Waislamu wa Xinjiang wanavyotekeleza ibada ya Kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa uhuru

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111157254517.jpg

Wiki iliyopita Waislamu zaidi ya bilioni moja kote duniani walianza kutekeleza nguzo ya nne ya Uislamu ambayo ni kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo China, ndani ya kipindi hiki Waislamu hutekeleza imani yao kwa uhuru bila kubanwa. Kwa hivyo kwa wale ambao hawajui mengi kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini China, wacha sasa Pili Mwinyi akupatie ukweli kulingana na kile ambacho amekiona na kukishuhudia kwa miaka yote hiyo.

Kwa wale ambao hawajawahi kufika China na kusikia maneno mengi hasa maneno mabaya kuhusu uislamu na China, wanaweza kujiuliza je Waislamu wa China wanafunga vipi mwezi wa Ramadhani wakati hawana uhuru wa kuabudu? Lakini wahenga wanasema “usisikilize maneno ya kuambiwa tu” ni vyema ukajionea mwenyewe ndio hapo unaweza kutolea maoni lile uliloliona.

Kwa mujibu wa sheria, Wachina wanaruhusiwa kufuata dini za Kiislamu, Kibudha, Kitao na Kikristo. Na tunapozungumzia mkoa wenye idadi kubwa ya Waislamu hapa nchini China, basi hatuwezi kuepuka kuutaja Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur. Kama sehemu nyingine nyingi duniani, Waislamu wa mkoa huo pia wameanza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa Waislamu, Ramadhani ni mwezi ambao aya za kwanza za Quran, za kitabu kitakatifu cha Uislamu, ziliteremshwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zaidi ya miaka 1,400 iliyopita. Hivyo wakati wa Ramadhani, Waislamu wote hutumia mwezi huu mtukufu kwa kufunga na kutafakari juu ya hali zao za kiroho. Makabila mbalimbali mkoani Xinjiang yakiwemo Hui na Uygur pia yanashiriki kwenye ibada hii.

Nakumbuka mwaka juzi yaani 2021, nilipotembelea mkoa huu wa Xinjiang nilibahatika kujionea mwenyewe Waislamu wanavyoshiriki kwenye ibada mbalimbali za dini kwa uhuru, na hata kupata nafasi ya kuongea na baadhi ya mashekhe na maimamu wa misikiti ya mji huo. Muhtaram Sherif ni Imamu wa Msikiti wa Yanghang, ambao ni mkubwa sana wilayani Urumqi. Anasema wakati wa Ramadhan, Waislamu wa huko wanajizuia kula, kunywa na kuvuta sigara kuanzia jua linapochomoza hadi linapozama.

Akielezea jinsi alivyoanza kujifunza kufunga, anasema alianza akiwa na umri mdogo sana, ambapo wakati huo alikuwa akimfuata baba yake aliyekuwa imamu pia kwa miaka thelathini. Muhtaram anaamini kuwa kufunga ni njia mojawapo ambayo Mungu anajaribu uvumulivu wa mtu. “Unapaswa kuzoea kushinda kutwa nzima bila ya kula na kunywa, pia unalazimika kujifunza kuishi na kuondokana na ugumu na vishwawishi vyote.” anasema Muhtaram

Wakati wa Ramadhan, Waislamu wengi huwa wanamiminika misikitini kusali. Mafunzo ya kiroho huwa yanawafanya kuondokana na mawazo na hisia potofu, kama vile kuwa na wivu, hasira kusengenya na hata kuwa na nia ya kufanya mambo mengine mabaya.

Xinjiang ni mkoa wenye miskiti mingi ipatayo 20,000, na katika kipindi hiki huwa wanaongeza muda wa ibada kutoka dakika 10 hadi saa mbili, ambapo wakiwa wamefunga wanapata kuwa karibu na Mungu na kukumbuka mateso wanayopitia watu wenye maisha duni.

Kawaida, ni lazima kwa Waislamu kuanza kufunga pale wanapofikia umri wa kubaleghe, hata hivyo kwa wagonjwa, wajawazito na wanawake wanaonyonyesha, wao wamesamehewa kufunga katika kipindi hiki kwa sharti kwamba watakapomaliza udhuru wao, walipe siku ambazo wamekula. Serikali za mitaa katika ngazi zote za Xinjiang kwa upande wao nazo zinalinda shughuli halali za kidini, na kulinda maamuzi ya kidini ya watu.

Mara Ramadhani inapomalizka kawaida kunakuwa na sikukuu ya Eid al-Fitr, ambayo inafanyika kwa siku tatu huko Xinjiang. Katika sikukuu hii familia na marafiki wanakutana pamoja na kula vyakula vitamu, huku wakipeana zawadi. Ramadhani pia inafungwa katika mikoa mingine hapa nchini China ikiwemo Beijing, Gansu na Ningxia.
 
Duh! Umeamua kuja na mada ya kuu promote uislam katika nchi ya kikomunisti kabisa, vipi andiko likaja la wakristo nchini china waadhimisha pasaka kwa shamrashamra nyingi? Kwani uislam imekuwa ni kitu gani mpaka kinaripotiwa hata sehemu ambazo si mukhtadha kutajataja mambo ya imani za kidini? Ndio kujitanua na kujieneza duniani?
 
Kaka na wewe sasa zamu yako kuleta mada ya kuu promote ukristo

WIVU TU
 
Duh! Umeamua kuja na mada ya kuu promote uislam katika nchi ya kikomunisti kabisa, vipi andiko likaja la wakristo nchini china waadhimisha pasaka kwa shamrashamra nyingi? Kwani uislam imekuwa ni kitu gani mpaka kinaripotiwa hata sehemu ambazo si mukhtadha kutajataja mambo ya imani za kidini? Ndio kujitanua na kujieneza duniani?
Wewe alikuzuia Nani kuleta mada ya Ku promote imani yako?

