Elections 2010 Mgombea Mwenza Dr Slaa

WaMzizima

Senior Member
Jun 25, 2009
152
41
Tukiwa bado katika dukuduku ya kuteuliwa Dr Slaa kugombea urais kwa kupitia Chadema swali najiuliza ni yupi anafaa kuwa mgombea mwenza wake, ukitilia maanani kuwa kwa mujibu wa katiba yetu huyu inabidi atokee Zanzibar. Ingekuwa vyema sana kama Chadema na CUF wangeshirikiana kwenye hili (nilishawahi kutoa hii hoja na baadhi ya WanaJF wanaaafiki na wengine kukataa i.e MM) na kumruhusu Hamad Rashid Mohammed au Fatma Maghimbi kuwa wagombea wenza wa Dr Slaa. Vilevile ingekuwa bora kama CUF wasimsimamishe Dr Lipumba na badala yake wamsapoti Dr Slaa kama ambavyo Chadema walivyofanya 1995 na 2000, maana tayari Lipumba kashagombea mara tatu. Haya ni maoni yangu. Hayo ni majina mawili tu ambayo yaminijia kwa haraka, lakini nina uhakika wapo wengine wenye uwezo...

Nawakilisha
 
Mohamed Rashid ni kifaa na kinauzika,ila huyo mdada nina wasiwasi naye kwa sababu hata CUF wenyewe wamemmwaga ktk kura za maoni.:nono:
 
Kama ingekuwa hivyo ingependeza zaidi na kujihakikishia ushindi wa mkubwa. Hata hivyo bado naamini viongozi wa CHADEMA wako makini, na muda ukiwadia watakuja na jina la mgombea mwenza ambalo linaweza kutikisa nchi. Tuvute subra!
 
nasikia kuna mtu mmoja huko zenj kwa sas kazi yake kupanda minazi, nasikia ndio atakuwa mgombea mweza, ni maarufu sana huko kwa maswla ya kukwea minazi

Probably hili ni la kwa ko mwenyewe, I dont believe kama nalo kakuagiza Rostam uandike...
 
Kama ni umaarufu, wa Dr Slaa unawatosha hata watu sita. Kwa sasa anayehitajika ni mgombea mwenza makini tu, sio lazima awe maarufu...
 
nasikia kuna mtu mmoja huko zenj kwa sas kazi yake kupanda minazi, nasikia ndio atakuwa mgombea mweza, ni maarufu sana huko kwa maswla ya kukwea minazi
Ulitaka kazi yake iwe FISADI?
wakwea minazi, wapanzi, wachimba kokoto, wapasua mbao hao ndio prospective leaders. siyo kama wewe mkimbisana na makaratasi kila kukicha pasipo kuwa na TIJA.
 
Kama ni umaarufu, wa Dr Slaa unawatosha hata watu sita. Kwa sasa anayehitajika ni mgombea mwenza makini tu, sio lazima awe maarufu...
Sawa lakini tutajuaje kama mtu yupo makini bila kuwa na track record? amefanya nini kutumikia umma ni lazima wagombea uongozi waonyeshe uadilifu na wawe na rekodi nzuri ya uongozi na kutetea maslahi ya umma na jamii kwa ujumla...
 
Tunataka kiongozi BIKIRA ambaye hana track kama mnazozitaka lakini ana uwezo wa kuongoza.
haya masuala ya uzoefu ktk uongozi ni ya KIJIMA. waachie wazungu. sisi tunataka fresh thinkers na siyo crap thinkers kama walivyo wa CCM
 
Wamchukue HAMAD na ngoma iwe imekwisha.

Wee Ndugu HAMAD wa CUF, weka TANZANIA mbele na CUF nyuma.

DO IT FOR YOUR TANZANIA.

Njoo uunganishe nguvu na Dr. Slaa na MSAFISHE NCHI.

Mstari umeshachorwa...... UKO NA SLAA AU UKO NA MAFISADI.
 
Tunataka kiongozi BIKIRA ambaye hana track kama mnazozitaka lakini ana uwezo wa kuongoza.
haya masuala ya uzoefu ktk uongozi ni ya KIJIMA. waachie wazungu. sisi tunataka fresh thinkers na siyo crap thinkers kama walivyo wa CCM

ni ngumu sana kwa siasa za kibongo, kumchagua mtu makini lakini asiye maarufu, watanzania wanachagua mtu na wala sio sera, hivyo kwa UMAARUFU wa Dr Slaa upate nguvu, unahitaji mgombea mwenza Maarufu
 
Here is where that part of constitution which is unconstitutional rules. Mgombea mwenza oyeeeeeee! Mtikila can help on how to go through this paradox
 
Hata mimi namkubali Hamad Rashid ila na amini hataka kama sheria itamzuia chadema watapata mgombe mzuri mwenza wa dr Silaa
 
Kwani haiwezekani kumngoa Hamad rashid CUF na kumleta CHADEMA?? huko CUF anajirostisha tu!
 
Katiba inasema hivi:
41.-(1) Baada ya Bunge kuvunjwa au kukitokea jambo jingine
lolote lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 38 na
inalazimu uchaguzi wa Rais kufanyika, kila chama cha siasa
kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha
kwa Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jina la
mwanachama wake
mmoja kinayetaka asimame kama mgombea
katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na jina la
mwananchama wake mwingine kinayempendekeza kwa nafasi
ya Makamu wa Rais
.

Kwa maana hiyo ni lazima mgombe mwenza awe mwanachama wa chadema! la sivyo yaweza kutokea yaliyomkuta Shitambala uchaguzi mdogo wa kule mbeya
 
kwa kuwa hakua muda wa kuwa mwanachama atapatikana tuuuu, hata toka tu, tetesi........isijekuwa ilikuwa ni ujasisu kwa Prof.Othuma?, nae angefaa sana
 
Katiba inasema hivi:

Kwa maana hiyo ni lazima mgombe mwenza awe mwanachama wa chadema! la sivyo yaweza kutokea yaliyomkuta Shitambala uchaguzi mdogo wa kule mbeya

Sawa kabisa, lakini kwa vile katiba haendi mbele kusema lazima awe ameisha kuwa mwanachama wa chama hicho kwa muda usiopungua myaka/myezi... bac kumbe aweza jiunga leo, kesho akwa mgombea mwenza! So please CUF, maslahi ya Taifa kwanza.. let the dude come to CHADEMA for VP post..
 
Back
Top Bottom