MEYA Jerry Silaa asema SIASA za UJAMAA na KUJITEGEMEA ni MBAYA, NYERERE alituharibu...

Meya Jerry Slaa asema SIASA ya UJAMAA na KUJITEGEMEA ilitufanya sisi WaTanzania kuwa Wavivu; Kuwa Wategemezi wa Serikali, kuliko kujitegemea Wenyewe....Source; MKASI

- Hatimaye kuna Mwanasiasa mwingine ambaye ameliona hili ambalo nimeliona siku nyingi sana na kulisemea sana hapa na kunileteea mfarakano na wanaompenda sana Mwalimu kwamba hawako tayari kusikia anakosolewa, nasema tena Mwalimu was great leader never ever again, lakini alikuwa na mpungufu mawili makubwa ya 1. KUTOKUJUA UCHUMI 2. HAKUPENDA KUHESHIMU SHERIA ZA JAMHURI na ni kwenye hizi hoja mbili tu ndipo Taifa letu lilipokwamba na hasa kwenye KUTOKUWA NA HESHIMA KWA SHERIA ZETU,

- I mean Kiongozi anaiba unamuita Kamati Kuu ya CCM, badala ya kumsweka Rumande na kumfikisha mahakamani matokeo Kiongozi mwizi aliyeiba Mtwara anahamishiwa Mbeya, wale mnaompenda sana Mwalimu fikeni pahali mkubali kwamba Mwalimu alikuwa binadam mwenye Mapungufu kama sisi wote wengine, ndipo mtatupa nafasi tunataka mabadiliko kuweza kujitafakari tulipokosea ndio maana Mwenyekiti Mao alisema:- "Ukiona watu wawili wanakubaliana kwa kila kitu na kwa muda mrefu sana ujue wote wagonjwa, au mmoja sio mzima."

- Tubadilike, naamuunga mkono 100% Meya Silaa kwa kuuona na kuusema wazi ukweli, kwamba siasa za Ujamaaa na Kijitegemea ndio zimetufikisha hapa tulipo hili taifa sasa tubadilike!!

KIDUMU CCM!!

LE MUTUZ
 
Simjui Mdingi wa Huyu Jamaa , lakini huyu meya anatakiwa aelewe historia ya Baba je kama nchi ingekuwa ya kibepari angepata nafasi ya kusoma na kuwa pilot? Nchi Jirani Marehemu Saitoti licha ya kuwa Prof wa Mathematics yaani mzuri kichwani, lakini ilibidi achukuwe hatua za kibinafsi za kuhamia umasaini na kuchukua jina la kimasai ili aweze kusoma, na huyo anayesema Nyerere hakujua uchumi, anatakiwa aelewe Mwl alikuwa ana jenga msingi wa uchumi wa baadae kama walivyo fanya China, India, Malaysia nk ndio maana akawekeza kwenye Elimu, Viwanda vidogo vidogo, na kuacha dhahabu mpaka tuwe na uwezo wa kuyachimba in large scale meanwhile kilimo na viwanda vingeweza kutatua matatizo yetu, tatizo kuna watu walihongwa na Rajani pajero kwa ajili a uchaguzi hao ndio walioua uchumi wa nchi, na mchezo huu walianza zamani toka wako wizara ya kilimo, walihongwa farasi
 
Cha kushangaza viongozi wetu wanajuwa kuwa watanzania wengi ni wavivu ila sie ndiyo tuko bize kupinga ukweli huu. Kita mwana east afrika anajuwa kuwa watanzania si wachapa kazi bali domo tu na kuuza unga kupata utajiri wa haraka haraka. Inabidi tuwajibike tusingoje kusukumwa jamani.
 
na hao waliochukuwa na wanajua uchumi au ku-embrace sera za kibepari je tumepiga hatua? kwa haraka haraka angalia thamani ya tshs dhidi ya kshs tume improve au? angalia hela ya msumbiji dhidi ya kwetu?
 