Why umpangie mwenzio?
 
Sijaelewa ina maana habari kuwa waislam wamefungwa jela na serikali ya China kuwazuia kuwa waislam ni uzushi?Hadi Ozil alipata shida Kwa hili
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Duh! Umeamua kuja na mada ya kuu promote uislam katika nchi ya kikomunisti kabisa, vipi andiko likaja la wakristo nchini china waadhimisha pasaka kwa shamrashamra nyingi? Kwani uislam imekuwa ni kitu gani mpaka kinaripotiwa hata sehemu ambazo si mukhtadha kutajataja mambo ya imani za kidini? Ndio kujitanua na kujieneza duniani?
Unamimba?nenda kajifungue
 
Wiki iliyopita Waislamu zaidi ya bilioni moja kote duniani walianza kutekeleza nguzo ya nne ya Uislamu ambayo ni kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo China, ndani ya kipindi hiki Waislamu hutekeleza imani yao kwa uhuru bila kubanwa. Kwa hivyo kwa wale ambao hawajui mengi kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini China, wacha sasa Pili Mwinyi akupatie ukweli kulingana na kile ambacho amekiona na kukishuhudia kwa miaka yote hiyo.

Kwa wale ambao hawajawahi kufika China na kusikia maneno mengi hasa maneno mabaya kuhusu uislamu na China, wanaweza kujiuliza je Waislamu wa China wanafunga vipi mwezi wa Ramadhani wakati hawana uhuru wa kuabudu? Lakini wahenga wanasema “usisikilize maneno ya kuambiwa tu” ni vyema ukajionea mwenyewe ndio hapo unaweza kutolea maoni lile uliloliona.

Kwa mujibu wa sheria, Wachina wanaruhusiwa kufuata dini za Kiislamu, Kibudha, Kitao na Kikristo. Na tunapozungumzia mkoa wenye idadi kubwa ya Waislamu hapa nchini China, basi hatuwezi kuepuka kuutaja Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur. Kama sehemu nyingine nyingi duniani, Waislamu wa mkoa huo pia wameanza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa Waislamu, Ramadhani ni mwezi ambao aya za kwanza za Quran, za kitabu kitakatifu cha Uislamu, ziliteremshwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zaidi ya miaka 1,400 iliyopita. Hivyo wakati wa Ramadhani, Waislamu wote hutumia mwezi huu mtukufu kwa kufunga na kutafakari juu ya hali zao za kiroho. Makabila mbalimbali mkoani Xinjiang yakiwemo Hui na Uygur pia yanashiriki kwenye ibada hii.

Nakumbuka mwaka juzi yaani 2021, nilipotembelea mkoa huu wa Xinjiang nilibahatika kujionea mwenyewe Waislamu wanavyoshiriki kwenye ibada mbalimbali za dini kwa uhuru, na hata kupata nafasi ya kuongea na baadhi ya mashekhe na maimamu wa misikiti ya mji huo. Muhtaram Sherif ni Imamu wa Msikiti wa Yanghang, ambao ni mkubwa sana wilayani Urumqi. Anasema wakati wa Ramadhan, Waislamu wa huko wanajizuia kula, kunywa na kuvuta sigara kuanzia jua linapochomoza hadi linapozama.

Akielezea jinsi alivyoanza kujifunza kufunga, anasema alianza akiwa na umri mdogo sana, ambapo wakati huo alikuwa akimfuata baba yake aliyekuwa imamu pia kwa miaka thelathini. Muhtaram anaamini kuwa kufunga ni njia mojawapo ambayo Mungu anajaribu uvumulivu wa mtu. “Unapaswa kuzoea kushinda kutwa nzima bila ya kula na kunywa, pia unalazimika kujifunza kuishi na kuondokana na ugumu na vishwawishi vyote.” anasema Muhtaram

Wakati wa Ramadhan, Waislamu wengi huwa wanamiminika misikitini kusali. Mafunzo ya kiroho huwa yanawafanya kuondokana na mawazo na hisia potofu, kama vile kuwa na wivu, hasira kusengenya na hata kuwa na nia ya kufanya mambo mengine mabaya.

Xinjiang ni mkoa wenye miskiti mingi ipatayo 20,000, na katika kipindi hiki huwa wanaongeza muda wa ibada kutoka dakika 10 hadi saa mbili, ambapo wakiwa wamefunga wanapata kuwa karibu na Mungu na kukumbuka mateso wanayopitia watu wenye maisha duni.

Kawaida, ni lazima kwa Waislamu kuanza kufunga pale wanapofikia umri wa kubaleghe, hata hivyo kwa wagonjwa, wajawazito na wanawake wanaonyonyesha, wao wamesamehewa kufunga katika kipindi hiki kwa sharti kwamba watakapomaliza udhuru wao, walipe siku ambazo wamekula. Serikali za mitaa katika ngazi zote za Xinjiang kwa upande wao nazo zinalinda shughuli halali za kidini, na kulinda maamuzi ya kidini ya watu.

Mara Ramadhani inapomalizka kawaida kunakuwa na sikukuu ya Eid al-Fitr, ambayo inafanyika kwa siku tatu huko Xinjiang. Katika sikukuu hii familia na marafiki wanakutana pamoja na kula vyakula vitamu, huku wakipeana zawadi. Ramadhani pia inafungwa katika mikoa mingine hapa nchini China ikiwemo Beijing, Gansu na Ningxia.
Propaganda tu hizi za kijinga za Mchina. Ndio zilizojaa kwenye ile channel yao ya CGTN.
 
Back
Top Bottom