Mdahalo wa Ugomvi: Ati Nyerere alikuwa Dikteta; aliua wengi...

Wananchi wengi sana walihamishwa kwenye sera ya vijiji vya ujamaa, huwezi kufananisha na hawa tunawaowahamisha kwenye kupisha miradi mikubwa kwa faida ya wengi! Ukiangalia population wise utakuta hata zaidi ya 50% ya watanzania waliondolewa kwenye makazi yao which is very significant. Niambie asilimia ngapi ya Watanzania wamehamishwa kipindi cha Mkapa na Kikwete.
 
  • Mahasimu wengi wa serikali ya Nyerere wameishi na kuzeeka wakiishi wakiwa huru; wengi makubwa yaliyowapata ni ama kwenda uhamishoni au kuhamishwa na kutupwa maeneo ya pembezoni. Yanayowakuta sasa hivi wapinzani wa Kikwete na yaliyowakuta wapinzani wa Mkapa....

Mzee Mwanakijiji,
How come mtu aliyekimbilia uhamishoni useme aliishi akiwa huru?! Hivi mimi leo hii mtu anipeleke Amerika na nisiwe na uwezo kuja kuwaona ndugu zangu TZ utasema naishi Amerika nikiwa huru?! c'mon brother!!!
 
Mkuu wangu hili tukio kwa kweli linadhihirisha tu unachokisema. Na ni vigumu kuona tunazuia vipi lisitokee tena
Ni kweli mkuu tutafute tume huru ichunguze na hatua zichukuliwe lakini suluhisho la kudumu katiba Mpya Uhai wa Binadamu ulindwe kwa nguvu zote! Kama sikosei USA miaka ya 2000(possibly 2001) Mkapa akiongoza TZ na USA Bush mtu mmoja alikwenda white house akiwa na bunduki anasema anataka KUMUUA rais BUSH ,walinzi wa ikulu walimpiga risasi ya ganzi mguuni akapelekwa hospitali akatibiwa na baadaye akapimwa akili kabla ya kufunguliwa mashitaka,ndani ya Muda mfupi CUF/Wazanzibari wakawa wamepanga kuandamana ijumaa zanzibar baaada ya swala ya Ijumaa VP Dr. Omari Ali Jumaa (Chinja chinja) akawaambia msiandamane na mkitoka masjid mtembee mmoja mmoja Imam mmoja baada ya swala akawa anajadili na wenzie polisi wakasema tawanyikeni na mtoke hapo akagoma na akatwangwa risasi ya Moto Kichwani na kufa.
Linganisha matukio hayo mawili Kukusudia kumuua rais ikulu -risasi ya Mguu ya Ganzi,tiba na kupima akili.
Kuandamana kudai haki/kukusanyika msikitini baada ya swala risasi ya moto kichwan kufai! Chukua hatua
 
Dikteta sio lazima aue. Kiongozi alilazimisha mawazo yake kuwa ni msingi wa maisha ya watu wengine tayari ni dikteta hata kama ana nia nzuri.

kama wale viongozi waliolazimisha mawazo yao kwa kusema "The right to keep and bear arms".
 
Mh,nachoka kama kwa mauaji haya ya serikali ya JK,bado tunaambiwa kuna aliyeuwa zaidi yake!!basi
Mungu tusaidie watanzania"
 
Huyu wa sasa ni zaidi ya dikteta, anauwa watu wazi wazi, anazuia uhuru wa vyombo vya habari pia anatumia rasilimalizetu hovyo wakati maisha ya wananchi wake ni duni!

Kunawakati uhuru wa vyombo vya habari umekua mkubwa kuliko sasa!?
 
Kwa bahati mbaya nayafahamau machache mno yaliyotokea enzi za utawala wa mwalimu simply because hadi anaondoka madarakani bado nilikuwa kinda nisiye na hamu yoyote ya kufahamu yale yanayotokea nje ya mtaani kwangu! Pamoja na hayo, bado nina uhakika na jambo moja ingawaje nalo halina mashiko yak u-justify mauaji yanayotokea hivi sasa! Jambo lenyewe ni kwamba, mazingira ya sasa; 1995-2012 na zama za mwalimu yapo tofauti sana! Narudia, utofauti wa mazingira bado hau-justify yanayotokea hivi sasa lakini sina shaka kwamba kama mazingira ya enzi za mwalimu nayo yangekuwa kama ya sasa basi huenda pasingekuwa na tofauti yoyote na haya yanayotokea sasa; na si ajabu huenda hali ingeweza kuwa mbaya zaidi kuliko sasa!

Pamoja na utofauti wa kimazingira, bado jambo moja lipo wazi pia. Nyerere hakuwa mstahimilivu kwa wale wanaompinga hususani katika uwanja wa siasa! Wapinzani wa mwalimu waliwekwa kizuizini na wengine kukimbilia uhamishoni na hata wengine kufungwa…! Nasikia hata kuna baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu ambao nao walipata kutandikwa bakora na mwalimu! Sina tafsiri mzuri ya kitendo kama hicho endapo kweli kilipata kutokea zaidi ya kuita ni udikteta na ukiukwaji hali ya juu wa haki za binadamu…..hawa walikuwa ni watu wazima lakini waliweza kutandikwa bakora!!

Oscar Kambona alikimbia nchi kwavile alifahamu nini kingemkuta endapo angeendelea kubaki nchini! Pamoja na kwamba Nyerere alikuwa mzito kutekeleza adhabu ya kifo ambazo zilitolewa na mahakama zake mwenyewe chini ya sharia ambazo alizipitisha mwenyewe; bado alifanya haraka ya kuhidhinisha adhabu ya kunyongwa hadi kufa dhidi ya muuaji wa Dr. Kleruu! Kwa kuwa muuaji wa Dr Kleruu alikuwa ni mpinzani wa sera za Ujamaa na Azimio la Arusha kwa vitendo, basi sina shaka kwamba hapa Nyerere alikusudia kutoa ujumbe kwa mwananchi yeyote ambae atakuwa mpinzani wa sera zake!

Aidha, Wale watu wazima hapa waache ushabiki, nawaomba watueleze ukweli. Inasemekana kwamba wakati wa operesheni ya vijiji vya ujamaa, kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu! Je, inawezekana kweli hapakutokea raia ambao walipoteza maisha wakati wa opersheni hiyo?!

Sasa ikiwa mwalimu alishindwa kabisa kuwavumilia wanafunzi na viongozi wenzake ambao alikuwa nao kwenye chama kimoja na serikali moja tena huku wengine wakiwa ni washirika wake; je angeweza kuvumilia kimbunga cha hivi sasa cha CHADEMA endapo hali hii ingetokea zama zake?! Sincerely, ASINGEWEZA na bila shaka huenda maafa yangekuwa ni makubwa maradufu kuliko ya hivi sasa!
 
Wananchi wengi sana walihamishwa kwenye sera ya vijiji vya ujamaa, huwezi kufananisha na hawa tunawaowahamisha kwenye kupisha miradi mikubwa kwa faida ya wengi! Ukiangalia population wise utakuta hata zaidi ya 50% ya watanzania waliondolewa kwenye makazi yao which is very significant. Niambie asilimia ngapi ya Watanzania wamehamishwa kipindi cha Mkapa na Kikwete.

Nafikiri hao wawekezaji wenu ndio tatizo la msingi kwa mambo yote haya, kwani wawekezaji wamekuja kupitia mlango wa nyuma tena kwa rushwa chafu, hivyo mnaona shida kung'oka kistaarabu mkiogopa kuja kuwajibishwa nyinyi pamoja na hao wawekezaji uchwara, nafikiri kuna haja ya kushughulika na wawekezaji kwanza halafu nyie mfuate baadaye
 
KInachosikitisha ni kuwa, Dk wenu Slaa ANAUA KABLA HAJAINGIA MADARAKANI! akiingia itakuwaje? uvunjifu wa sheria anaouvunja slaa ndio chanzo cha police kuingia katika mgogoro na wananchi! na inapelekea watu wengi kuuawa na wengine kuumizwa vibaya! je na Slaa nae aingizwe katika record ya kuua kabla hajaukwa urais?
 
  • Idadi ya raia waliouawa kwenye mikono ya vyombo vya dola kati ya utawala wa Mkapa na Kikwete inazidi kwa mbali sana idadi ya waliouawa na vyombo vya dola kwa zaidi ya miongo miwili ya utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
  • Kiasi hicho pia kinazidi sana kile cha wale ambao hukumu ya kifo dhidi yao imetekelezwa.
  • Idadi ya watu waliotekelezewa hukumu ya kifo chini ya utawala wa Kikwete inazidi pia wale waliotekelezewa wakati wa utawala wote wa Nyerere.
  • Idadi ya watu waliohamishwa katika makazi yao kupisha wawekezaji wakubwa wa kimataifa chini ya utawala wa Kikwete na Mkapa inazidi sana watu waliohamishwa kwa ajili ya kujenga vijiji vya ujamaa (siyo kupisha wawekezaji).
  • Waandishi wa habari ambao wamejikuta matatani mahakamani na hata kupoteza maisha idadi yao ni wengi zaidi wakati wa Mkapa na Kikwete kuliko wakati wa Nyerere.
  • Mahasimu wengi wa serikali ya Nyerere wameishi na kuzeeka wakiishi wakiwa huru; wengi makubwa yaliyowapata ni ama kwenda uhamishoni au kuhamishwa na kutupwa maeneo ya pembezoni. Yanayowakuta sasa hivi wapinzani wa Kikwete na yaliyowakuta wapinzani wa Mkapa....

Lakini ni Nyerere ambaye anatajwa kuwa ni dikteta na kuwa alikuwa anakandamiza haki za wananchi. Inawezekana

Ahai yangu Mwanakijiji,

Kumbuka kila watu na karne na zama zao.

Ukinyumbulisha zaidi utaona enzi za Nyerere hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari. Kulikuwa na Chama kimoja tu cha siasa, vyombo vya habari vilimilikiwa na Serikali na habari zote kabla kwenda hewani zilihakikiwa na Serikali.

sasa hivi kuna uhuru mkubwa ana wa waandishi wa habari.

Lakin ni bora mtu akupige risasi na kukuuwa kuliko kukufungia kimawazo na kuzuia kutumia taaluma yako. Mfano ni Tuntemeke Sanga. au Mwalimu Kazibure wa Kibaha Sec. Huku ni kubaya zaidi ni bora kuuwawa.

Wakti wa Nyerere wengi walikimbia nchi sababu tu ukitofautiana na Nyerere.

Mimi naamini wazi Nyerere alikuwa ni zaidi ya Dikteta kwani yeye alicheza kwa kuzimiliki akili za wa Tz.

Poleni sana

Mzee Mwanakijiji,

Sijui hii thread yako unataka kutuambia nini mie nichoweza kusema uhuru wa vyombo vya habari ambao tunao hivi sasa umechangia sie kufahamu mambo mengi yanayofanywa na serikali, huwezi kufananisha na wakati wa Nyerere kulikuwa hakuna uhuru wa vyombo vya habari.

Wakati wa Nyerere upatikanaji wa habari na mijadala kama hii vilikuwa hakuna Nyerere mpaka anamaliza utawala wake wananachi hawakuwahi hata kuangalia bunge kupitia tv wala kuhoji chochote katika utawala wake na kuna watu wengi baada ya kuondoka Nyerere wamejitokeza na kulalamika walivyokandamizwa na utawala wa Nyerere, labda tujiulize kwa nini wapinzani wa Nyerere ndani ya chama chake walikimbilia nje ya nchi walikuwa wanahofia nini.

Fanya utafiti hujue kina nani walipoteza maisha wakati wa Nyerere, sio kuwasemea watanzania waamini mapenzi yako, kila tawala zina wakati wake na kila tawala zina mazuri yake na mabaya yake na kila tawala zinafanya mauuwaji.
 
Last edited by a moderator:
  • Idadi ya raia waliouawa kwenye mikono ya vyombo vya dola kati ya utawala wa Mkapa na Kikwete inazidi kwa mbali sana idadi ya waliouawa na vyombo vya dola kwa zaidi ya miongo miwili ya utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
  • Kiasi hicho pia kinazidi sana kile cha wale ambao hukumu ya kifo dhidi yao imetekelezwa.
  • Idadi ya watu waliotekelezewa hukumu ya kifo chini ya utawala wa Kikwete inazidi pia wale waliotekelezewa wakati wa utawala wote wa Nyerere.
  • Idadi ya watu waliohamishwa katika makazi yao kupisha wawekezaji wakubwa wa kimataifa chini ya utawala wa Kikwete na Mkapa inazidi sana watu waliohamishwa kwa ajili ya kujenga vijiji vya ujamaa (siyo kupisha wawekezaji).
  • Waandishi wa habari ambao wamejikuta matatani mahakamani na hata kupoteza maisha idadi yao ni wengi zaidi wakati wa Mkapa na Kikwete kuliko wakati wa Nyerere.
  • Mahasimu wengi wa serikali ya Nyerere wameishi na kuzeeka wakiishi wakiwa huru; wengi makubwa yaliyowapata ni ama kwenda uhamishoni au kuhamishwa na kutupwa maeneo ya pembezoni. Yanayowakuta sasa hivi wapinzani wa Kikwete na yaliyowakuta wapinzani wa Mkapa....

Lakini ni Nyerere ambaye anatajwa kuwa ni dikteta na kuwa alikuwa anakandamiza haki za wananchi. Inawezekana

Ila ng'we hii bado haijakamilika ili analysis ikamilike vizuri tena kwa haki kabisa. Maana kadri wanavyojitahidi kumchafua Nyerere, ndivyo wanavyomsaidia kumpa nafasi ya pekee kabisa ya jinsi uongozi wa nchi yetu unavyokwenda kwenda toka uhuru. Mimi ni mpenzi wa nchi yangu ya Tanzania bila kumdharau wala kumdhalilisha yoyote. Udini, ukabila, rushwa na kupendeleana yanatupeleka? Status Quo mpya ya Taifa hili ni kama wananchi wa kawaida comes after some few top officials with their counterparts called wawekezaji
 
Kwa maana hiyo mauwaji ni ruksa kwa kila utawala? 50 years on ruling how many have you killed dude?
 
Ila ng'we hii bado haijakamilika ili analysis ikamilike vizuri tena kwa haki kabisa. Maana kadri wanavyojitahidi kumchafua Nyerere, ndivyo wanavyomsaidia kumpa nafasi ya pekee kabisa ya jinsi uongozi wa nchi yetu unavyokwenda kwenda toka uhuru. Mimi ni mpenzi wa nchi yangu ya Tanzania bila kumdharau wala kumdhalilisha yoyote. Udini, ukabila, rushwa na kupendeleana yanatupeleka? Status Quo mpya ya Taifa hili ni kama wananchi wa kawaida comes after some few top officials with their counterparts called wawekezaji

Tatizo la watetezi wa Nyerere cku zote mnakosa hoja zenye mashiko na kukimbilia kuwaita majina yasiyofaa wale wote wanaoeleza -ve side za Nyerere!! Ni kawaida kila anayesema mabaya ya Nyerere akina nyie kukimbilia kwamba "tunamchafua" na wengine kudai kwamba eti tunatumwa na kwamba tuna chuki dhidi yake! Mkuu wangu Ndahani, mazingira ya kisiasa na kijamii yaliyopo hivi sasa ndo ingekuwa wakati wa Nyerere basi hali ingekuwa mbaya maradufu! Jaribuni kumtetea Nyerere kwa hoja badala ya kujificha kwenye viroja...!!!
 
