Tukiwa bado katika dukuduku ya kuteuliwa Dr Slaa kugombea urais kwa kupitia Chadema swali najiuliza ni yupi anafaa kuwa mgombea mwenza wake, ukitilia maanani kuwa kwa mujibu wa katiba yetu huyu inabidi atokee Zanzibar. Ingekuwa vyema sana kama Chadema na CUF wangeshirikiana kwenye hili (nilishawahi kutoa hii hoja na baadhi ya WanaJF wanaaafiki na wengine kukataa i.e MM) na kumruhusu Hamad Rashid Mohammed au Fatma Maghimbi kuwa wagombea wenza wa Dr Slaa. Vilevile ingekuwa bora kama CUF wasimsimamishe Dr Lipumba na badala yake wamsapoti Dr Slaa kama ambavyo Chadema walivyofanya 1995 na 2000, maana tayari Lipumba kashagombea mara tatu. Haya ni maoni yangu. Hayo ni majina mawili tu ambayo yaminijia kwa haraka, lakini nina uhakika wapo wengine wenye uwezo...
Nawakilisha
Nawakilisha