MEYA Jerry Silaa asema SIASA za UJAMAA na KUJITEGEMEA ni MBAYA, NYERERE alituharibu...

Kifupi, kuna tofauti kubwa mno kati ya UONGOZI wa awamu ya KWANZA wa nchi yetu na ulifuata mpaka sasa. Mfumo wa awamu ya kwanza kama ungeendelea huyu bwana asingekuwa hapo kwani ulikuwa hauruhusu kiongozi kupokea mshahara tu kila mwezi na kisha kustaafu.
 
Tatizo Tanzania hatuongozwi na siasa za itikadi, bali siasa za ushabiki wa watu. That whale of an apparatchik Horace Kolimba, aliyekuwa groomed in the art of loyalty na Nyerere na the likes of Sokoine, kusomea mambo ya siasa za itikadi na kupata uongozi wa juu kabisa katika politburo ya CCM alisema CCM haina dira wala muelekeo, maana yake hata yenyewe haijui inafuata itikadi gani.

Forget about itikadi, we seem to excel in the art of unnecessary evasiveness and ubiquitous obfuscation. Hata mji mkuu haujulikani kama ni Dar au Dodoma, mmoja ukiwa "de facto" wakati mwingine ni "de jure".

Kwa hiyo nikimsikia mtu anasema with clarity anaamini nini, kiwe kizuri au kibaya, nampa point kwa kusema clearly tu tujue amesiamamia wapi.Kabla hata sijaanza kuangalia aliposimamia wapi. Maana si dogo hilo katika siasa zetu za leo ambazo Thomas Sankara angeweza kuwaita viongozi wetu karibu wote "fence sitting chameleons".

Pia, hata kum fault Jerry Slaa ni kazi, kwa sababu hata ukitaka kumbana kwa suala la "collective responsibility", chama hakina a cohesive and comprehensive policy ya kusema ifuatwe. Ni kama vile kila mmoja ana interpret documents kivyake, documents ambazo ziko highly open to interpretation to begin with, what with the contradictory Arusha Declaration and Zanzibar U-Turn.

Sasa kama mtu kama Kingunge Ngombale Mwiru, party stalwart, kaukumbatia ubepari mpaka kafisadi mpango wa ukusanyaji wa kodi kituo cha mabasi Ubungo, utamlaumu vipi Jerry Silaa kwa kusema ukweli kwamba huu Ujamaa ulikuwa ni charade tu?

Angalau huyu kawa mkweli, kakataa unafiki.

Ingawa huko kwenye habari za "makalio" kumekosa decorum, then again, decorum has never been Mikasi's strong suit.
 
Nadhani na wewe ni mvivu kati ya hao anaowasema Jerry, mwenzio anakuja na analysis wewe unaruruka tu na vineno vya kanga. JF ni mahali pa kujifunza vilvile kama huna la maana ni bora kukaa kimya. Hivi leo CCM ni chama cha namna gani? mbona hamtangazikwamba kinafuata mrengo wa Kibepari, hapa Nape anaweza kuja na kusema CCM ni chama cha kijamaa. Hivi leo wataka kuniambia hizo nchi unazosema zinalima sana ni za kibepari unajua wamefika hapo? Kwa akili yako unadhani walilala na kuamka wakaanza kuwa mabepari, toka tupate uhuru mnaongoza nchi na siasa ya Ujamaa na kujitegemea. Jerry Slaa kwakuwa ni Meya ana fursa za burebure ndiyo anaona kwamba ana uwezo wa kujituma na kuwa bepari?

Huyo mama FF kwakweli point zake hua zinaniboaga sana, mara nyingi kila anachochangia hua anamatamo wa chuki kwanza, mfano wa huyo Nyerere mwenyewe, huyu mama ni miongoni mwa watu wanaomchukia sana Nyerere, anyway, nije kwenye point.

Kwakiasi fulani, nakubaliana na Jerry Silaa, kwakiasi fulani mfumo wa ujamaa na kujitegemea umetufanya Watanzania wengi kua wavivu sana, angalia hata viongozi wetu type ya hao walioko madarakani, kila wakati wanawaza kusaidiwa tu, kwa wafanyakazi wa taasisi za kiserikali ndio usiseme, kitu kidogo sana unaweza kusubiri hata mwezi mzima hujatekelezewa, wakati mwingie sio kwasababu wanataka rushwa, urasimu tu usiokua na sababu, hivi kwamfano, wizara zinasababu gani ya kua na Waziri, Naibu waziri (Wizara nyingine manaibu waziri wako 2, mfano Madini na Nishati) halafu Katibu mkuu, wote hao wanafanya nini? Ni matokeo ya huo ujamaa na kujitegemea, well, kila kitu kina faida na hasara zake, kama tungeanza na mfumo wa Kibepari, ninahakika familia za akina Kikwete, Lipumba, Mkapa n.k wasingeweza kwenda shule na kua na vyeti hivi walivyo navyo na then wasingeweza kua na nafasi walizo nazo leo, ujamaa na kujitegemea ndio ulisababisha wapate elimu kwasababu, siasa hiyo ilifanya hata watoto wa masikini nao wasome, Pinda kajitambulisha kwetu kama mtoto wa mkulima, sina hakika kwa umri huo alionao na huko anakotoka Mpanda huko, kama wazazi wake wangeweza kumsomesha, kumdharau Nyerere katika hili nako ni kuona kwa kutmia mawani ya mbao.
 