Wapenzi wa Ujamaa na Kujitegemea msimuandame sana huyu dogo kwani anawaza kuendana na mfumo uliopo.
Hata hivyo anastahili pongezi. Yeye ni MKULIMA ambaye ni meya wa manispaa katika jiji kubwa, aliyeweza kusoma simultaneously (Electronics Science & Communication + ATEC + Certificate in law) na sasa hivi anasoma tena kwa wakati mmoja (Masters (ESAMI) + LLB(OUT)) ili kuweza kulima kisasa (kipepari).
Ninyi na UJAMAA wenu uliokuwa na misingi lakini ikakosa watu wa kuisimamia na hivyo ujamaa ukashindwa, kizazi kipya na Ubepari usiokuwa na misingi ambao hatujui hatma yake kwa sasa!
 
- Hatimaye kuna Mwanasiasa mwingine ambaye ameliona hili ambalo nimeliona siku nyingi sana na kulisemea sana hapa na kunileteea mfarakano na wanaompenda sana Mwalimu kwamba hawako tayari kusikia anakosolewa, nasema tena Mwalimu was great leader never ever again, lakini alikuwa na mpungufu mawili makubwa ya.....

Sasa TUAMBIA ni Siasa Gani CHAMA CHA MAPINDUZI inachozifuata ? na Hizo SIASA Zinajua UCHUMI na KUHESHIMU SHERIA za JAMHURI? MBONA BADO MAFISADI bado wapo ndani ya hiyo SERIKALI PAPA zaidi ya wakati wa Mwl. ?

Hatujaona VITABU vya kuelezea siasa ya sasa ya chama cha mapinduzi; Mnaogopa nini?
 
- Hatimaye kuna Mwanasiasa mwingine ambaye ameliona hili ambalo nimeliona siku nyingi sana.....KIDUMU CCM!!

LE MUTUZ
Mkuu ni kweli Mwl alikuwa Binadamu wa kawaida na Mwansiasa kama Wanasiasa wengine lakini hakuwa Mwanasiasa wa kawaida kama Mstahiki Meya wetu.
Umeshawahi kukisoma/kukiona kijitabu kidogo kwa jina TUJISAHIHISHE? Hiki kitakuthibitishia kuwa Mwl alikuwa mwepesi wa kuona alipokosea na kukubali makosa yake.
Leo hii kwa hawa Viongozi wetu wa kizazi cha dot com nani yuko tayari ku-admit makosa yake?
Ok Mwl hakujua uchumi nani aliasisi sera ya Umiliki wa njia kuu za Uchumi kuwa chini ya Wananchi?
Ukifuatilia hotuba za Hayati Mwl kuhusu kumhamisha kiongozi aliyekosea hapa na kumpeleka pale utajua kwa nini alifanya hivyo ukisikiliza wakati tunapata Uhuru alikuwa na wasomi wangapi wazawa ambao wangemsaidia katika kuongoza Nchi!
Ni kweli Mwl hakuwa Malaika lakini alikuwa kiongozi ambaye mfanowe haujapatikana.
 
He is right

Nyerere pamoja na mema yake yote na nia njema yake yote, alilea wezi kama akina chenge, JK, EL, na vilaza kama akina kingunge, malechela nk
 
- Hatimaye kuna Mwanasiasa mwingine ambaye ameliona hili ambalo nimeliona siku nyingi sana....KIDUMU CCM!!

LE MUTUZ

Hata sasa watu wameiba hela za EPA wakaambiwa warudishe badala wapelekwe mahakamani, hata kama ela zilikuwa nyingi bado hakuna umuhimu wa kuokoa hela alafu kuwaacha wahalifu nje, tukirudi nyuma kwenye point, nakubaliana na wewe kila kiongozi ana mapungufu yake including Nyerere pia kwa zama zile misimamo ya kisiasa ilikuwa ni kawaida kutokana na mfumo wa kidunia ambao ulikuwa umegawanyika katika sehemu mbili (yaani sera za mashariki na sera za magharibi), wale walioamua kufuata upande wa mashariki maana yake walikuwa hawana urafiki na watu wa magharibi. Na ndio maana kuna nchi kama Tanzania zenyewe zikajiweka kando kwa kutamka kwamba wao ni nchi zisizofungamana na upande wowote inapokuja kwenye issue za siasa za nje kwa kuwa ugomvi wa mashariki na magharibi ilionekana kama nchi hauwahusu na siasa za ndani zikawa ndio hizi tunazozipigia kelele za ujamaa na kujitegemea ambazo zina faida kwa kiwango flani especially enzi zile nchi ilipokuwa bado changa maana hata shule tu ilikuwa ni za kuhesabu pia zina mapungufu.

Tatizo kubwa tulilonalo ni WAY FORWARD maana tupo awamu ya nne na muda mchache ujao tutaingia awamu ya tano lakini bado tunajadili tumefika hapa kwa sababu ya utawala wa awamu ya kwanza ambao umeisha miaka 29 iliyopita kwani kwangu tunachojadili hapa ni theories ambazo kiukweli hata leo hii ikatamkwa kabisa nchi yetu ni ya kibepari kama mtu hujitambui utabaki kubaki pale pale pia hata kama itamkwe kwamba nchi ni ya Ujamaa na kujitegemea pia kama hujitumi utabaki hapa hapa

Tumefika hapa kutokana na viongozi wetu kutudanganya kwamba wao ndio kila kitu huku na mwisho wa siku wananchi wame-loose hope kwa kuwa fedha kidogo inayokusanywa inatumiwa vibaya mwisho wa siku kila mtu anabaki kuiangalia serikali hata kwa mambo madogo kama ya utapaji takataka
 
Sasa TUAMBIA ni Siasa Gani CHAMA CHA MAPINDUZI inachozifuata ? na Hizo SIASA Zinajua UCHUMI na KUHESHIMU SHERIA za JAMHURI? MBONA BADO MAFISADI bado wapo ndani ya hiyo SERIKALI PAPA zaidi ya wakati wa Mwl. ?

Hatujaona VITABU vya kuelezea siasa ya sasa ya chama cha mapinduzi; Mnaogopa nini?

- Huwezi kurekebisha nyumba bila kwenda kwenye foundation yake ni simple common sense!! wala hauhitaji PhD!! kujua kwamba foundation ya taifa letu ilikuwa na matatizo na ndio tunayopigana nayo sasa hakuna mapya hapa!! Mafisadi walikuwepo siku zote, wakiharibu hapa wanahamishiwa pale au hujui?

- Waacheni wananchi wa Taifa hili wajadili Taifa lao bila kutishwa tishwa kwa sababu wanajadili Mapungufu ya Mwalimu, please lioneeni huruma hili taifa!!

Le Mutuz
 
Hata sasa watu wameiba hela za EPA wakaambiwa warudishe badala wapelekwe mahakamani....

- Hela aliiba Meneja wa Gapex kutoka Musoma, enzi za Awamu ya kwanza alifanywa nini? Sasa ndio iwe EPA afadhali hao wanarudisha, SUKITA ilianza na kufa under nani? Air Tanzania ilianzishwa na kuuliwa under utawala wa nani? waliohusika walifanywa nini Mkuu? Waacheni wananchi alijadili Taifa lao bila kuwatisha, infact kuna muandishi wa habari aliyejaribu sana kufuatilia kufa kwa Gapex, akaishia kuitwa Ikulu na Butiku na kutishiwa sana na wiki iliyofuata akahamishiwa Ubalozini UK, please wacheni wananchi wazungumze,

- Jerry Silaa ni kichwa sana namuaminia sana na niliwahi hata kuandika articel kub wa sana kukitaka chama changu kimpe nafasi kubwa kwenye chama ninashukuru sana kwamba chama changu kilisikia, amesema anachoamini kuwa ndio tatizo na wewe sema lako sio kukubisha bisha bila hoja za msingi hapa, Mwalimu alikuwa binadam kama wengine wote kuna mtu mmoja hap anashauri nikasome kitabu cha kujikosoa cha Mwalimu huyo huyo aliyetuwekea foundation mbovu hili taifa, ndio huwa ninajiuliza sana hivi hili taifa tulilogwa na nani hasa? that we cant think right kila siku kutetea mediocre tu!!

Le Mutuz
 
- Huwezi kurekebisha nyumba bila kwenda kwenye foundation yake ni simple common sense!! wala hauhitaji PhD!! kujua kwamba foundation ya taifa letu ilikuwa na matatizo na ndio tunayopigana nayo sasa hakuna mapya hapa!! Mafisadi walikuwepo siku zote, wakiharibu hapa wanahamishiwa pale au hujui?

