Mei Mosi 2012: JK akasirishwa na utafunaji wa pesa za umma, wahusika kukiona...

Rais Jakaya Kikwete leo katika mei mosi amejibu madai yote yaliyotolewa na CHADEMA kwamba CCM na serikali yake inashindwa kushughulikia matatizo katika uchumi ikiwemo mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira kwa vijana, kupungua kwa uzalishaji na matumizi makubwa ya serikali ukilinganisha na mapato. Rais Kikwete ametoa majibu ya kina namna ambavyo kila tatizo limeshughulikiwa vizuri. Rais Kikwete amejibu pia madai ya CHADEMA kuwa ameshindwa kushughulikia ufisadi ikiwemo ambao umetajwa kwenye ripoti za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali. Rais Kikwete ameeleza kwa kina namna ambavyo toka mwaka 2007 Serikali imechukua hatua sahihi. Hotuba hiyo ya Kikwete imerejesha matumaini ya wananchi kwa CCM na kwa serikali iliyoko madarakani.
Please wait downloading is on process..............0.5%!
 
JK ana 'double standards'. Mkwe.re sio mtu wa kuaminika hata siku 1. He has two timing thinking, anasema hivi kumbe anamaanisha vile. Upunguani tu.
 
JK kumbe anajua ubadhirifu halmshauri tangu siku nyingi. Kumbe alimwita Uttoh akawachane Mawaziri na Makatibu Wakuu.
Blackbold:kama unayosema ni sahihi basi kuna tatizo kwa mkuu wa kaya katika kushughulikia mambo kwa haraka.
 
JK kumbe anajua ubadhirifu halmshauri tangu siku nyingi. Kumbe alimwita Uttoh akawachane Mawaziri na Makatibu Wakuu.
Hamna kitu,anajikosha tu Baada ya kuona mchele ushamwagika Hadharani, sidhan hata kama alikuwa na taarifa Bunge litajadili hiyo kitu katika level ile, sidhan kama hii ndo taarifa ya kwanza ya CAG kuonesha wizi wa Serkali yenu ya Magamba.
Kama hajui ni kwanini TZ Maskin angelijua hilo, acheni kumsifia Bwana enu,
Mark my words, move ilikuwa ni kumng'oa yeye, na hili litatekelezeka tu, mark my words.
 
jk sio kwamba amefanya kila kitu vibaya. Yapo machache aliyofanya vizuri kama hilo la cag. Tatizo ni kwamba mengi ameyafanya vibaya mno, kama kutowafikisha wahalifu kwenye vyombo vya sheria.
 
Rais JK amesema amefurahishwa taarifa ya CAG imepewa nafasi yake kujadiliwa na mapendekezo ni mazuri.
Serikali imejipanga kuyatekeleza.
Yeye kama Rais ndio alipendekeza reports za CAG ziwekwe wazi bunge na wananchi wazisome na kujadili.

UPDATES
-alimuagiza CAG aimarishe ofisi yake.
-sheria ya ukaguzi iliboreshwa na CAG alipewa mamlaka zaidi
-hakuna chombo nchini chenye mamlaka ya kumuondoa au kumdhibiti CAG
- CAG akigundua kuna hali ya wizi, akabidhi wahusika kwenye vyombo vya dola wakati uchunguzi unaendelea

Hakuna baraza jipya la mawaziri
Hapo kwenye red hata rais hana mamlaka ya kumuondoa CAG
Hili la kwamba ni yeye ameamua kuziweka wazi ni uongo maana hata miaka mingine ya nyuma kabla ya uongozi wake zilkuwa ninawekwa wazi lakini kwa sababu wabunge wa ccm hawakuwa wanajua kazi zao zilibaki kuangaliwa bila kuzifanyia chochote na hata maamuzi yao yalipokuwa hayatekelezwi bado hawakuwa na la kufanya.
Kwa mfano si bunge lilikuwa likiombwa baadhi ya hasara za wizi zifutwe? sasa kama ilikuwa ni siri waliombwaje wabunge ruhusa ya kufuta zile hasara zilizotokana na wizi kwenye wizara na halmashauri? Uongo una mwisho wake na mwisho wake ni huu.
 
Awawajibishe na si kuongea ongea ahakikishe anapiga chini mawaziri wote wabovy, piga chini wakuu wa mikoa na wilaya wabovu,piga chini wakurugenzi wabovu piga chini yaani piga chini wanafiki wote akimaliza kama na yeye anapenda ajipige chini!
 
Rais anasema UWONGO, kwani angekuwa anamaanisha anachokiseam basi leo hii wale jamaa si mawaziri tena walisha fukuzwa siku nyingi sana.

Tatizo kwenye hotuba yake hakuna sehemu ya maswali na majibu. Otherwise watu wangemuumbua.
 
