Elections 2010 Mgombea Ubunge wa CCM Serengeti "abwaga manyanga"

hii ni kweli au ndo friday as usual?

Hakuna cha furahi day mkuu, hii habari ccm hawapendi kabisaaaa kuisikia.

Mpasuko wa kura za maoni ndio unaowatafuna, wananchi wanasema hawawezi kuchaguliwa mbunge na watu wanne.

Kwa taarifa yako, Dk. Kebwe kwa kushirikiana na mwenyekiti wa ccm wilaya, m/kiti wa halmashauri ya wilaya, Diwani kata ya Kebanchabancha na Katibu wa ccm wilaya waliingiza kadi feki za ccm na kuzisambaza katika matawi ya ccm tarafa ya ngoreme, wakati huo wakaondoa majina ya baadhi ya wana ccm tarafa ya Ikorongo waliokuwa wakimuunga mkono Dr. Wanyancha. Hapo ndipo sokomoko lilipoanzia. Hata baada ya Dr. Wanyancha kuombwa na ccm taifa kumsaidia Kebwe, wananchi walimuonya Wanyancha asithubutu kumuombea kura Dk. Kebwe, isipokuwa tu amuombee kura JK, na huo ndio mpango mzima.
 
hii itakuwa habari njema. Lakini kama upepo ni mbaya hata asipojitoa bado wananchi watamtosa tu. Jamaa wa mkoa wa Mara huwa hawapendi upuuzi. "Amang'ana kasarikire mura"

Ahahaha ahahaha ahahaha........Kiburunye, umenichekesha sana hapo kwenye maandishi mekundu. Nimekumbuka mambo ya pale Burunga.
 
Watasema CCM wameiba Kura!Tutakumbushana November!!!

Suala la kuiba kura halina ubishi, ni kawaida yenu ccm kuiba kura na kutumia ufisadi mnapoona mmezidiwa.

Uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, kinyang'anyiro cha udiwani kata ya Mugumu mjini(sasahivi imegawanywa) kulikuwa na mgombea wa ccm akikabana koo na mgombea wa cuf. Wananchi waliamua kumpigia kura mgombea wa cuf, pamoja na ccm kugawa rushwa kwa wapiga kura. Baada ya kura kuhesabiwa na kuthibitika kuwa mgombea wa cuf ameibuka kidedea, ccm walijaribu kumpa rushwa wakala wa mgombea wa cuf lakini akawakatalia katakata.
Kwahiyo inaposemwa ccm wanaiba kura na ni mafisadi ushahidi upo.
 
Sio huyo tu bali hali ni ngumu kila mahari. Jamaa mmoja amenishuhudia kuwa wao kwenye mikutano lazima wapewe nauri na hela ya kula! Mambo ni magumu kila mahali.

WE ACHA TU TAR 31/10/10 USUBIRI KUONA MABADILIKO YA KIHISTORIA!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom