Nani atakuwa Mgombea Mwenza wa Samia mwaka 2025?

Mkwawa mnyalukoro

JF-Expert Member
Oct 11, 2017
232
136
Kuna kosa la kiufundi lilifanyika ambalo kwasasa linamgharimu mama kwenye Siasa za Tanganyika.

Kosa hili la Kiufundi lilifanyika tarehe 30 Mwezi wa tatu mwaka 2021 ambapo alifanya Uteuzi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na aliyepata Uteuzi huu si mwingine bali ni Dr. Philip Mpango.

Kwa muundo wa Serikali yetu Rais anapotokea Zanzibar anahitaji kuwa na Makamu wa Rais mwenye ushawishi mkubwa wa Kisiasa upande wa Tanganyika.

Hii ni kwasababu Tanganyika ina idadi kubwa ya wananchi ambao ni takribani Milioni sitini (Milioni 60) huku Zanzibar ikiwa na wananchi wanaokaribia Milioni 2.

Kwasababu hii pamoja na sababu za utofauti wa Kisiasa na Kitamaduni baina ya watu wa Bara na Visiwani ni dhahiri kuwa upande huu wa Muungano (Tanganyika) wenye Idadi kubwa ya wananchi takribani Milioni 60 ni lazima upate mwakilishi mwenye nguvu na ushawishi katika Serikali ili kuweza kumsaidia Rais.

Ni lazima tukubali si mambo yote yanaweza kufanywa na kila mtu. Kuna wanaoweza masuala ya michezo na wengine hawawezi, kuna wanaoweza masuala ya sanaa na wengine hawawezi, kuna wanaoweza masuala ya Kisayansi na wengine hawawezi vilevile kuna wanaoweza masuala ya Kisiasa na Uongozi na wengine hawana karama hizo.

Mfano ni Mzee Philip Mangula
Alikuwa kwenye Chama cha Mapinduzi na akapata Uongozi wa juu kabisa na kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Kila alipozunguka nchini alizunguka kwa msafara na kupokelewa kwa misafara na heshima kubwa sana.

Alikuwa na uwezo wa kuajiri wanachama, kupendekeza wagombea na mambo kadha wa kadha.

Mzee Mangula alipoondolewa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM alikwenda kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa lakini alianguka vibaya kwa wanachama walewale ambao walikuwa wakimuheshimu na kumpokea kwa misafara na shangwe pindi akiwa Katibu Mkuu.

Hii inaashiria dhahiri kuwa si kila mtu anaweza kuwa na ushawishi wa kisiasa.

Dr. Mpango ni Mtendaji
amefanya kazi za Kiuchumi na kutumikia kwenye mamlaka ya mapato Tanzania. Si mwanasiasa, hivyo hana ushawishi kwa wananchi.

Hata Ubunge aliupata kwa Uteuzi na baadae kwa Uchaguzi ambao nchi nzima walipitishwa wagombea wa Chama kimoja. Katika Uchaguzi Huru na wa Haki ni ngumu sana kwa Dr. Mpango kushinda hata nafasi ya Kiti cha Udiwani.

Lakini kingine Dr. Mpango hakijui Chama cha Mapinduzi wala Siasa zake hivyo kisiasa ni liability kwa mama, hata katika hotuba ya mama siku ya uteuzi wake alisema.

"Dr Mpango ni Mchumi mahiri hivyo atanisaidia kwenye masuala ya Kiuchumi na kudhibiti Matumizi lakini kubwa zaidi nimeangalia wote lakini nilipofika kwa Dr. Mpango niliona ametulia hana hili wala lile (Hana ushawishi wa kisiasa) nimeona kwasasa niende naye"

Hapa unaweza kuona kuwa sababu kuu ya uteuzi wake ni kutokuwa na nguvu kisiasa pamoja na taaluma ya uchumi, kimsingi Rais anakuwa na washauri wengi wa kiuchumi.

Wapo washauri wa Rais, wapo Mawaziri na Manaibu waziri na wachumi wao katika wizara zao, wapo wachumi katika vyombo vyetu vya kiusalama hivyo hakukuwa na haja ya kumteua Makamu wa Rais mchumi ili amshauri Rais kuhusu Uchumi.

Uteuzi wa Makamu wa Rais/Mgombea mwenza kwa Siasa za nchi nyingi Duniani ni uteuzi wa Kisiasa.

Ni uteuzi unaomsaidia Mgombea Urais/Rais kuongeza kura na ushawishi kwa kundi fulani la wananchi.

Kwa mfano, hayati Rais Magufuli alikuwa na watu wawili wa kuwateua kuwa wagombea wenza wake ambao ni Rais wa Zanzibar Dr. Mwinyi na Mh. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Lakini ili kuwainua wanawake na kupata kura za wanawake akamteua Rais Samia kuwa Mgombea mwenza wake.

Hata Rais wa Marekani Mh. Joe Biden alimteua Kamala Harris ili awe Mgombea mwenza wake ili apate kura za wanawake, watu weusi na walatino.

Tukienda Kongo
Rais Felix Tshisekedi alimteua Vita Kamerhe kugombea naye kwasababu ana ushawishi mkubwa kwa jamii yake kubwa ambayo iliweza kumuongezea kura. Kenya wagombea wakubwa wote wa Urais walichukua wagombea wenza toka kwenye kabila la Wakikuyu,

Rais Ruto alimchukua Rigathi Gachagua huku Mzee Raila Odinga akimchukua Martha Karua yote hii ni kutafuta kura kwenye jamii ya Wakikuyu ambayo ndio jamii yenye Idadi kubwa ya watu nchini Kenya.

Tukirudi nyuma kipindi ambacho Mh. Ally Hassan Mwinyi alipokuwa Rais wa pili wa Tanzania alikuwa na Makamu wa Rais wenye ushawishi mkubwa kwa wananchi wa Tanganyika.

Joseph Sinde Warioba, John Malecela na Cleopa Msuya haya yalikuwa Majabari ya Kisiasa Tanganyika,

Hawa waliweza kusema na kusikika na kumsaidia Rais Mwinyi kupata Kura za Watanganyika.

Walikijua Chama cha Mapinduzi kwa itikadi na falsafa zake na walikuwa na uzoefu mkubwa katika masuala ya Uongozi.

Hivyo uteuzi wao ulimuongezea faida Mh. Rais Ally Hassan Mwinyi katika masuala ya Kiutawala kwa upande wa Tanganyika.

Kwasasa Rais Samia anakosa nguvu ya kisiasa Tanganyika kwasababu hana watu wanaokubalika wenye uwezo wa kumuombea kura na ndio maana inagharimu kufanya mikutano na kuleta watu, inagharimu kumtangaza kwenye vyombo vya habari na Mabango nchi nzima, inagharimu kutumia Wapinzani kumnadi n.k

Haya yangeweza kuepukika ikiwa angekuwa na timu ya watu wazuri wenye kukubalika na Watanganyika,

Kwa mantiki hii mama hana jinsi ni lazima ajiandae kusuka kikosi kipya kitakachoweza kumsaidia kupata kura za Watanganyika.

Tofauti na hapo kwa Timu hii aliyonayo ya akina Kante, Pogba na Mbappe aliyoiimba msanii Roma ajiandae kuanguka ama kufanya Uchaguzi kama ule wa mwaka 2020 ambapo kwa mazingira ya sasa ni ngumu mno Uchaguzi kama ule kujirudia.

Kikosi hiki anachotakiwa kusuka ni lazima kianze na Mgombea mwenza ambaye atamsaidia kupata kura za Tanganyika.

Hawa ni baadhi ya wanasiasa wanaosemwa sana kuwa wagombea wenza wa mama ili kumsaidia kupata kura za Tanganyika mwaka 2025.

Mh. Benard Membe
Mh. Membe ni Kiongozi mzoefu, waziri wa mambo ya nje mstaafu na jasusi mbobezi wapo baadhi watu wanaomtaja kuja kumsaidia mama kupeperusha bendera katika Uchaguzi wa mwaka 2025 ingawa kutofautiana na Serikali ya Hayati Rais Magufuli kunatia doa wasifu wake kwasababu kundi kubwa la wananchi bado linaamini katika falsafa za Hayati Rais Magufuli,

Dr. Emmanuel Nchimbi

Ni mwanasiasa mzoefu ndani ya Chama cha Mapinduzi na Serikali, anaungwa mkono na iliyokuwa Timu ya Mh. Lowassa, naye hakubaliki kwa kwa wananchi wa Tanganyika na hajawa na rekodi nzuri katika Uongozi wake.

Pia baada ya jina la Lowassa kukatwa alikuwa ni miongoni mwa Viongozi waliopewa adhabu na Kamati kuu ya CCM hii imemfanya aonekane kama ni mwanasiasa mbishi.

Ni uamuzi mgumu sana kumchukua mwanasiasa anayeonekana ni mbishi kuwa mgombea mwenza wako kwasababu inaweza ikatokea siku Makamu wa Rais akambishia Rais wake.

Jambo la mwisho ni Uhasama baina ya Timu Lowassa na Timu Msoga.

Timu Lowassa wakipata nafasi ni lazima watahakikisha wanalipa kisasi kwa Timu Msoga kwasababu ya kuharibu mipango yao yote kwa kulikata jina la Mh. Lowassa.

Mh. Kassim Majaliwa
Alikuwa hatambuliki sana kwenye medani za Kisiasa lakini baada ya kuteuliwa na Hayati Rais Magufuli kuwa Waziri mkuu ameonesha uwezo mkubwa sana kwenye nafasi hii pia kwasasa amekuwa ndiye Kiongozi mwenye kukubalika zaidi na Watanzania,

Kwa kiasi kikubwa wananchi wanaamini kuwa Mh. Majaliwa ndiye malaika mlinzi wa Serikali ya Rais Samia,

Wanaamini ndiye anayemsaidia Rais Samia kwa kiasi kikubwa akifuatiwa na Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe, Utumishi wake katika nafasi ya waziri mkuu utakoma katika kipindi cha miaka 10.

Umri wake bado unadai na ndiye mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kwa wananchi. He's too young to retire from Politics hivyo ni lazima aendelee kulitumikia Taifa.

Kama mama ataendelea kumtumia atakuwa amecheza kete bora sana ambayo itamsaidia kupata kura za Watanganyika.

Mh. Job Ndugai
Baada ya kujiuzulu kwenye nafasi ya Spika Mh. Job Ndugai ameendelea kuwa Mbunge na ameendelea kukiunga mkono Chama chake na Serikali ya Rais Samia. Ni mwanasiasa mkongwe ingawa naye hana ushawishi kwa wananchi wa Tanzania bara hivyo hawezi kumuongezea mama kura.

Huenda mama akamtumia kwa kumfanya awe mgombea mwenza wake ili kumfuta machozi ya kuondoka kwenye nafasi yake ya Uspika, inawezekana ingawa kwenye kura hatoweza kumuongezea,

William Lukuvi

Ni mwanasiasa mkongwe na mzoefu na amekuwa kwenye Siasa kubwa kwa muda mrefu ingawa kwasasa amepotea kidogo,

Nafasi yake kuwa Mgombea mwenza ni ndogo sana kwasababu alishawahi kutoa kauli zilizoonekana si nzuri kwa Wazanzibar. Rais wa sasa anatokea Zanzibar ni ngumu kumchukua mgombea mwenza asiyeheshimu Wazanzibar.

Mh. George Simbachawene
Ana haiba ya kuwa Kiongozi mkubwa lakini hana ushawishi kwa wananchi wa Tanzania bara ingawa jina lake linasemwa, kete hii haiwezi kumuongezea mama kura za Watanganyika.

Mh. Innocent Bashungwa

Naye jina lake linatajwa tajwa ingawa bado ni mchanga kisiasa na hana ushawishi kwa wananchi wa Tanzania bara hivyo hawezi kumuongezea mama kura.

Hussein Bashe

Ni Mwanasiasa mzuri na mwenye maarifa makubwa, amekuwa akiongeza ushawishi kwa wananchi siku hadi siku kutokana na hoja na mawazo yake. Ni miongoni mwa Mawaziri wanaofanya kazi vizuri sana kwenye Serikali ya Rais Samia.

Changamoto kubwa aliyonayo ni watu walio nyuma yake, Timu ya Mh. Lowassa.

Humo wamo watu kama Rostam, Fred, Nchimbi na wengine wengi.

Pia Mtandao huu unaishi na Kisasi dhidi ya Timu ya Msoga kwasababu ya kukatwa jina la Mh. Lowassa hivyo wakipata nafasi ni lazima watalipa kisasi.

Kingine ni asili ya Bashe,
Bashe ni Mtanzania mwenye asili ya Kisomali ambapo kwenye nafasi hizi kubwa za nchi asili nayo huzingatiwa sana hivyo anakosa nafasi hii.

Unafikiri mama amchukue mwanasiasa gani ili aweze kupata kura za Watanganyika?

Screenshot_2023-04-28-21-25-19-70_a23b203fd3aafc6dcb84e438dda678b6.jpg
 
NANI KUWA MGOMBEA MWENZA WA RAIS SAMIA 2025?

Kuna kosa la kiufundi lilifanyika ambalo kwasasa linamgharimu mama kwenye Siasa za Tanganyika,

Kosa hili la Kiufundi lilifanyika tarehe 30 Mwezi wa tatu mwaka 2021 ambapo alifanya Uteuzi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na aliyepata Uteuzi huu si mwingine bali ni Dr. Philip Mpango,

Kwa muundo wa Serikali yetu Rais anapotokea Zanzibar anahitaji kuwa na Makamu wa Rais mwenye ushawishi mkubwa wa Kisiasa upande wa Tanganyika,

Hii ni kwasababu Tanganyika ina idadi kubwa ya wananchi ambao ni takribani Milioni sitini (Milioni 60) huku Zanzibar ikiwa na wananchi wanaokaribia Milioni 2,

Kwasababu hii pamoja na sababu za utofauti wa Kisiasa na Kitamaduni baina ya watu wa Bara na Visiwani ni dhahiri kuwa upande huu wa Muungano (Tanganyika) wenye Idadi kubwa ya wananchi takribani Milioni 60 ni lazima upate
mwakilishi mwenye nguvu na ushawishi katika Serikali ili kuweza kumsaidia Rais,

Ni lazima tukubali si mambo yote yanaweza kufanywa na kila mtu,

Kuna wanaoweza masuala ya michezo na wengine hawawezi, kuna wanaoweza masuala ya sanaa na wengine hawawezi, kuna wanaoweza masuala ya Kisayansi na wengine hawawezi vilevile kuna wanaoweza masuala ya Kisiasa na Uongozi na wengine hawana karama hizo,

Mfano ni Mzee Philip Mangula,
Alikuwa kwenye Chama cha Mapinduzi na akapata Uongozi wa juu kabisa na kuwa Katibu Mkuu wa CCM,

Kila alipozunguka nchini alizunguka kwa msafara na kupokelewa kwa misafara na heshima kubwa sana,

Alikuwa na uwezo wa kuajiri wanachama, kupendekeza wagombea na mambo kadha wa kadha,

Mzee Mangula alipoondolewa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM alikwenda kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa lakini alianguka vibaya kwa wanachama walewale ambao walikuwa wakimuheshimu na kumpokea kwa misafara na shangwe pindi akiwa Katibu Mkuu,

Hii inaashiria dhahiri kuwa si kila mtu anaweza kuwa na ushawishi wa kisiasa,

Dr. Mpango ni Mtendaji
amefanya kazi za Kiuchumi na kutumikia kwenye mamlaka ya mapato Tanzania,

Si mwanasiasa, hivyo hana ushawishi kwa wananchi,

Hata Ubunge aliupata kwa Uteuzi na baadae kwa Uchaguzi ambao nchi nzima walipitishwa wagombea wa Chama kimoja,

Katika Uchaguzi Huru na wa Haki ni ngumu sana kwa Dr. Mpango kushinda hata nafasi ya Kiti cha Udiwani,

Lakini kingine Dr. Mpango hakijui Chama cha Mapinduzi wala Siasa zake hivyo kisiasa ni liability kwa mama,

Hata katika hotuba ya mama siku ya uteuzi wake alisema

""Dr Mpango ni Mchumi mahiri hivyo atanisaidia kwenye masuala ya Kiuchumi na kudhibiti Matumizi lakini kubwa zaidi nimeangalia wote lakini nilipofika kwa Dr. Mpango niliona ametulia hana hili wala lile (Hana ushawishi wa kisiasa) nimeona kwasasa niende naye"

Hapa unaweza kuona kuwa sababu kuu ya uteuzi wake ni kutokuwa na nguvu kisiasa pamoja na taaluma ya uchumi,

Kimsingi Rais anakuwa na washauri wengi wa kiuchumi,

Wapo washauri wa Rais, wapo Mawaziri na Manaibu waziri na wachumi wao katika wizara zao, wapo wachumi katika vyombo vyetu vya kiusalama hivyo hakukuwa na haja ya kumteua Makamu wa Rais mchumi ili amshauri Rais kuhusu Uchumi,

Uteuzi wa Makamu wa Rais/Mgombea mwenza kwa Siasa za nchi nyingi Duniani ni uteuzi wa Kisiasa,

Ni uteuzi unaomsaidia Mgombea Urais/Rais kuongeza kura na ushawishi kwa kundi fulani la wananchi,

Kwa mfano,
Hayati Rais Magufuli alikuwa na watu wawili wa kuwateua kuwa wagombea wenza wake ambao ni Rais wa Zanzibar Dr. Mwinyi na Mh. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,
Lakini ili kuwainua wanawake na kupata kura za wanawake akamteua Rais Samia kuwa Mgombea mwenza wake,

Hata Rais wa Marekani Mh. Joe Biden alimteua Kamala Harris ili awe Mgombea mwenza wake ili apate kura za wanawake, watu weusi na walatino,

Tukienda Kongo
Rais Felix Tshisekedi alimteua Vita Kamerhe kugombea naye kwasababu ana ushawishi mkubwa kwa jamii yake kubwa ambayo iliweza kumuongezea kura,

Kenya wagombea wakubwa wote wa Urais walichukua wagombea wenza toka kwenye kabila la Wakikuyu,

Rais Ruto alimchukua Rigathi Gachagua huku Mzee Raila Odinga akimchukua Martha Karua yote hii ni kutafuta kura kwenye jamii ya Wakikuyu ambayo ndio jamii yenye Idadi kubwa ya watu nchini Kenya,

Tukirudi nyuma kipindi ambacho Mh. Ally Hassan Mwinyi alipokuwa Rais wa pili wa Tanzania alikuwa na Makamu wa Rais wenye ushawishi mkubwa kwa wananchi wa Tanganyika,

Joseph Sinde Warioba, John Malecela na Cleopa Msuya haya yalikuwa Majabari ya Kisiasa Tanganyika,

Hawa waliweza kusema na kusikika na kumsaidia Rais Mwinyi kupata Kura za Watanganyika,

Walikijua Chama cha Mapinduzi kwa itikadi na falsafa zake na walikuwa na uzoefu mkubwa katika masuala ya Uongozi,

Hivyo uteuzi wao ulimuongezea faida Mh. Rais Ally Hassan Mwinyi katika masuala ya Kiutawala kwa upande wa Tanganyika,

Kwasasa Rais Samia anakosa nguvu ya kisiasa Tanganyika kwasababu hana watu wanaokubalika wenye uwezo wa kumuombea kura na ndio maana inagharimu kufanya mikutano na kuleta watu, inagharimu kumtangaza kwenye vyombo vya habari na Mabango nchi nzima, inagharimu kutumia Wapinzani kumnadi n.k

Haya yangeweza kuepukika ikiwa angekuwa na timu ya watu wazuri wenye kukubalika na Watanganyika,

Kwa mantiki hii mama hana jinsi ni lazima ajiandae kusuka kikosi kipya kitakachoweza kumsaidia kupata kura za Watanganyika,

Tofauti na hapo kwa Timu hii aliyonayo ya akina Kante, Pogba na Mbappe aliyoiimba msanii Roma ajiandae kuanguka ama kufanya Uchaguzi kama ule wa mwaka 2020 ambapo kwa mazingira ya sasa ni ngumu mno Uchaguzi kama ule kujirudia,

Kikosi hiki anachotakiwa kusuka ni lazima kianze na Mgombea mwenza ambaye atamsaidia kupata kura za Tanganyika,

Hawa ni baadhi ya wanasiasa wanaosemwa sana kuwa wagombea wenza wa mama ili kumsaidia kupata kura za Tanganyika mwaka 2025,

Mh. Benard Membe
Mh. Membe ni Kiongozi mzoefu, waziri wa mambo ya nje mstaafu na jasusi mbobezi wapo baadhi watu wanaomtaja kuja kumsaidia mama kupeperusha bendera katika Uchaguzi wa mwaka 2025 ingawa kutofautiana na Serikali ya Hayati Rais Magufuli kunatia doa wasifu wake kwasababu kundi kubwa la wananchi bado linaamini katika falsafa za Hayati Rais Magufuli,

Dr. Emmanuel Nchimbi
Ni mwanasiasa mzoefu ndani ya Chama cha Mapinduzi na Serikali, anaungwa mkono na iliyokuwa Timu ya Mh. Lowassa,
naye hakubaliki kwa kwa wananchi wa Tanganyika na hajawa na rekodi nzuri katika Uongozi wake,

Pia baada ya jina la Lowassa kukatwa alikuwa ni miongoni mwa Viongozi waliopewa adhabu na Kamati kuu ya CCM hii imemfanya aonekane kama ni mwanasiasa mbishi,

Ni uamuzi mgumu sana kumchukua mwanasiasa anayeonekana ni mbishi kuwa mgombea mwenza wako kwasababu inaweza ikatokea siku Makamu wa Rais akambishia Rais wake,

Jambo la mwisho ni Uhasama baina ya Timu Lowassa na Timu Msoga,

Timu Lowassa wakipata nafasi ni lazima watahakikisha wanalipa kisasi kwa Timu Msoga kwasababu ya kuharibu mipango yao yote kwa kulikata jina la Mh. Lowassa,

Mh. Kassim Majaliwa
Alikuwa hatambuliki sana kwenye medani za Kisiasa lakini baada ya kuteuliwa na Hayati Rais Magufuli kuwa Waziri mkuu ameonesha uwezo mkubwa sana kwenye nafasi hii pia kwasasa amekuwa ndiye Kiongozi mwenye kukubalika zaidi na Watanzania,

Kwa kiasi kikubwa wananchi wanaamini kuwa Mh. Majaliwa ndiye malaika mlinzi wa Serikali ya Rais Samia,

Wanaamini ndiye anayemsaidia Rais Samia kwa kiasi kikubwa akifuatiwa na Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe,

Utumishi wake katika nafasi ya waziri mkuu utakoma katika kipindi cha miaka 10,

Umri wake bado unadai na ndiye mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kwa wananchi,

He's too young to retire from Politics hivyo ni lazima aendelee kulitumikia Taifa,

Kama mama ataendelea kumtumia atakuwa amecheza kete bora sana ambayo itamsaidia kupata kura za Watanganyika,

Mh. Job Ndugai
Baada ya kujiuzulu kwenye nafasi ya Spika Mh. Job Ndugai ameendelea kuwa Mbunge na ameendelea kukiunga mkono Chama chake na Serikali ya Rais Samia,

Ni mwanasiasa mkongwe ingawa naye hana ushawishi kwa wananchi wa Tanzania bara hivyo hawezi kumuongezea mama kura.

Huenda mama akamtumia kwa kumfanya awe mgombea mwenza wake ili kumfuta machozi ya kuondoka kwenye nafasi yake ya Uspika, inawezekana ingawa kwenye kura hatoweza kumuongezea,

William Lukuvi
Ni mwanasiasa mkongwe na mzoefu na amekuwa kwenye Siasa kubwa kwa muda mrefu ingawa kwasasa amepotea kidogo,

Nafasi yake kuwa Mgombea mwenza ni ndogo sana kwasababu alishawahi kutoa kauli zilizoonekana si nzuri kwa Wazanzibar,

Rais wa sasa anatokea Zanzibar ni ngumu kumchukua mgombea mwenza asiyeheshimu Wazanzibar,

Mh. George Simbachawene
Ana haiba ya kuwa Kiongozi mkubwa lakini hana ushawishi kwa wananchi wa Tanzania bara ingawa jina lake linasemwa, kete hii haiwezi kumuongezea mama kura za Watanganyika.