Tatizo la watetezi wa Nyerere cku zote mnakosa hoja zenye mashiko na kukimbilia kuwaita majina yasiyofaa wale wote wanaoeleza +ve side za Nyerere!! Ni kawaida kila anayesema mabaya ya Nyerere akina nyie kukimbilia kwamba "tunamchafua" na wengine kudai kwamba eti tunatumwa na kwamba tuna chuki dhidi yake! Mkuu wangu Ndahani, mazingira ya kisiasa na kijamii yaliyopo hivi sasa ndo ingekuwa wakati wa Nyerere basi hali ingekuwa mbaya maradufu! Jaribuni kumtetea Nyerere kwa hoja badala ya kujificha kwenye viroja...!!!

Wewe ndio una hoja?
 
  • Idadi ya raia waliouawa kwenye mikono ya vyombo vya dola kati ya utawala wa Mkapa na Kikwete inazidi kwa mbali sana idadi ya waliouawa na vyombo vya dola kwa zaidi ya miongo miwili ya utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
  • Kiasi hicho pia kinazidi sana kile cha wale ambao hukumu ya kifo dhidi yao imetekelezwa.
  • Idadi ya watu waliotekelezewa hukumu ya kifo chini ya utawala wa Kikwete inazidi pia wale waliotekelezewa wakati wa utawala wote wa Nyerere.
  • Idadi ya watu waliohamishwa katika makazi yao kupisha wawekezaji wakubwa wa kimataifa chini ya utawala wa Kikwete na Mkapa inazidi sana watu waliohamishwa kwa ajili ya kujenga vijiji vya ujamaa (siyo kupisha wawekezaji).
  • Waandishi wa habari ambao wamejikuta matatani mahakamani na hata kupoteza maisha idadi yao ni wengi zaidi wakati wa Mkapa na Kikwete kuliko wakati wa Nyerere.
  • Mahasimu wengi wa serikali ya Nyerere wameishi na kuzeeka wakiishi wakiwa huru; wengi makubwa yaliyowapata ni ama kwenda uhamishoni au kuhamishwa na kutupwa maeneo ya pembezoni. Yanayowakuta sasa hivi wapinzani wa Kikwete na yaliyowakuta wapinzani wa Mkapa....

Lakini ni Nyerere ambaye anatajwa kuwa ni dikteta na kuwa alikuwa anakandamiza haki za wananchi. Inawezekana

Je, CCM yote inatatizo la 'pyschopath'?
 
naomba habari hizi uzipeleke pia kwa baraza la maaskofu Tanzania. nani mtakatifu kati ya Mkapa, Nyerere na Kikwete?

Nadhani hakunae hata mmoja sema nyerere alijawa na busara ya hali ya juu na hakuwa kimya pale palipokuwa na tatizo alijua wajibu wake pasipokuangalia mwelekeo wa upepo
 
Mzee Mwanakijiji,
Naloweza kusema tu kwa leo ni kwamba we are out of control! Hili linchi linajiendesha lenyewe kama gari bovu na hakika JK uongozi umemshinda. Haijulikani leo rais wetu ni nani, bunge na mahakama vyote ni vyombo visivyokuwa na mwongozo isipokuwa kwa maslahi ya watu. Hizi ndio athari kubwa za mfumo tulochukua na nakuhakikishia haijalishi nani atakuwa madarakani mambo haya hayatakwisha kesho..

Je yataisha kwa mimi wewe na wengine kuishia kulalamika kwenye keyboard zetu pasipokuchukua hatua thabiti za kuikosoa serikali yetu kwa matendo yao mabaya na kandamizi dhidi ya raia wake?
 
Mzee Mwanakijiji with all due respect nakuomba ipitie ID hii Mlyafinono kuna kitu not normal Nashindwa kuongea moja kwa moja nisije kuwa navunja kanuni za JF, ila pitia thread zake zote na last started thread utapata jibu ni kwa nini yupo kimya mpaka leo hasa baada ya kuuwawa Daud Mwangosi?

Siyo kwamba yupo kwenye mazishi bado?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom