Mdahalo wa Ugomvi: Ati Nyerere alikuwa Dikteta; aliua wengi...

Watakuja wakina zomba waseme idadi ya watu ya kipindi cha Nyerere haikuwa kubwa Kama sasa hivi lakini bado naungana na wewe kwasababu ukijaribu kutafuta wastani utakuta vipindi vya hawa maraisi watatu wameua kipitiliza ukilinganisha na kipindi kile cha Nyerere ambacho hata neno fisadi halikuwahi kutajwa midomoni mwa wananchi

Kipindi hicho mafisadi ndo walikuwa wanaitwa wahujumu uchumi ambapo hilo neno ndo limekuwa derived to fisadi
 
Watakuja wakina zomba waseme idadi ya watu ya kipindi cha Nyerere haikuwa kubwa Kama sasa hivi lakini bado naungana na wewe kwasababu ukijaribu kutafuta wastani utakuta vipindi vya hawa maraisi watatu wameua kipitiliza ukilinganisha na kipindi kile cha Nyerere ambacho hata neno fisadi halikuwahi kutajwa midomoni mwa wananchi

Kipindi hicho mafisadi ndo walikuwa wanaitwa wahujumu uchumi ambapo hilo neno ndo limekuwa derived to fisadi, kama ntakuwa sijakosea ndivyo ilivyo
 
Wabunge 8 wa bunge la 1965 walifukuzwa bungeni sababu ya kudai mfumo wavyama vingi akiwemo Joseph kasela bantu wa tabora na modestus chogga wa iringa kusini na waliwekwa vizuizini mpaka wakafa

Waliuwawa, au walikufa tu. Au kufia kizuizini ni kuuwawa outright?
 
Two wrongs don't make a right. To be honest, I've seen members like Zomba, Ritz etc endeavoring to drag Nyerere's name through the mud

And I've been asking myself why this topic? Is it meant to pacify us in the face of grief?

I wish I knew what was going through your mind when you thought of this topic/motion. It is dividing us just when we were supposed to come together and speak with one voice

As far as I'm concerned Daudi Mwangosi murder is a watershed moment in public perceptions of state violence after Dr. Ulimboka incident

I got goose bumps when I heard Ritz supporting such brutality. Where is this country headed?

"Many more will have to suffer many more will have to die"
 
Kwa tulioishi awamu zote tukiwa watoto, teenagers and then watu wazima tunaweza kutofautisha clearly tawala hizi tatu yaani za Nyerere, Mwingi, Mkapa na Kikwete. Mkapa ndiye aliyeanzisha serikali ya Kidikteta kwa kumwua Imran Kombe then akaanzisha police brutality kuzima maandamano na kukandamiza haki za wananchi huku akianzisha makampuni na kujimilikisha rasilimali za taifa. Jk ameingia kwa mtazamo wa kujineemesha zaidi kuliko kuwasaidia wananchi huku akilazimisha kuwapumbaza waTZ wa kizazi hiki ambacho hakidanganyiki.

Since watu hawadanganyiki kirahisi imembidi JK kuwalazimisha wadanganyike na hiki ndicho kinachofanyika sasa. Wanataka kulazimisha watu waendelee kuamini kuwa CCM ndicho chama pekee kinachowafaa na hata pale asilimia 90% ya watanzania inapoona ni uongo na kuamua kusupport harakati za mabadiliko Polisi wanatumia nguvu na hiki ndich chanzo cha kuua kwenye mikutano ya M4C.

Mauaji hayataishia hapo ndugu zangu yataendelea na inabidi ieleweke kuwa CCM hawataachia madaraka kwa hiari kama Kenya(KANu) Zambia(ZANU-PF), Malawi n.k. bali itabidi maafa yatokee jumuhiya ya Kimataifa iingilie na watu wapelekwe the Hague ndo nchi ichukuliwe na chama kingine. Still we have a long way to go. Aluta Continua!!! Mungu yuko upande wetu
 
naomba habari hizi uzipeleke pia kwa baraza la maaskofu Tanzania. nani mtakatifu kati ya Mkapa, Nyerere na Kikwete?

Tango 73 hapa tunajadili mambo yaliotokea katka awamu zote za uongozi wa taifa letu Tanzania, sio rais muislamu na mkristo. tatizo lenu dini mpaka damuni! changia thread sio maaskofu!
 
Teh!teh!teh! Mnamzungumzia bi-kilembwe yule aliyekuwa analazimisha watu wakubali rangi nyeupe useme nyeusi na rangi nyeusi useme nyeupe?kaz kwelikweli
 
  • Idadi ya raia waliouawa kwenye mikono ya vyombo vya dola kati ya utawala wa Mkapa na Kikwete inazidi kwa mbali sana idadi ya waliouawa na vyombo vya dola kwa zaidi ya miongo miwili ya utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
  • Kiasi hicho pia kinazidi sana kile cha wale ambao hukumu ya kifo dhidi yao imetekelezwa.
  • Idadi ya watu waliotekelezewa hukumu ya kifo chini ya utawala wa Kikwete inazidi pia wale waliotekelezewa wakati wa utawala wote wa Nyerere.
  • Idadi ya watu waliohamishwa katika makazi yao kupisha wawekezaji wakubwa wa kimataifa chini ya utawala wa Kikwete na Mkapa inazidi sana watu waliohamishwa kwa ajili ya kujenga vijiji vya ujamaa (siyo kupisha wawekezaji).
  • Waandishi wa habari ambao wamejikuta matatani mahakamani na hata kupoteza maisha idadi yao ni wengi zaidi wakati wa Mkapa na Kikwete kuliko wakati wa Nyerere.
  • Mahasimu wengi wa serikali ya Nyerere wameishi na kuzeeka wakiishi wakiwa huru; wengi makubwa yaliyowapata ni ama kwenda uhamishoni au kuhamishwa na kutupwa maeneo ya pembezoni. Yanayowakuta sasa hivi wapinzani wa Kikwete na yaliyowakuta wapinzani wa Mkapa....

Lakini ni Nyerere ambaye anatajwa kuwa ni dikteta na kuwa alikuwa anakandamiza haki za wananchi. Inawezekana
mada zako ziku hizi zimepoteza muelekeo kabisa, hivi unajua kilichotokea kwenye villagelization na sera ya ujamaa ya nyerere?

Waliouawa kipindi cha Nyerere unaweza kuwajua wakati vyombo vya habari vyote vilikuwa vyake? sidhani kama mkapa na kikwete wametekeleza hukumu za vifo, labda kipindi cha mwinyi, lete data otherwise hizi ni porojo kama si poyoyo. waandishi wapi unaoongelea?

Akina mkapa na mzalendo na RTD? hivi wewe mwanakijiji umepeleka wapi akili zako? mbona unadicelerate kuliko kuaccelerate? unaongelea mahasimu wapi? akina kambona na akina babu? muulize huko kaburini alipo hayati timtemeke sanga.
Inshort, this is PUMBA.
 
Hili la Iringa, inawezekana kabisa mungu anataka tuonesha jambo.......mtego wa kwanza kuimaliza CDM umekwama.....kuna tetesi kuna bomu lilikuwa mikononi mwa polisi, lilitakiwa kuwekwa mfukoni mwa marehemu, ionekane ni wafuasi wa CDM na amekwenda na silaha mkutanini! , bahati mbaya likalipuka, sasa angalia wameshaanza sema alijufunga mabomu kuwadhuru polisi
 
Mzee Mwanakijiji with all due respect nakuomba ipitie ID hii Mlyafinono kuna kitu not normal Nashindwa kuongea moja kwa moja nisije kuwa navunja kanuni za JF, ila pitia thread zake zote na last started thread utapata jibu ni kwa nini yupo kimya mpaka leo hasa baada ya kuuwawa Daud Mwangosi?
JB tumekusoma mkuu,hebu tuvute subira kidogo then kitaeleweka tuu.
 
