Kamishna wa ardhi Dar matatani, atuhumiwa kubadilisha hati ya mfanyabiashara Matunda

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Sakata la mgogoro wa eneo wa mfanyabiashara maarufu Mkoani Dar es salaam Valence matunda limeingia sura mpya baada ya kamishna wa ardhi Dar kutuhumiwa kuhusika kubadilisha hati kinyume na utaratibu

Akiongea na vyombo vya habari mfanyabiashara huyo amesema Kamishna huyo anadaiwa kukaidi maagizo ya mahakama baada ya kupewa hati ya zuio kutoka mahakamani ya kutokufanya chochote katika january Mwaka 2024 lakini yeye February 21 anadaiwa kubadilisha majina ya hati licha ya kuwa na zuio hilo (CAVIET)

Pamoja na hayo ametuhumiwa kutoa notisi of deposit kwa maana ya dhamana iliyowekwa kwenye hatu kwa mtu mwingine wakati hati halisi au original ikiwa kwa mfanyabiashara Matunda na hakuwahi kuisalimisha na mahakama haijawahi kumuandikia barua ya kubadilisha hati hiyo

Mfanyabiashara huyo ameshangaa inekuwaje hati ipatikane mara mbili wakati kulikuwa na amri mahakamani ya kumtaka kutokufanya mabadiliko yeyote kwenye hati hiyo lakini yeye aliendelea

Mfanyabiashara huyo amelalamika pia kunyimwa (search)maelezo ya umiliki wa eneo husika

Matunda amesema kwamba eneo alikuwa ameingia makubaliano ya na akawa ameshaingiziwa fedha billion moja lakini kutokana na hujuma zilizofanyika fedha hizo zilirudishwa

Akijibu tuhuma hizo kamishna wa Ardhi Mashaka Kyando amesema serikali haina mgogoro na mfanyabiashara huyo na hajabadilisha hati na suala la kubadilisha hati linafuata utatibu

Ameongeza kwamba kama ana changamoto anatakiwa amuone Waziri wa ardhi kufikisha lawama zake kwa kuwa yeye ni mfanyabiashara mkubwa ana uwezo wa kumuona na kuhusu suala la search afuate utaratibu alipe elfu arobaini atabaini umiliki wa eneo hilo

"Mimi nahusikaje wakati ulimuona Waziri akitangaza maamuzi ya Serikali yale ni maamuzi ya wizara natekeleza maaamuzi ya serikali na akitaka kujua lile eneo ni la nani atafute (Search)

Kingine nachofahamu suala hilo lipo mahakamani na kwa mujibu wa sheria tunatakiwa tuiachie mahakama inalisikiliza

Matunda amemuomba Rais wa Tanzania Dkt Samia kuingilia mgogoro huo kwa kuwa kamishna huyo ametoa hati mbili bandia (fake)wakati hati halisi(original)ya umiliki wa eneo hilo anayo yeye na ikihitajika anaweza kuiwasilisha.
IMG-20240312-WA0002.jpg
IMG-20240312-WA0001.jpg
IMG-20240312-WA0000.jpg
 
Huyu Waziri wenu wa Ardhi atawaingiza cha kike hamtaamini.
Anatolea maamuzi site bila documents.Kuna mzee mmoja alionyesha nyumba hii hapa ilikua yangu huko bunju na waziri akaamini wakaanza kumtafuta muhusika.
 
Back
Top Bottom