MY TAKE
1. Anaonekana yuko very much concernedna huu wizi sasa sijui atachukua hatua gani.
2. Hivi kwa nini katka level yamkoa/wilaya wasiwe wanazijadili izi taarifa za CAG to the respective region/district pamoja na utumbo wao kuwekawa hadharani hasa kwenye vile vikao vinavyo involve madiwani ili angalau kuwe na seriousness.
3. Kama CAG alishapewa rungu la kukabidhi polisi wahalifu mbona hawa mawaziri ndo kwanza twaambiwa sound za CAG.

Wewe humjui JK....
 
Rais anasema UWONGO, kwani angekuwa anamaanisha anachokiseam basi leo hii wale jamaa si mawaziri tena walisha fukuzwa siku nyingi sana.

Tatizo kwenye hotuba yake hakuna sehemu ya maswali na majibu. Otherwise watu wangemuumbua.

Mngeyajuwa bila yeye kurekebisha mfumo wa ukaguzi? mngeyajuwa bila yeye kubuni kamati za kusimamia wizara na taasisi na idara?

Sasa mmeyajuwa na ushahidi mnao mnangoja nini kwenda kushitaki? kama hamjui namna ya kushtaki, muulizeni Mtikila.
 
Ni kweli kabisa katika utawala wa awamu ya nne umeimarisha ofisi ya ukaguzi ya Taifa. Vijana wengi wamesomeshwa katika taaluma mbalimbali. Nadhani pia kuna political will ya kuisaidia ofisi hii ndio maana hata report zimekuwa za wazi na zinagonga hasa.

Ni kweli kabisa mkuu. Madudu haya hayakuanzia kwa JK, ila kwa kuwa JK kaja wakati ambao hana jinsi zaidi ya kuachia mambo wazi, maana akibania yeye wengine watavujisha na kujadiliwa kama scandal. Ukiangalia taarifa za EPA etc zilikuwepo na walizibania ila kwa kuwa zilivujishwa na watu kuzisoma kwa ku 'double click' tu iliwalazimu kujifanya wapo deep.

JK anaweza kujipatia credit kuwa ameacha Govt kuwa wazi, lakini kwa upande mwingine ni kwamba asingekuwa wazi na kuziachia report hizi ni dhahiri urais wake ungekuwa rehani maana tungekuwa tunajadili kashfa kila siku. Weakness kubwa sana ya JK ni

  1. Kutaka kuonekana yupo serious na masilahi ya nchi bila kumuumiza yeyote yule. Yaani yeye kutaka kuonekana ni mwema kwa kila mtu, ndiyo maana anaachie taarifa za wengine ziwe public kwa hisia kuwa labla wahusika wataacha wakiandamwa na public criticism. Hapo amekoea kwelikweli.
  2. Kujifanya kuwa yeye hahusiki na mambo mengi na wakati mwingine kuwa tayari kuwabebesha mzigo watu wengine kwa ahadi ya kuwalinda
  3. Kuogopa kuwashughulikia watu ambao walimkingia kifua kuhakikisha kuwa anaitwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Haya ni madhara makubwa sana katika kutawala bila kuingiliwa. Watu ambao wanafahamu mambo yako mengi ya nyuma ya pazia 'waufanya mateka urais wako'. Yaani ni kama vile mtu anapicha zako mbaya na anajua akiziweka public wewe unakuwa huna thamani anapokutaka umfanyie mambo ambayo ni kinyume na sheria na ukikataa anakuanika.

Ni kweli kabisa 'transparency is the key to good governance', but transparency without taking legal actions for those who are implicated is useless.
 
Binafsi nampongeza kwa hatua yake ya kumwongezea nguvu CAG, lakini sikubaliane na hatua yake ya kuwabembeleza hao mawaziri yeye ndo tunamtambua kama rais wetu, asifanye mchezo tutaiondoa ccm 2015!
 
Hiyo ni misemo ya watu wavivu, wazembe, wasiowajibika nk. Iko misemo mingi ya aina hiyo ya watu wa aina hiyo.
 
Rais JK amesema amefurahishwa taarifa ya CAG imepewa nafasi yake kujadiliwa na mapendekezo ni mazuri.
Serikali imejipanga kuyatekeleza.
Yeye kama Rais ndio alipendekeza reports za CAG ziwekwe wazi bunge na wananchi wazisome na kujadili.

UPDATES
-alimuagiza CAG aimarishe ofisi yake.
-sheria ya ukaguzi iliboreshwa na CAG alipewa mamlaka zaidi
-hakuna chombo nchini chenye mamlaka ya kumuondoa au kumdhibiti CAG
- CAG akigundua kuna hali ya wizi, akabidhi wahusika kwenye vyombo vya dola wakati uchunguzi unaendelea

Hakuna baraza jipya la mawaziri

Cag mwenyewe kilaza alishindwa kukamata wizi wa jairo tutamwamini vipi?
 
Back
Top Bottom