Mdau wa Usafiri Mwanza: Nauli kutoka Dar-Mwanza iongezeke mpaka Tsh 83,861

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Zingatia Hii Kauli Nauli Zitapanda na Kila Kitu Kitapanda

Kiongozi wa Nchi anaamasisha wafanya biashara Kuongeza Bei ya Bidhaa bila hata aibu

---
Mwakilishi wa Kampuni ya usafirishaji Happy Nation, Ally Siddy Urasa, leo Aprili 13, 2022 katika mkutano wa wadau kujadili nauli za mabasi ya usafiri amependekeza nauli ya Dar es Salaam-Mwanza ipande hadi Sh. 83,861.
.
Katibu wa Umoja wa Usafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Salaam, Selemani Kimomwe amesema umoja huo unapendekeza bei ya nauli iongezeke kwa Sh. 400 "kwa maoni yetu tunaomba ongezeko la Sh. 400 kutoka kila nauli, mfano nauli ya 500 ipande kuja 900.
.
Tutaelewana Tu Si Mmesema Anaupiga Mwingi.
usafiri.jpg
 
Naona wamefocus na wamiliki wa vyombo vya usafiri tu, vipi wananchi aa kawaida au wasubiri tu maamuzi yatakayotoka hapo?
 
Kama mafuta yalikuwa 2500 yakaongezeka mpaka 2900 hilo ni ongezeko la 16%

Basi nauli iongezeke kwa range inayokaribiana na asilimia hiyo.

Mf nauli ya 50,000tsh. 16% ya nauli hiyo ni 8000. Hivyo nauli ichezee kwenye 58000tsh.
Hapo ni kwa kuangalia kigezo cha mafuta tu.
 
Back
Top Bottom