Mh. Innocent Bashungwa
Naye jina lake linatajwa tajwa ingawa bado ni mchanga kisiasa na hana ushawishi kwa wananchi wa Tanzania bara hivyo hawezi kumuongezea mama kura.

Hussein Bashe
Ni Mwanasiasa mzuri na mwenye maarifa makubwa, amekuwa akiongeza ushawishi kwa wananchi siku hadi siku kutokana na hoja na mawazo yake,

Ni miongoni mwa Mawaziri wanaofanya kazi vizuri sana kwenye Serikali ya Rais Samia,

Changamoto kubwa aliyonayo ni watu walio nyuma yake, Timu ya Mh. Lowassa,

Humo wamo watu kama Rostam, Fred, Nchimbi na wengine wengi,

Pia Mtandao huu unaishi na Kisasi dhidi ya Timu ya Msoga kwasababu ya kukatwa jina la Mh. Lowassa hivyo wakipata nafasi ni lazima watalipa kisasi,

Kingine ni asili ya Bashe,
Bashe ni Mtanzania mwenye asili ya Kisomali ambapo kwenye nafasi hizi kubwa za nchi asili nayo huzingatiwa sana hivyo anakosa nafasi hii.

Unafikiri mama amchukue mwanasiasa gani ili aweze kupata kura za Watanganyika?View attachment 2602909
Bora Bashe, Simbachawene na Inno japo mwenye sifa Stahiki ni Simbachaweno ingawa namuona kama PM ajaye..

Bashe ishu ya Dini itagoma ,Inno ni too Young ,

The rest ni magalasa hamna kitu,hata hivyo Bado VP Mpango Yuko vizuri kiutendaji..

Mwisho kabisa hakuna Wapinzani wa kumshinda Raia Samia labda washindane huko kwenye Ubunge..
 
Kuna yule jamaa alikua anapima samaki Kwa ruler being sukuma gang and pro Magu nadhani atamnadi vilivyo mama na kumuongezea kura

Nje ya mada : mama atakabiliwa na upinzani mkali sana labda a print form moja kama mwendazake
 
Kumbe mazingaombwe yote ya Mahakamani na Cyprian Musiba, ilikuwa kuja kuuza sura hapa. Hapana kwa Membe abakie awe kachero tu....
Job Ndugai for President
Mwenza.....Halima Mdee. Mdee achukue Kadi kule CCM

Raisi wangu Samia ni mpaka apitishwe na Chama ndio nitaweza toa tathmini.
 
Mpango anaendelea na mama mpaka 2030. Iwe ndani ya chama au nje watawala hawachaguliwi na wananchi isipokuwa huchaguliwa na WASIOJULIKANA. La sivyo maalim, dr Bilal wangeshakuwa marais wa Zenj.

Kikwete angekuwa rais tangu 1995.
Lowassa angekuwa rais mwaka 2015.

Acha kupoteza muda. Mpango atadumu tena hivi ni mkatoliki na mama ni mwislamu basi combination imekamilika.
 
Nafasi hapo ni mmoja tu kwa Kassim majaliwa
 
Mpango anaendelea na mama mpaka 2030. Iwe ndani ya chama au nje watawala hawachaguliwi na wananchi isipokuwa huchaguliwa na WASIOJULIKANA. La sivyo maalim, dr Bilal wangeshakuwa marais wa Zenj.
Kikwete angekuwa rais tangu 1995.
Lowassa angekuwa rais mwaka 2015.
Acha kupoteza muda. Mpango atadumu tena hivi ni mkatoliki na mama ni mwislamu basi combination imekamilika.

Hivi kumbe enzi za Kikwete Ghalib bilal alikuwa mkristo dhehebu la KKKt eeehh
 
Back
Top Bottom