Mfanyabiashara Said Mohammed Saad wa Home Shopping Center (GSM Foundation)

Jamani lazima mtumie akili... hivi mnadhani yeye ni mjinga, ukiwa na ile list na ukajua jinsi ya kuitumia lazima uachane na umasikini. Nadhani wenyewe mnaweza ku conect dots ... wale kwenye list ndio wafadhili wa CCM, ndio wabia kwenye biashara na ndio wasafishaji hela chafu... unaambiwa tu tuna taarifa zako uko kwenye list hivyo angalia bana unatutoa vipi...
True that.
 
CDM wajipange sana sana la sivyo watavurugwa na kusambaratika!!kuna mamluki wengi sana ndani CDM kazi kuvuruga chama!!wakiweza kusimama vizuri wanachukua nchi bila ubishi!
 
Mimi ningekusifia sana kama maelezo haya ungeyapeleka vyombo husika kama Polisi, PCCB na hata kwa mwanasharia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi na kisha suala hilo kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

Kuweka hapa ambapo watu makini wanajua fika una choyo na husda ya mafanikio ya Bw Said Saad.

Kumbuka kuwa NI wajibu wa kila Mtanzania kutii sharia zenu. Ukipitia Katiba yenu Sharia namba 15 ibara ya 6 ya mwaka 1984 kifungu cha 26 imeweka wazi kabisa na inasema hivi
26​
.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na
sheria za Jamhuri ya Muungano.(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa nasheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba​
na sheria za nchi.
 
Majungu tuu na fitina ilovuka mipaka! Kama una ushahidi kwa nini usipeleke kunapohusika ili hatua za isheria zikafuatwa au unatumiwa na mshindani wake wa kibiashara?

ipo harufu ya majungu ni mlebanon akarejeshwa kwao yemen. alimpa mimba kabla ya ndowa kinyume na utaratibu wao wa yemen , uraia mtanzania na saudi arabia kaatuwacha kwenye mataa hapo !:sleepy:
 
Majungu tuu na fitina ilovuka mipaka! Kama una ushahidi kwa nini usipeleke kunapohusika ili hatua za isheria zikafuatwa au unatumiwa na mshindani wake wa kibiashara?

WE ushaambiwa polisi wakienda wanapewa posho wanatambaa sasa huo ushahidi aupeleke wapi labda kwa kikwete ndio mtu wa mwisho lakini kwa mtazamo tu inaonekana system yote kaiweka mfukoni
 
Umeongea mengi sana kuhusu Said kuna ya ukweli kuhusu majengo lakini mengine naona una sababu zako binafsi...halafu ilo ghorofa unalosema lipo Swahili na Udoe sio Swahili na Msimbazi Mbona huyo RPC wa siku nyingi sana mkuu.

Mkuu kama mzalendo na unapenda nchi yako kwa nini huu ushahidi wako usipeleke polisi.

Yeye kafanya uchunguzi na kutuletea hapa akiwa anajua kabisa hapa JF kuna watu wenye upeo zaidi. Kuliko kumbeza na kumkatisha tamaa ni bora ikajadiliwa nini kifanyike, na hii itasaidia hata wengine wenye tetesi kutokukaa nazo
 
mazuri walofanya mbona hayajasemwa?

Hata kama kafanya mazuri mengi huu uchafu hauwezi toka hasa hili la madawa ya kulevya na kuweka vituovya polisi mikononi mwake. Kwakweli wale waliotusaidia issue za EPA karibuni tujadili hili jamani.
 
Apeleke Polisi ipi tena, Hivi bado watu wanaimani na polisi? kwani wao hawaingii JF, wakasoma na kufanyia kazi! Ukipeleka polisi taarifa hii atajulishwa mwenyewe hata kabla fail la kesi hio halijafunguliwa. Ukimwona mhalifu yupo uraiani basi ujue polisi wapo nyuma yake, Minilipeleka taarifa ya kituo kimoja cha kuuza mafuta taarifa ya mafuta yaliyochakachuliwa niliwaona wakichakachua na pampu zimeminywa nikawapa taariafa polisi,tbs, watu wa vipimo, dk 6 toka nimetoa taarifa nikakuta kituo kimefungwa na saa moja baadae ndo wanafika wanakuta wahusika hawapo na kituo wamefunga, ndo basi stori ikaishia hapo, palipo na uhalifu ndipo polisi walipo.
Umeongea mengi sana kuhusu Said kuna ya ukweli kuhusu majengo lakini mengine naona una sababu zako binafsi...halafu ilo ghorofa unalosema lipo Swahili na Udoe sio Swahili na Msimbazi Mbona huyo RPC wa siku nyingi sana mkuu.

Mkuu kama mzalendo na unapenda nchi yako kwa nini huu ushahidi wako usipeleke polisi.
 
Nafikiri mfumo wa nchi ndo unamlinda. Kama haya ni kweli naamini kabisa yupo juu ya sheria. Ingekuwa enzi za mwalimu angeozea jela huyu.
 
Mimi ningekusifia sana kama maelezo haya ungeyapeleka vyombo husika kama Polisi, PCCB na hata kwa mwanasharia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi na kisha suala hilo kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

Kuweka hapa ambapo watu makini wanajua fika una choyo na husda ya mafanikio ya Bw Said Saad.

Kumbuka kuwa NI wajibu wa kila Mtanzania kutii sharia zenu. Ukipitia Katiba yenu Sharia namba 15 ibara ya 6 ya mwaka 1984 kifungu cha 26 imeweka wazi kabisa na inasema hivi
26​
.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na
sheria za Jamhuri ya Muungano.(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa nasheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba​
na sheria za nchi.

Mkuu usijidharau wala kui underestimate JF,mi naona kafanya jambo jema tu,kaipa heshima yake JF kuiletea mada hii idadavuliwe
 
Naanza kuhisi hatari iliyopo kama hali ikiendelea hivi nchi tutazidi kuiweka rehani,inauma sana! Yaani mtu anafanya anavyojisikia kisa tu ni kwamba anawalinda waheshimiwa kwa rushwa! Naamini vyombo vya usalama vinajua lakini uwajibikaji ndio tatizo.bado tuna safari ndefu!
 
jamani tukiambiwa mambo yaliyoshiba kama haya tusikimbilie kusema ni wivu. mnataka data za aina gani ili muamini?, au nyie mnaomtetea ndio vibaraka wake mnaogopa kukosa vibarua. tumewachoka mafisadi, tafadhali tuungane kuwapinga na sio kuwatetea.kwahio nyie mmefurahi kuona watu wanapigwa risasi???
 
miaka kadhaa imepita Rev Mtikila alisema Watanzania tumelala, tumedungwa sindano ya ganzi, tukadai ametutukana, si ndio hii sasa? au unadhani ganzi mpaka hosp?
 
Ze Popobawa ndilo ambalo
Agosti mwaka huu lilitumika kumteka nyara Mlebanoni
mfanyabiashara ambaye ana
duka la vitu vya ndani Mtaa
wa Morogoro karibu na
makutano ya barabara za
Morogoro na Bibi Titi na baadaye kumwingilia kinyume
cha maumbile kisha
kumpeleka kwa nguvu Uwanja
wa ndege wa Mwalimu
Nyerere kumrejesha kwao
Yemen kinyume cha taratibu.
Mbona maelezo yk yanapingana
 
Huyu mwenye home Shoping ni rafiki yake sana Suleiman Kova kuna askari central alishaniambia hili hapa na conect dot
 
Back
Top Bottom