Kweli watanzania tuamke
tuhuma huchunguzwa na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria
wanaotuhumiwa hujitetea...ikionekana ni uzushi basi wamepona; ikionekana si uzushi ni kweli...waadhibiwe ili liwe fundisho kwa wengine. ...kila mtu ataogopa kuchezea mali ya umma; kuiba mali ya umma; kuhujuhu uchumi; kukwepa kodi.....waovu na mafisadi ni wachache katika jamii....walio wengi ni masikini....(masikini waungane kutafuta haki yao dhidi ya wahujumu uchumi)
azimio la arusha ni ukombozi pekee dhidi ya wahujumu uchumi
AZIMIO LA ARUSHA HILI HAPA.....DAWA YA WAHUJUMU UCHUMI, MAFISADI, WEZI, WAKWEPA KODI, NA KILA AINA YA UOZO KATIKA JAMII (JISOMEE).....TUNAWEZA KULIHARIRI AZIMIO ILI LIKIDHI MUKTADHA WA SASA WA TANZANIA KWA MFANO: LILIPOANDIKWA LILIZINGATIA CHAMA KIMOJA...SASA TUNA VYAMA VINGI TANGU 1992. KWA HIYO TUNAWEZA KULIBORESHA AZIMIO HILI ILI LITUONGOZE KUKABILIANA NA WAHUJUMU UCHUMI......SIO WENGI NI WACHACHE KATIKA JAMII YETU
SEHEMU YA TANO
AZIMIO LA ARUSHA
Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika
Community Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka
29/1/67, inaazimia ifuatavyo:-
A. VIONGOZI
1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au
mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au
kikabaila.
2. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote.
3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.
4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi
5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama
vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya
34
Kiserikali. Viongozi kutokana na kifungu cho chote cha
Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye
vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki
kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe).
B. SERIKALI NA VYOMBO VINGINE
1. Inaipongeza Serikali kwa hatua zote ilizokwisha chukua
mpaka hivi sasa katika kutimiza siasa ya Ujamaa.
2. Inaihimiza Serikali, bila kungojea Tume ya Ujamaa, ichukue
hatua zaidi za kutimiza siasa yetu ya Ujamaa kama
ilivyoelezwa katika Tamko la TANU juu ya Ujamaa.
3. Inahimiza Serikali kutengeneza mipango yake kwa
kutegemea uwezo wa nchi hii kuiendesha mipango hiyo na
wala isitegemee mno mikopo na misaada ya nchi za
ng'ambo kama ilivyofanya katika mpango wa maendeleo ya
miaka mitano. Halmashauri Kuu ya Taifa inaazimia mpango
huo urekebishwe ili ulingane na siasa ya kujitegemea.
4. Serikali ione kuwa mapato ya wafanyakazi nje ya Serikali
hayapitani mno na yale ya wafanya kazi Serikalini.
5. Serikali itilie mkazo sana njia za kuinua maisha ya wakulima.
35
6. Inahimiza NUTA, Vyama vya Ushirika, TAPA, UWT, TYL.,
mashirika yote ya Serikali, kuchukua hatua ili kutekeleza
siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
C. UANACHAMA
Wanachama wafundishwe kwa ukamilifu imani ya TANU ili
waielewe, na wakumbushwe wakati wote umuhimu wa kuishika
imani hiyo.