Mdau historia ya uchumi wa nchi yetu inaelekea imekupiga chenga. Sababu za kutetereka kwa uchumi wa Tz wakati wa awamu ya kwanza haikuwa ni sababu ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kulikuwa na ssbabu nyingi mbali mbali mfano kusaidia vita vya ukombozi vya nchi zilizokuwa zikitawaliwa Africa, hii ilidrain sana uchumi wetu. Kuangushwa kwa makusudi kwa bei ya mazao tunayo zalisha uliofanywa na nchi za kibepari baada ya utaifishaji uliofanyika wa njia kuu za uchumi. Kulitokea vipindi vya ukame mbali ulioathiri kilimo. Vita dhidi ya nduli Amin wa Uganda vilathiri sana uchumi wetu. Vita baridi kati ya East West block nayo iliathiri sana usipokuwa upande wa mabepari wanakwamisha uchumi na maendeleo yenu. Pamoja na hayo yote maendeleo yalikuwa mapana sana. Elimu watu wslisoma bure matibabu bure, Kisomo cha watu wazima kiliendelea sana. Viwanda vingi sana vilijengwa, wataalam wengi wa fani mbali mbali walisomehwa eg madakitari ma engineers,marubani n.k. Sitashangaa kuona kiongzi leo yupo madarakani lakini mbumbumbu wa siasa za nchi yake.
 
Last edited:
Sikubaliani na hoja yake kuhusu usimamizi wa sheria za majengo. Unapotoa vibali, lazima ufuatilie sio kukaa ofisini na kuja na visingizio
 
Jerry Silaa ni mfano mzuri wa kiburi (arrogance) ambayo aghalabu huwanyemelea binadamu waliopata ngekewa ya mafanikio kidogo. Ironically hawa binadamu wanaopata "mafanikio" ya haraka haraka kwa njia za mashaka ndio wanaoonesha zaidi kiburi cha namna hiyo. Mifano ipo mingi. Unakutana na kijana amehonga-honga all his/her way up, akishafika sasa, simply kwasababu anaweza kusimama mbele za watu wakamsikiliza basi nasaha zake zitakua: "....vijana wasikae tu kulia lia oh serikali hili serikali lile...watu wajitume, wafanye kazi kwa bidii watafanikiwa tu...kama mimi!!" ukweli wa mambo wa "kujituma" kwake "anausahau" kidogo. Kwa sie wengine tunaojua ukweli wa harakati za watu kama hao tunapata shida kweli...

Ninakubaliana nawe asilimia 100%. Sikiliza hadithi za Mhe Lowassa na wa aina zake za kulaumu eti Watanzania ni wavivu, wanakaa vijiweni kupiga soga, hawapendi kufanya kazi, nk. nk. Hawa watu wanaiba kodi ambazo ni nguvu ya watu hao hao maskini, wanajitajirisha kwa wizi halafu wanageuka na kujiona wao ni bora na wachapa kazi:( Katika mfumo wa kleptocracy (ufisadi) kama ambao umetamalaki kwa sasa hautoi fursa sawa kwa wananchi kuweza kujiendeleza kwa namna yo yote ile. Ni wale tu wachache walio na access ya pesa za umma, pesa za walipa kodi (wizi uliohalalishwa) ndio wanaoonekana wamefanikiwa ambao ndio huo Mhe Jerry Slaa anaita 'ubepari'!!!! na wengine wote ni 'wavivu', 'wategemezi wa serikali', nk. Inatia hasira sana.
 
The same old tired argument. Nadhani kumlaumu marehemu JKN kwa matatizo yetu ya kiuchumi tulio nayo leo is a very poor excuse. The real question ambao viongozi wetu wanabidi waweke bayana including Mstahiki Meya Silaa ni how are they utilised the abundant mineral resources ambazo JKN aliziacha intact. The point is marehemu JKN ameacha hii nchi haina madeni. Look at the national debt now. Why is sky rocketing exponentially while the country has the largest Gold and Diamond reserves nevermind other minerals such as Tanzanite. Sisi ndio tulitakiwa kuwakopa Marekani na China. But whenever the leaders want to hide their own incompetency, unfortunately 'Nyerere' becomes the scapegoat!
 
Miaka michache tu toka kifo cha Muasisiile misingi ys ujamaa na kujitegemeawa taifa hili na Chama tawala anapatikana Meya toka Chama kilichoasisiwa na Hayati Mwl Nyerere tena Meya msomi mwenye uthubutu wa kusema "Nyerere alituharibu" Kweli?....!
CCM iko katika hstari kubwa sana ya kukosa kabisa viongozi wenye akili na maono ya kiwango Mwalimu
Kwa statements kama za huyu Meya ambaye vile vile ni mjumbe wa NEC ya CCM, ni jambo la kusikitisha.

Tatizo kubwa hata huo ubepari unaoongelewa hawajui hata jinsi ya kuuiga.

Kinachosikitisha ni vijana wadogo ambao wala hawaelewi hata misingi ya ujamaa na kujitegemea kwa context ya Mwalimu, ati wakiukosoa hadharani!

Mbaya zaidi ni ukweli kuwa ni misingi ya usawa ns kuenzi ubinadamu kitu kilichoenziwa na Mwalimu ndiuo kimewafikisha hapo walipo.
Ukweli huo huo utadhihirisha kuwa kama si mwalimu wengi wao wangekuwa watwana na manamba ndani ya nchi yao.
 
are you his father?

is mbarack ,his official name?
au analitumia nyumbani?

Derivation Barack, is Baraka, Mbaraka, Mabrouk, Mbaruku, Mubarak, Mbarak, Mbalaka, Balaka or mBarack.

Ever heard of Bakili? that is Bakari, ever heard of Shaka Zulu? that is Sheikh Zulu.

Why is it so hard for you to understand?
 
Sidhani na wala sikutegemea kinda kama Jerry Silaa kuwa na ubavu wa kumkosoa Mwalimu kisera kiitikadi na hata kimaadili.
A. H. Mwinyi mwenyewe, kiongozi wa kusifika alisha sema akijilinganisha na Mwalimu yeye ni kichuguu!!!

Sijui huyu Silaa anapata wapi ujasiri wa kukosoa sera za Mwalimu, ilhali si msomi wa itikadi hiyo.
Isingekuwa sera za Mwalimu pengine baba zake wasingemfikisha hapo alipo.
Tatizo mtu anapokuwa amekula na kushiba , yule asiye na maadili huvimbiwa na kutapikia miguu ya waliomfikisha hapo.

Nyerere mwenyewe alijikosoa na akasema "mabaya" yake yaacheni mfate yale mazuri, mimi sijaliona mpaka leo.

Jerry Slaa ana haki ya kukosoa, anajuwa tulipotoka na hajajijaza ujinga mliojijaza nyinyi kufikiria kuwa kila alilofanya Nyerere ni jema. Nyerere na Siasa yake ya majaribio, Ujamaa na Kujitegemea ilitufikisha tukawa maskini hohehahe.
 
Nyerere ni Rais wa kwanza hakukosea kutupeleka kwenye sera za kijamaaa alipatia,,sema tu nchi zlizokuwa kwenye mambo hayo ya ujamaa ndizo zlizokuja kuzidiwa baadae na mfumo wa kibepari...kama hapo bongo tungekuwa na mfumo wakibebari tokea zamani wengi hapo bongo nchi ingekuwa ilishauzwa zamani ,na ingekuwa inamilikiwa na watu wachahce,watu wasingeweza kujenga nyumba kama wanavyofanya au waluvyofanya kipindi cha nyuma,angalia kenya sehemu kubwa ya ardhi yao inamilkiwa na watu wachache tofauti na TZ kwa muda huu tungekuwa masikini sana,suala la kulemazwa na mfumo sio kweli!! yeye Jery kasema tu kama mawazo yake lkn kwa upande wangu yuko wrong kabisa.sema tu kil mfumo una mazuri na mababya yake ndio uniambie tu.
 
Nyerere mwenyewe alijikosoa na akasema "mabaya" yake yaacheni mfate yale mazuri, mimi sijaliona mpaka leo.

Jerry Slaa ana haki ya kukosoa, anajuwa tulipotoka na hajajijaza ujinga mliojijaza nyinyi kufikiria kuwa kila alilofanya Nyerere ni jema. Nyerere na Siasa yake ya majaribio, Ujamaa na Kujitegemea ilitufikisha tukawa maskini hohehahe.
Faiza - Mwl. Nyerere ndiyo alisaini mikataba ambayo Taifa la Tanzania linapata 3% ya mauzo ya madini?
 
Last edited by a moderator:
Jerry Slaa anatakiwa kuondolewa kwenye uongozi maana hajui siasa ya chama chake. Rasmi ccm bado itikadi yake ni ujamaa na kujitegemea. Sasa kama viongozi wanajua wametuingiza kwenye ubepari wananchi tunachoona ni ufisadi na wizi mtupu unaendelea kwa kisingizio cha ubepari. Kama alivyosema Mw Nyerere ubepari ni unyama.
 
Ndio maana kavaa kanzu na msuli
teh teh meipenda hii,atleast tumempata mtu wa kumfanyia mental exorcism.
 
Faiza - Mwl. Nyerere ndiyo alisaini mikataba ambayo Taifa la Tanzania linapata 3% ya mauzo ya madini?

Nyerere hajasaini mkataba hata wa Tanzania kupata 0.

Kumbuka hiyo asilimia 3 imeshapandishwa na kuwa 4, halafu uelewe hiyo ipo siku zote mpaka pale mtaji wa waliowekeza utakapo rudi, Tax zinakuwepo kama kawaida na marupurupu mengine kibao.

Isitoshe, hivi wewe ulikatazwa kwenda kuchimba madini?
 
Back
Top Bottom