Bora kuwa dikteta kwa maslahi ya nchi na watu wake.kuliko kuwa dikteta kwa maslahi binafsi au ya chama.utawala wa mkapa na kikwete ni kwa maslahi binafsi wananchi wamewekwa mbali sana na ndio mana serikali imejaa washkaji na mashemeji mpaka wakwe wamo.Hatuwezi kuendelea na utawala huu wa chama na serikali.hayo ni maoni yangu.R.I.P MWL Nyerere.
 
Mkuu Chama hapa unakiri kuwa Mwangosi ameuwawa na serikali,wakati baadhi ya post zako unalaumu Chadema moja kwa moja...nadhani umegundua kuandika vitu tofauti na dhamira yako lazima moyo uumie kwa unafiki.!

Kumbe hujawashitukia,
Tokea jana jioni wameshagundua kuwa inawaharibia hii kitu na sasa wamegeuka kuwa IGP na RPC wachukuliwe hatua.
 
  • Idadi ya raia waliouawa kwenye mikono ya vyombo vya dola kati ya utawala wa Mkapa na Kikwete inazidi kwa mbali sana idadi ya waliouawa na vyombo vya dola kwa zaidi ya miongo miwili ya utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
  • Kiasi hicho pia kinazidi sana kile cha wale ambao hukumu ya kifo dhidi yao imetekelezwa.
  • Idadi ya watu waliotekelezewa hukumu ya kifo chini ya utawala wa Kikwete inazidi pia wale waliotekelezewa wakati wa utawala wote wa Nyerere.
  • Idadi ya watu waliohamishwa katika makazi yao kupisha wawekezaji wakubwa wa kimataifa chini ya utawala wa Kikwete na Mkapa inazidi sana watu waliohamishwa kwa ajili ya kujenga vijiji vya ujamaa (siyo kupisha wawekezaji).
  • Waandishi wa habari ambao wamejikuta matatani mahakamani na hata kupoteza maisha idadi yao ni wengi zaidi wakati wa Mkapa na Kikwete kuliko wakati wa Nyerere.
  • Mahasimu wengi wa serikali ya Nyerere wameishi na kuzeeka wakiishi wakiwa huru; wengi makubwa yaliyowapata ni ama kwenda uhamishoni au kuhamishwa na kutupwa maeneo ya pembezoni. Yanayowakuta sasa hivi wapinzani wa Kikwete na yaliyowakuta wapinzani wa Mkapa....

Lakini ni Nyerere ambaye anatajwa kuwa ni dikteta na kuwa alikuwa anakandamiza haki za wananchi. Inawezekana
Kwa maelezo haya unathibitisha kuwa Nyerere aliua, Mkapa aliua, Kikwete anaua (Mwinyi hukumtaja, hakuua?). Kwa ufupi hao uliowataja waliua/au vyombo vyao vya dola viliua.

Nadhani hakuna haja ya kutaka kujua nani kaua zaidi, ikiwa wote waliua hilo linatosha kujua kuwa TANZANIA TANGU UHURU VIONGOZI WETU NI WAUAWAJI.
 
Watetezi hamna hoja na badala yake kila anayeongea tofauti hamna lolote zaidi ya kusema tuna chuki na Nyerere.....huko no kukosa hoja kwenyewe kama hujui!

Wewe ulilo nalo lipi? Hizi kelele na kushindwa kabisa kuongoza watu? Nionyeshe lako la ziada linalokupa ushupavu wa kusema wengine hatuna lolote....maana anayedhani amesimama aangalie asianguke.Uzuri hakuna lililo siri kwenye mambo ya kuongoza public.
 
Dictator ni mtawala wa mabavu (hasa aliyetiwalia madaraka) asiyefuata demokrasia.
 
Mhh...Sisi slow learners tunapata shida sana kujua Kiranga ni mtu/kitu cha namna gani. Hasa tukifuatilia comment zake kwenye post nyingi za MMKJJ. Poor slow learners that is we!

Sasa sio wewe tu unayejionyesha slow, bali hata Mwalimu wako pia.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom