama ameweza kuwaita Madaktari alishindwaje kuongea nao mapema? Hao wazee wangejua wasingejitokeza kwan huyo JK ndo mdhulumu wao kwa mambo yao ya East Afrika,nawaambia watalala sana barabarani,na wenyewe wafanye mgomo wakuongea nae ili waonyeshe msisitizo wa madai yao ya East Afrika
 
Pasco.. you missed ujumbe mzima wa MAT; soma tamko lao. Wamesema kwa ufupi wanaweza kulazimishwa kurudi kazini lakini hawawezi kulazimishwa kufanya kazi na kuwa hawatoa ushirikiano wowote kwa Nkya na Mponda. Well THOSE CONDITIONS STILL REMAIN. Na wameenda mbali na kutangaza hao kuwa ni maadui wa sekta ya afya. In other words wamekubali kufa defiantly! K

Hao watu wawili hawawezi kuendelea kuwemo kwenye baraza la mawaziri. Na Kikwete atazungumza na wazee j'tatu na akifanya mabadiliko yoyote ya baaraza la mawaziri Mponda na Nkya wataondolewa ndio utaona ushindi wa hoja ya madaktari. Kwangu, nimewaheshimu zaidi madaktari baada ya tamko lao.
Mkuu MMM na Mkuu Pasco nadhani kati ya serikali na madokta hakuna mshindi. Watu wakikaa katika majadiliano huwa hakuna mshimdi kunakuwa na makubaliano ya pande zote mbili: give and take. Dhana ya ushindi ni kwamba mmoja huchukua kila kitu; katika vita mshindi huchukua nyara.

Kama kuna mshindi hapa basi ni wale wagonjwa waliokuwa mahospitalini wakiugulia bila kupata huduma za madaktari ila baada ya makubaliano kati ya serikali na madaktari basi hao wagonjwa watapata huduma.
 
Yaani, kwa jinsi alivyofanya inaonesha kabisa kuwa hajui kupima mambo kwa uzito unaostahili. Kama alikuwa na uwezo wa kukaa na madaktari na kumaliza within hours, kilimshinda nini Januari nzima na Februari nzima? Binafsi naamini anastahili kubebeshwa lawama za moja kwa moja; kwani, kama alikuwa na uwezo wa kulazimisha madaktari kurudi kazini kwa kuwaita Ikulu kitu gani kilimzuia kufanya hivyo the first time wametangaza nia ya mgomo na kusababisha watu wadhurike wakati yeye anpeperuka kama kipepeo?

Mkuu MMM ile dhana ya kwamba Rais JK ni mzuri (mchapakazi) lakini anaangushwa na wasaidizi wake unaisemeaje katika muktadha huu ambapo inaonekana wasaidizi wake wameshindwa kutatua tatizo kwa wiki kadhaa lakini yeye amefanikiwa kutatua tatizo kwa masaa sita tu aliyokaa na madaktari?
 
Well, haiwezekani kuwalaumu wasaidizi wake kwani ni yeye ndio anawateua na yeye anaweza kuwawajibisha. Sasa ni mara ngapi atalalamikia wasaidizi wake? Waziri Mkuu hawezi kumwajibisha waziri yeyote sasa inakuwaje Rais anamuacha waziri mkuu kushuhughulikia jambo asilokuwa na uwezo nalo? WM Pinda hakuweza kumwajibisha Mponda wala Nkya sasa ni kweli ameshindwa?

Ingekuwa ni wasaidizi wake tungeona watu wanawajibishwa mbele kwa mbele lakini so far hakuna anayewajibishwa! The buck stop with the president. Ndicho nilichoandika wakati ule kuhusu tepidity ya Rais. HIvi kama angeweza kuahirisha safari ya Davos kwa masaa machache kushughulikia mgogoro wa madaktari isingeweza kuzuia mgomo kuendelea kama alivyofanya jana?
 
Mimi sikuunga mkono mgomo wa kwanza wa madaktari na de facto na huu wa pili sikuunga mkono. Ila kuna kitu kimenishangaza zaidi kwenye huu mgomo wa pili: hivi nani aliwashauri madaktari wampe ultimatum mtu ambaye hawajawahi kukaa naye mezani kwenye majidiliano? Mimi nilitegemea madaktari kwanza wangeomba kukutana na Rais wamweleza kumkataa kwao waziri na naibu wake face to face, then kutokana na responce yake ndio wangekuja na reaction. Sasa wao wamereact mahali ambapo hakukuwa na action! Utampaje Rais taarifa ya kutaka atengue uteuzi wake kwa kupitia vyommbo vya habari? Je, viongozi wa mgomo walimuandikia Rais barua ya kumtaka afukuze kazi mawaziri? Rais hafanyi kazi kwa kutumiaa vyombo vya habari. Mimi nadhani madaktari wakubali tu kuwa hawakupata ushauri unaotosheleza kujenga hoja madhubuti na kwamba utatuzi wa kweli utapatikana iwapo watajikaza "kiume" na kufuatilia madai yao hatua kwa hatua, haya mambo ya ultimatum no no no...

Ninachoweza kusema kwa sasa ni kwamba madaktari wameniaibisha sana.

Swala la kuongea na wazee wa Dar es Salaam linapaswa liendelee kuwepo ingawa mazungumzo yao sio lazima yawe public.
 
Ukitaka kujua madhara la ombwe la uongozi katika Tanzania angalia mgomo wa madaktari. Chimbuko lake, ulivyoshughulikuiwa na wizara, Waziri mkuu na hatimaye makuu wa nchi. Je huu uongozi utaleta kasi ya maendeleo kama wananchi wanavyotarajia?
 
..Huwa najiuliza hivi pale Ikulu kuna nini, "nna mashaka pale Getini kuna kitu kimewekwa ukiingia tu kutaka kuonana na Baba Riz unalainika". Walianza Chadema na issue ya Katiba wakalainika, leo hii na Madaktari wamelainika.
Kuna nini Ikulu.

.."Ikulu ni mahali patakatifu"...Mwl. JKN
 
Sidhani kama kuna umuhimu. Wazee hawana jipya ni kuwasumbua tu na kuwapotezea muda wa kunywa gahawa tu. Huwezi kuleta mabadiliko ya kweli kwa kutumia wazee. Zamani ilikuwa inawezekana kwani mfumo wa kupata taarifa ulikuwa duni na ulitegemea vikao vya nyumbani baada ya msosi wa usiku. Leo tuna teknolojia kila kitu kipo wazi
 
Wamerudi bila madai yao mapya ya Mponda na Nkya kuwachishwa kazi, walisema hawarudi kazini mpaka hao waachishwe kazi. Kwa hiyo wamerudi "unconditional".

Wamesema wamekualiana na Kikwete kuwa madai yao atayashughulikia madai yao kwa uzito unaostahili kwa hiyo inawezekana uzito huo atauchukua jumatatu mbele ya hao wanaoitwa wazee wa Dar ikiwa ni pamoja nakuwawajibisha mawaziri hao
 
Madaktari wameitikisa nchi, serikali, ccm, baba mwanaasha n.k VIMETIKISIKA!Na wanaodhan limeisha wasubir utekelezaj kama wa kipumbav wa jk KINAANZA UPYA ZAID!Msiogope kufa kwa kuukumbatia umaskin n upumbav
 
Well, haiwezekani kuwalaumu wasaidizi wake kwani ni yeye ndio anawateua na yeye anaweza kuwawajibisha. Sasa ni mara ngapi atalalamikia wasaidizi wake? Waziri Mkuu hawezi kumwajibisha waziri yeyote sasa inakuwaje Rais anamuacha waziri mkuu kushuhughulikia jambo asilokuwa na uwezo nalo? WM Pinda hakuweza kumwajibisha Mponda wala Nkya sasa ni kweli ameshindwa?

Ingekuwa ni wasaidizi wake tungeona watu wanawajibishwa mbele kwa mbele lakini so far hakuna anayewajibishwa! The buck stop with the president. Ndicho nilichoandika wakati ule kuhusu tepidity ya Rais. HIvi kama angeweza kuahirisha safari ya Davos kwa masaa machache kushughulikia mgogoro wa madaktari isingeweza kuzuia mgomo kuendelea kama alivyofanya jana?
Mkuu kwa jinsi mambo yalivyoenda huoni kuna kitu kinataka kuwa justified hapo?
 
..Huwa najiuliza hivi pale Ikulu kuna nini, "nna mashaka pale Getini kuna kitu kimewekwa ukiingia tu kutaka kuonana na Baba Riz unalainika". Walianza Chadema na issue ya Katiba wakalainika, leo hii na Madaktari wamelainika.
Kuna nini Ikulu.

Hakuna chochote getini zaidi ya kuwa ikulu ina nguvu ya nchi nzima, ni rahisi unapoitwa pale na Rais kuongelea hoja husika, kuweza kulegeza msimamo, isitoshe kuitwa ikulu kwa maana yangu naona ni heshima ya pekee ambayo mwananchi anaweza kuipata, kwahiyo ulegevu unakuwa mwepesi zaidi kuliko huko mitaani donbosco, starlight au kwengineko. Ni maoni tu.
 
Madaktari baada ya kuongea na Pinda kimsingi walikubaliana kuacha mgomo kwasababu madai yao ya msingi yalikubaliwa na kuwa yatashugulikiwa, lakini kwa condition ya kuwatoa waziri na naibu wake

JK alipo ongea nao alichofanya ni kuwafanya warudi kazini bila ya condition yao ya kutaka Mponda na Nkya waondolewe kwanza
Ni vizuri tukumbuke pia kiini cha mgomo huu wa pili ilikuwa ni condition yao ya kutimuliwaa Mponda na Nkya kwanza ndio warudi kazini

Ndio maana Pasco anasema unconditional
 
Well, haiwezekani kuwalaumu wasaidizi wake kwani ni yeye ndio anawateua na yeye anaweza kuwawajibisha. Sasa ni mara ngapi atalalamikia wasaidizi wake? Waziri Mkuu hawezi kumwajibisha waziri yeyote sasa inakuwaje Rais anamuacha waziri mkuu kushuhughulikia jambo asilokuwa na uwezo nalo? WM Pinda hakuweza kumwajibisha Mponda wala Nkya sasa ni kweli ameshindwa?

Ingekuwa ni wasaidizi wake tungeona watu wanawajibishwa mbele kwa mbele lakini so far hakuna anayewajibishwa! The buck stop with the president. Ndicho nilichoandika wakati ule kuhusu tepidity ya Rais. HIvi kama angeweza kuahirisha safari ya Davos kwa masaa machache kushughulikia mgogoro wa madaktari isingeweza kuzuia mgomo kuendelea kama alivyofanya jana?

Tatizo lako tangu padre mwenzako aangushwe umekosa objectivity kwenye kila JAMBO linalomhusu JK lazima utafanya spinning ionekana JK amekosea..lol

Subiri 2015 mkuu acha ulokole uliopitiliza..Pinda kama ameshindwa si angepeleka ripot kwa mkubwa wake ..pinda ni zigo lisilo na maana amewekwa kwa maomba maalum ya pengo period..baada ya kulalamika kwamba wakatoliki wameachwa oh...ops
 
Mwanzo alijuwa safarini Davos, akamwachia Pinda akamaliza kila kitu. Mara ya pili alikuwa akipanda mlima Kilimanjaro, amerejea Ikulu, kawakaribisha chai, kamaliza kila kitu!. Kwa hili la madaktari, tukubali tukatae JK anastahili pongezi!.
Mkuu Pasco,nianze na hii kauli yako baada ya kufuatilia majadiliano. Kwa hili, Rais Kikwete hastahili pongezi au huruma kabisa. Nitafafanua kwanini hastahili pongezi lakini kwanza nashindwa kuelewa kwa hakika unasimamia wapi.

Umeandika mgomo umekwisha na watu wawe kitu kimoja hakuna mshindi au aliyeshindwa. Naendelea kukusoma ukisema mgomo umekwisha 'unconditional' na umerudia mara nyingi sana. Ukifuatilia thread zako za nyuma na hasa zile zilizosema' watakiona cha mtema kuni' n.k. napata taabu kukubali kuwa hakuna ushabiki na je tumebaki watu wamoja bila kuwa na loser or winner na kama unasimamia ulichoandika au una chagiza ushabiki!

Kuhusu Kikwete, unafahamu kuwa Rais ana mamlaka makubwa sana juu ya usalama wa raia. Ni yeye peke yake anayeweza kutengua au kuidhinisha adhabu kama ya kifo. Ni rais ambaye ni mtumishi namba 1, mwajiri wa watumishi wa umma na mwajiriwa wa wananchi. Hakuna nafasi ya Rais kufanya uzembe au kosa linalogharimu maisha ya watu halafu tukampongeza. Kuna msemo unasema 'The buck stops with him'

Nikupe mfano, Marekani kulikuwa na mgonjwa katika mashine'life support' ambaye madaktari walisema hawezi kuishi bila mashine na hawana la kufanya. Mgogoro kati ya mumewe na wanafamilia wa mgonjwa ulikuwa ni je mashine itolewe au isitolewe? Kesi ilienda mahakama kuu ya Marekani hadi senate na hata Rais (Bush) kwani maamuzi ya senate alipaswa ayatie saini ili yawe sheria. Wakati senate ikiwa na kikao cha dharura Rais Bush alikatiza mapunziko yake kutoka Ranchi yake Mexico na kurudi Ikulu akisubiri kutia saini ya mgogoro wa mgonjwa mmoja ambao haukuwa wa dharura.

Kwa mfano huo tu wa uwajibikaji wa marais wa wenzetu, na nguvu kubwa aliyonayo Rais wetu hata ya kuamua hatima ya maisha ya mtu, inasikitisha sana kuona hakuweza kushughulikia tatizo hilo kwa kiwango cha Urais, mwajiri na mwajiriwa wa wananchi. Mgogoro unaohusisha hospitali kubwa za rufaa ulitosha kumrudisha nyumbani hata kama alikuwa katika hotuba UN. Kwa bahati mbaya maumivu ya mgomo yatabaki kwa waathirika na nchi isiyo na takwimu kama yetu tutabaki kuamini hakuna madhara, ukweli ni kuwa mamia na maelfu ya watu wamedhurika sana.

Kuna mwenzetu hapa JF kama walivyowengine alipoteza mtoto mikononi na hadi kumlazimu kuzunguka na mtoto wake aliyepoteza maisha mikononi.

Kuna wagonjwa wameletwa kwa rufaa na nduguz zao hawapo Dar ambao wamekutwa na mauti bila 'dignity'.
Kuna watu wapo katika madeni makubwa ya hospitali za binafsi kutokana na mgomo.
Watu wote hao wanaposikia kuna wenzetu wanampongeza Rais na si kumutuhumu ni kuwaongezea machungu yasiyo ya lazima.

Tatizo hili lilipaswa liingiliwe kati na Rais kwa maamuzi yoyote yaleharaka sana, hakufanya hivyo na kuacha akina Pinda wakiwa hawana la kufanya au kutojua wafanye nini.

Hapa kuna mapungufu makubwa ya uongozi (lack of leadership) na kumpongeza ni kuimarisha na kutukuza uzembe kwa gharama za Watanzani. Jambo hili halihitaji political score point hata kidogo.

Mkuu Pasco, Rais JM Kikwete, hakushauri kwa ufasaha, hakutumia weledi kama mzazi na kiongozi, hakutumia uzoefu kama kiongozi alioupata mgomo wa mwanzo na hakuwajibika katika kushughulikia mgogoro huu kama kiongozi wa taifa.

Ni wazi amekosa sifa za uongozi hata kama angefanya kikao na malaika.
Hakumaliza mgogoro kwa kufuata kanuni na misingi ya uongozi. Hakulinda mali na maisha ya Watanzaniakama katiba inavyomtaka.

Haihitaji kupongezwa bali kukumbushwa kuwa mikono yake imjeaa damu ya Raia wasio na hatia.
 
Kuna mwenzetu hapa JF kama walivyowengine alipoteza mtoto mikononi na hadi kumlazimu kuzunguka na kichanga chake kilichopoteza maishamikononi.

Kuna wagonjwa wameletwa kwa rufaa na nduguz zao hawapo Dar ambao wamekutwa na mauti bila 'dignity'.
Kuna watu wapo katika madeni makubwa ya hospitali za binafsi kutokana na mgomo.
Watu wote hao wanaposikia kuna wenzetu wanampongeza Rais na si kumutuhumu ni kuwaongezea machungu yasiyo ya lazima.

Tatizo hili lilipaswa liingiliwe kati na Rais kwa maamuzi yoyote yaleharaka sana, hakufanya hivyo na kuacha akina Pinda wakiwa hawana la kufanya au kutojua wafanye nini.

Hapa kuna mapungufu makubwa ya uongozi (lack of leadership) na kumpongeza ni kuimarisha na kutukuza uzembe kwa gharama za Watanzani. Jambo hili halihitaji political score point hata kidogo.

Mkuu Pasco, Rais JM Kikwete, hakushauri kwa ufasaha, hakutumia weledi kama mzazi na kiongozi, hakutumia uzoefu kama kiongozi alioupata mgomo wa mwanzo na hakuwajibika katika kushughulikia mgogoro huu kama kiongozi wa taifa.

Ni wazi amekosa sifa za uongozi hata kama angefanya kikao na malaika.
Hakumaliza mgogoro kwa kufuata kanuni na misingi ya uongozi. Hakulinda mali na maisha ya Watanzaniakama katiba inavyomtaka.

Haihitaji kupongezwa bali kukumbushwa kuwa mikono yake imjeaa damu ya Raia wasio na hatia.

Haya tumekusikia nenda kachape kazi jenga taifa..

Acha kulaumu JK kila siku, do your part...

Mdrs wameshaelewa walikuwa wamelewa wameelewesha wameelewa..

Nchi hii ina watu mil.40, matatizo lukuku toka enzi ya st. nyerere..

chapeni kazi no easy ride...mshahara na maslahi ni mchakato..go and tell them
 
Haihitaji kupongezwa bali kukumbushwa kuwa mikono yake imjeaa damu ya Raia wasio na hatia.

HIli itabidi tuzidi kulionesha kwa sababu kama aliweza kukaa nao kwa masaa machachef na wakasitisha mgomo kilichomfanya ashindwe kufanya hivyo kwa wiki mbili za mwanzo za mgomo ni nini? Kama mgomo umeweza kumalizwa na Rais kwanini haukuweza kuzuiliwa toka mwanzo na Rais? tena hadi mgomo wa pili unaanza kwa siku tatu halafu wapo wanataka tuimbe "hongera Kikwete, hongera Kikwete"?
 
Back
Top Bottom