Mei Mosi 2012: JK akasirishwa na utafunaji wa pesa za umma, wahusika kukiona...

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
MAY DAY 2012:JK - MJADALA WA BUNGENI JUU YA KAMATI NA REPORT YA CAG

Anasema ukiwa kiongozi lazima uwe nangozi nene!

Alifurahishwa na ule mjadala kwa kuupa uzito taarifa ya CAG

Anasema amejipanga kutekeleza mapendekezo hayo b'se hata kujadili taarifa ya kuijadili ni matashi yake ijadiliwe bungeni. Kabla ya hapo izi taarifa zilikuwa haziwekwi wazi.

Anasema kwenye hamashauri kuna mchwa wanakula noti za serikali.

Lengo lake juu ya huu ukaguzi nikuhakikisha na fedha za umma zatumika ipasavyo!

Sheria iliyomwanzisha CAG inamlindakuondolewa maana kuna wakati anaikosoa mpaka ikulu.

Anasisitiza kuwa wanaobainika naubadhilifu CAG kabidhi kwa PCCB na kwa Polisi kwenye ibara ya 27.

So far kuna wakaguzi 378 hii yote nikuiwezesha ofisi ya CAG pamoja na kuwajengea ofisi zao kimkoa!

Anasema hamashauri wanatumia ela kamaUbani wa kilioni yaani hazina mwenyewe.

Aliajiri wahasibu 795 ili watawanywemikoani kusiwe na excuse ya halmashauri kutokuwa na competentaccountants. Mwaka jana 72 halmashauri zilipewa hati safi mwaka janaso kuna improvement toka 56.

Wizara 50 good mashaka 10 ie kwa mwaka jana.

Value for money audit ikaanzishwaambapo mpaka maengineer wanatumika.

Kila idara ameweka wakaguzi wa Ndaniambaye anawajibika kwa Chief Internal Auditor na sio kwa mkurugenzi/wala kwa katibu mkuu wa mahala husika.

Kutakuwa na uwazi kwenye mgao wa fedhaza serikali na jinsi zinavyotumika.

Na speech ndo imeisha hakuna kipya kwa wafanyakazi ingawa kasema kutakuwa na nyongeza ya mshahara kwa next fiscal year


MY TAKE
1. Anaonekana yuko very much concernedna huu wizi sasa sijui atachukua hatua gani.
2. Hivi kwa nini katka level yamkoa/wilaya wasiwe wanazijadili izi taarifa za CAG to the respective region/district pamoja na utumbo wao kuwekawa hadharani hasa kwenye vile vikao vinavyo involve madiwani ili angalau kuwe na seriousness.
3. Kama CAG alishapewa rungu la kukabidhi polisi wahalifu mbona hawa mawaziri ndo kwanza twaambiwa sound za CAG.
 
"Kuwa kiongozi lazima uwe na NGOZI nene" (JK hotuba ya mei mosi, 2012).....Tafakari???
 
Rais JK amesema amefurahishwa taarifa ya CAG imepewa nafasi yake kujadiliwa na mapendekezo ni mazuri.
Serikali imejipanga kuyatekeleza.
Yeye kama Rais ndio alipendekeza reports za CAG ziwekwe wazi bunge na wananchi wazisome na kujadili.

UPDATES
-alimuagiza CAG aimarishe ofisi yake.
-sheria ya ukaguzi iliboreshwa na CAG alipewa mamlaka zaidi
-hakuna chombo nchini chenye mamlaka ya kumuondoa au kumdhibiti CAG
- CAG akigundua kuna hali ya wizi, akabidhi wahusika kwenye vyombo vya dola wakati uchunguzi unaendelea

Hakuna baraza jipya la mawaziri
 
Huyu JK hana jipya. Analete misemo na mambo yake ya ngomani, wakati sisi wananchi tunataka uwajibikaji wa Serikali.
Hayo mambo ya 'ngozi nene' akamwambie mwanae mwanaasha...
 
Na ni jk Alomteua CAG, hongera jk kwa hili hakuna mwenye ubavu wa kupinga,na amewapa mamlaka ya kushtaki moja kwa moja! Hakuna Rais alieiwezesha ofisi hii kwa vitendea kazi kama ndugu Rais!
 
Ni kweli kabisa katika utawala wa awamu ya nne umeimarisha ofisi ya ukaguzi ya Taifa. Vijana wengi wamesomeshwa katika taaluma mbalimbali. Nadhani pia kuna political will ya kuisaidia ofisi hii ndio maana hata report zimekuwa za wazi na zinagonga hasa.
 
JK kumbe anajua ubadhirifu halmshauri tangu siku nyingi. Kumbe alimwita Uttoh akawachane Mawaziri na Makatibu Wakuu.
 
Awapongeza wa bunge kwakazi waliyoifanya kule Bungeni kwa jinsi walivyo jadi taarifa ya CAG na kawaomba taarifa zote za CAG zijadiliwe bungeni na zipewe mda mrefu wakujadiliwa!Kawahaidi kutekeleza yale yaliyosemwa kwenye taarifa ya CAG
JK achukizwa na ubadhirifu wa pesa za umma serikali za Mitaa na Wizarani.
Kwa hotuba hii ya JK mawaziri wanapigwa chini shortly!!
 
Na ni jk Alomteua CAG, hongera jk kwa hili hakuna mwenye ubavu wa kupinga,na amewapa mamlaka ya kushtaki moja kwa moja!

JK hayo unayosema ni kweli?, au unapitisha upepo?. Ngoja tuone wale wezi wa kwenye riport ya CAG kama watashtakiwa.
 
Na ni jk Alomteua CAG, hongera jk kwa hili hakuna mwenye ubavu wa kupinga,na amewapa mamlaka ya kushtaki moja kwa moja! Hakuna Rais alieiwezesha ofisi hii kwa vitendea kazi kama ndugu Rais!

na TAKUKURU JE?
 
JK atueleze ya current report cause kutueleza ya 2007 ilhali tupo 2012 haiingii akilini kabisa! Ubadhirifu wa wilaya ya Bagamoyo nani asiyeujua unamuhusisha waziri wa sheria kwa sasa mama Selina Kombani vilevile mtoto kipenzi wa mkuu!
 
JK hayo unayosema ni kweli?, au unapitisha upepo?. Ngoja tuone wale wezi wa kwenye riport ya CAG kama watashtakiwa.

usipate kigugumizi kukiri kuwa utayari wa RAIS ndo umefanya tukajua tuliyoyajua,na usisite kumpongeza kwa hatua hii ya kwanza maana hao wenzie walopita hata hii wameshindwa,jiulize Accounting package ya chama chako mlonunua toka kwa Josephine mshumbuz ilifata taratibu za manunuzi?? CAG angekuwa anapita huko mngedai katumwa kuwavuruga!
 
Back
Top Bottom