Mhache
JF-Expert Member
- Jun 20, 2008
- 345
- 24
Huu ni mwezi mtukufu kwa waumini wa dini ya Kiislamu. Mimi na mmoja wa wapenda dini. Dini ni njia ya kumcha Mungu au kumcha unayemwamini. Mimi ni mkazi wa Manzese Uzuri. Sifa mojawapo ya eneo hili ni msongamano wa nyumba ka utitiri wa sisimizi. Mlango wa nyumba yako unatazamana na wa jirani, si ajabu hata milango ya vyoo vinaangaliana.
Kero ninayoipata ni ndugu zetu hawa wakati huu wa mfungo kuweka mikanda ya dini yao na kufungulia redio kwa sauti ya juu hasa wakati wa jioni. Inakuwa ni kero kwetu kwani sisi wengine inabidi tuzime viredio vyetu vya mkulima tusikilize mikanda yao ambayo wakati mwingine tunashindwa kuielewa. Kwani hatuna mafundisho ya dini hiyo.
Ninajiuliza nifanye nini? Au nikae kimya nisubiri fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu.