Membe awavaa wanasiasa wanaojisafisha masikitini, mkanisani

Pigo moja, pigo lenye nguvu, pigo takatifu. Angalau kuna mtu amenyanyua mdomo kuwaambia ukweli viongozi wa dini. Lakini kwa ushabiki wetu uchwara kuna watu wataona kwamba mungu wao ametukanwa kumbe waliopewa live ni waponyaji wa roho zetu, na siyo huyu mwizi wa mali zetu anazozitapanya sasa hivi.

Hivi humuogopi Pasco wewe? Subiri akushukie kama mwewe baada ya kudaka mshiko wake. Shauri yako!
 
Jamaa anadhani kwamba kwa kufanya hivyo anajitakasa, kumbe anachokifanya ni money laundering, tena kwa kutumia nyumba za ibada. Bila kutubu Mungu hawezi kumsamehe. Maskini urais unamuendesha mbio, anazunguka kama pia. Tayari amesha-book hafla hadi za mwakani aalikwe.

Kweli jamaa kapania, lakini urais huu mbona atakuwa ameusotea sna maskini halafu hataupata.
 
Pigo moja, pigo lenye nguvu, pigo takatifu. Angalau kuna mtu amenyanyua mdomo kuwaambia ukweli viongozi wa dini. Lakini kwa ushabiki wetu uchwara kuna watu wataona kwamba mungu wao ametukanwa kumbe waliopewa live ni waponyaji wa roho zetu, na siyo huyu mwizi wa mali zetu anazozitapanya sasa hivi.
Hapa mkuu jamaa amemaliza bila kuangaliua sura!
Hapa Lowassa analimwa kijembe cha bila kukwepeshewa sura!
Hakika ukifuta Harambeeza makanisa, sielewi baadhi ya wanasiasa watapitia njia gani kuwakamata washabiki!
Nadhani wapo wanasiasa ambao wametenga billions kwaajili ya kuzipenyeza popote wanapoona watu wanadhiki, ili tu kuteka akili zao kwa 2015!
Membe naye yumo kwenye mkondo mbovu!...Yeye alianza kampeni zamani sana, na anadhani mbinu zake hazijulikani.
Wote vipofu hawa!
 
Wote vipofu hawa
!

Hapo kwenye red hebu tudadavulie tuelewe. Mimi nadhani hoja siyo kupiga kampeni na tungefurahi kama huyu bwana angekuwa anapita kwa wananchi kuendesha mikutano ya hadhara na kujinadi maana si dhambi kujitangaza na kutangaza nia yako. Tatizo ni huu mtindo aliouiga kutoka Kenya ambako hata misiba inageuka kuwa majukwaa ya kisiasa. Kama ulivyosema, harambee za kwenye nyumba za ibada zikifutwa, jamaa atakuwa amewekwa plasta mdomoni.
 
Hivi Membe anadhani anaweza kuwa Raisi,hana personality hiyo,kumchagua inaweza kuwa janga kuu la kitaifa,wote na Sumaye na Lowasa hakuna Raisi hapo.Kwanza shangaa anaongelea wanasiasa wanaotumia taasisi za dini wakati naye yuko na hao hao,sasa which is which.

wacha wajidanganye wamsimamishe ili iwe aibu yao. Bwana akauliza "ni nani atatoka na kwenda kudanganya mfalme, malaika mmoja akatoka"
 
Huyu jamaa na mnafiki kweli, anazungukia kwenye Harlan za dini kuonya wale wanaotumia dini...what a joker!
 
Huu ndio uongozi.jambo la kupandikiza udini ni jambo la kukemea tena kwa sauti kubwa. Kauli hii inanikumbusha msemo wa Mwanazuoni Samwel Huntngton, mwandishi wa kitabu cha "Clash of Civilization" akisema, " mambo yanayotuunganisha ni muhmu zaidi kuliko yale yanayotugawa".

Dini zetu hazituunganishi bali zinatugawa. Makabila yetu hayatuunganishi bali yanayotugawa, vyama vyetu havituunganishi bali vinatugawa. Tunaunganishwa na utaifa wetu, tnaunganishwa na utu wetu. Haya ndio mambo ambayo kiongozi yoyote muhimu wa nchi hii katika ngazi yoyote anapaswa kuyasimamia.
 
CCM Ingekuwa treni ningeiita "a runaway train without a driver". Kinachokera ni kwamba kwenye mavurugu yao hata wananchi tunaathirika.
 
Pamoja na kuwa wote wawili ni mafisadi/wapambe wa mafisadi, membe anaweza kutuambia huyo 'anayejisafisha' alichafuka lini na tangu achafuke serikali na chama cha membe wamemuwajibisha vipi?! Vurugu ktk nchi hii zitaletwa na ccm ya akina membe na serikali yao legelege... Hivi anajua ubalozi wa Libya unapeperusha bendera gani?
 
for me lowassa is better than member..in fact than all members of the cabinet..lowassa atleast kuna kitu tangible anaweza kutuonyesha amefanya,membe atatuonyesha nini?usiniambie lowassa fisadi sababu ccm hakuna asiyekuwa fisadi,wanatofautiana viwango na kulingana na sehemu ya ulaji uliyowekwa.
 
yeye alipoamua kusilimu kipindi hiki ili kutuhadaa wakristu na kwa upande mwingine waislamu nani amemuuliza kama si mnafiki. Acheni kuchafuana wakati wote mnawahadaa watz kutumia kicho la dini. Membe huwezi aminika japo tunajua mnafanyiana umafia kutafuta uraisi. Leteni mbadala wa namna ya kutatua kero za wananchi siyo kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Ni heri Kikwete mara mia kuliko wewe.
 
for me lowassa is better than member..in fact than all members of the cabinet..lowassa atleast kuna kitu tangible anaweza kutuonyesha amefanya,membe atatuonyesha nini?usiniambie lowassa fisadi sababu ccm hakuna asiyekuwa fisadi,wanatofautiana viwango na kulingana na sehemu ya ulaji uliyowekwa.
membe katuonyesha kwamba siyo fisadi
 
Mbona sarakasi za Urais zimekamata mijadala kila kona ya Taifa hili kuliko hata mijadala ya shughuli za maendeleo, kama kweli tunge Invest akili zetu na jitihada zetu ktk shughuli za kujiongezea kipato na uchumi wa Taifa hili, naamini leo tungekua tunaongea kwa mtazamo tofauti.

Ufike wakati tuwaambie wanasiasa na wapiga debe wote kwamba bado kuna miaka 3 zaidi mbele, na bado tuna Rais anayeliongoza Taifa hili. Hiyo mijadala ilitakiwa ipewe nafasi kama Taifa letu lingekua limekosa Serikali inayotawala na kama tungekua hatuna Rais. Enough is Enough. Tuelekeze Fikra, Akili na Jitihada zetu ktk kuinua uchumi wa Taifa hili.
 
Hii kitu Lowassa vs. Membe inanikera kweli kweli. Imekaa kinafi nafiki kwa upeande wa Membe. Wanamkandia Lowassa nje kwenye majukwaa nje ya chama chao lakini wakirudi kwenye vikao vyao huko ndani na Lowassa akiwepo wanaufyata mkia. Hii inamaanisha nini kama si tabia ya umbea wa kike kwa upande wa Membe?

Watu wengine tunasympathize na Lowassa si kwa sababu hatujui ufisadi wake, bali tunachukizwa na umbea na unafiki wa maadui zake. Bora kiongozi fisadi kuliko kiongozi mnafiki. Anaweza kuuza hata nchi kwa unafiki wake huu huu.
 
for me lowassa is better than member..in fact than all members of the cabinet..lowassa atleast kuna kitu tangible anaweza kutuonyesha amefanya,membe atatuonyesha nini?usiniambie lowassa fisadi sababu ccm hakuna asiyekuwa fisadi,wanatofautiana viwango na kulingana na sehemu ya ulaji uliyowekwa.

Whatever it is! Alichokisema Membe siyo cha kupuuzwa hata kidogo...... nafikiri inabidi apongezwe kwa kumfunga paka kengere. Wakati tunapigana na hii dhana ya udini unaoshamili kila siku kwenye siasa, haiwezekani kiongozi wa siasa kila mwezi yuko kwenye makanisa anafanya Harambee na kuchangia mamillion ya pesa bila hata kuulizwa anazitoa wapi??? Kwa ujumla Membe yuko sawa whether anatafuta Urais or not!!!
 
Kuna mwenye guts za kumuuliza?:shock:
 
Pigo moja, pigo lenye nguvu, pigo takatifu. Angalau kuna mtu amenyanyua mdomo kuwaambia ukweli viongozi wa dini. Lakini kwa ushabiki wetu uchwara kuna watu wataona kwamba mungu wao ametukanwa kumbe waliopewa live ni waponyaji wa roho zetu, na siyo huyu mwizi wa mali zetu anazozitapanya sasa hivi.

Membe hajaremba maneno,kasema moja kwa kwa moja na mwenye masikio na asikie.
Bravo
OTIS
 
Back
Top Bottom