- Waacheni wananchi wa Taifa hili wajadili Taifa lao bila kutishwa tishwa kwa sababu wanajadili Mapungufu ya Mwalimu, please lioneeni huruma hili taifa!!

Le Mutuz

Sasa Hata HAUJUI ni SIASA GANI CHAMA CHA MAPINDUZI inaziendesha? HIYO SIO AIBU? Unawaachia wananchi wanajua nini? kweli tutafika?

Sasa; Mnavyosafiri ni PESA za nani Mnazozichota? na Mkifika huko Mnawambia wananchi kuwa Siasa za Ujamaa na Kujitegemea Zimekufa????

Au Mnanyamaza KIMYA? Hakuna anayetangazia Wananchi VIJIJINI na NCHI NZIMA... kwaninni?????
 
- Hela aliiba Meneja wa Gapex kutoka Musoma, enzi za Awamu ya kwanza alifanywa nini? Sasa ndio iwe EPA afadhali hao wanarudisha, SUKITA ilianza na kufa under nani? Air Tanzania ilianzishwa na kuuliwa under utawala wa nani? waliohusika walifanywa nini Mkuu? Waacheni wananchi alijadili Taifa lao bila kuwatisha, infact kuna muandishi wa habari aliyejaribu sana kufuatilia kufa kwa Gapex, akaishia kuitwa Ikulu na Butiku na kutishiwa sana na wiki iliyofuata akahamishiwa Ubalozini UK, please wacheni wananchi wazungumze,

- Jerry Silaa ni kichwa sana namuaminia sana na niliwahi hata kuandika articel kub wa sana kukitaka chama changu kimpe nafasi kubwa kwenye chama ninashukuru sana kwamba chama changu kilisikia, amesema anachoamini kuwa ndio tatizo na wewe sema lako sio kukubisha bisha bila hoja za msingi hapa, Mwalimu alikuwa binadam kama wengine wote kuna mtu mmoja hap anashauri nikasome kitabu cha kujikosoa cha Mwalimu huyo huyo aliyetuwekea foundation mbovu hili taifa, ndio huwa ninajiuliza sana hivi hili taifa tulilogwa na nani hasa? that we cant think right kila siku kutetea mediocre tu!!

Le Mutuz

CHANGE the WORLD BILLBOARD USIDANGANYE ULIMWENGU CCM ni CHAMA CHA KIBEPARI

Party of the Revolution
Swahili: Chama Cha Mapinduzi
ChairmanJakaya Kikwete
Secretary-GeneralAbdulrahman Kinana
FounderJulius Nyerere
Abeid Karume
Vice Chairman (Mainland)Philip Mangula
Vice Chairman (Zanzibar)Ali Mohamed Shein
Founded5 February 1977
Merger ofTANU and ASP
HeadquartersDodoma, Tanzania
NewspaperUHURU
Youth wingUmoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Women's wingUmoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Parents' wingWazazi
Membership (2013)6.4 million [SUP][1][/SUP]
IdeologyFormerly: African socialism
Political positionCentre-left
International affiliationSocialist International
Colors
National Assembly
258 / 354

Election symbol
hoe and hammer
Website
www.ccm.or.tz
Party flag
Politics of Tanzania
Political parties
Elections
Chama cha Mapinduzi (CCM) (Party of the Revolution in Swahili) is the ruling political party of Tanzania.
 
Sasa Hata HAUJUI ni SIASA GANI CHAMA CHA MAPINDUZI inaziendesha? HIYO SIO AIBU? Unawaachia wananchi wanajua nini? kweli tutafika?

Sasa; Mnavyosafiri ni PESA za nani Mnazozichota? na Mkifika huko Mnawambia wananchi kuwa Siasa za Ujamaa na Kujitegemea Zimekufa????

Au Mnanyamaza KIMYA? Hakuna anayetangazia Wananchi VIJIJINI na NCHI NZIMA... kwaninni?????

- U know jina lako ni kubwa sana humu JF, lakini unanishangaza sana hoja unazoandika unasema nini hasa mkuu? Jerrry Silaa amesema anayoona ni sababu iliyotufikisha hapa hili taifa, mambo ya elimu ya bure, mambo ya Mwenyekiti wa Tawi la CCM kiwandani kuwa na nguvu kuliko Mkurugenzi wa Kiwanda, mambo ya kuwapa mashamba makubwa wananchi waiokuwa na uwezo wa kuyatunza na kuyaendesha, mambo ya wanafunzi kushinda mashambani kuliko darasani, ndio yametufikisha hapa, sasa tubadilike hakuna jinsi tena!!

- I mean unaniuliza maswali very cheap kwani Viongozi wa Chadema wanaposafiri kwenda UK na USA kufungua matawi ya Chadema yenye wanachama watano tu huku Songea hawana tawi kabisa huwa wanapata wapi hizo pesa? Please maaan be like your name mkuu!!

Le Mutuz

Le Mutuz
 
CHANGE the WORLD BILLBOARD USIDANGANYE ULIMWENGU CCM ni CHAMA CHA KIBEPARI

Party of the Revolution
Swahili: Chama Cha Mapinduzi
ChairmanJakaya Kikwete
Secretary-GeneralAbdulrahman Kinana
FounderJulius Nyerere
Abeid Karume
Vice Chairman (Mainland)Philip Mangula
Vice Chairman (Zanzibar)Ali Mohamed Shein
Founded5 February 1977
Merger ofTANU and ASP
HeadquartersDodoma, Tanzania
NewspaperUHURU
Youth wingUmoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Women's wingUmoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Parents' wingWazazi
Membership (2013)6.4 million [SUP][1][/SUP]
IdeologyFormerly: African socialism
Political positionCentre-left
International affiliationSocialist International
Colors
National Assembly
258 / 354
Election symbol
hoe and hammer
Website
www.ccm.or.tz
Party flag
Politics of Tanzania
Political parties
Elections
Chama cha Mapinduzi (CCM) (Party of the Revolution in Swahili) is the ruling political party of Tanzania.

- Kiwe kisiwe it does not matter, it is what it is! ila hakuna tena elimu ya bure, wala mishahara bila kazi kama zamani!!

Le Mutuz
 
- U know jina lako ni kubwa sana humu JF, lakini unanishangaza sana hoja unazoandika unasema nini hasa mkuu? Jerrry Silaa amesema anayoona ni sababu iliyotufikisha hapa hili taifa, mambo ya elimu ya bure, mambo ya Mwenyekiti wa Tawi la CCM kiwandani kuwa na nguvu kuliko Mkurugenzi wa Kiwanda, mambo ya kuwapa mashamba makubwa wananchi waiokuwa na uwezo wa kuyatunza na kuyaendesha, mambo ya wanafunzi kushinda mashambani kuliko darasani, ndio yametufikisha hapa, sasa tubadilike hakuna jinsi tena!!

- I mean unaniuliza maswali very cheap kwani Viongozi wa Chadema wanaposafiri kwenda UK na USA kufungua matawi ya Chadema yenye wanachama watano tu huku Songea hawana tawi kabisa huwa wanapata wapi hizo pesa? Please maaan be like your name mkuu!!

Le Mutuz

Le Mutuz

Kweli na NDIO ELIMU ya BURE lakini hapo sasa HAUONI GAP ya ELIMU ingeongezeka kati ya WAKRISTO na WAISLAMU? Is that an issue right now? that Muslim still were underprivileged?

Kwahiyo Pamoja na ELIMU kwa BURE; SHULE kutaifishwa bado watu nchini hawaoni USAWA sasa yeye JERRY SLAA sidhani wazazi wake walizaliwa GONGO la MBOTO lakini ni SIASA za NYERERE za UJAMAA na KUJITEGEMEA ndizo zilizohamisha watu au wananchi sehemu moja hadi nyingine kujaribu kuondoa UKABILA

Na Angalia JERRY SLAA U-MEYA anafanya part time; FULL TIME yeye ni MKULIMA angalia @ his AGE anaweza kupata ARDHI sehemu yoyote NCHINI yenye RUTUBA; William nadhani umetembelea KENYA au Una Marafiki wakenya wenye pesa au Ulisikiliza Debate za wanaotaka Urais kenye they way LAND issue is a HOT BUTTON

Hakuna Umilikaji wa ARDHI kama HAPA; ARDHI HAIOZI tutafika ni sawasawa na MADINI; NYERERE alijua tuna MADINI hakutaka kuleta WAZUNGU waje waanze kufanya scramble for our Minerals... alitaka tuamke tujue jinsi dunia inavyokwenda

sasa hivi tunajua Makosa ya ZAIRE waliyoyafanya; NIGERIA waliyoyafanya na tuna MACHO yamefunguka na ni Makubwa
yeah Hatukuendelea sana; lakini KENYA wako MBELE zaidi yetu?? la hasha; UGANDA Je? la Hasha; Zambia Sidhani... Zimbabwe ndio inakwenda chini...

So what we do have PEACE... and our LAND....
 
Wakati tunapata uhuru, Nyerere alikuwa na miaka nane zaidi ya Jerry Silaa wa leo.
Kiongozi wa Tanganyika kubwa kijiografia ikiwa na miundo mbinu tata. Wasomi wachache. Changamoto nyingi kutokana na mfumo wa mataifa makubwa yenye mivuto tofauti. Hali yenye tete ila watu wnye matumaini makubwa baada ya ukoloni.Pamoja na hayo yote, aliishi kwa malengo yake. Aliamini katika umoja wa waafrika kujiletea maendeleo wenyewe, alipigania uhuru wa Afrika, alijitahidi kutokomeza ukabila (kwa kiswahili na kupeleka watendaji katika maeneo yasiyo ya kwao), aliunganisha Tanganyika na Zanzibar na kuweka azimio la Arusha. Kwa muda aliofanya kazi alipoona sera zake hazijafanikiwa, alipisha wengine wafanye.

Leo miaka 28 baada ya yeye kutoka madarakani ambayo ni umri ulio karibu na umri wa kati kwa nusu ya watanzania (vijana) hakuna nuru. Nusu ya hiyo miaka ni baada ya kifo chake. Kimetushinda nini kufanya mabadiliko makubwa?

Akiwapo madarakani tulifanikiwa kuongoza kwenye mambo ya elimu na afya. Shilingi iliwahi kuwa na thamani kubwa. Tulitoka kwenye kusafirisha chakula nje na kuingiza chakula kwa kiasi kikubwa. Kuna kipindi uchumi uliyumba na wananchi waliiona hali hii katika maisha yao ya kawaida.
Leo elimu hoi, afya hoi, uchumi tunaambiwa unakua, watu wanakufa na njaa wakati hata ukame haupo, utapiamlo tunaongoza, deni la ndani linakua, viwanda hoi, kila kitu ilimradi tu.

Miaka aliyo nayo Jerry Silaa na wengine wengi viongozi wanaochipukia, ndio umri ambao Nyerere alianza kupigania uhuru. Alikuwa na changamoto nyingi za kihistoria kama tulizonazo leo lakini aliongoza angalau kufika mahali fulani.
Hawa kina Jerry Silaa na wengine tunaojiita wasomi na viongozi wa leo tunaouthamini ubepari na kutweza siasa za Nyerere tumefanya nini kikubwa hata hapo tunapoongoza? Nina uhakika udhaifu wetu ni mbaya kuliko aliounyesha Nyerere na mara mia hata huo uongozi tusingepewa.
Hii ni sawasawa na kumlaumu babu yako kwa nini hakukubali kuchukuliwa utumwa Marekani kusudi wewe uzaliwe marekani. Sawasawa na kumlaumu babu yako marehemu kwa nini hakumiliki kijiji kizima ili wewe leo uwe tajiri. Kazi bure. Kifupi hatuna maana ya kuendelea kuishi.
 
- Kiwe kisiwe it does not matter, it is what it is! ila hakuna tena elimu ya bure, wala mishahara bila kazi kama zamani!!

Le Mutuz

Mtu mpuuzi kama huyu eti naye ni kiongozi ndani ya CCM,chama kinacho jinasibu kama chama cha wakulima na wafanyakazi! Ni mlevi ambaye hajui hali ya umasikini uliokithiri kwa Watanzania milioni kadhaa! Anatwambia watoto wa familia hizi masikini wasipate msaada wa serikali kusoma bure!!!

Mwalimu Nyerere aliamini kwamba msaada wa msingi wa kusaidia wananchi masikini ni kuwapa elimu watoto wao. Sishangai wajinga kama huyu wanaona msaada muhimu ni kumkopesha afanye umachinga,wakati watoto wake hawaendi
 
Back
Top Bottom