MEYA Jerry Silaa asema SIASA za UJAMAA na KUJITEGEMEA ni MBAYA, NYERERE alituharibu...

Derivation Barack, is Baraka, Mbaraka, Mabrouk, Mbaruku, Mubarak, Mbarak, Mbalaka, Balaka or mBarack.

Ever heard of Bakili? that is Bakari, ever heard of Shaka Zulu? that is Sheikh Zulu.

Why is it so hard for you to understand?

nasisitiza na kukumbusha tena ubongo wako ni mkubwa sana , jaribu kuutumia wote ,,,, na siyo lazima kila kitu ushinde kwenye maisha.
 
Nyerere mwenyewe alijikosoa na akasema "mabaya" yake yaacheni mfate yale mazuri, mimi sijaliona mpaka leo.

Jerry Slaa ana haki ya kukosoa, anajuwa tulipotoka na hajajijaza ujinga mliojijaza nyinyi kufikiria kuwa kila alilofanya Nyerere ni jema. Nyerere na Siasa yake ya majaribio, Ujamaa na Kujitegemea ilitufikisha tukawa maskini hohehahe.
Nchi kama malawi, zaire ya mobutu, rwanda, burundi, togo, ivory coast etc etc kama ubepari ni mzuri zingekua mbali kimaendeleo kuliko sisi. Tofautisha ubepari katika nchi zilizokua na makoloni na zilizotawaliwa. Huku kwetu ubepari ni kunyonywa tu na kuporwa na mabepari kupitia mabepari uchwara kama kina rostam na viongozi wala rushwa. Kenya kupata katiba mpya hadi wanaunda tume ya maridhiano utadhani ndio wamepata uhuru kwa madhila waliopata tangu kupata uhuru wakiwa na sera za ubepari.
 
Na wewe mtoto wa juzi kama huyo Jerry Slaa au vipi?
Kijana mwenyewe wala hajablehe katika siasa na hajui anachoongea.
Umenena sawa labda kasikia kuhusu ubaya wa ujamaa kutoka kwa baba yake bepari uchwara kwani wakati ujamaa unawakomboa watanzania toka makucha ya ubepari na kuwarudishia heshima yeye alikua ananyonya.
 
Anayetukana ujamaa ni wa kuogopwa kama ukoma Nyerere angeendesha ubepari hakuna kiongozi angesoma wa leo ,tusilewe madaraka raka hili ni kosa la kikwete kuteua watu kama huyu kamati kuu bila kufikiri huyu kijana hana busara kabisa amekuliafamilia ya kitajiri baba rubani hajuishida za watanzania masikini,anaposema wavivu je serikali yake inaviwanda vingapi watu wameacha kwenda kufanya kazi au huyu jerry ameanzisha Godown ya cement pale mombasa ukonga ,je ameajiri watu wangapi au amewaita watu hawataki kazi shame on this boy ni Mujinga tu
Kamekalia kula rushwa hadi kumevimbiwa halafu kanadhani ni mafanikio ya ubepari
 
Nyerere mwenyewe alijikosoa na akasema "mabaya" yake yaacheni mfate yale mazuri, mimi sijaliona mpaka leo.

Jerry Slaa ana haki ya kukosoa, anajuwa tulipotoka na hajajijaza ujinga mliojijaza nyinyi kufikiria kuwa kila alilofanya Nyerere ni jema. Nyerere na Siasa yake ya majaribio, Ujamaa na Kujitegemea ilitufikisha tukawa maskini hohehahe.
Inaelekea wewe na huyo kinda wako kiakili ngoma droo.
Argument yako inajipinga maana umeshindwa kuitumia falsafa ya kujitegemea in practice kwa kutegemea kuwa mtu fulani atakuendeleza.
Hata falsafa ys JK itawashinda kwa vile wala hamuelewi kuwa ya kuambiwa, changanya na za kwako.
 
CCM iko katika hstari kubwa sana ya kukosa kabisa viongozi wenye akili na maono ya kiwango Mwalimu
Kwa statements kama za huyu Meya ambaye vile vile ni mjumbe wa NEC ya CCM, ni jambo la kusikitisha.

Tatizo kubwa hata huo ubepari unaoongelewa hawajui hata jinsi ya kuuiga.

Kinachosikitisha ni vijana wadogo ambao wala hawaelewi hata misingi ya ujamaa na kujitegemea kwa context ya Mwalimu, ati wakiukosoa hadharani!

Mbaya zaidi ni ukweli kuwa ni misingi ya usawa ns kuenzi ubinadamu kitu kilichoenziwa na Mwalimu ndiuo kimewafikisha hapo walipo.
Ukweli huo huo utadhihirisha kuwa kama si mwalimu wengi wao wangekuwa watwana na manamba ndani ya nchi yao.

Tumwulize Mstahiki Meya swali rahisi tu: Je Tanzania kama Nchi tikichuma Kibepari tukafaidi matunda ya Nchi yetu kama Wajamaa kuna tatizo gani?
Hivi Meya wetu hajui kuwa Serikali na Raia wake wanategemeana? Ili Serikali itimize majukumu yake kwa Wananchi Meya hajui kuwa itategemea kodi zao? Na Wananchi wanapolipa kodi zao si wanategemea Serikali yao iwajibike kwao? Hata hili Meya halijui?
 
Nyerere hajasaini mkataba hata wa Tanzania kupata 0.

Kumbuka hiyo asilimia 3 imeshapandishwa na kuwa 4, halafu uelewe hiyo ipo siku zote mpaka pale mtaji wa waliowekeza utakapo rudi, Tax zinakuwepo kama kawaida na marupurupu mengine kibao.

Isitoshe, hivi wewe ulikatazwa kwenda kuchimba madini?
FYI - Mwl. JKN left those minerals so that you and I could benefit; but due to poor leadership we got more than 20 Trillion TZS in Debt with nothing to show. I wonder if that is what you call economic development?
 
Umenena sawa labda kasikia kuhusu ubaya wa ujamaa kutoka kwa baba yake bepari uchwara kwani wakati ujamaa unawakomboa watanzania toka makucha ya ubepari na kuwarudishia heshima yeye alikua ananyonya.
Ni vema sasa kujiuliza kuwa kijana mpaka anakuwa mNEC hajui historia yake, ni muafaka sasa kujiuliza kafika fikaje huko bila kuwa na uelewa wa historia ya chama.
Matokeo ya kuua vyo vya chama kama Kivukoni ndio matokeo yake, tunapata viongozo mediocre.
 
Ujamaa bado hupo kwa kiasi kikubwa sema tu namna unavyotumika ndivyo sivyo.

Kwa kiasi kukubwa ujamaa unaonekana sana vijijini kuliko mijini.

Sawa tulialibiwa na Rais wa kwanza katika sera ya ujamaa,vipi kuhusu
ile sera pacha ya kujitegemea?

Kwani ni sera pacha ujamaa yaani kujitegemea ndio iliyovunja nguvu ya wajamaa
walio wengi ambao ndio hao hao leo hii wamegeuka kuwa mabepari.

Kwa mtazamo wangu tafsiri ya ujamaa na kujitegemea ilibeba dhana mbili za ukomonist na ile ya
ubepari (ukomonist=ujamaa,kujitegemea=ubepari).

Kwa mantiki hiyo ni wazi kabisa wale waliopinga ujamaa leo hii ndio mabepari kwani ni hao
hao ndio waliopelekea kuvunjwa kwa azimio la arusha lililounganisha dhana mbili hizo.
 
Imebidi kumfanyia due diligence huyu mstahiki,lakini nimeona hii comment humu JF,

Mara ya kwanza kulisikia jina la jerry slaaa ni humu ndani jf,na mazungumzo yalikuwa ya kumfagilia wakati anagombea unaibu meya wa ilala,sasa hivi karibuni wakati natazama tv,nikaona kitu cha kushangaza sana,siku ya kwanza nimemuona huyo jerry slaa akiwapokea warembo wa miss tanzania ofisini kwake na mazungumzo yasio na kichwa wala miguu,siku ya pili ndio nilibaki mdomo wazi baada ya kumuona huyo jerry slaa ndani ya limousine akiwasindikiza hao warembo kwenda kwenye kambi ya miss tanzania pamoja na matarumbeta na sare ya khanga kwa watumishi wa manispaa ya ilala.

Sasa nimekuwa na maswali kibao kuhusu huyo jerry slaa
je jerry slaa ni nani hasa kimtazamo na kimisimamo
yeye agenda zake hasa ni zipi katika mipango yake ya kuwa naibu meya????
Kwa nini anaonekana kuwa na washabiki wakati binafsi namuona
kama ni immature politician ambaye hana lolote zaidi ya kuwa
young but empty personality.????
Tafadhalini kama kuna mtu humu ana mfahamu vizuri huyo jerry slaa ningependa kufahamu
je yeye haoni ni ujinga mtupu kwa yeye kufunga ofisi na kuingia kugharamia limousine na khanga za sare kwa kuwasindikiza warembo tu kambini??????????
Mwenye CV yake tafadhali tupostie.
 
Kwa hiyo ubepari na utegemezi ndiyo sera nzuri. eeh? Naona Kikwete anawakilisha kweli na bakuli mkononi.

Rais wa Kwanza aliyefuta utegemezi kutoka asilimia 60% wakati wa Nyerere mpaka kufikia 30% wakati wake ni Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete, na bado inashuka. Upo hapo ulipo?
 
FYI - Mwl. JKN left those minerals so that you and I could benefit; but due to poor leadership we got more than 20 Trillion TZS in Debt with nothing to show. I wonder if that is what you call economic development?

You can never get a loan if you are unable to repay. Simpo rule.
 
Inaelekea wewe na huyo kinda wako kiakili ngoma droo.
Argument yako inajipinga maana umeshindwa kuitumia falsafa ya kujitegemea in practice kwa kutegemea kuwa mtu fulani atakuendeleza.
Hata falsafa ys JK itawashinda kwa vile wala hamuelewi kuwa ya kuambiwa, changanya na za kwako.

Falsafa iliyofeli into practice.
 
Nchi kama malawi, zaire ya mobutu, rwanda, burundi, togo, ivory coast etc etc kama ubepari ni mzuri zingekua mbali kimaendeleo kuliko sisi. Tofautisha ubepari katika nchi zilizokua na makoloni na zilizotawaliwa. Huku kwetu ubepari ni kunyonywa tu na kuporwa na mabepari kupitia mabepari uchwara kama kina rostam na viongozi wala rushwa. Kenya kupata katiba mpya hadi wanaunda tume ya maridhiano utadhani ndio wamepata uhuru kwa madhila waliopata tangu kupata uhuru wakiwa na sera za ubepari.

Huko kulikuwa na madikteta si mabepari. Fikiri, Hapa tulikuwa na dikteta aliyetufanya wote "guinea pigs" wake kutufanyia majaribio ya falsafa yake ya Ujamaa na Kujitegemea iliyoshindwa akawaacha 90% ya watu kuwa misukule, kila inayoambiwa, "ahsante baba", Nyerere akijichekesha na yenyewe inacheka, hata haijui ianchekelea nini, ikitoka hapo inawahi foleni za sukari, kilo moja kwa kaya moja kwa wiki nzima (siku ikiwepo).

Upo hapo ulipo?
 
Miaka michache tu toka kifo cha Muasisi wa taifa hili na Chama tawala anapatikana Meya toka Chama kilichoasisiwa na Hayati Mwl Nyerere tena Meya msomi mwenye uthubutu wa kusema "Nyerere alituharibu" Kweli?....

Kijana aliye msomi ni yule anayekumbuka alikotoka.
Kwa tafsiri nyepesi inaonekana kana kwamba anamtuhumu marehemu ili tu
asiwe na huruma kwa wale anaowaongoza kwa kuzingatia kuwa siku zijazo
jiji la Dar es Salaam litakuwa si jiji la kijamaa tena kwa maana ya kuishi.
 
Back
Top Bottom