Mdahalo wa Ugomvi: Ati Nyerere alikuwa Dikteta; aliua wengi...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
  • Idadi ya raia waliouawa kwenye mikono ya vyombo vya dola kati ya utawala wa Mkapa na Kikwete inazidi kwa mbali sana idadi ya waliouawa na vyombo vya dola kwa zaidi ya miongo miwili ya utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
  • Kiasi hicho pia kinazidi sana kile cha wale ambao hukumu ya kifo dhidi yao imetekelezwa.
  • Idadi ya watu waliotekelezewa hukumu ya kifo chini ya utawala wa Kikwete inazidi pia wale waliotekelezewa wakati wa utawala wote wa Nyerere.
  • Idadi ya watu waliohamishwa katika makazi yao kupisha wawekezaji wakubwa wa kimataifa chini ya utawala wa Kikwete na Mkapa inazidi sana watu waliohamishwa kwa ajili ya kujenga vijiji vya ujamaa (siyo kupisha wawekezaji).
  • Waandishi wa habari ambao wamejikuta matatani mahakamani na hata kupoteza maisha idadi yao ni wengi zaidi wakati wa Mkapa na Kikwete kuliko wakati wa Nyerere.
  • Mahasimu wengi wa serikali ya Nyerere wameishi na kuzeeka wakiishi wakiwa huru; wengi makubwa yaliyowapata ni ama kwenda uhamishoni au kuhamishwa na kutupwa maeneo ya pembezoni. Yanayowakuta sasa hivi wapinzani wa Kikwete na yaliyowakuta wapinzani wa Mkapa....

Lakini ni Nyerere ambaye anatajwa kuwa ni dikteta na kuwa alikuwa anakandamiza haki za wananchi. Inawezekana
 
naomba habari hizi uzipeleke pia kwa baraza la maaskofu Tanzania. nani mtakatifu kati ya Mkapa, Nyerere na Kikwete?
 
Mwanakijiji
Acha tumalize haya Mwangosi (R.I.P) hakuna serikali isiyoua duniani; Nitajie moja kwenye historia ya dunia hii

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu Chama hapa unakiri kuwa Mwangosi ameuwawa na serikali,wakati baadhi ya post zako unalaumu Chadema moja kwa moja...nadhani umegundua kuandika vitu tofauti na dhamira yako lazima moyo uumie kwa unafiki.!
 
Tuliza akili yako siilaumu Chadema kwa kifo cha Mwangosi namlaumu Dr. Slaa na tamaa zake; tafadhali usitie maneno yako kwenye kinywa changu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mzee Mwanakijiji,
Naloweza kusema tu kwa leo ni kwamba we are out of control! Hili linchi linajiendesha lenyewe kama gari bovu na hakika JK uongozi umemshinda. Haijulikani leo rais wetu ni nani, bunge na mahakama vyote ni vyombo visivyokuwa na mwongozo isipokuwa kwa maslahi ya watu. Hizi ndio athari kubwa za mfumo tulochukua na nakuhakikishia haijalishi nani atakuwa madarakani mambo haya hayatakwisha kesho..
 
Mkuu wangu hili tukio kwa kweli linadhihirisha tu unachokisema. Na ni vigumu kuona tunazuia vipi lisitokee tena
 
Mkuu wangu hili tukio kwa kweli linadhihirisha tu unachokisema. Na ni vigumu kuona tunazuia vipi lisitokee tena
Ni Ujasiri wa kufanya kile ambacho hakikutegemewa. Kesi hii ipelekwe mahakama za kimataifa ikiwa hatutapewa majibu sahihi nani aliyetoa amri ya kutumia nguvu ya ziada katika mauaji haya. Hizo picha ni ushahidi mkubwa sana zikienezwa ktk kila TV station maarufu duniani...
 
...Maneno mazito sana haya na ni ukweli mtupu. Nyerere kama alivyowahi kuzungumza mwenyewe hakuwa perfect kama kiongozi alikuwa na mapungufu yake chungu nzima lakini kamwe ubora wake kama kiongozi hauwezi hata siku moja kufananishwa na mafisadi waliomfuatia akina Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Alijitahidi sana katika kuboresha maisha ya Watanzania pamoja na kuwa na vyanzo vichache vya mapato na kupigwa vita sana na nchi za magharibi.

Pamoja na matatizo makubwa aliyoyapata kama Kiongozi kama vile kupigwa vita na nchi za magharibi, vita na Idi Amin, vyanzo duni vya mapato lakini mafanikio yake hasa katika nyanja za elimu bado yanaonekana katika sehemu mbali mbali duniani ambapo wasomi wengi walioko katika nchi hizo ni wale waliosoma kupitia sera za Mwalimu na pia juhudi zake za kuleta mshikamano miongoni mwa Watanzania ambapo sasa zinavurugwa na magamba bado zinaonekana hadi hii leo hata hii JF tunaweza kusema kwamba mshikamano unaonyeshwa hapa kwa asilimia kubwa umechangiwa na Mwalimu. Badala ya kuwepo hapa kimakabila tupo hapa kama Watanzania.

Mzee Mwanakijiji,
Naloweza kusema tu kwa leo ni kwamba we are out of control! Hili linchi linajiendesha lenyewe kama gari bovu na hakika JK uongozi umemshinda. Haijulikani leo rais wetu ni nani, bunge na mahakama vyote ni vyombo visivyokuwa na mwongozo isipokuwa kwa maslahi ya watu. Hizi ndio athari kubwa za mfumo tulochukua na nakuhakikishia haijalishi nani atakuwa madarakani mambo haya hayatakwisha kesho..
 
Ni Ujasiri wa kufanya kile ambacho hakikutegemewa. Kesi hii ipelekwe mahakama za kimataifa ikiwa hatutapewa majibu sahihi nani aliyetoa amri ya kutumia nguvu ya ziada katika mauaji haya. Hizo picha ni ushahidi mkubwa sana zikienezwa ktk kila TV station maarufu duniani...
Katika kadhia hii ni Helen Kijo Bisimba peke yake ndio ameongea la maana jana mchana kwa kusema Kituo cha sheria na haki za binadamu hakitotowa tamko lolote kuhusu mauwaji haya bali wanakwenda moja kwa moja kwenye Mahakama ya kimataifa kuishtaki Serikali, muda wa matamko ambayo hayafanyiwi kazi umepita.
 
Watakuja wakina zomba waseme idadi ya watu ya kipindi cha Nyerere haikuwa kubwa Kama sasa hivi lakini bado naungana na wewe kwasababu ukijaribu kutafuta wastani utakuta vipindi vya hawa maraisi watatu wameua kipitiliza ukilinganisha na kipindi kile cha Nyerere ambacho hata neno fisadi halikuwahi kutajwa midomoni mwa wananchi
 
Kwa muono wangu Nyerere aliua sana! tatizo tu ni hakukuwa na vyombo vya habari vingi na huru kureport kama ilivo leo may be,most deaths went unreported. Uelewa/mwamko wa watu kufuatilia habari ulikuwa mdogo mno. Tunaona tu sasa vyombo vinavyomilikiwa na serikali vinavojaribu kuchakachua habari kwa maslahi ya ccm(rejea reporting ya gazeti la habari leo) inshu hii ya Daud,,sembuse enzi hizo kulipokuwa na chombo kimoja tu owned by Gvt?
 
Please, make an effort to separate between opinion and facts; remember, you are entitled to your own OPINION but not your own FACTS;
 
Hii thread ingependeza kuwepo kule kwa jukwaa la great thinkers, hapa tutaitia najisi tu na hisia zetu kuliko facts
 
Back
Top Bottom