Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,986
- 156,264
CCM ya leo ni chama cha kifisadi
Hajanielewa Mkuu nilitaka kumrudisha Uarabuni halafu nimtightmama toto ni kama nakuona vile ulichomaanisha kwa Faiza
Nadhani na wewe ni mvivu kati ya hao anaowasema Jerry, mwenzio anakuja na analysis wewe unaruruka tu na vineno vya kanga. JF ni mahali pa kujifunza vilvile kama huna la maana ni bora kukaa kimya. Hivi leo CCM ni chama cha namna gani? mbona hamtangazikwamba kinafuata mrengo wa Kibepari, hapa Nape anaweza kuja na kusema CCM ni chama cha kijamaa. Hivi leo wataka kuniambia hizo nchi unazosema zinalima sana ni za kibepari unajua wamefika hapo? Kwa akili yako unadhani walilala na kuamka wakaanza kuwa mabepari, toka tupate uhuru mnaongoza nchi na siasa ya Ujamaa na kujitegemea. Jerry Slaa kwakuwa ni Meya ana fursa za burebure ndiyo anaona kwamba ana uwezo wa kujituma na kuwa bepari?
Hajanielewa Mkuu nilitaka kumrudisha Uarabuni halafu nimtight
Jerry Silaa ni mfano mzuri wa kiburi (arrogance) ambayo aghalabu huwanyemelea binadamu waliopata ngekewa ya mafanikio kidogo. Ironically hawa binadamu wanaopata "mafanikio" ya haraka haraka kwa njia za mashaka ndio wanaoonesha zaidi kiburi cha namna hiyo. Mifano ipo mingi. Unakutana na kijana amehonga-honga all his/her way up, akishafika sasa, simply kwasababu anaweza kusimama mbele za watu wakamsikiliza basi nasaha zake zitakua: "....vijana wasikae tu kulia lia oh serikali hili serikali lile...watu wajitume, wafanye kazi kwa bidii watafanikiwa tu...kama mimi!!" ukweli wa mambo wa "kujituma" kwake "anausahau" kidogo. Kwa sie wengine tunaojua ukweli wa harakati za watu kama hao tunapata shida kweli...
CCM iko katika hstari kubwa sana ya kukosa kabisa viongozi wenye akili na maono ya kiwango MwalimuMiaka michache tu toka kifo cha Muasisiile misingi ys ujamaa na kujitegemeawa taifa hili na Chama tawala anapatikana Meya toka Chama kilichoasisiwa na Hayati Mwl Nyerere tena Meya msomi mwenye uthubutu wa kusema "Nyerere alituharibu" Kweli?....!
are you his father?
is mbarack ,his official name?
au analitumia nyumbani?
Sidhani na wala sikutegemea kinda kama Jerry Silaa kuwa na ubavu wa kumkosoa Mwalimu kisera kiitikadi na hata kimaadili.
A. H. Mwinyi mwenyewe, kiongozi wa kusifika alisha sema akijilinganisha na Mwalimu yeye ni kichuguu!!!
Sijui huyu Silaa anapata wapi ujasiri wa kukosoa sera za Mwalimu, ilhali si msomi wa itikadi hiyo.
Isingekuwa sera za Mwalimu pengine baba zake wasingemfikisha hapo alipo.
Tatizo mtu anapokuwa amekula na kushiba , yule asiye na maadili huvimbiwa na kutapikia miguu ya waliomfikisha hapo.
Faiza - Mwl. Nyerere ndiyo alisaini mikataba ambayo Taifa la Tanzania linapata 3% ya mauzo ya madini?Nyerere mwenyewe alijikosoa na akasema "mabaya" yake yaacheni mfate yale mazuri, mimi sijaliona mpaka leo.
Jerry Slaa ana haki ya kukosoa, anajuwa tulipotoka na hajajijaza ujinga mliojijaza nyinyi kufikiria kuwa kila alilofanya Nyerere ni jema. Nyerere na Siasa yake ya majaribio, Ujamaa na Kujitegemea ilitufikisha tukawa maskini hohehahe.
Faiza - Mwl. Nyerere ndiyo alisaini mikataba ambayo Taifa la Tanzania linapata 3% ya mauzo ya madini?
Hana pointi, hicho alichoandika unaona sio pointi?Huna point.
Nchi zinazolima zaidi duniani ni zile zenye mfumo wa Kibepari.